Datasets:
text
stringlengths 0
24.2k
| label
class label 6
classes |
---|---|
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema, itafanya misafara ya kutangaza utalii kwenye miji minne nchini China kati ya Juni 19 hadi Juni 26 mwaka huu.Misafara hiyo itatembelea miji ya Beijing Juni 19, Shanghai Juni 21, Nanjig Juni 24 na Changsha Juni 26.Mwenyekiti wa bodi TTB, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.“Tunafanya jitihada kuhakikisha tunavuna watalii wengi zaidi kutoka China hasa tukizingatia umuhimu wa soko la sekta ya utalii nchini,” amesema Jaji Mihayo.Novemba 2018 TTB ilifanya ziara kwenye miji ya Beijing, Shanghai, Chengdu, Guangzhou na Hong Kong kutangaza vivutio vya utalii sanjari kuzitangaza safari za ndege za Air Tanzania.Ziara hiyo inaelezwa kuzaa matunda ikiwa ni pamoja na watalii zaidi ya 300 kuja nchini Mei mwaka huu kutembelea vivutio vya utalii. | 0uchumi
|
PENDO FUNDISHA-MBEYA RAIS Dk. John Magufuri, ametangaza kuwafukuza
kazi wakurugenzi wote wa halmashauri ambao watabainika kukiuka sheria ya
ufutaji wa tozo za ushuru wa mazao. Alisema baada ya kuingia madarakani, Serikali
iliondoa tozo 80, miongoni mwa hizo tozo ushuru wakulima ambao walikuwa
wakilipa mazao kutoka halmashauri moja kwenda nyingine. Rais Dk. Magufuli, aliyasema hayo juzi alipokuwa
akiwahutubia wakazi wa Wilaya ya Kyela katika ziara ya kikazi ya siku 10 mkoani
Mbeya. Alisema, sheria ya ufutaji wa tozo hizo
zilipitishwa na Bunge hivyo hakuna mtu yoyote wa kuitengua na kwamba Mkurugenzi
atakaye itengua atakuwa umevunja sheria na anawajibu wa kufukuzwa kazi. Alisema licha ya kupitishwa kwa sheria hiyo wapo
baadhi ya watendaji wameendelea kuwatoza ushuru wananchi kwa kisingizio cha
kupandisha ukusanyaji wa mapato hilo jambo sitaki kulisikia. “Wapo watendaji
wanasema kufutwa kwa ushuru kunapunguza mapato, narudia kwa viongozi wote, wakurugenzi,
watendaji wote wa halmashauri msiwatoze wananchi ushuru wa mzigo wowote usio
zidi tani moja,”alisema. Hata hivyo, alitoa wito kwa watendaji kuzingatia
sheria ya kuwalinda wakulima na ndio maana serikali iliziondoa tozo 80. | 1kitaifa
|
Mwandishi Wetu -Singida BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 katika wilaya kadhaa nchini. Misaada iliyotolewa na benki hiyo inayoongoza kwa kutengeneza faida kati ya benki zote zinazofanya biashara humu nchini ndani ya miezi mitano mwaka huu, inahusisha vifaa vya ujenzi, madawati na vifaa vingine vinavyowezesha ukamilishaji wa miradi ya afya,elimu na usalama wa raia. Benki ya NMB imeshatoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 kwa mikoa ya Kanda ya Kati. Akifafanua kuhusu misaada hiyo wakati akikabidhi msaada wa madawati na vitanda kwa baadhi ya shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani ingida, Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB, Nsolo Mlozi, alibainisha kuwa misaada hiyo ya zaidi ya Sh milioni 200 iliyotolewa imelenga sekta ya elimu, afya na majanga kwa mikoa mitatu ya Kanda ya kati. Akikabidhi msaada wa madawati na vitanda kwa baadhi ya shule za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, MkoaniSingida, katika shule ya Sekondari ya New Kiomboi, Mlozi alisema fedha hizo zilizotolewa na NMB zimetumika kununua madawati, viti vya shule za sekondari,vitanda na vifaa tiba kwenye sekta ya afya. Aidha, alisema lengo la misaada hiyo ni kuunga mkono juhudi za serikali kuwahudumia wananchi kwenye sekta mbalimbali. Pia alisema misaada hiyo imekabidhiwa kwa baadhi ya shule, zahanati, hospitali katika mikoa ya Singida, Dodoma na Manyara. Pia NMB walikabidhi madawati 250 na vitanda 80 vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 29.5 kwa baadhi ya shule za Wilaya ya Iramba mkoani humo. Katika hatua nyingine, Benki hiyo imevipatia kituo cha Polisi Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro pamoja na shule ya msingi Msowelo mabati 160 yenye thamani ya Sh5 milioni kwa ajili ya kuezekea maboma. NMB iliamua kutoa msaada huo ikiwa ni mpango wa kuzipunguza baadhi ya changamoto kwa taasisi za serikali hapa nchini, Meneja wa NMB kanda ya mashariki, Baraka Ladislaus, alisema na kubainisha kuwa msaada huo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ili kusaidia kuinua miradi ya maendeleo. Baraka alisema kuwa kati ya mabati hayo, kituo cha polisi wilaya kimepa tamabati 80 huku shule ya msingi Msowelo nayo ikipata mabati 80. | 0uchumi
|
TIMU ya taifa ya Tanzania, Serengeti Boys jana ilijiweka katika nafasi fi nyu katika mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Uganda kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Uganda waliandika bao lao la kwanza katika dakika ya 15 lililofungwa na Kawooya Andrew akiunganisha wavuni krosi ya Najibu Viga huku lile la pili likifungwa na Asaba Ivan katika dakika ya 27 Najib Yiga.Serengeti Boys iliendelea kulala, Yiga aliifungia Uganda bao la tatu na la ushindi na kuifanya Serengeti kushika mkia katika Kundi A na kuacha simanzi kwa wapenzi wa soka nchini. Serengeti Boys inasubiri mchezo wa mwisho dhidi ya Senegal huku Nigeria ikisonga mbele baada ya kushinda mchezo wake wa awali kwenye uwanja huo na kufikisha pointi sita baada ya kushinda ule wa ufunguzi dhidi ya Tanzania. | 2michezo
|
Na AGATHA CHARLES – DAR ES SALAAM ALIYEKUWA Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa katika Sekretarieti ya Chama cha ACT-Wazalendo, Habibu Mchange, amejiondoa uanachama wa chama hicho na kujiweka kando na siasa. Taarifa ya uamuzi huo wa Mchange ilisambazwa jana katika mitandao ya kijamii, ikionyesha kuandikwa naye huku ikiambatanishwa na namba yake ya simu. Katika andiko hilo, Mchange aliyewahi kuwa mwanachama wa Chadema kabla hajahamia ACT Wazalendo, alisema aliamua kujitoa rasmi katika ushiriki wa aina yoyote ya siasa ili apate muda zaidi wa kusimamia shughuli zake za kijasiriamali. Mchange alisema ameamua kujiengua na siasa ili kutoa fursa na huduma sawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa. “Kwa moyo mkunjufu kabisa na kwa mapenzi mema na taifa langu, ninathibitisha kwamba nimejitoa rasmi katika ushiriki wa aina yote ya siasa ili nipate muda mwingi zaidi kufanya na kusimamia shughuli zangu za kijasiriamali zinazonitaka nitoe fursa na huduma sawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa,” alisema Mchange. Alisema kutokana na uamuzi huo ambao aliomba uheshimiwe, lolote atakalolifanya lisihusishwe na chama bali iwe ni msimamo wake mwenyewe kama mtu huru asiye na chama. “Ninafahamu kuwa mwanachama wa chama cha siasa ni haki yangu ya kikatiba, lakini nimeamua kuihifadhi kwa sasa mpaka hapo nitakapoona inafaa kufanya vinginevyo. Ninawatakia kila la heri waliokuwa wanachama wenzangu wa ACT Wazalendo katika kuyafikia malengo ya msingi ya uanzishwaji wa chama hicho,” alisema Mchange. Mchange alisema kujiondoa kwake kusihesabiwe kama sehemu ya kukwamisha au kurudisha nyuma matarajio na au malengo ya chama hicho bali ichukuliwe kama chachu ya kufika mbali. “Msivunjike moyo, msirumbane, pendaneni, heshimianeni na shikamaneni ili mfikie lengo. Nitabaki na kuendelea kuwa ndugu yenu, rafiki na swahiba. Zaidi Mtanzania mwenzenu. Tutaendelea kushirikiana katika mambo yote ya kijamii na kimaisha yasiyohusiana na mlengo wa kiitikadi wa kisiasa,” alisema Mchange. Mchange alishika nafasi mbalimbali katika chama hicho ikiwamo Katibu wa Mipango na Mikakati, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu. MTANZANIA Jumapili lilimtafuta Mchange kwa simu kuthibitisha andiko hilo, lakini hakuweza kupatikana. Alipotafutwa Ofisa Habari wa ACT-Wazalendo, Abdallah Khamis, alikiri andiko hilo kuwa ni la Mchange. Mchange anakuwa mwanasiasa wa tatu kuondoka ACT-Wazalendo mwaka huu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba kuachia nafasi yake na kwenda masomoni nchini Kenya, Aprili mwaka huu. Miezi michache baadaye, Novemba mwaka huu mwanasiasa Moses Machali naye alitangaza kujiondoa rasmi chama hicho na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dk. John Magufuli. Machali aliwahi kuwa Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi kabla ya mwaka jana kushindwa kutetea jimbo lake kupitia ACT-Wazalendo. | 1kitaifa
|
MAJADILIANO kati ya aliyekuwa Mkurugenzi wa zamani wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kulthum Mansoor anayekabiliwa na mashitaka ya utakatishaji fedha na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), yamekufa baada ya pande hizo kushindwa kuafi kiana.Wakili wa Utetezi, Elia Mwingira alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Godfrey Isaya wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa. Alidai mazungumzo kati ya pande hizo, yamekufa kwa kushindwa kuelewana, hivyo aliomba mahakama iwaelekeze upande wa mashitaka kukamilisha upelelezi. Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai kuchelewa kwa upelelezi, kumesababishwa na upande wa utetezi ambao waliandika barua kwa DPP, hivyo aliomba waeleze wamefikia wapi.“Mazungumzo yalikufa kwa sababu tulishindwa kuelewana, hivyo tunaomba waharakishe upelelezi kwani kesi ni ya muda mrefu,”alidai Mwingira. Oktoba 30, mwaka jana upande wa utetezi waliieleza mahakama hiyo kwamba mteja wao ameandika barua kwa DPP, kuomba kuingia makubaliano na kukiri makosa yake.Baada ya kueleza hayo, Hakimu Isaya aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 20 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Kulthum anakabiliwa na mashitaka manane ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha Sh bilioni 1.477.Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 2013 na Mei 2018, mshitakiwa alighushi barua ya ofa ya Agosti 13, 2003 kwa madhumuni ya kuonesha kuwa barua hiyo, imetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo huku akijua kuwa sio kweli.Katika mashitaka ya pili inadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017 katika maeneo ya Upanga ndani ya Wilaya ya Ilala, mshitakiwa kwa kudanganya alijipatia Sh milioni 5.2 kutoka kwa Alex Mavika ambaye ni mfanyakazi wa Takukuru, kama malipo ya kiwanja kilichopo Kijiji cha Ukuni Bagamoyo.Pia inadaiwa kati ya tarehe hizo, Kulthum alijipatia Sh milioni tatu kutoka kwa Wakati Katondo, kama malipo ya kiwanja kilichopo maeneo ya Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.Mshitakiwa huyo pia alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Ofisa wa Takukuru, Gogo Migutah kama malipo ya kiwanja kilichopo eneo hilo hilo. Katika mashitaka ya tano, inadaiwa Kulthum alijipatia Sh milioni saba kutoka kwa Ekwabi Majungu ambaye pia ni ofisa wa Takukuru kama malipo ya kiwanja hicho.Kulthum anadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017, maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathminu, alijipatia Sh milioni saba kutoka kwa John Sangwa kama malipo ya kiwanja cha eneo hilo.Indaiwa mshitakiwa akiwa mwajiriwa wa Takukuru, alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Rose Shingela kwa ajili ya malipo hayo. Katika mashitaka ya utakatishaji fedha inadaiwa kati ya Januari 2013 na Mei 2018 huko maeneo ya Upanga, mshitakiwa alijipatia Sh 1,477,243,000 wakati akijua kuwa fedha hizo ni haramu na ni zao la kosa tangulizi la kughushi. | 1kitaifa
|
Mwandishi
Wetu – butiama MKUU wa majeshi
mstaafu, Jenerali David Msuguri, ameadhimisha miaka 100 tangu azaliwe Januari
4, 1920. Licha ya
uwezo wake wa kutembea kupungua, Jenerali Msuguri ambaye amelitumikia Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa miaka 55 na miezi saba, ameadhimisha miaka 100
akionekana mwenye nguvu tofauti na wengine wanaotimiza umri huo. Mkuu huyo
mstaafu wa majeshi aliadhimisha kumbukumbu hiyo jana nyumbani kwake Wilaya ya
Butiama mkoani Mara kwa kufanya ibada ya misa takatifu iliyoongozwa na Askofu
wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Musoma, Michela Msongazila. Mwonekano wa
Jenerali Msuguri mwenye nguvu na zaidi kufikisha umri mrefu, ulimlazimisha
Askofu Msongazila kuzungumzia siri hiyo,
akisema kuwa inatokana na kuishi maisha ya nidhamu ya kijeshi na kumtukuza
Mungu. Akiwa
ameketi kwenye kiti maalumu upande wa meza kuu, na zaidi akiwa ameambatana na
familia yake, akiwamo mkewe Maria, Jenerali Msuguri alishiriki kikamilifu ibada
hiyo iliyochukua saa kadhaa. Tukio
lililoibua gumzo na shangwe ni wakati kwaya ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Rwamkoma walipokuwa wakiimba ambapo Jenerali Msuguri aliwaomba wasaidizi wake
kumsaidia kwenda walipo wanakwaya hao na kujumuika nao huku akionekana kuwa na
bashasha. Jenerali Msuguri
ana historia ndefu na ya kipekee ndani na nje ya jeshi, akiwahi kushiriki vita
ya pili ya dunia. Lakini pia ndiye
aliyeongoza ushindi wa vita ya mwaka
1979 akiwa Mkuu wa Majeshi wa Tanzania kumwondoa Rais wa Uganda, Idd Amin Dada. Akizungumza
katika ibada ya maadhimisho ya Jenerali Msuguri kutimiza miaka 100, Askofu Msongazila
amewataka Watanzania kudumisha amani na utulivu, hasa katika kipindi hiki ambacho
nchi inaelekea katika Uchaguzi Mkuu. MAMBO
YANAYOPASWA KUZINGATIWA Askofu
Msongazila alisema yapo mambo ya muhimu ambayo Watanzania kwa umoja wao
wanatakiwa kuzingatia ili kuhakikisha kunakuwa na amani na utulivu kwa miaka
yote. Alitaja
mambo hayo kuwa ni pamoja na haki, kuheshimiana, kusikilizana, mazungumzo
pamoja na kuvumiliana. Aliongeza
kuwa Watanzania wanapaswa kuhakikisha kuwa wanakuwa na woga mbele za Mwenyezi
Mungu na maridhiano. Askofu
Msongazila alisema kuwa mambo yote haya yanapaswa kufanywa bila kujali umri, cheo,
wadhifa au nafasi ya mtu katika jamii. Alisema bila
mambo hayo kuzingatiwa, amani na usalama wa nchi vitakuwa hatarini jambo ambalo
asingependa litokee kutokana na misingi imara ya amani iliyojengwa na waasisi
wa taifa hili. KUWAENZI NA
KUWALINDA WAZEE Pia aliiomba
Serikali kuwaenzi na kuwalinda wazee wote nchini kwa kuwapa huduma bora
wanazostahili ili waweze kuishi vizuri. Alisema
wazee wametumikia nchi katika nafasi mbalimbali kijamii na kiserikali, hivyo ni
vema wakapewa heshima wanayostahili, ambayo ni ulinzi na kuenziwa na Serikali
ili nao waweze kuona umuhimu wao na mchango wao waliotoa katika jamii. VIWANGO BIMA
YA AFYA Askofu Msongazila
alisema katika suala la afya, Serikali inapaswa kuangalia upya viwango vya bima
ya afya kwa maelezo kuwa gharama ziko juu kiasi kwamba wazee hao hawawezi
kuzimudu. Akitolea
mfano viwango vya bima, alisema wazee wanatakiwa kulipia Sh 984,000 ili kuweza
kupata huduma ya afya kiasi alichokitaja kuwa ni kikubwa kutokana na wengi wao
kustaafu na watashindwa kumudu gharama hizo. Alisema
huduma ya afya ni miongoni mwa mambo muhimu kwa wazee, hivyo gharama inapokuwa
kubwa kwa namna moja ama nyingine wengi wao watashindwa kumudu kutokana na
ukweli kwamba hawana uwezo wa kuzalisha tena mali. AWAASA
VIJANA Aidha Askofu
Msongazila aliwaasa Watanzania hasa vijana kuwa na nidhamu ya maisha na kufanya
mazoezi mbalimbali pia kuzingatia utaratibu wa ulaji wao ili waweze kuwa na
maisha marefu zaidi. NDOA NA MKE
MMOJA KATI YA SITA Kuhusu
maisha ya kiimani ya Msuguri, Askofu Msongazila alisema takribani miaka mingi
iliyopita alianza mchakato wa kurudi kanisani kwa kuandika barua. Alisema
pamoja na barua, pia alikuwa na mazungumzo naye ambapo baadaye aliamua kufunga
ndoa na mke wake mmoja kati ya sita aliokuwa amewaoa kimila. KAULI YA
SERIKALI Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa
Mara, Adam Malima alisema Serikali inatambua mchango wa Jenerali Msuguri katika
maendeleo ya nchi kwa ujumla, hivyo busara zake zitaendelea kutumika miaka
yote. Alisema kuwa
kutokana na juhudi zake, Jenerali Msuguri aliwezesha Jeshi la Wananchi Tanzania
kuwa miongoni mwa majeshi bora na yenye kuheshimiwa duniani na kuwataka Watanzania
wengine kuiga mfano wake ili kutumikia nchi kwa moyo mmoja. Malima
alisema kuwa Jenerali Msuguri alijitolea maisha yake kuhakikisha ulinzi na usalama
wa nchi unakuwapo ambapo alifanikiwa kushinda kwenye vita ya Tanzania na Uganda
aliyoiongoza. ALICHOSEMA
JENERALI MSUGURI Akitoa
shukrani katika hafla hiyo, Jenerali Msuguri aliwashukuru wote waliohudhuria hafla
hiyo na kwamba yote yaliyozungumzwa na wasemaji ni ya kweli, huku akisisitiza
kuwa yumkini alifanya zaidi ya hayo. Alisema kuwa
baada ya kustaafu jeshini ambako alitumika kwa miaka 55 na miezi saba, aliamua
kurudi kijijini kwao Butiama ambako ndiko alikozaliwa na kwamba ndiko
atakapozikwa mara atakapofariki dunia. HUYU NDIYE
MSUGURI Taarifa fupi
ambazo zinapatikana katika mitandao, zinamwelezea Jenerali David Msuguri kwamba
alizaliwa Januari 4 mwaka 1920 huko Butiama mkoani Mara. Mwaka 1942 Msuguri
alijiunga katika vikosi vya jeshi la Mwingereza – King’s African Rifles (KAR)
na baadae alifanya nao kazi nchini Madagascar. Alianza kama
‘Private’ na mwaka 1957 utawala wa Uingereza ulianzisha cheo cha ‘effendi’
ndani ya KAR, walichopewa maofisa waandamizi wa kiafrika waliokuwa wakifanya
vizuri ambapo Msuguri naye alipewa cheo hicho. Desemba 1961,
Tanganyika ikawa nchi huru na vikosi vya KAR vilihamishiwa katika vikosi vipya
vya Jeshi la Tanganyika – Tanganyika Rifles. Cheo cha
‘effendi kiliachwa muda mfupi baadaye na mwaka 1962 Msuguri akapandishwa cheo
na kuwa Luteni. Wakati wa
maandamano ya Tanganyika Rifles ya Januari 1964, Msuguri alikuwa kituo cha
Tabora. Vikosi vya
waasi vilivyojaribu kuondoa na kuchukua nafasi ya maofisa wao wa Kiingereza,
walimtangaza Msuguri kuwa Meja. Jenerali Msuguri
alipanda vyeo na kufikia hadi kuwa katika nafasi ya Brigedia. Mwaka 1979
alipandishwa cheo na kuwa Meja Jenerali na kuongoza JWTZ, na kukusanya vikosi kuvamia
Uganda kufuatia kuzuka kwa Vita ya Uganda na Tanzania mwaka 1978. Mwaka 1980 Msuguri
aliteuliwa kuwa Mkuu wa JWTZ na Desemba 30 mwaka huo Rais wa Awamu ya Kwanza
Mwalimu Julius Nyerere alimpandisha cheo na akawa Luteni Jenerali. Februari 7,
1981 aliyekuwa Rais wa Uganda, Milton Obote alimpa Msuguri mikuki miwili kwa
heshima ya ushindi wa vita. Vita ambazo
amepigana ni pamoja na vita ya pili ya dunia – World War II (Battle of
Madagascar), Vita ya Kagera – Uganda – Tanzania War (Battle of Simba Hills,
Battle of Masaka, Battle of Lukaya). Alitangazwa
kustaafu Agosti 31, 1988 na baada ya hapo alihamia Butiama mkoani Mara aliko
hadi sasa. | 1kitaifa
|
['Huenda Manchester United ikasubiri ukaguzi wa mchezaji wa kiungo cha mbele raia wa Ufaransa Anthony Martial, mwenye umri wa miaka 23, kabla ya kuruhusu uhamisho wa mkopo wa mchezaji wa kimataifa wa Chile Alexis Sanchez, mwenye umri wa miaka 30, kwenda Inter Milan. (Guardian)', 'Paris St-Germain imeambia Real Madrid itatafakari kumuuza mchezaji wa Brazil wa kiungo cha mbele Neymar, mwenye umri wa miaka 27, iwapo mchezaji wa klabu hiyo ya Uhispania mwenye miaka 19 na mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr iatakuwa sehemu ya makubaliano ya kudumu. (AS)', 'Wakurugenzi wa Barcelona wamekutana Jumatatu kujadili ombi la mchezaji wao wa zamani Neymar. (Marca)', 'Huenda Inter Milan ikamgeukia mchezaji wa kiungo cha mbele wa Manchester City Wilfried Bony, mchezaji huyo wa Ivory Coast mwenye miaka 30 kwa sasa haichezei klabu yoyote baada ya kuachiwa na Swansea msimu wa joto. (Goal.com)', 'Mchezaji wa kimataifa wa Serbia Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, ameitisha mazungumzo na meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer baada ya kuipoteza nafasi yake ya kwanza huko Old Trafford. (Mirror)', 'Arsenal ipo tayari kumruhusu mchezaji wa kimataifa wa Uhispani Nacho Monreal kujiunga na Real Sociedad wiki hii iwapo mchezaji huyo wa miaka 33 na mchezaji wa kiungo cha ulinzi ataomba kuondoka. (Sun)', 'Javi Gracia anapigania kuokoa nafasi yake kama meneja wa Watford baada ya kuanza msimu wa ligi kuu England kwa kushindwa mara tatu. (Telegraph)', 'Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham anaelekea kupata mkataba mpya ambao huenda ukaongeza zaidi ya mara mbili malipo ya mchezaji huyo wa miaka 21 raia wa England ya £50,000 kwa wiki(Telegraph)', 'Wawakilishi wa Christian Eriksen hawatofikiria pendekezo la mkataba wa Tottenham la malipo ya £200,000 kwa wiki na mchezaji huyo wa miaka 27 ambaye mkataba wake hivi sasa unamalizika msimu ujao wa joto anatumai kupata uhamisho kwenda Uhispania. (Mirror)', 'Eriksen ni kama amejiuzulu kusalia Tottenham katika kipindi kifupii, huku ndoto yake ya kujiunga na Real Madrid au Barcelona msimu huu wa joto ikishindwa kufanikiwa. (Mail)', 'Winga wa Celta Vigo Pione Sisto, mwenye umri wa miaka 24, anakaribia kujiunga na Torino baada ya uhamisho kwenda Aston Villa kutofanikiwa. (Marca)', 'Mabingwa wa Italia Sampdoria wanataka kumsajili winga wa Swansea anayeichezea timu ya taifa ya Ghana Andre Ayew, mwenye umri wa miaka 29, kwa mkopo kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya (Star)', 'Mlinzi wa Manchester United Luke Shaw, mwenye miaka 24, huenda akawa nje kwa hadi mwezi mmoja kutokana na jeraha katika msuli wake wa paja. (Talksport)', 'Huenda Sunderland ikawasilisha ombi la pili kwa mlinzi wa Sheffield Morgan Fox, 25 hapo kesho Jumatano (Newcastle Chronicle)', 'Jurgen Klopp anaamini mbinu yake ya usimamizi inaongeza uwezekano wa yeye kwenda mapumzikoni wakati kipindi chake cha usimamizi kitakapomalizika Liverpool mwaka 2022. (Times)', 'Kevin De Bruyne ameunga mkono mchezaji wa zamani wa timu ya Manchester City , Vincent Kompany kuwanyamazisha wakosoaji na kufungua ufanisi wa nafasi yake mpya kama bosi wa Anderlecht, baada ya kujizolea pointimbili katika mechi nne za kwanza msimu huu. (Manchester Evening News)', 'TETESI ZA JUMATATU', 'Mchezaji wa kiungo cha kati wa Spurs na timu ya taifa ya Kenya Victor Wanyama amepewa mkataba wa miaka mitano kwa malipo ya £65,000- kwa wiki na Club Bruges wakati anapokaribia kukamilisha uhamisho. (Scottish Sun)', 'Kalbu ya Fiorentina katika ligi ya Serie A inajitayarisha kuwasilisha ombi kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United na timu ya taifa ya Brazil Fred, mwenye umri wa miaka 26. (Calciomercato)', 'Norwich itamfukuzia kipa wa Stoke na timu ya taifa ya England Jack Butland, mwenye umri wa miaka 26, ifikapo Januari na iwapo thamani yake itashuka. (Sun)', 'Bordeaux inataka kumchukua mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal na Misri Mohamed Elneny, mwenye umri wa miaka 27, kwenda Ligue 1 kwa mkopo. (Foot Mercato)', 'Leeds inatarajiwa kuanza mara moja mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha kati Kalvin Phillips kuhusu mkataba mpya. Mchezaji huyo wa miaka 23 anataka kulipwa £40,000 kwa wiki ili kuendelea kusalia Elland Road. (Football Insider)', 'Aliyekuwa beki kamili wa Chelsea Filipe Luis, mwenye umri wa miaka 34, amekataa ombi la Manchester City, Lyon na Borussia Dortmund msimu huu wa joto kabla ya kujiunga na Flamengo kutoka nchini anakotoka Brazil. (Globo Esporte)', 'Aliyekuwa beki wa kulia wa Leicester Danny Simpson, mwenye umri wa miaka 32, anafanya mazungumzo na klabu ya Ligue 1 - Amiens kuhusu uhamisho. (Sun)', 'Meneja wa Chelsea Frank Lampard amemkaribisha mchezaji wa kiungo cha kati wa Exeter Ben Chrisene kufanya mazoezi na klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 15 kutoka timu ya vijana wa timu ya taifa England alifanikiwa kucheza katika kikosi cha kwanza mwezi huu. (Sun)'] | 2michezo
|
SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) linakuja na Bima ya Kilimo, itakayosaidia kuunga mkono jitihada za serikali za kujenga uchumi wa viwanda.Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Sam Kamanga amesema kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa na ndicho kinachotoa malighafi nyingi za viwandani nchini, hivyo aina hiyo ya bima itasaidia kujenga uchumi wa viwanda.Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Maonesho ya 42 ya Sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa, amesema NIC inaunga mkono jitihada za serikali za ujenga uchumi wa viwanda na kwamba aina hiyo ya bima itakuwa pia mkombozi wa wakulima pale majanga yanapowafika.Amewataka Watanzania hususani wakulima, kuichangamkia aina hiyo ya bima kwani ina manufaa sana kwa wakulima na taifa kwa ujumla.Kamanga aliwataka Watanzania kutembelea banda lao ili waweze kupata elimu kuhusu aina ya bima wanazotoa na pia kujiunga na bima mbalimbali.Alisema shirika lake limeimarisha huduma yake ya bima ya magari kwa nchi za Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) ili kuondoa udanganyifu. Alisema huduma hiyo kwa sasa imewekwa katika mfumo wa kidijiti hali ambayo inazuia bima bandia.“Kwa sasa tuko kwenye kidijiti, hali ambayo inatuwezesha kuziba mianya yote ya udanganyifu,” amesema.Amefafanua kuwa, udanganyifu ulikuwa unaikosesha serikali mapato na kwamba shirika lake limeziba mianya yote ya upotevu wa mapato.Kamanga amesema, kwa sasa shirika lake linafanya kazi kisasa na liko kwenye ushindani na makampuni mengine ya bima.Amewatoa hofu wateja wake kuhusu ulipwaji wa fidia kwa muda muafaka na kwamba, NIC ya sasa inamjali mteja na hakuna ucheleweshaji wa malipo iwapo itathibitika madai ni ya kweli.“Tunalipa fidia kwa wakati ikithibitika madai ni ya kweli na hatuna njoo kesho….tunatoa huduma kisasa,” amesema. | 0uchumi
|
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kuidumisha hali ya amani na utulivu ambayo ndio msingi wa mafanikio yanayoendelea kupatikana hivi sasa na yatakayopatikana baadaye.Dk Shein aliyasema hayo juzi katika risala yake ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2019 aliyoitoa kupitia vyombo vya habari, Ikulu mjini Zanzibar. Alisema katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya mwaka 2018, mafanikio makubwa yamepatikana ambayo yamechangiwa na kuwepo kwa amani, mshikamano, umoja na mapenzi yaliopo.Aidha alisema hali hiyo ya amani imewavutia washirika wa maendeleo ambao wanaridhika na jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na hivyo kuiunga mkono katika mipango yake ya maendeleo. “Tukiwa tunaukaribisha Mwaka Mpya wa 2019, nachukua fursa hii kwa niaba ya wananchi wote wa Zanzibar kuwashukuru kwa dhati washirika wetu wa maendeleo kwa kuendelea kutuunga mkono, tunathamini mikopo, misaada na ushauri tulioupata kutoka kwao,” alisema Dk Shein. | 1kitaifa
|
STOCKHOLM, SWEDEN SERIKALI ya Sweden
imemrudisha nyumbani balozi wake nchini China kuhusiana na kuhusika kwake
katika mkutano wenye utata uliohusisha binti wa muuza vitabu mwenye asili ya
mataifa hayo mawili, ambaye anashikiliwa na China. Balozi Anna
Lindstedt, aliondoka Beijing juzi, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Sweden
alisema. Tukio lilianza
kwa Angela Gui, ambaye baba yake, Gui Minhai anaaminika kutekwa na makachero wa
China mwaka 2015, kuandika kwenye mtandao wa jamii kuhusu mkutano huo na
Lindstedt. Gui alikuwa mmoja
wa wauza vitabu watano wa Hong Kong waliokamatwa. Vitabu wanavyouza vimekuwa
vikiikosoa vikali China. Gui, ambaye
alisomea shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Cambridge Uingereza, amekuwa akiendesha kampeni mitandaoni
ya kutaka kuachiwa kwa baba yake. Mwezi uliopita, Lindstedt
alikaribishwa katika mkutano na kundi la wafanyabiashara wa China waliodai kuwa
na ukaribu na Chama cha Kikomunisti cha China. Gui alisema watu
hao walimshinikiza akubali kuingia makubaliano ambayo yatamfanya aache kuzungumza hadharani
kuhusu kesi ya baba yake na kumuahidi angetumikia kifungo cha miaka mitano na kuachiwa. Wizara ya Mambo
ya Nje ya Sweden ilisema haikupewa taarifa za kuwapo mkutano huo uliohudhuriwa
na Lindstedt, ambaye kwa sasa anakabiliwa na uchunguzi wa ndani. Kwa mujibu wa Gui,
Lindstedt aliwasiliana naye na kusema kuna mbinu mpya kuhusu kesi ya baba yake
na kumtaka ahudhurie mkutano na wafanyabiashara hao mjini Stockholm,” Gui aliandika
mtandaoni. Akapanda ndege
kuelekea Stockholm na kufikia katika hoteli waliyopanga kukutana, ambako alipelekwa
kwenye ukumbi alikoonana na watu hao. “Kulikuwa na
vinywaji vingi vya kulevya na maswali mengi ya ajabu ajabu,” Gui aliandika. “Lakini kwa
sababu Balozi Lindstedt alikuwapo na alionekana kuridhika na kila kinachoendelea,
nikadhani ni mkutano ulioandaliwa na wizara ya mambo ya nje ya Sweden.” Anasema mmoja wa
wafanyabiashara alimpa ofa ya kufikia makubaliano ambayo baba yake angeenda mahakamani na
kufungwa jela miaka michache ili binti aache kuandika hadharani kuhusu
kushikiliwa kwa baba yake. Kwa mujibu ya
maelezo ya Gui, Lindstedt alionekana kuunga mkono mpango huo, akimwambia kuwa China
inaanzisha mpango mpya wa diplomasia na
iwapo ataendelea kutoa matamko mitandaoni China inaweza kuiadhibu Sweden. | 3kimataifa
|
KAMPUNI ya Kuhifadhi Mafuta ya Tanzania (Tiper) imesema gawio la Sh bilioni sita iliyotoa kwa wanahisa wake, ambao ni serikali na Kampuni ya ADDAX-ORYX GROUP ya Uswisi, ni ongezeko kutoka kiwango cha Sh bilioni moja iliyotoa katika miaka ya mwisho ya 2000.Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi hisa kwa serikali ambayo ilipewa Sh bilioni tatu, Mwenyekiti wa bodi wa kampuni hiyo, Profesa Abdulkarim Mruma amesema, kiasi hicho ni ongezeko la wastani wa karibu Sh bilioni mbili katika kipindi cha kati ya mwaka 2010 hadi 2013.“Uongozi wa kampuni unaona fahari kubwa kuweza kusimamia uendeshaji na kuweza kukuza gawio kwa wanahisa wake,’’ amesema.Akizungumzia mpango wa upokeaji wa mafuta kwenye ghala moja, ambapo kampuni hiyo inatarajia kuwa kituo pekee cha upokeaji wa mafuta yote yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam, Prof Mruma amesema manufaa yanayotarajiwa kupatikana kutokana na mpango huo yameshajadiliwa na kupokewa vyema na wadau wote.“ Faida za mpango huu zipo wazi ambazo ni pamoja na udhibiti bora wa kiwango cha mafuta kinachoingia nchini, kupunguza upotevu na wizi wa mafuta, kuzifanya gharama za ucheleweshaji wa meli zinazolipwa sasa kwa wamiliki wa nje wa meli kuwa mapato ya serikali.’’Amesema ili kufanikisha mradi huu, Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER imepitisha mpango mahususi wa uwekezaji wa zaidi ya dola za Marekani milioni ishirini na mbili ndani ya kipindi cha 2018 mpaka 2019.“Tumeazimia kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta kwa asilimia 50 kutoka mita za ujazo 213,000 mpaka meta za ujazo 319,000 kwa kujenga matangi mawili mapya yenye mita za ujazo 80,000 kila moja na kukarabati tangi moja lililokuwa la mafuta ghafi lenye ujazo wa mita za ujazo 46,000.’’Ametaja azimio lingine kuwa ni kutandika bomba la pili la mafuta ya petroli kati ya Kurasini na Kigamboni, kuongeza uwezo wa kusukuma mafuta kwa zaidi ya asilimia 50 kwa kujenga kituo kipya cha kusukumia mafuta ambacho kitakuwa na mashine sita mpya na kukarabati mfumo wa kuzima moto ili kuweza kuongeza kiwango na kufikia viwango vinavyokubaliwa kimataifa ili kuhakikisha mafuta yako salama ndani ya ghala la TIPER.“Mpango huu wa upanuzi wa ghala unafanikishwa kwa fedha inayotokana na mapato ya ndani pamoja na mkopo wa dola milioni 15 kutoka benki,’’ ametaja.Amesema mafanikio ya mradi huo, yatakuwa ni chanzo cha kushughulikia miradi mingine kama Ghala Maalumu la Forodha, ambalo litavutia mafuta mengi kuingia nchini ili kuboresha nguvu ya ushindani na kuifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa bandari, mkakati itakayovutia uingizaji wa kiwango kikubwa cha mafuta kwa ajili ya biashara ya nchi jirani katika ukanda huu. | 0uchumi
|
Na SAMWEL MWANGA
SERIKALI Wilaya ya Maswa imewaonya wamiliki wa pikipiki zinazosafirisha abiria maarufu kwa jina la bodaboda kuhakikisha madereva wanaowakabidhi pikipiki hizo ni wale waliopata mafunzo ya usalama barabarani.
Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dk. Seif Shekalaghe alipofunga mafunzo ya usalama barabarani yaliyoandaliwa na uongozi wa wilaya kwa waendesha pikipiki za kubeba abiria mjini Maswa.
Aliwataka madereva hao kuheshimu kazi hiyo kwa kuwa inawapatia kipato hivyo kuzingatia sheria za usalama barabarani na siyo vinginevyo.
DC alisema wamiliki wake wanapaswa kutambua kuwa hiyo ni fursa ya uchumi hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanawakabidhi pikipiki watu wenye ujuzi.
“Wamiliki wa bodaboda mnawekeza fedha nyingi katika kununua bodaboda lakini wengi wenu mnawakabidhi madereva ambao hawana mafunzo na wanakuwa chanzo cha ajali za barabarani.
“Hakikisheni wamepewa mafunzo na ambao hawana wasaideni wapate kuepuka kupoteza pikipiki zenu na nguvu kazi ya taifa kwa ajali ambazo siyo za lazima,”alisema.
Alisema lengo la wilaya hiyo kuandaa mafunzo hayo ni kuwafanya waendesha pikipiki hizo wawe salama pamoja na kujali usalama wa watumiaji wengine wa barabara na kuepusha ajali zisizokuwa za lazima na kupata leseni za udereva.
Pia aliwataka madereva hao kuunda vikundi vyao kwa kuwa na Chama cha Bodaboda wilayani humo serikali iweze kuwasaidia kwa kuwapatia mikopo waweze kwa siku za baadaye kumiliki pikipiki zao binafsi na hata bajaj na Hiace.
“Undeni vikundi ambavyo mtavisajili na serikali itawasaidia kupata mikopo muweze kujitegemea maana waendesha bodaboda mlio wengi hizo pikipiki mnazofanyia kazi ya kubeba abiria si zenu.
“Hivyo ni vizuri kila mmoja akawa anamiliki pikipiki yake hata ikibidi muweze kumiliki bajaji na hata Hiace,”alisema.
Mkuu wa Usalama Barabara Wilaya ya Maswa, Bwire Essore alisema ajali nyingi zinazotokea barabara na kusababisha watu wengi kufariki dunia na kupata vilema.
Alisema nyingi zinasababishwa na waendesha bodaboda wengi ambao hawana mafunzo ya usalama barabarani. | 1kitaifa
|
NA CHRISTOPHER MSEKENA MWIMBAJI wa nyimbo za Injili, Ussy Charugamba, amesema katika wakongwe kwenye tasnia hiyo, anamkubali zaidi Rose Mhando kwa kuwa amewaonyesha njia waimbaji wengi. Bosi huyo wa Ussy Production, ameliambia MTANZANIA kuwa anajiona mwenye bahati kufanya kazi na Rose Mhando kwa kumshirikisha kwenye wimbo wake unaoitwa ‘Wema’ ambao utakuwa kwenye albamu yake ya sita. “Rose Mhando ana mchango mkubwa kwenye tasnia hii, amefungua milango kwa waimbaji wengi kufanya hiki wanachokifanya sasa, binafsi najiona mwenye bahati na ninajivunia kufanya kazi na mkongwe huyu, naomba tumpe heshima yake,” alisema Charugamba. | 4burudani
|
MBUNGE wa Makambako, Deo Sanga maarufu Jah People (CCM), ameshauri Rais John Magufuli kuongezewa kipindi kimoja cha uongozi ambacho badala ya kumaliza urais mwaka 2025, akae hadi mwaka 2030.“Rais wetu (Magufuli) ana maono makubwa ya kuifikisha mbali nchi yetu, hivyo aombewe awe rais wa kudumu, aongezewe kipindi kimoja hadi mwaka 2030, “Mimi na wenzangu tutatembea nchi nzima kumuombea…ikifika mwaka 2021 wabunge tuanze kutembea nchi nzima kumuombea Rais Magufuli aongezewe muda,” alisema Sanga.Mbunge huyo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, alitoa maoni yake hayo wakati akichangia Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2019/2020 yaliyowasilishwa juzi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.Naye Mbunge wa Kijitoupele, Shamsi Vuai Nahodha (CCM) alisema Rais Magufuli ana maono ya kulipeleka Taifa mbali zaidi na kuachana na kupitisha bakuli kwa wafadhili kuombaomba, hivyo kuwataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili Taifa lijitosheleze. Kwa upande wake, Mbunge wa Kilombero, Peter Lijuakali (Chadema)alisema “Inasikitisha wabunge wana mawazo ya kutaka Katiba ifanyiwe marekebisho makubwa ili rais aongezewe muda…inafedhehesha sana.”Hata hivyo, Rais Magufuli mara kadhaa ameshasema hana mpango wa kuongeza muda wa uongozi na ikifika muda wake wa kuachia madaraka, atafanya hivo tarehe hiyohiyo anayotakiwa kufanya hivyo. Mbunge wa Moshi Mjini, Jaffar Michael (Chadema) alitaka wafanyabiashara wa masoko kutopewa vitambulisho vya ujasiriamali kwani kumesababisha halmashauri kukosa mapato na kushindwa hata kulipia gharama za kusafisha masoko hayo.Mbunge wa Kuteuliwa, Abdallah Bulembo (CCM), alitaka Wizara ya Madini na Tume ya Madini kuwasimamia watendaji wao wanaowanyima leseni wachimbaji madini walio safi, wasio na matatizo na wanaotaka kulipa kodi. Mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Jaku Hashim Ayoub (CCM) aliitaka serikali kuwapeleka Zanzibar viongozi mashuhuri wanaotoka nje ya nchi wanaotembelea Tanzania. | 1kitaifa
|
Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ambapo mshindi mbali na kutwaa taji hilo, pia atapata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Afrika. Pia mshindi huyo atakabidhiwa kitita cha Sh milioni 50.Homa na presha kwa mashabiki na viongozi mbalimbali wa timu hizo imekuwa kubwa na wengi wao tayari wametoa ahadi mbalimbali kwa lengo la kuwapa hamasa wapambanaji wao kuweza kushinda mchezo huo na kupaa nafasi hiyo ya kuungana na Yanga ili kubeba bendera ya taifa kwenye michuano ya kimataifa.AHADI KWA WACHEZAJI Wabunge mbalimbali ambao ni mashabiki wa timu ya Simba wametoa ahadi ya Sh milioni 20 endapo timu yao itaifunga Mbao na kutwaa taji hilo kama ambavyo wamekusudia.Mbali na wabunge nao, viongozi wa timu hiyo wameahidi kutoa asilimia kubwa ya fedha za zawadi kwa wachezaji wao endapo watafanikiwa kutwaa taji hilo na kupata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.Simba ndiyo wenyeji katika mchezo huo wa leo na tayari wamewasili Dodoma tangu juzi saa 12 za jioni wakitokea Morogoro, ambako waliweka kambi ya muda kujiandaa na mchezo huo pekee kwao katika kurudi kwenye michuano ya kimataifa baada ya kuikosa kwa muda mrefu.Kocha wa Simba amesema huo ni mchezo muhimu kwao na ni lazima wacheze kwa nguvu ili kuhakikisha wanapata ushindi utakaowafanya kutimiza kile walichokikusudia ambacho ni kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.Mcameroon huyo alisema anatambua kuwa mchezo utakuwa mgumu, lakini wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi kwa sababu wamewasoma vya kutosha wapinzani wao na hakuna shaka kwamba mambo yatakuwa mazuri.“Mbao ni timu nzuri lakini katika mchezo wa kesho (leo) watatusamahe kwani tumejipanga vizuri kuhakikisha tunashinda na kuirudisha hadhi ya Simba, lengo ni kushiriki michuano ya kimataifa na ni lazima litimie,” alisema Omog.Kocha huyo alisema kikosi chake hakina mchezaji majeruhi, hivyo anaamini mipango yake itakwenda sawa na kumaliza mchezo huo mapema ili kutwaa taji hilo ambalo msimu uliopita walilikosa baada ya kutolewa hatua ya robo fainali na Coastal Union.Mbao, timu ambayo inapewa sapoti kubwa na mashabiki wa Yanga ndiyo ya kwanza kuwasili Dodoma siku nne na kufanya mazoezi ya kutosha kwenye uwanja wa Jumhuri. Timu hiyo inayofundishwa na kocha Etienne Ndyariagije, imekuwa na matumaini makubwa ya kufanya maajabu mengine leo kwa kuifunga Simba na kutwaa taji hilo.Kuelekea mchezo huo nao kama ilivyo kwa Simba tayari wamepoka ahadi mbalimbali kutoka kwa viongozi na wakazi wa Mwanza kuwa endapo watashinda. Mmoja anayeongoza kampeni za Mbao ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela ameahidi kuwapa basi kubwa la kusafiria timu hiyo endapo wataifunga Simba na kutwaa ubingwa wa Kombe la FA.Pia kiongozi huyo alisema wakazi wa Mwanza wamechanga kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili yao hivyo wanapaswa kucheza kwa nguvu ili kuhakikisha wanatwaa taji hilo. “Mnatakiwa kucheza kwa nguvu na kuipigania timu yenu msiogope majina nyie na wachezaji wa Simba hamna tofauti tena pengine nyie mna uwezo mkubwa sema hamjapata bahati ya kusajiliwa huko ila hiyo ndiyo nafasi pekee kujitangaza,” alisema Mongela.Kocha wa Mbao alisema mchezo wa fainali utakuwa mzuri na wamejipanga kumaliza shughuli hiyo mapema kutokana na maandalizi waliyofanya kuelekea mchezo huo. Kocha huyo alisema pamoja na kwamba atamkosa mshambuliaji wake tegemezi Bernad Mujweaki anayesumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, ana imani na washambuliaji waliopo fiti kuelekea mpambano huo wa leo.“Tunaiheshimu Simba ni timu kubwa ukilinganisha na sisi Mbao, wanatuudhi kwa mambo mengi hata wachezaji wangu wengi hapa wanatamani kuichezea timu hiyo, lakini tumejipanga lengo letu likiwa ni ushindi ili kuhitimisha kazi tuliyoianza huko nyuma,” alisema Ndyariagije.Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 10 za jioni hapa Dodoma na endapo hadi dakika 90 mshindi atakuwa hajapatikana mchezo huo utaongezwa dakika 30 na kama pia hakutakuwa na timu iliyopata ushindi utaamuliwa na mikwaju ya penati. Wachezaji | 2michezo
|
BRUSSELS, UBELGIJI
VIONGOZI wa Ulaya wametangaza wataendelea kuunga mkono makubaliano ya nyuklia ya Iran muda mfupi baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutangaza kujitoa kutoka mkataba huo.
Wakati Umoja wa Mataifa (UN), Ulaya, Iran, Urusi na China zikiishangaa Marekani, Israel na Saudi Arabia zimeshangilia uamuzi wake huo. Licha ya uamuzi wa Trump, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeapa kufanya kazi pamoja na mataifa yote yaliyosalia katika mkataba huo huku zikiitaka Marekani kutovuruga utekelezwaji wake. Mataifa mengine yaliyosaini mkataba huo wa 2015 ni Urusi na China, ambazo zimesema pia zitaendelea kuyaunga mkono kutokana na manufaa yake kwa dunia. Juzi Rais wa Iran, Hassan Rouhani alisema watashirikiana na mataifa ya Ulaya ,China na Urusi kunusuru makubaliano hayo bila uwapo wa Marekani. Aidha jana, Kiongozi wa Kiroho wa Iran, Ayatollah Ali Khamanei aliilaani Marekani kwa uamuzi wake huo huku wabunge wa Iran wakichoma moto bendera ya Marekani kwa uamuzi wake huo. Bila kufafanua Ayatollah Ali Khamenei alimtuhumu Rais Trump kwa uongo na kuonya nchi yake haipaswi pia kuziamini Uingereza, Ufaransa na Ujerumani. Makubaliano hayo ya 2015 yaliizuia Iran kuendelea na mpango wake wa nyuklia huku UN ukikubali kuiondolea vikwazo vilivyowekwa pamoja na, Marekani na Ulaya.
Katika taarifa yake kwenye runinga juzi, Rais Trump alisema Marekani inajiondoa katika mkakati huo wa pamoja (JCPOA). Aliutaja kuwa mkataba mbaya unaopendelea upande mmoja na ambao haungeweza kufikiwa.
Mbali na kutaka kuilinda Marekani na washirika wake, alisema mkataba huo umeweka masharti hafifu kuhusu mipango ya nyuklia ya Iran na kwamba haikuwekewa vikwazo vyovyote kuhusu nyendo zake ikiwamo nchini Syria, Yemen na kwingineko.
Rais huyo aliongezea kuwa makubaliano hayo hayakuangazia utengezaji wa silaha za masafa marefu za Iran.
Amesema kuwa atarudisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo ambavyo vilikuwa wakati makubaliano hayo yalipotiwa saini mwaka 2015. Wizara ya Fedha Marekani imesema vikwazo vya kiuchumi havitawekwa dhidi ya Iran mara moja bali baada ya kipindi cha kati ya miezi mitatu na sita ijayo. Mshauri wa masuala ya usalama wa Taifa nchini Marekani John Bolton ameripotiwa akionya mataifa ya Ulaya yanayofanya biashara na Iran yatalazimika kuisitisha katika kipindi cha miezi sita la sivyo ziwekewe vikwazo na Marekani. Aliyekuwa Rais wa Marekani Barrack Obama ambaye alichukua jukumu kubwa katika makubaliano hayo alisema katika mtandao wa Facebook kuwa makubaliano hayo yanalinda maslahi ya Wamarekani. ”Kujiondoa katika makubaliano hayo ya pamoja kunaiweka Marekani katika hali mbaya na washirika wake wa karibu katika makubaliano ambayo wajumbe wakuu wa taifa letu, wanasayansi na wapelelezi wetu walijadiliana na kuafikia”, alisema. Lakini Saudi Arabia ambayo ni hasmu mkuu wa Iran pamoja na Israel kupitia Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu zimeeleza kuunga mkono hatua ya Trump kujiondoa kutoka katika mkataba huo walioutaja janga. | 3kimataifa
|
Na FESTO POLEA-DAR ES SALAAM KATI ya redio zaidi ya 100 na runinga zaidi ya 20 zilizopo nchini, ni vituo vitatu tu vikiwamo vya Mlimani tv, Azam tv na Joy Fm ya Kigoma ndivyo vilivyolipa mirabaha kwa kutumia kazi za wasanii nchini. Mkaguzi wa Hakimiliki kutoka Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota), Paul Mabula, alisema kutokana na kukumbwa na changamoto nyingi ikiwamo kufukuzwa na baadhi ya wamiliki wanapokwenda kuwataka walipe mirabaha hiyo, wamelazimika kuwaandikia TCRA ili wajue cha kufanya zaidi. “Tumeiandikia TCRA ili itusaidie katika changamoto tunazokumbana nazo wakati wa kudai mirabaha kwenye vituo vya redio na runinga, baa na maeneo mengine mengi,” alisema Mabula. Mabula aliongeza kwamba Cosota inakabiliwa na idadi ndogo ya maofisa ambapo kwa sasa ina maofisa sita na inawawia vigumu katika mapambano ya kazi za ukusanyaji wa fedha za mirabaha inayofanyika nchi nzima. “Vipo vituo vilivyotaka tuvipeleke wanavyodaiwa lakini licha ya kufanya hivyo, hakuna vituo vilivyolipa zaidi ya hivyo vitatu,” alieleza Mabula jana kwenye ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Ilala jijini hapa. Hata hivyo, licha ya kusikitishwa na hali hiyo, baadhi ya wasanii na viongozi wa mabaraza ya wasanii nchini wameitaka Cosota kushirikisha mabaraza ya wasanii ili watoe watu wao wasaidie shughuli za ukusanyaji mirabaha kwa ajili ya manufaa ya kazi zao. | 4burudani
|
NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM WAAMUZI kutoka nchini Somalia wamepangwa kuchezesha mechi ya hatua ya awali ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kati ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na Malawi ‘The Flames’ utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam keshokutwa. Mtandao wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuhusu mchezo huo namba 13 kanda ya Afrika, umeonyesha kuwa mwamuzi wa kati atakayepuliza kipenga atakuwa ni Haji Wiish. Mwamuzi msaidizi namba moja anatarajia kuwa ni Hamza Abdi, mikoba ya msaidizi namba mbili itashikwa na Salah Omar, huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Bashir Olad. Tayari kikosi cha Stars kimeshaanza maandalizi ya mchezo huo tokea Ijumaa iliyopita chini ya Kocha Mkuu Charles Mkwasa, Msaidizi wake, Hemed Morocco na Kocha wa Makipa, Peter Manyika. Kuhusu ujio wa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa, aliliambia MTANZANIA jana kuwa wote watawasili leo. “Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), wao wanamalizia mechi yao leo (jana) ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kesho (leo) watatua nchini hata Mrisho Ngassa naye tunamtarajia kesho (leo),” alisema. Wakati huo huo, timu ya Malawi imewasili jana asubuhi nchini ikiwa na msafara wa watu 26 wakiwemo wachezaji 20 wa kikosi hicho wakiwa tayari kabisa kuivaa Stars. Mchezo wa marudiano utafanyika Malawi kwenye Uwanja wa Kamuzu Jumapili hii na bingwa wa jumla atafuzu kwa raundi wa pili kwa kumenyana na Algeria kabla ya kutinga hatua ya makundi. | 2michezo
|
UUNGANISHAJI maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) kwa mkopo umeshika kasi katika maeneo mbalimbali huku mamlaka ikisema inakwenda hatua kwa hatua na wakazi wote jijini watapata maji.Akizungumza hivi karibuni katika kipindi cha ‘Tunatekeleza’ kinachorushwa na chaneli ya TBC One ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kila Alhamisi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Cyprian Luhemeja ameifafanua utaratibu unaopaswa kufuatwa ili kupata maji hayo ya mkopo.Akijibu maswali ya mtangazaji ikiwamo la kutaka kufahamu utaratibu unaopaswa kufuatwa na watu walio mbali na umbali ulioidhinishwa kuunganisha wateja chini ya mradi kuepuka vishoka, Luhemeja alisema mwananchi anatakiwa kuwa na fomu ya utambuzi kutoka serikali ya mtaa.Amesema mwananchi akifika ofisi za Dawasa anapaswa kupewa mkaguzi wa eneo lake na umbali unaoruhusiwa ni meta 50 kutoka kwenye bomba na kuongeza kuwa kama mteja yuko umbali zaidi ya hapo, inabidi wapeleke bomba la inchi mbili au tatu ili kuingiza wateja wengine.Akizungumzia hatua za kupata mkopo, alisema wakishafanya ukaguzi na kila mmoja akapata gharama ya kuunganishiwa maji, huduma ikipatikana wanaandikishiana mkataba unaomwezesha kulipa kwa awamu kwa miezi sita mpaka miezi 12.Akizungumzia maeneo yenye mabomba yasiyotoa maji na yale yasiyo na mabomba, Luhemeja alisema mradi huo wa usambazaji maji haujafikia asilimia 60. Ofisa mtendaji huyo alisisitiza kuwa wananchi hawahitaji kupata huduma kupitia watu wa kati ambao katika miaka takribani minne iliyopita, walikuwa wakitapeli.Kwa mujibu wa Luhemeja, gharama ya kulipa maunganisho ya kwanza ni kati ya Sh 200,000 na Sh 350,000 kulingana na umbali jambo ambalo ilikuwa mzigo kwa baadhi ya watu kulipa kwa mkupuo.Chini ya utaratibu huo wa kukopesha wateja, Dawasa imetekeleza kwa vitendo agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa alilotoa Novemba mwaka jana wakati akizindua mradi wa maji wa Kiwalani.Alitaka Dawasa kuhakikisha inaunganisha wananchi wa eneo hilo maji kwa mkataba walipe kidogo kidogo kwani malengo ya serikali ni kuona watanzania wanapata maji kwa asilimia 90.Katika hatua nyingine, Luhemeja alizungumzia kuhusu mita za maji za kabla ya matumizi kama zinazotumiwa na Shirika la Umeme (Tanesco) na kusema majaribio kwa wateja wakubwa 11 yamekamilika na mwaka ujao wa fedha zitaandaliwa mita 1,000.Baada ya muda watapeleka huduma hiyo majumbani. Akizungumzia wanaolimbikiza madeni, ofisa huyo mtendaji alisema wateja wa Dar es Salaam sasa wako vizuri katika kulipia ankara zao.Kwa mwezi, Dawasa ina wastani wa ankara kati ya Sh bilioni 11 mpaka 12 na inakusanya takribani Sh bilioni 11.2 sawa na asilimia 90.Amesema hivi karibuni walizindua kampeni ya ‘Tunawahitaji’ kwa ajili ya wananchi waliokatiwa maji kwa muda mrefu na hawana uwezo wa kulipa. Wamewaita na kuingia nao mkataba hivyo wakilipa ankara za sasa, wanalipia na asilimia ndogo ya zamani.Amesema wakilipa miezi sita na Dawasa ikaridhia, itafuta madeni yaliyobaki na kusisitiza kuwa huduma ya maji haipaswi kuwa vita, hivyo ni lazima iwe rafiki kwa sababu ni huduma ya watu. | 1kitaifa
|
Shabalala aliumia juzi usiku nyama za paja katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya URA ambapo Simba ilishinda bao 1-0.Katika mchezo huo mchezaji huyo aliumia dakika ya 64 na anatarajiwa kuwa nje kwa takribani wiki sita. “Tshabalala ameumia na atakuwa nje karibu wiki sita, kwa kweli kutanigharimu,” alisema.Aidha kocha huyo alisema amefurahishwa na kiwango kikubwa kilichooneshwa na wachezaji wake licha ya kupoteza nafasi nyingi.Alisema aliamua kutumia kikosi anachokitumia kwenye Ligi Kuu baada ya kuona wachezaji ambao hawapati nafasi walimuangusha alipowapanga kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Jamhuri.Aliwataka wachezaji anaowapa nafasi kwenye michuano hiyo kuitumia kwa kucheza vizuri wamshawishi kuwapanga kwenye michezo mingine. | 2michezo
|
NIMEKUWA nikikagua kwa umakini sana video za wasanii mbalimbali hususan wa Bongo Fleva katika ubora wake ili kujiridhisha kama bajeti za kushutia wanazozitaja zinalingana na ukweli halisi kwa kuzingatia mambo mbalimbali ya kiweledi. Kwenye kwaliti sio inshu lakini kwenye uhalisia ndiyo inshu na kichupa kikibamba na kuwa poa kwa levo inakuwa njema, kinapagawisha na kila mida unataka kukikagua manake hakikuchoshi. Nimegundua kitu katika video za Diamond Platnumz tangu alipoanza kitambo chake (back) hadi kufikia levo yake ya sasa (front), mabadiliko ni makubwa katika kutendea haki vichupa vyake kwa jinsi anavyoshuti manake tangu mida ile ya ‘Kamwambie’ kisha kupitia ‘Mbagala’ na baadaye ‘My Number One’ hadi kudondokea kwenye ‘Utanipenda?’. Si tu katika ubora unaoridhisha lakini kikubwa ni simulizi kueleweka hata kama utapima kwa vigezo vya kiweledi zaidi, kimojawapo ni kukicheki kichupa kimya kimya na kama ‘scenes’ zinaleta stori inayoeleweka basi hiyo ni mukide kabisa. Lakini engo nyingine ni hisia na kuigiza matukio ambapo Platnumz wa zamani na wa sasa kadiri anavyoendelea ni tofauti, kama ulivyomuona katika ‘Utanipenda’ alivyoigiza ukachala hata zile ‘gesture’ yaani hisia za usoni zinajiakisi inavyopaswa. Kwa levo hiyo ya uwezo wa kukubalisha simulizi kwenye kichupa kwa kujikita vyema kuigiza matukio yanayohusika safari yako Diamond uliyoianzia ‘Mbagala’ haipaswi kuishia kwenye vichupa tu, kwa nini usiende matawi mengine ukaigiza muvi kabisa wewe kama wewe kwa stori ya kivyako na songi zako zikawa soundtraki za kusindikizia matukio ya hiyo muvi!? Kule mbele kwa wenzetu waliotutangulia ni kawaida kabisa msanii wa mikong’osio kujikita kwenye muvi manake muvi nazo bila nyimbo haziendi kwani zitaboa, basi kama ni hivyo hata hapa kwetu inawezekana sio kwa kushirikishwa vipande flani tu lakini kuwa muvi kamili ya kwako mwenyewe msanii husika. Manake iko hivi kwako Almasi a.k.a Diamond kwa Kitasha, kama ni mshale ulioibuka zama zile (back) ukakitwa lakini hadi sasa bado unapaa kwenye levo nyingine (front) basi mshale upae zaidi, kwa kuchupa kwenye kiwango kingine itadhihirisha kuwa ulipofikia sio mwisho wa vidato unavyopaswa kukwea. Inapendeza kukwea levo kwenye nyanja mbadala manake umethibitisha mauwezo yako kwa kuwapiga tafu wengine kupitia WCB hadi wale wa levo yako wasiomaindi watu kuchonga wametinga kwenye lebo yako akiwemo Rich Mavoko. Sasa kama ni hivyo basi songa huku kwenye levo mbadala ushushe muvi moja au mbili inatosha manake vichupa vyako vinajieleza, kwamba ukiongozwa na muongozaji mwenye uwezo kama ilivyo kwenye vichupa basi haina shaka kuwa itakuwa poa na kitu kitakachoibuka kitakuwa mwake mwake kabisa babake mwenyewe. Inawezekana ni kujipanga tu kukamilisha inshu hiyo ambayo inakuchagiza uitimize kisha kila kitu kitakuwa levo nyingine mpya manake hiyo ndiyo ‘front’ unayopaswa kuifikia kutokea ‘back’ uliyotoka kitambo kile. Kwa sasa tatizo sio Mbagala na umehama Tandale ukiishi Madale na bila shaka watu wako watakupenda zaidi ukitia maguu kwenye Bongo Muvi. | 4burudani
|
Kadhalika, serikali imetakiwa kudhibiti matumizi ya dola nchini, hatua ambayo itasaidia kuimarisha thamani ya Shilingi ambayo kushuka kwake kunasababisha bidhaa zinazoingia nchini kupanda bei.Akichangia Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/16, Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola, alisema kuachwa kwa nchi yetu kuwa kama dampo la bidhaa za nje ambazo zingeweza kuzalishwa hapa nchini ni sababu mojawapo ya thamani ya Shilingi ya Tanzania kuyumba.“Leo hii (jana), Dola moja ya Marekani imefikia Sh 2,075… Hii ni kwa sababu tunasaka sana dola ili kuleta nchini bidhaa ambazo tunaweza kuzizalisha hapa nchini,” alisema akielekeza lawama kwa Wizara ya Viwanda na biashara kwa kushindwa kuhakikisha viwanda vinachanua nchini kama ilivyokuwa miaka ya 1970.Katika kuthibitisha maneno yake, Lugola alikuja na fuko la bidhaa, nyingi zikiwa zimetoka Kenya na China ambazo alizimwaga juu ya meza yake na kuzionesha moja baada ya nyingine.“Hili ni dodoki kutoka China, lingeweza kuzalishwa Tanzania, hii ni pamba ya masikioni, hiki ni kiberiti toka Kenya,” alisema akiendelea kutaja na kuonesha bidhaa zingine kama njiti za kutolea nyama kwenye meno, pipi, rula, penseli na kadhalika.Naye Mbunge wa Igunga, Dk Dalally Kafumu, alisema kupungua kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani pia kunachangiwa na matumizi yasiyodhibitiwa vyema ya dola.“Ukienda kwa nchi za wenzetu hawakuruhusu kununua bidhaa kwa dola. Ukitoa dola wanakuambia kachenji pale kwa sababu wanajua kwa kutumia dola holela ni rahisi pia kuzitorosha nje ya nchi yao,” alisema.Dk Kafumu alisema tatizo lingine lililochangia kuanguka kwa thamani ya pesa yetu ni kufungwa kwa migodi miwili ya dhahabu huku kukiwa hakuna mpango wa kuifungua upya au kufungua mingine zaidi.“Migodi miwili imefungwa kwa sababu wakati mwingine tunawasema vibaya wawekezaji,” alisema na kuongeza kwamba kwa tabia hiyo wawekezaji wengi wa madini watatukimbia. | 0uchumi
|
KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameandika barua kwenda kwa Wenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akiwataka wasaidie kuzuia chama hicho kisifutiwe usajili wa kudumu, ikiwezekana kwa kuzungumza na Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli.Alisema hayo mjini Kigoma katika mkutano wa pamoja wa viongozi wa mkoa na wale wa Jimbo la Kigoma Mjini, akieleza hatua ambazo chama hicho imechukua kukabiliana na hatua ya serikali kupitia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kutangaza hatua ya kutaka kukifuta chama hicho. Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, alisema kuwa wameandika barua kwa Mwenyekiti wa SADC ambaye ni Rais wa Namibia na tayari imeshamfikia mwenyekiti huyo kwa ajili ya kufanyiwa kazi.Katika kulipa uzito suala hilo, Zitto alisema wamemuandikia barua Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa wakimuomba azungumze na Rais Magufuli ili aone umuhimu wa kukisaidia chama hicho kisifutiwe usajili. Pia, alisema kuwa chama kimeandika barua kwenda kwa Mwenyekiti wa EAC, Paul Kagame ambaye ni Rais wa Rwanda na nakala kutumwa kwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.Kiongozi huyo wa ACTWazalendo alieleza kuwa chama hicho pia kimeandika barua kwa mabalozi wa nchi mbalimbali za Afrika na mabalozi wa Ulaya wanaowakilisha nchi zao nchini na tayari barua zote zimefika kwa wahusika kutokana na uharaka wa jambo hilo ili waweze kulifanyia kazi haraka. Pamoja na hatua hizo, Zitto alisema kuwa pia wamechukua tahadhari za hatua za kisheria kwa ajili ya kuzuia msajili kukifuta chama hicho, akisema kuwa kufutwa kwa chama hicho kutakuwa na athari kubwa kisiasa kwa nchi na viongozi mbalimbali wa chama hicho na wananchi wakiwemo wabunge, madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa. | 1kitaifa
|
Na Mwandishi wetu, Mbeya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara ambao hawajakadiriwa Kodi ya mapato kwa kipindi kinachoishia Marchi 31, mwaka huu kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kukadiriwa na kulipa Kodi zao kabla ya Juni 30,2020. Hayo yamezungumzwa leo jijini Mbeya na Kaimu Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Stephen Kauzeni ambaye amewahimiza hayo wakati wa kampeni ya uhamasishaji wa ulipaji kodi inayoendelea mkoani humo. Aidha amewakumbusha wafanyabiashara wote ambao mwaka wao wa mahesabu unaishia Desemba 31,2019 kuwasilisha ritani zao TRA kabla ya mwisho wa mwezi huu. Amesema kwa upande wa wafanyabiashara wanaolipa kwa awamu lakini bado hawajakadiriwa kodi zao ni vyema wakafika TRA ili wakadiriwe na walipe mapema kabla ya tarehe ya mwisho ili kuepuka adhabu na riba. “Tunawatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao ya biashara ili kuwakumbusha na kuwahimiza wale ambao bado hawajafanyiwa makadirio, wakakadiriwe na wawahi kulipa kodi zao kwa wakati bila bughudha kuliko kusubiri siku ya mwisho kabisa”, amesema. Kauzeni ameongeza kuwa, kutokana na janga la ugonjwa wa korona, TRA isingependa kuona msongamano wa watu katika ofisi zake na kwamba imewalazimu maofisa wake kuwafuata walipakodi kwenye maeneo ya biashara zao ili kuwapa elimu ya kodi na kuwasisitiza wakailipe kwa. “Ni wajibu wa mlipakodi kulipa kodi zake kwa wakati lakini pia TRA ina wajibu wa kutoa elimu pamoja na kumkumbusha mlipakodi kulipa kodi na ndiyo maana tumewafuata huku madukani kwao kuwapatia elimu na kuwahimiza kulipa kodi kwa wakati,’’ amesema Kauzeni. Amesema kwa wafanyabiashara ambao mwaka wao wa hesabu unaishia Desemba 31, 2019 wanatakiwa kuhakikisha wanawasilisha ritani zao kabla au Juni 30, 2020 ili ritani zao ziweze kuhakikiwa na kufanyiwa kazi kwa wakati kwa mujibu wa sheria za kodi zinavyoelekeza. “Niwasihi walipakodi wafuate sheria ya Usimamizi wa kodi na kuwasilisha ritani zao ziweze kufanyiwa kazi mapema”, amesisitiza Kauzeni. Kauzeni amesema kampeni hii ya uhamasishaji ulipaji kodi kabla ya Juni 30, 2020 inalenga kuwakumbusha walipakodi kulipa kodi zao kwa wakati pamoja na kuongeza hamasa ya ulipaji kodi kwa hiyari miongoni mwa wafanyabiashara na watoa huduma zinazolipiwa kodi kama vile mawakili, wahasibu na fani zingine zilizosajliwa. Amesema kampeni hii ya utoaji elimu na uhamasishaji ulipaji kodi kwa wakati na hiyari inaendelea katika mkoa wa Mbeya na wilaya zake. | 0uchumi
|
NEW YORK, MAREKANI NYOTA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Shaffer
Smith maarufu kwa jina la Ne-Yo, ameweka wazi kuwa hajala nyama wala vitu
vyovyote vinavyotokana na wanyama kwa miaka miwili sasa. Msanii huyo mwenye umri wa miaka 39, amedai
kwa kipindi hicho chote alikuwa anakula vyakula vinavyotokana na mimea huku
akiamua kuachana kabisa na suala la nyama na mayai. “Ninapenda maisha ninayoishi kwa sasa, ni
miaka miwili sasa tangu nimebadilisha mfumo wangu wa maisha, sura yangu kwa
sasa inanawiri, uzito umepungua kwa kiasi kikubwa,” alisema msanii huyo. Aliongeza kwa kusema, alifanya maamuzi hayo
baada ya kuangailia kipindi cha runinga ambacho kilikuwa kinaonesha ‘afya ni
nini’, hivyo kilimfanya achukue maamuzi hayo hasa baada ya kugundua kwamba
ulaji wa nyama na mayai kwa wingi unaweza ukasababisha baadhi ya magonjwa. | 3kimataifa
|
RAMADHAN HASSAN -DODOMA WAZIRI wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika, amezitaka
wizara pamoja na taasisi zote kuhakikisha zinawalipa mishahara pamoja na
stahili zote watumishi ambao wamepandishwa madaraja kulingana na nafasi walizo
nazo sasa. Pia ameagiza
upandishaji wa madaraja kwa watumishi na wapewe nafasi ya upendeleo wale ambao
wanakaribia kustaafu. Hatua hiyo
imekuja kutokana na wajumbe wa Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi katika Utumishi
wa Umma kumlalamikia kwamba baadhi ya watumishi wamekuwa wakipandishwa
madaraja, lakini hawalipwi stahiki zao. Akizungumza
na waandishi wa habari Dodoma jana wakati akizindua na kufungua mkutano wa
baraza hilo, Waziri Mkuchika
alisema kumekuwa na malalamiko
katika maeneo mbalimbali nchini kuwa watumishi ambao Serikali ilitoa maagizo
kuwa wapandishwe madaraja, mishahara yao imebaki kama ilivyokuwa awali. “Nilikuwa
mkoani Ruvuma, huko pia nimekutana na malalamiko ya kutosha, kila mtumishi
analalamika kuwa kapanda daraja, lakini mshahara bado haujapanda,” alisema
Mkuchika. Alisema
kutokana na hali hiyo, viongozi wa Serikali wanaohusika na suala hilo
wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanalifanyia kazi ili kuweza kuwapatia stahili zao
watumishi wote waliopanda madaraja. Pia aliagiza
katika upandishaji wa madaraja kwa watumishi, wapewe nafasi ya upendeleo wale
ambao wanakaribia kustaafu. “Serikali
ilitangaza upandishaji wa madaraja kwa wale wenye sifa, lakini pia wanaotakiwa
kupatiwa kipaumbele ni wale ambao wanakaribia kustaafu katika utumishi wa umma
ili waweze kupata stahiki ambazo zitawawezesha kujikimu kule wanakokwenda,”
alisema Mkuchika. Alisema Novemba mosi, 2017, Serikali iliidhinisha
watumishi wapatao 85,000 waliokasimiwa katika bajeti ya mwaka 2015/16
kupandishwa vyeo. “Awamu
nyingine ya upandishaji wa vyeo imefanyika Mei 1, 2019 ambapo watumishi 193,166
waliokasimiwa katika bajeti ya mwaka 2017/18 wamepandishwa vyeo,” alifafanua
Mkuchika. Aliwapongeza
watumishi wote wa umma nchini ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kukusanya
na kusimamia mapato ya Serikali ambayo yanatumika katika kuboresha miundombinu
mbalimbali. “Nyie ndiyo
mmekuwa mkikusanya haya mapato ya Serikali, niwapongeze kwa kiasi kikubwa kwani
hapo zamani kabla ya hii awamu ya tano, tulikuwa tukikusanya kwa mwezi kiasi
cha Sh bilioni 800, lakini hivi sasa
imefikia hadi Sh trilioni 1.7 kwa mwezi kiasi ambacho tunatakiwa kushikilia
hapohapo,” alisema. Aliwataka
watumishi wa umma waliopo chini ya Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora,
kuhakikisha wanakuwa wa mfano katika suala la kupinga rushwa na kufanya kazi
kwa uadilifu bila ya kuchagua maeneo ya kwenda kufanya kazi. “Rushwa
katika ofisi za umma imekuwa kikwazo kwa wananchi wetu tunaowatumikia, naomba
katika ofisi yangu watumishi wangu muwe watu wa mfano, ambao mtakuwa
hamjihusishi na rushwa hata kidogo ili kuakisi jina la utawala bora,” alisema. Makamu
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Leah Ulaya, alisema changamoto ambazo zimekuwa kero
kwa watumishi ni upandishwaji wa madaraja bila kuzingatia stahiki nyingine
ikiwemo mishahara. “Tunakuomba
mheshimiwa waziri suala hili lifanyiwe kazi ili sisi watumishi ambao tumepata
fursa ya kupanda madaraja tuweze kupata stahiki zetu kulingana na miongozo ya
utumishi wa umma,” alisema Ulaya. | 1kitaifa
|
*Puma
yaungana na Umoja wa Mataifa kuadhimisha wiki ya nenda kwa usalama barabara Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam KAMPUNI ya Mafuta Energy Tanzania imeungana na
Shirika la Umoja wa Mataifa kuadhimisha wiki ya usalama barabarani huku kampuni
hiyo ikitoa wito kwa madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani
kwa lengo la kuokoa maisha ya watoto. Kwa mujibu wa Kampuni ya Puma ni kwamba moja ya
vipaumbele vyao ni suala la usalama barabarani ndio maana imeona umuhimu wa
kuungana na shirika hilo kubwa duniani kuadhimisha siku hiyo kwa kutoa elimu
kwa madereva wa vyombo vya moto nchini Tanzania. Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji
wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah amewaambia waandishi wa habari kuwa
wameamua kuitumia siku hiyo kutoa elimu kwa madereva ikiwa ni sehemu ya
Maadhimisho ya Wiki ya Kimataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ‘UN-Global
Road Safety Week (UNGRSW).’ “Puma tumeungana na shirika hili kutoa elimu,
ambapo kwetu Tanzania imetoa wanafunzi wa Shule ya Msingi na Bunge ambao ni
mabalozi wa elimu ya usalama barabarani hususani kwa mkoa wa Dar es Salaam. “Pia tumeamua kuwatumia watoto kutoa elimu ya usalama barabarani lengo letu Puma ni kuhakikisha wanaanza kupata uelewa kuhusu masuala ya usalama barabarani,” amesema Dhanah. Kwa upande wake Meneja Programu wa usalama
barabarani, Neema Swai amesema kauli
mbiu ya mwaka huu ni ‘Sema Usikike, Okoa Maisha’ na kufafanua maadhimisho hayo
huadhimishwa kila baada ya miaka miwili. “Kila siku watoto ndio wanaotumia barabara
kwenda shule na kurudi nyumbani, wasipokuwa na elimu ya kutosha tutawapoteza
wengi. Mmoja wa wanafunzi walioshiriki kutoa elimu, Godbless
Mlacha anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Bunge, amesema
wanawashauri madereva kuacha kutumia
vilevi au kwenda mwendo kasi wakiwa barabarani kwa kuwa maisha yao yanakua
hatarini. “Nahitaji kuishi ili nitimize ndoto zangu,
uzembe wa dereva unaweza kuondoa uhai wangu au kunipa kilema cha kidumu.
Nimechagua kupaza sauti ili kumaliza hili tatizo,” amesema Mlacha. | 1kitaifa
|
NA JESSCA NANGAWE BEKI wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa, Hamis Yusuph, amemtaka Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, kumpa nafasi beki wake chipukizi, Hajji Shaibu ‘Ninja’, ili kumjengea kujiamini na kuonyesha kipaji chake na si kumuweka benchi. Yanga leo itashuka dimbani kuvaana na Njombe Mji, iliyopanda daraja katika Uwanja wa Sabasaba, uliopo Njombe. Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, beki huyo alisema Ninja amekuwa mchezaji mwenye bidii sana, endapo atapata nafasi ana uwezo mkubwa wa kuja kuwa zao bora kwa timu yake ya Yanga. “Ninja ni beki mzuri na akubali kukabiliana na changamoto akiwa kwenye timu kubwa, suala la kuzomewa ni kawaida kwa wachezaji, pia kikubwa kocha angekuwa anamtumia katika mechi nyingi ili kumpa kujiamini ili aweze kukabiliana na timu mbalimbali,” alisema Yusuph. Alisema kuwa, Ninja anapaswa kuiga mfano wa beki wa sasa wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ambaye alianza kama yeye kwa kuzomewa, lakini alijifunza kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali hadi kufika hapa alipo. Ninja alisajiliwa na Yanga akitokea katika timu ya Taifa Jang’ombe ya Visiwani Zanzibar kwa mkataba wa miaka miwili, lakini ameonekana kutoaminiwa sana na kocha Lwandamina, huku akimuweka benchi katika baadhi ya michezo. | 2michezo
|
Sherehe ya tuzo hizo iliyofanyika kwa mara ya 29 ilifanyika jijini Paris ambapo kampuni mbalimbali zilishinda. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuonesha tuzo hiyo, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao amesema kuwa hiyo ni habari njema si tu kwa kampuni bali kwa taifa kwa ujumla kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja wake.“Tuzo hii imetolewa jijini Paris, Ufaransa mwishoni mwa Oktoba ambapo kampuni ya Business Initiative Directions (BID) ndio waandaaji wakuu wa tuzo hizi ambazo zimefanyika mara ya 29 kwa mwaka huu,” alisema na kuongeza:“Utolewaji wa tuzo hii ulihusisha marais, wakurugenzi, viongozi wa kampuni na wafanyabiashara kwa ujumla ambao walikuwa wanapendekeza majina ya kampuni inayostahili tuzo hiyo kutoka sehemu mbalimbali duniani.”Katika upigaji huo wa kura, hufanyika kwa siri bila ya hata kampuni inayopigiwa kura kujua. Baada ya upigaji huo wa kura kampuni ya StarTimes ndiyo pekee kutoka nchini Tanzania ilijinyakulia tuzo hiyo ya heshima.“Wateja wetu na Watanzania kwa ujumla wao ndio sababu kubwa mpaka sisi kutunukiwa tuzo hii. Ningependa Watanzania wafahamu kuwa ushindi wa tuzo hii sio wa kampuni pekee bali ni kwa Tanzania kwa ujumla kwani StarTimes ndio kampuni pekee iliyotunukiwa tuzo hii,” alisema.Aliishukuru serikali kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa kampuni zinazokuja kuwekeza nchini kuwahudumia wananchi wake. “Ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru tena Watanzania kwa kuendelea kutuamini na kutuunga mkono katika shughuli zetu na wakae mkao wa kula kwa kampeni zetu kabambe zinazoendelea kuzinduliwa hivi karibuni,” alisema. | 0uchumi
|
Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM BAADHI ya wenyeviti wa Serikali za mitaa wa Chama cha Wananchi (CUF), Mkoa wa Dar es Salaam, wamemuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad huku wakigomea uamuzi wa kuitwa kuhojiwa na Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba. Kutokana na hali hiyo wamesema kuwa kiongozi huyo hana sifa ya kufanyakazi wala kuwahoji kwani alishapoteza sifa ya kukiongoza chama hicho kwa mujibu wa katiba ya CUF. Licha ya hali hiyo viongozi hao pia wameunga mkono tamko la Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani, Saed Kubenea la kushirikiana katika operesheni yao inayojulikana kwa jina la ‘Ondoa Msaliti Buguruni’(OMB) iliyotangazwa kuanza hivi karibuni. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwa niaba ya wenyeviti hao, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtambani Manispaa ya Kinondoni, Bakari Kasubi alisema Profesa Lipumba hana sifa ya kuwaita kwani alishafukuzwa uanachama ndani ya chama hicho. “Tunasikia eti wanaojiita viongozi wa chama walipora mamlaka isiyo yao wanaandaa utaratibu wa kuwaita baadhi ya wawakilishi wa chama, madiwani, wabunge na viongozi wa serikali za mitaa kwa kile kinachoitwa kwenda kuhojiwa na kamati ‘feki’ ya maadili ya chama, hatuwezi kuhojiwa na watu hao,’’ alisema Kasubi. Alisema wao wenyeviti wanaunga mkono juhudi na mwelekeo uliochukuliwa na chama chao kutokana na maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na msimamo wa chama uliotolewa na Katibu Mkuu wao Maalim Seif Sharif Hamad. Alisema wenyeviti wanaungana kupinga maamuzi ya RITA mbele ya Mahakama Kuu kwa kufungua kesi ambayo kwa mujibu wa kifungu cha 26 kwa kukiuka taratibu za sheria ya wadhamini na kesi nyingine zinazohusiana na hujuma ambazo walitaja kuwa ni fedha za ruzuku. “Tunapingana kwa nguvu zote njama na mipango ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi kwa kushindwa kuheshimu hadhi na nafasi yake mbele ya jamii na kujiingiza katika vitendo vya hovyo vyenye muelekeo wa kutaka kuiharibia mustakabali wa CUF na kuwaathiri wadau mbalimbali walioshiriki katika kuasisi na kuijenga kwa takribani miongo miwili na nusu sasa,’’alisema Kasubi. Alisema wanampinga Profesa Lipumba kwa kukubali kutumiwa na CCM kwa masilahi yao binafsi na kushindwa kuthamini mchango wa CUF katika kujenga demokrasia nchini. “Lipumba leo amekuwa mtu wa kuweweseka ameshindwa kutumia taaluma yake kwa masilahi ya taifa, kila kukicha anatafuta msaada kwa vyombo vya dola ili kufanikisha dhamira yake, ameshindwa kukemea vitendo viovu vinavyoendelea kufanywa na wafuasi wake wanapohudhuria mahakamani, kushambulia waandishi wa habari kauli za kashfa na kejeli dhidi ya viongozi ,’’alisema . Aliongeza kuwa wito wao kwa wanachama na viongozi wa CUF kujiandaa vyema kukabiliana na mfumo kandamizi wa demokrasia nchini na kuwashughulikia wale waliowaita vibaraka wanaotumika katika kuharibu demokarsia na kukivuruga chama hicho. | 1kitaifa
|
HARARE, ZIMBABWE
FAMILIA zaidi ya 100 zilizotimuliwa na mke wa Rais Robert Mugabe, Grace kutoka makazi yao mashambani, zimeitaka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC kuingilia kati.
Hilo linakuja huku ripoti zikisema mahakama ilitoa hukumu kuzuia uamuzi huo wa Grace, ambaye anatafuta namna ya kupanua himaya yake ya kilimo katika eneo la Mazowe.
Baada ya wanakijiji wa Mazowe kufungua kesi, Mahakama Kuu ilitoa amri ya kuwataka polisi kutowaondoa wanakijiji hao kutoka shamba hilo la Arnold.
Wanakijiji hao wamekuwa wakiishi katika miliki hiyo kwa miaka 17, shukrani zikiiendea sera tata ya mageuzi ya ardhi ya Rais Mugabe, ambayo ilishuhudia wazalendo wakitumia nguvu kuwatimua wazungu kutoka mashamba yao.
Lakini inaonekana polisi wamepuuza amri ya mahakama ya kuzuia utekelezaji wa timua timua hiyo kwa manufaa ya mke wa rais.
Mwakilishi wa wanakijiji hao, ambao sasa hawana makazi, Innocent Dube, alikaririwa akisema wamelazimika kuwasilisha malalamiko yao SADC baada ya kuonekana hawawezi kupata msaada nchini hapa.
Waliwasilisha malalamiko hayo kupitia ubalozi wa Afrika Kusini nchini hapa kwa vile Swaziland, ambayo ni mwenyekiti wa sasa wa SADC haina ubalozi.
"Waliweza kupokea shauri letu na mawasiliano yetu na kutuahidi kututafuta,” Dube alikaririwa akisema. | 3kimataifa
|
Hadija Omary, Lindi Jumla ya mashauri 161 ya utelekezwaji wa watoto yameripotiwa katika Shirika
la usaidizi wa kisheria mkoani Lindi, Lindi Women Paralegals (LIWOPAC)
katika kipindi cha mwaka 2019/2020. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Cosma Bullu mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa
anazungumza na MTANZANIA DIGITAL ofisini kwake. Bullu alisema kati ya mashauri 558 yaliyopokelewa katika shirika hilo
mashari 430 yaliripotiwa na wanawake huku
mashauri 161 yalihusiana na wanaume kutelekeza familia na watoto wadogo
hasa watoto wachanga. Alisema kwa zaidi ya asilimia 78 ya mashauri hayo wanaoongozwa
kulalamikiwa ni wanaume ambao wamezaa nje ya ndoa. Bulu pia alisema kuwa hali ya baadhi ya wanaume kutelekeza watoto na kulelewa na mzazi mmoja kwa
kiasi kikubwa hupelekea uwepo wa watoto wa mitaani. Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Lindi, Richard
Kimaro alisema kuwa ushirikiano katika malezi ya mtoto kati ya wazazi, walezi
pamoja na jamii unahitajika kwa kiwango kikubwa ili kuhakikisha kunakuwa na ulinzi na usalama wa mtoto. Kimaro aliongeza kuwa Suala la ulinzi wa mtoto ni jukumu la jamii nzima,
mlezi na mzazi mmoja mmoja kwa nafasi yake katika ngazi ya familia pamoja na
serikali kwa ujumla. Alisema mzazi, jamii na serikali wakishirikiana hawataweza hata siku
moja kuwaona watoto wakiwa mitaani wanazurura muda ambao wanatakiwa kuwa
shuleni nasi tubaki kimya. | 1kitaifa
|
Brighiter Masaki – Dar es Salaam Miss Tanzania 2004, Faraja Nyalandu na Mwanamuziki Grace Matata wamelamba dili la ubalozi wa Kampuni ya Usafiri wa Anga ya Travelstart katika kampeni ya kuwafikia wateja kwenye huduma zitolewazo na kampuni hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar, Meneja wa Travelstart, Robert Othman anasema wameamua kufanya kampeni hiyo ili kuweza kuwafikia wateja kwa haraka kutumia mitandao. “Tumeamua kufanya kampeni hii kwa muda wa miezi miwili, kutakuwa na mashindano kwa watu wote, hii tumeona ni njia pekee ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuwa nasi kwa kipindi kirefu. “Kwenye matangazo yetu ya barabarani, endapo mtu akipita maeneo yenye matangazo yetu, akiona mdudu aina ya nyuki, kipepeo na konokono apige picha na atume kwenye mtandao wetu atakuwa amejipatia fursa ya kusafiri kwa gharama za kampuni yetu. “Safari hizo kwa washindi watasafiri kwa muda wa siku mbili, kwa wale ambao watapata bahati ya kwenda nje ya nchi na nchi ambazo watakwenda ni Thailand, Jordan, Amsterdam, Dubai au Mauritius na kwa mikoa ya hapa tutaangalia huenda tukasafirisha kwenda labda Ngorongoro, Serengeti, Zanzibar na sehemu nyingine,” anasema meneja huyo. | 4burudani
|
Mwandishi wetu, Tanga WAFANYABIASHARA wa Mkoa wa Tanga, wamesema hawaoni shidakulipa kodi baada ya kuona utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleoinayofanywa na Rais Dk. John Magufuli kupitia kodi zao. Hayo yalizungumzwa na wafanyabiashara wakati wa kampeni ya elimukwa mlipakodi inayoendelea mkoani humo ambako maafisa wa Mamlakaya Mapato Tanzania (TRA) kutoka Makao Makuu kwa kukishirikiana namaafisa wa TRA mkoa wa Tanga. Maafisa hao waliwatembelea wafanyabiashara kwenye maduka yaoyaliyopo barabara za namba jijini Tanga kwa lengo la kuwaelimisha nakuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati.Sambamba na hilo, maafisa hao pia waliweza kusikiliza kerozinazowakabili wafanyabiashara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusikiliza maoni yao kama mpango wa kutengeneza mazingira rafiki kati yao naTRA.Thabiti Salimu ambaye ni mfanyabiashara wa Ukwaju wa jumla na rejarejakatika eneo la barabara za namba amesema kuwa, atamshangaamfanyabiashara atayekwepa kulipa kodi hususani katika kipindi hikiambacho wameshuhudia miradi mingi ikitekelezwa kupitia kodi zao. “Rais Magufuli anatumia kodi zetu vizuri, tunaona utekelezaji wa miradimingi ya maendeleo hivyo lazima tuendelee kulipa kodi la sivyo kazi yautekelezaji wa miradi hii itakwama,” alisema Salimu. Naye Dina Mbenu, mfanyabiashara wa vipuli vya pikipiki amesema kuwa,ikiwa wafanyabiashara watakwepa kulipa kodi watasababisha madhara yakiuchumi na kuathiri jitihada za serikali za kuboresha miundombinuikiwemo barabara. Amesema hatua ya maafisa wa TRA kuwatembelea kwenye maduka yaokwa lengo la kuwahamasisha kulipa kodi na kusikiliza kero na maoni yaoinawasaidia kutopoteza muda kwenye ofisi za TRA wakisubiri kuhudumiwa. Kwa upande wake Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi Julius Mjenga amesemazoezi la kuwatembelea wafanyabiashara ni endelevu na kabla ya kufanyikaTanga, zoezi hilo limeshafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza,Mbeya na Morogoro. Amesema lengo la kufanya hivyo ni kutoa elimu ya kodi, kuwakumbushawafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati, kusikiliza maoni yao pamoja nachangamoto kwa ajili ya kuzitatua.Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure, aliwaombawafanyabiashara kuunga mkono zoezi linalofanywa na maafisa wa TRA lautoaji elimu ya kodi, kusikiliza maoni na changamoto zao kwa kuwa zoezi hilo linalenga kuboresha huduma kwa mlipakodi.“Niwaombe wafanyabiashara wote mkiwaona maafisa wanatembelea,msifunge maduka, wapokeeni na kuwapa ushirikiano kwa kuwa wanalengakuwaelimisha na kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenyebiashara zenu ambazo kwa pamoja tunaweza kuzitafutia ufumbuzi,”alisema Owure. Amesema zoezi hilo la utoaji wa elimu ya kodi kwa wafanyabiasharamkoani humo linatarajiwa kumalizika Juni 30, 2020 na kwamba lengo likiwani kutaka kuwafikia wafanyabiashara wengi mkoani hapo. | 0uchumi
|
AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM Daktari
Bingwa wa Upasuaji Mifupa na Magonjwa ya Ajali
kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Dk. Kennedy Nchimbi
amesema binadamu huzaliwa akiwa na mifupa 300 lakini anapokuwa mtu mzima
huungana na kuwa 206 Dk. Nchimbi
amesema baadhi ya mifupa hiyo kuungana na kutengeneza mifupa mikubwa. Dk.
Nchimbi amesema ukomavu wa mifupa (Ossifications), kwa kawaida binadamu
anapokuwa mtu mzima wa miaka 25 mifupa hiyo huungana kwani anapokuwa mdogo
mifupa ina kuwa imeachana hivyo anavyozidi kukua ndivyo inavyoungana. Amesema
kuna sehemu mifupa inakuwa haijafunga hivyo ikihesabiwa inakuwa mingi zaidi na
baadae zinaungana kwa kuwa ni za ukuaji ndio maana hurefuka. “Zaidi
ya nusu ya mifupa ya mwili wa binadamu ipo kwenye mikono na miguu na kati ya
mifupa 206 mifupa 106 ipo kwenye mikono na miguu,” amesema Dk. Nchimbi. Aidha
ameeleza kwamba sehemu ambazo zinagawanyika kabla ya kukomaa zinaruhusu kukua (Growth plates epiphyceal plate), mfano mfupa wa paja kabla ya miaka 25 binadamu wa kawaida mfupa huo unaweza kuwa na sehemu tatu hadi
nne tofauti lakini ukubwani huonekana
mmoja tu. “Ndio
maana hata mtoto anapozaliwa fuvu la kichwa unaweza kulibana na huwezi kufanya hivyo baada ya kukomaa hata akina mama wanaopitiliza siku za kujifungua
yaani wiki 40, hawezi kujifungua kwa njia ya kawaida ina kuwa ni shida,”namesema. | 5afya
|
Kwa mujibu wa matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa leo, Alhamisi, shule 10 zilizofanya vizuri zaidi kwenye mtihani huu kitaifa zinatoka katika mikoa kmbalimbali.Shule hizo ni pamoja na Kemebn, St. Francis Girls ya Mbeya, Feza Boys ya Dar es Salaam, Canossa ya Dar es Salaam na Anwarite Girls ya Kilimanjaro.Nyingine ni Precious Blood ya Arusha, Marian Boys ya Pwani, St Augustine Tagaste ya Dar es Salaam, Maua Seminari ya Kilimanjaro na Musabe Boys ya Mwanza.Shule 10 zilizoibuka kidedea kwenye mitihani ya kidato cha pili ni pamoja na St. Francis ya Mbeya, Kemebos ya Kagera, Centennial Christian Seminary ya Pwani, Thomas More Machrina ya Pwani, Bethel Sabs Girls ya Iringa na St. Augustine Tagaste ya Dar es Salaam.Shule nyingine ni pamoja na Bright Future Girls ya Dar es Salaam, Anwarite Girls ya Kilimanjaro, Feza Girls ya Dar es Salaam na Canossa pia ya Dar es Salaam. | 1kitaifa
|
UKARABATI mkubwa uliofanywa katika Bandari ya Kisumu nchini Kenya umeifanya bandari hiyo ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nchini humo kuwa kichocheo cha uchumi wa taifa hilo na Afrika Mashariki kwa ujumla.Wananchi wa Kenya wana hamu kubwa kuona bandari hiyo ikizinduliwa rasmi katika kiwango cha hali ya juu tofauti na ilivyokuwa awali ambapo utendaji wake ulikuwa usio wa viwango.Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, wakuu wa nchi zote sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanatarajiwa kuhudhuria siku ya uzinduzi wa bandari hiyo unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.Bandari ya Kisumu imefanyiwa ukarabati mkubwa kwa gharama ya Sh bilioni tatu za Kenya, ingawa kuna mipango ya kuifanyia marekebisho makubwa zaidi ambapo Sh bilioni 22.5 zitatumika.Rais Uhuru Kenyatta pamoja na mjumbe wa Umoja wa Afrika (AU) katika Maendeleo ya Miundombinu, Raila Odinga, wataongoza uzinduzi wa mradi huo unaotajwa kuwa wa kihistoria kutokana na kwamba utanufaisha mataifa yote ya Afrika Mashariki kwa wakati mmoja. | 1kitaifa
|
Na LUCY SAID (TURDARCO) MTAYARISHAJI wa muziki kutoka studio ya Fish crab, maarufu kwa jina la Lamar, amesema uwepo wa studio nyingi nchini haumtishi kwa kuwa uwezo wake bado ni mkubwa japokuwa yupo kimya. Akizungumza na MTANZANIA jana, alisema wasanii wengi hapa nchini wamefungua studio kwa ajili ya kufanya kazi zao pamoja na kazi za watu wengine, tofauti na miaka iliyopita na ushindani ulikuwa mdogo. “Uwepo wa studio nyingi haunitishi na hauniathiri kwa kuwa kinachohitajika ni ujuzi na uwezo wa kufanya kazi hiyo. “Msanii daima atabaki kuwa msanii na huwezi kumlinganisha na prodyuza kwani wana ujuzi tofauti japo ni mara chache sana kwa msanii kuwa prodyuza, lakini prodyuza kuwa msanii inawezekana. “Kikubwa ni uwezo, nina taaluma ya maandalizi ya muziki hivyo sina wasiwasi na wingi wa studio, bado uwezo wangu upo pale pale,” alisema Lamar. Lamar aliongeza kwa kusema ameamua kuweka muziki kando kwa muda ili kuendeleza biashara zake kama vile ‘Car wash’ na vitu vingi vinavyohusu magari. | 4burudani
|
MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM KATIKA kuthibitisha kuwa imepania kupindua
meza, kikosi cha timu ya Taifa Tanzania ‘ Taifa Stars’, tayari kimetua Sudan, kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kusaka
tiketi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji Wanaocheza Ligi za
Ndani(Chan), utakaopigwa Ijumaa hii jijini Khartoum. Timu hizo zilipoumana katika mchezo wa
kwanza uliochezwa Septemba 22, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Sudan
iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stars. Ili kuishinda Sudan na kutinga hatua ya
makundi, Stars itatakiwa kupata ushindi wa kuanzia mabao 2-0,
zitakaporudiana kesho kutwa. Kikosi cha Stars kiliondoka Kigali juzi
usiku kwenda Khartoum, baada ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya
Rwanda uliochezwa Uwanja wa Amahoro na
kumalizika kwa suluhu.
Mchezo huo huo wa kujipima ubavu ulikuwa kukidhi matakwa ya Kalenda ya
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Mchezo wa marudiano
kati ya Stars na Sudan utakaopigwa Uwanja wa Omdurman, wenye
uwezo wa kuchukua watazamaji 65,000. Sababu ya kikosi
cha Stars kuunganisha moja kwa moja Sudan, zinalengwa na kuwapa muda wa kuzoea
hali ya hewa wachezaji wa kikosi hicho.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo wao na Rwanda juzi, Kaimu Kocha Mkuu wa Stars,
Etienne Ndayiragije alisema aliridhishwa na suluhu waliyoipata na kudai kuwa,
mchezo dhidi ya Rwanda ulikuwa kipimo
sahihi kwao . “Nashukuru kwa
mchezo kumalizika salama, nimeridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji
wangu, nakiri kwamba tulipata mtihani
sahihi kulingana na kazi iliyo mbele
yetu. “Mchezo huu
utatusadia sana katika maandalizi yetu kuelekea mechi ya marudiano na Sudan,
kuna vitu vichache vya kufanyia kazi na bado tuna muda wa kurekebisha, lakini
vijana walicheza kwa kufuata maelekezo yangu, nimefurahishwa na hali hiyo,”
alisema kocha huyo raia wa Burundi. | 2michezo
|
WIKI hii, Julai 1, Benki ya Dunia iliingiza Tanzania katika kundi la nchi zenye kipato cha kati. Hizi ni habari njema hata pamoja na kwamba wapo wanaoona kuna mapungufu fulani fulani katika utendaji. Hatua ya kutoka katika umaskini na kupanda kwenda katika hatua nyingine ya juu huusisha suala zima la uchumi au maendeleo ya kiuchumi. Lakini pamoja na hayo maendeleo ya kiuchumi huguswa na vitu au mambo mengi mfano kutenda haki, amani, usalama, utulivu nakadhalika. Mtu yeyote anapokuwa katika mazingira yenye kutenda haki, amani, utulivu humwezesha kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kuwa mzalendo kwa nchi yake ikiwa ni pamoja na kulipa kodi. Sasa mazingira yanapokuwa tofauti na hayo, ndiyo ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya nchi . Kwa sababu hiyo sisi tunaweza kusema tumekuwa mabalozi wazuri wa kusisitiza suala la haki kila wakati, kwa sababu tumekuwa tukiamini haki ni msingi wa mambo yote mazuri. Na ndio maana tumekuwa tukikosa na wakati mwingine kukumbusha kutenda haki hasa katika vyombo vile vya kimaamuzi na kiutendaji. Tumekuwa tukisisitiza kwamba vyombo hivyo vinapaswa kutambua wajibu wao kuwa ni kutafuta namna ya kutatua matatizo na si kuyaongeza. Yapo baadhi ya matukio si yote ambayo yamefanywa na vyombo hivyo na hivyo kutoa taswira ya kukomoa au kuumiza baadhi ya watu kwa makusudi. Tumekuwa tukisisitiza hayo kutokana na kuwapo kwa ripoti ambazo zinaonyesha kuwa barani Afrika kwa muda mrefu sasa watu wameumizwa na vitendo vya kudhulumiwa haki zao msingi. Kwa mujibu wa ripoti hizo hata kutopea katika umaskini wa kimawazo, na hivyo wengi kuhadaika na kauli za wanasiasa, viongozi na watu wenye nafasi katika jamii, msingi wake ni dhuluma ya haki zao za msingi. Kwa misingi kama hiyo sisi kama chombo cha habari tunao wajibu wa kukumbusha kwamba vyombo hivyo kila inachofanya kabla ya kutoa uamuzi wowote basi vitambue vinao wajibu wa kuchunguza, kusikiliza, kubadilisha na kuboresha. Zipo nyakati tumeshuhudia vyombo hivi vikichukua uamuzi wa ghafla hata katika masuala nyeti sana katika mifumo ya sheria, utumishi nk. Vyombo hivi vinapaswa kutambua kwamba chochote kitakachofanyika bila kufuata misingi hiyo tuliyoitaja hapo juu kitakwenda kuathiri mustakabali mwema wa Taifa letu. Wakati fulani aliyepata kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Benedikto wa XVI, alitoa changamoto kubwa kwa watawala wa dunia. Kwa maneno yake mwenyewe alisema; “jamii yenye haki hujengwa na wanajamii wenye haki”. Maana yake tukitaka kujenga jamii yenye haki hatuna budi sisi wenyewe kuwa wenye haki. Kiongozi huyo alikwenda mbali na kusema; wao kama kanisa hawana mbinu za kiufundi wala nafasi ya kuingilia mambo ya siasa moja kwa moja lakini alibainisha wazi utume ambao alisema kama kanisa haliwezi kuuacha hata kidogo ni ule wa kuutangaza ukweli. Ukweli si jambo ambalo linapaswa kubebwa na taasisi zetu za kidini tu bali hata katika serikali zetu na taasisi zake, mahakama zetu, vyombo vya ulinzi na uslama kama Jeshi la Polisi, Bunge nk. Kuna msemo mmoja kwamba; ukweli ndio utakaowaweka watu wote huru: iwe katika siasa au katika nyanja yoyote ya kijamii. Kwa sababu hiyo tunaamini ujenzi wa jamii yenye misingi ya haki ni wajibu wetu sote lakini serikali, mahakama na Bunge linawajibika kujenga dhamira hiyo. Mahakama itambue kama ni taasisi ya kupigania haki, serikali ni wakala wa haki vivyo hivyo hata Bunge. viongozi wakiwamo wale wa kisiasa, na wananchi watambue kuwa wao ni wawajibikaji katika shughuli za kijamii na iwapo wote hawa watauzingatia ukweli ndani ya dhamiri zao zilizojengwa juu ya ukweli na ukweli tupu, basi jamii ina uhakika wa kujenga haki na amani na matokeo ya hayo ni kupaa kimaendeleo. | 0uchumi
|
TANZANIA inakisiwa kuwa na vifo vya watu 150,000 kwa mwaka vinavyotokana na kuumwa na mbwa wenye ugonjwa wa kichaa.Akitoa takwimu hizo jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Tanzania, Dk Martin Ruheta amesema ripoti ya Wizara ya Afya ya mwaka 2017, inaonesha kwamba katika mwaka huo kulikuwa na matukio 28,000 ya watu kuumwa na mbwa wenye vichaa na kuambukizwa ugonjwa huo.Amesema takwimu za kidunia, zinaonesha kwamba zaidi ya 60,000 wanafariki dunia kutokana na kuumwa na mbwa wenye vichaa na vifo vingi vinatokea katika Bara la Afrika na Asia, hasa kwa watoto wa vijijini.Dk Ruheta amesema, Septemba 28 mwaka huu, ni Siku ya Maadhimisho ya Kidunia ya Kudhibiti Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa; na nchini hapa, maadhimisho yatafanyika kwa kutoa elimu katika taasisi mbalimbali zikiwemo shule kuhusu ugonjwa na namna ya kuudhibiti.Amesema maadhimisho hayo pia yatatoa elimu kuhusu gharama za tiba kwa mtu aliyepatwa na virusi vya kichaa cha mbwa kwamba inagharimu dola za Marekani 44 ambayo ni gharama kubwa kuliko kuchanja mbwa huyo kunakogharimu dola saba tu.Dk Ruheta alisema kiuchumi, ni rahisi na vizuri zaidi kuwekeza katika kuchanja mbwa kwa lengo la kuzuia kuliko gharama za kutibu mgonjwa aliyepatwa na ugonjwa ambao wengi wao ni jamii ya vijijini."Kwa kushirikiana wadau mbalimbali nchini wakiwemo wananchi na taasisi na kuungana na taasisi za kimataifa, azma ya kutokomeza ugonjwa huo ifikapo 2030 duniani lazima itimie kwani kuifanya nchi bila ugonjwa huo inawekana," amesema.Amesema kutokana na mkakati huo wa kidunia, hapa nchini, mkakati wa majaribio umeandaliwa kwa ushirikiano wa wizara zenye dhamana ya afya ya binadamu na mifugo kwa kuweka mpangokazi wa kulinda afya ya pamoja.Amesema ugonjwa wa kichaa cha mbwa ulianza kutambuliwa nchini mwaka 1932/33, tangu hapo ugonjwa huo umekuwa ukisambaa katika maeneo mbalimbali mikoani.Alisema ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni ugonjwa tishio kwa binadamu na unampata binadamu aliye karibu na mbwa aliyeathirika ambapo akiumwa au kuguswa, anaweza kupata. | 1kitaifa
|
EDITHA KARLO SERIKALI mkoani Kigoma imeamuru kukamatwa na kuchukuliwa kwa leseni zao za biashara kwa wafanyabiashara watano wa mjini Kigoma ambao walikamatwa wakiuza sukari kwa bei ya juu tofauti na bei elekezi ya Sh 3200 iliyowekwa na serikali. Hatua hiyo imekuja kutokana na ziara ya ukaguzi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya Kigoma na viongozi wa wilaya hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Kigoma, Samson Anga ambapo walifanikiwa kuwakamata wafanyabiashara watano wilayani humo wakiuza sukari kwa kukiuka bei elekezi ya serikali ya sukari ya Sh 3200 baada kukutwa wakiuza kilo moja ya sukari kwa Sh 3700. Mkuu huyo wa wilaya aliamuru kukamatwa na kuhojiwa kwa watu hao kuhusiana na hali hiyo, kufunga maduka yao na kuchukua leseni zao za biashara hadi hapo hatua za kisheria dhidi yao zitakapomalizika.Katika ziara hiyo Mkuu huyo wa wilaya alitembelea Soko Kuu la mjini Kigoma, Soko la Nazareth ambako alifunga maduka matatu na eneo la Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mkoani Masanga na kuamuru kuchukuliwa kwa leseni za wafanyabiashara hao wakisubiri utekelezaji wa hatua za kisheria dhidi ya makosa yanayowakabili. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara hiyo Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa ziara hiyo ya kushtukiza ni sehemu ya mpango mkakati wa kusimamia utekelezaji wa maelekezo na maagizo ya serikali kuona yanafuatwa na kutekelezwa na wafanyabiashara hao na kwamba sheria itachukua mkondo wake kwa wale wote watakaotiwa hatiani. “Serikali imejiridhisha kwamba hakuna uhaba wa sukari nchini na hakuna sababu ya bei ya bidhaa hiyo kupanda kwa kiwango hicho na wafanyabiashara wote wanatakiwa kufuata bei elekezi iliyotolewa na serikali na si kuwaumiza wananchi,” alisema DC Anga | 1kitaifa
|
Makocha hayo wa kigeni wamekuwa wakilipwa fedha nyingi na kuzisababishia timu zinazoingia mikataba nao kubeba mzigo kubwa wa gharama za kuwagharamia mishahara, posho sambamba na uendeshaji wa timu.Pia Mbunge huyo ameishauri Serikali kuona uwezekano wa kuwatumia makocha wazawa wenye uwezo wa kuifundisha timu ya taifa ‘Taifa Stars’ badala ya kuendelea kuwaleta makocha wa kigeni ili kupunguza gharama kubwa ya fedha ambazo zingeweza kuwasomesha makocha wazawa kufikia ngazi za juu za ukocha.Mbunge huyo alisema hayo juzi wakati wa ufunguzi wa kozi ya walimu wa mpira wa miguu ngazi ya leseni C ambayo inatambuliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) mjini Morogoro.Kwa mujibu wa Abood, Tanzania imekuwa na makocha wengi wa ngazi mbalimbali ambao wana uwezo mkubwa wa ufundishaji sawa na makocha wa kutoka nje ambao wanaletwa na klabu hasa za Simba na Yanga.Mbali na Simba na Yanga, pia klabu za Azam FC, Stand United ya Shinyanga, Coastal Union ya Tanga, Kagera Sugar na Ruvu Shooting ni miongoni mwa timu za Ligi Kuu zenye makocha wa kigeni.Hata hivyo, Coastal Union hivi karibuni ilimtumia virago kocha wake, James Nandwa kutoka Kenya.Alisema kinachokosekana ni kujengewa uwezo wao ili kufikia viwango vya kimataifa na wale wenye viwango hivyo hawapewi nafasi ya kuutumia ujuzi wao kwenye timu mbalimbali za soka na hata katika timu ya soka ya Taifa.“Tunao makocha wazuri wazawa kuwazidi hawa wakigeni wanaoletwa na timu zetu...ninaona hakuna tofauti kati ya ufundishaji wa kocha wa kigeni na huyu mzawa uwezo wao unalingana na pengine wanazidiwa na makocha wetu wa nyumbani,” alisema mbunge huyo mpenzi wa soka.Hivyo alisema ni vyema fedha zinazotumika kuwaleta makocha wa kigeni kufundisha nchini, zingetumika kuboresha viwango vya ujuzi kwa makocha wandani ili watumike kufundisha timu mbalimbali za nyumbani.“Hizi gharama za kuwalipa makocha wa nje basi fedha hii ingetumika kuwalipia mafunzo makocha wetu vyuo vya nje ili wakirudi watumikie nchi yao,” alibainisha Abood.Alisema kilichopo sasa ni kasumba ambazo zimepitwa na wakati na kwamba kama mdau na mbunge, anakusudia kuliwasilisha suala hilo serikalini ili lifanyiwe kazi.“Nchi nyingi zinatumia makocha wao wa ndani na zimepata mafanikio makubwa kisoka na hili linajidhihirisha wakati kwa aliyekuwa kocha mkuu wetu Joel Bendera mwaka 1980,” alisema mbunge huyo akimzungumzia kocha huyo mzawa aliyeifikisha Tanzania katika fainali zake za kwanza na za mwisho za Kombe la Mataifa ya Afrika.Aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kutobweteka na ngazi hiyo, bali wazidi kuendelea katika hatua nyingine ili wawe makocha wa kimataifa. | 2michezo
|
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM KANISA la Free Pentecoste (FPTC) limetoa mwongozo kwa waumini wake kwa lengo la kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona. Mwongozo huo wenye vipengele 20 ni maagizo ya Askofu Mkuu wa FPCT, Stevie Mulenga, kwa makanisa na taasisi za kanisa hilo unaoelekeza Jumapili ibada iwe moja tu ama mbili kwa kanisa kubwa kwa waumini wachache. Akizungumza na MTANZANIA jana, Askofu Mulenga alisema waumini wameitikia, hivyo utekelezaji wa maagizo hayo umekuwa rahisi. “Wanatekeleza kwa sababu tumeona makanisani tulishawaambia wahakikishe kuna ndoo za maji yanayotiririka, watu wanavaa barakoa, ibada pia tumezifupisha si ndefu, harusi tulishaondoa, kama itafungwa ndoa hakuna sherehe yanatekelezwa kabisa. “Kuketi kwa mita moja moja tunalifanya japo lina shida shida, lakini tunalifanya, mahali pengine kwenye watu wengi tumeshaanzisha ibada mbili watu wanaweka viti mpaka nje. “Na kwa matukio yanayotokea sasa hivi wala imekuwa si ngumu tena, hata kama mtu hakufa kwa corona, lakini kwa sababu ipo kila mtu anakubali kuvaa barakoa, kila mtu anaepusha maisha yake na imekuwa ni rahisi zaidi,” alisema Askofu Mulenga. Mwongozo huo uliosainiwa na Katibu Mkuu wa FPCT, Mchungaji George Mwita, unaelekeza semina, makongamano na warsha zote zisitishwe zikiwemo zile za kitaifa na za kiidara. Aidha inaelekezwa majuma maalumu ya idara za kanisa yawe na programu moja – kuhudumu Jumapili ibadani. “Sherehe za harusi zisizo muhimu kipindi hiki nazo zimesitishwa, maziko yawe na watu wachache na matanga katika misiba yamesitishwa kwa sasa,” inasomeka sehemu ya mwongozo huo. Maelekezo mengine ni kuwepo kwa vitakasa mikono na sabuni za kunawia mikono milangoni makanisani na majumbani, na utaratibu wa kuketi wa mita moja. “Salamu za kupeana mikono na kukumbatiana zimesitishwa makanisani kwa sasa, waimbaji wafuate utaratibu sahihi unaoshauriwa wa matumizi ya vipaza sauti makanisani,” ilisomeka sehemu ya mwongozo huo. Aidha mwongozo huo unaelekeza ibada ziwe fupi za saa mbili na nusu kama mwongozo wa ibada unavyosema, Jumapili ibada iwe moja tu ama mbili kwa kanisa kubwa kwa waumini wachache. Imeshauriwa ibada nyingine moja tu ya maombi ifanyike katikati ya juma kama Jumatano, programu nyingine nje ya ibada zinazokusanya watu wengi Jumapili na siku nyingine zisitishwe. Vilevile ubatizo wa maji mengi ufanyike makanisani katika mazingira salama kwa wachache tu, ushiriki wa meza ya bwana uzingatie kanuni zote za kiafya kama ilivyo siku zote. “Wanaohisi kuwa na dalili za maambukizi ya corona wanaombwa kumwona daktari, tuwe waangalifu na tafsiri potofu za kiimani kuhusu corona. Tufanyie kazi taarifa sahihi zinazotolewa na Serikali na uongozi wa FPCT kuhusu corona. “Idara za Afya na Theolojia FPCT zielimishe waumini wa makanisa yetu kuhusu corona, tuendelee kuomba Mungu makanisani dhidi ya tatizo hili ili Mungu alinusuru taifa letu,” unasema mwongozo huo. MAKANISA MENGINE Hivi karibuni Kanisa Katoliki lilisema katika kupambana na corona wanaongozwa na sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali, maelekezo ya Wizara ya Afya na mengine yanayotolewa na waziri mkuu. “Mfano kama ibada ilikuwa inachukua masaa mawili na nusu kwanini tusiifanye iwe ya saa moja, kadiri unapowaweka watu muda mfupi unapunguza hatari ya maambukizi,” alisema Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima alipozungumza na vyombo vya habari. Kanisa hilo pia liliwashauri waumini wake kama kuna uwezekano wasogeze mbele matukio mbalimbali ikiwemo harusi hadi janga la corona liishe ili waje kufanya pamoja na sherehe. Padri Kitima alisema kuna mazoea ya watu kuingiza shamra shamra ambayo ni hulka ya binadamu, lakini akasisitiza kuwa zinahatarisha zaidi zoezi la kuzuia maambukizi. “Kama unadhani lazima mtoto wako apate ubatizo, kipaimara hakuna shida masharti ndiyo hayo, au nyie wachumba wawili mnasema tulishapanga kufunga ndoa mwezi wa nne, mje kanisani mtafunga mko wawii na wasimamizi kwa umbali wa mita moja moja, lakini hakuna sherehe,” alisema Padri Kitima. Aidha alisema sakramenti zitaendelea kutolewa kwa kuzingatia maelekezo ya kitaalamu. “Kuna sakramenti nyingine mtu amekaribia kufa huwezi kumnyima ubatizo, huwezi kumnyima kupokea sakramenti ya ndoa, lazima itatolewa, lakini unakuta ni mgonjwa na padri ameelekezwa namna ya kutoa kulingana na mazingira asiambukizwe na asiambukize wengine,” alisema Padri Kitima. Hata hivyo Kanisa Katoliki Jimbo Katoliki la Rulenge – Ngara mkoani Kagera, lilitangaza kusitisha ibada za misa, maadhimisho mengine yanayokusanya waumini wengi kanisani na sala za jumuiya kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia Aprili 19. Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza, naye alitangaza kusitisha ibada zote kuanzia Aprili 26. | 1kitaifa
|
Na Ras Inno, JUMA moja lililopita Shirika la Kutetea Haki za Binadamu Duniani ‘Amnesty International’ lilitoa taarifa iliyotonesha kidonda cha madhila yaliyotokea nchini Nigeria miongo mitatu na nusu na ushei iliyopita, ambayo inawezekana dunia imeshayasau kutokana na kuangazia zaidi migogoro mingine inayofukuta kwa sasa katika maeneo mbalimbali. Serikali ya Nigeria imekanusha vikali yaliyobainishwa katika taarifa hiyo ya Amnesty inayotaja matukio ya mwaka mmoja uliopita lakini ikikumbusha machungu ambayo bado hayajasahaulika kwa walioumizwa. Ripoti hiyo imebainisha kwamba vikosi vya usalama vya Serikali vimewaua watu takribani 150 katika maandamano ya kuunga mkono jimbo lililoko Kusini Mashariki la Biafra linalotaka kujitenga, kwa kuwatwanga risasi waandamanaji wanachama wa kundi la waasilia wa Biafra (IPOB) katika matukio mbalimbali kwa muda wa mwaka mmoja uliopita hadi Agosti mwaka huu. Ni vuguvugu jipya linalozidi kukanganya mustakabali wa utulivu wa Taifa hilo kubwa barani Afrika, kwa kuwa bado halijamaliza matatizo ya Boko Haram Kaskazini Mashariki na sekeseke linaloendelea katika jimbo la Kusini la Delta. Kilichoanzisha hamkani mpya Biafra ni mwendelezo wa manung’uniko ya watu wa kabila la Igbo wanaoishi huko kwa eneo lao kupuuzwa kwa ukosefu wa maendeleo, miundombinu duni ya huduma za kijamii zikiwamo hospitali na shule pia wanasiasa weledi kutoka eneo hilo kutoteuliwa kushika nyadhifa serikalini. Vuguvugu hilo jipya liliibuka baada ya kiongozi wa IPOB, Nnamndi Kanu kutiwa kizuizini aliporejea Nigeria kutoka Uingereza anakoishi na kufunguliwa mashtaka ya uhaini kutokana na kuendesha redio yake jijini London inayodaiwa kuchochea kushambuliwa kwa vikosi vya Serikali. Kinachobainishwa na Amnesty ni kikonyo tu cha kina halisi kilichotokea wakati wa vita ya Biafra iliyorindima kuanzia mwaka 1967 hadi 1970, wakati jimbo hilo lililipojitangazia madaraka kamili na kujipa jina kutokana na ghuba iliyoko Kusini mwake na kujumuisha makabila mengine ya Waefik, Waibibio, Waanang, Waejang, Waeket, Waibeno na Waijaw. Taifa hilo lililojitenga lilisababisha mgawanyiko wa msimamo kwa wanachama wa umoja wa nchi huru za Afrika kwa kutambuliwa rasmi na nchi za Gabon, Tanzania, Ivory Coast na Zambia na nje ya Afrika lilitambuliwa na visiwa vya Haiti na kupata msaada kutoka kwa baadhi ya nchi zikiwamo Israel, Ufaransa, Uhispania na jumuya mbalimbali za kidini. Lakini baada ya mapigano ya miaka miwili na nusu Biafra ilishindwa na kurudishwa upya kwa Nigeria, kutokana na mbinu iliyolaaniwa vikali duniani kote iliyotumiwa na majeshi ya Nigeria kwamba “adui yako msababishie njaa” kwa kulizingira jimbo hilo na kusababisha baa la njaa lililoua wakazi milioni tatu wa eneo hilo. Kimsingi Biafra ilidaiwa kuwapo kabla hata Nigeria haijapata uhuru kutoka kwa wakoloni, kwa jina la ‘Biafara’ ikiunganisha maneno ghuba ‘Bay’ iliyokaliwa na watu wanaotokana na kizazi cha ‘Ephraim’ kwa kujinasibisha na Mto Nun ulioko Kusini mwa Nigeria ambalo ni jina la baba wa Joshua wa kabila la Ephraim anayesimuliwa kwenye Biblia linalomaanisha: ‘Baraka ya Mungu’ kwenye nchi aliyopewa. Kwa kuamini hivyo ubishani uliozaa mkanganyiko huo unasababishwa na mgawanyiko wa kiimani unaoligubika Taifa la Nigeria, ingawa kinachoigusa dunia kutokana na ripoti ya Amnesty hakihusiani na mashiko hayo bali haki za binadamu zinazokandamizwa, hususani ikikumbukwa kuwa Rais wa sasa wa Nigeria Muhammadu Buhari aliyewahi kutawala kijeshi mnamo miaka ya 1980 alikuwa Brigedia Meja aliyeongoza vikosi vya Serikali dhidi ya majeshi ya Biafra katika mapambano hayo, ambapo majeshi hayo yalishutumiwa kwa ukatili mkubwa na ni Buhari huyo huyo aliyetamka mwaka jana kuwa kulikoni kuruhusu vuguvugu la harakati za Biafra kujitenga kuibuka upya na kuligawanya Taifa la Nigeria, ni heri Taifa zima lizame bahari na kuangamia. Ni msimamo unaodhihirisha kuwa mgogoro huo haujamalizika bado kwani mashiko yaliyogawa msimamo wa OAU bado yanazua hisia, hata wakati Mwalimu Nyerere alipotetea msimamo wa Taifa letu kuitambua Biafra alisisitiza kuwa: “Kutokana na imani kwamba kila binadamu duniani anastahili kuwa na mahala anapopaita kwake bila kubughudhiwa, lakini wanachofanyiwa sasa watu wa Biafra ni sawa na Wayahudi walivyofanyiwa na Hitler ingawa wamebahatika kupata nchi waliyokimbilia kujinusuru na kujitangazia uhuru. Kwa muktadha huo tunalazimika kukosoa mgawanyiko wa OAU na kuitambua Biafra kama Taifa kamili ili kutimiza dhima kuwa madhumuni ya jamii na mifumo ya kisiasa ni kuwastawisha wanadamu”. Biafra ni kama pembe la ng’ombe lisilofichika lililoibuliwa upya kwa taarifa ya Amesty International na kukumbusha vuguvugu la mgawanyiko uliojitokeza wakati wa vita ya kujitenga, ingawa nchi nyingi barani Afrika ziliiunga mkono Serikali ya Nigeria iliyoongozwa na Jenerali Yakubu Gowon dhidi ya vikosi vya Biafra vilivyoongozwa na Chukwuemeka Odumegwu Ojukwu lakini zilifanya hivyo kwa kuhofia kufanikiwa kujitenga kwa Biafra kungeamsha hamasa za jamii zilizotaka kujitenga ndani ya mataifa mengine barani hapa. Ingawaje Afrika haijawahi kufanikiwa kuwa na sauti moja dhidi ya migogoro mingi huku mingine ikisababisha mapigano yanayoishia kufanikiwa kujitenga na kuanzishwa taifa jipya, kama ilivyotokea kwa Eritrea iliyopigana na kujitenga kutoka Ethiopia. | 1kitaifa
|
MAHAKAMA ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara, imewahukumu raia watatu wa China kulipa faini ya Sh milioni 105 kila mmoja au kwenda jela miaka sita baada ya kukiri makosa mawili ya kusafi risha madini kwa nia ya kuyapeleka nje ya nchi bila ya kibali.Watuhumiwa hao walilipa faini na kuikwepa jela. Chini ya Hakimu Mkazi Veronika Mugendi, waliohukumiwa ni Yong zhe Ye (32), Chang Shaobo (31) na Xaolin Wang (25).Hata hivyo, dereva wao, Mtanzania Heneriko Shija (51), amebaki katika kesi hiyo baada ya kukanusha na shauri lake litatajwa Septemba 20, mwaka huu. Aidha mali ambazo ni dhahabu kilo 28.116, gari walilokuwa nalo, na mashine ya kufanyia utafiti zimetaifishwa na mahakama na kuwa mali ya umma. Kukamatwa kwa raia hao wa China wakitorosha madini kinyume cha sheria kwenda nje ya nchi,wanafikisha idadi ya raia wa nchi hiyo kukamatwa wilayani Tarime kuwa 6 katika kipindi cha mwezi mmoja. Wengine waliokamatwa awali na kufikishwa mahakamani hapo hivi karibuni ni Li Ninghi, Wang Xialong na Wang Zungsong ambao walikamatwa na vifurushi tisa vyenye kilo 300.75 za madini yakiwemo ya dhahabu wakiwa na gari aina ya Toyota Landcruiser VX V8 yenye namba za usajili KBW 515 L wakishtakiwa kwa makosa mawili ya kusafirisha madini bila kibali na uhujumu uchumi.Katika kosa la kwanza kila mmoja alihukumiwa kulipa faini ya Sh milioni 5 ama kifungo cha mwaka mmoja na kosa la pili kulipa faini ya Sh milioni 100 ama kifungo cha miaka 5.Walilipa faini, gari na madini vilitaifishwa. Katika kesi ya uhujumu uchumi namba 51/2019 iliyotolewa hukumu juzi Septemba 6 na Hakimu Mugendi ya Wachina hao wengine watatu Yongzhe Ye, Chang Shaobo na Xaolin Wang, walikiri mashitaka yao mawili ya kusafirisha madini bila kibali na uhujumu uchumi. Walikuwa wakitetea na Mwanasheria Joseph Mugabe. Awali wanasheria wa Serikali, Venance Mayenga na Aininus Kainunura walidai mahakamani hapo kuwa Wachina hao wamekuwa wakijishughulisha na utafiti wa madini katika maeneo ya Nyasirori Wilaya ya Butiama.Walidai Agosti 12, mwaka huu saa 3 usiku katika kizuizi cha Komaswa barabara kuu ya Musoma kwenda Sirari wakiwa na gari aina ya Toyota Hilux yenye namba T 994 DHC wakiwa wamefunika matunda aina ya matikiti, walikamatwa na vifurushi 21 vya madini na chupa mbili wakisafirisha kinyume cha sheria bila ya kuwa na vibali vya kusafirisha madini hayo kwa nia ya kuyapeleka nje ya nchi bila kufuata utaratibu. | 1kitaifa
|
KULWA MZEE -DAR ES SALAAM VIGOGO sita wa Kampuni ya Viettel Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Halotel, Son Nguyen (46), wanaokabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh bilioni 78, wanaendelea kusota rumande wakisubiri majibu kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini. Washtakiwa hao ambao kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani Machi 27 mwaka huu, jana walisomewa kesi yao kwa njia ya Mahakama Mtandao ambapo upande wa Jamhuri ulidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba upelelezi haujakamilika. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai upelelezi haujakamilika na akaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa utetezi, Benedict Ishabakaki akijibu alidai waliandika barua kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kumaliza kesi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) hivyo wanaendelea na mazungumzo na ofisi ya DPP. Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja hizo, alisema mazungumzo yakikamilika kabla ya tarehe ya kutajwa tena Julai 22 mwaka huu washtakiwa wataletwa kwa hati ya wito. Awali ilidaiwa kuwa washtakiwa hao Aprili 21 mwaka huu waliandika barua kwa DPP kukiri makosa. Barua hiyo inadaiwa ilipokewa, majadiliano yalianza na yalikamilika kwa kiasi kikubwa, kinachosubiriwa ni hati ya kuipa mamlaka Mahakama ya Kisutu kuendelea na shauri hilo kutoka kwa DPP. Mbali na Nguyen washtakiwa wengine ni Nguyen Minh (40) na Vu Tiep wote ni Mameneja wa Halotel, Ha Than (39) ambaye ni Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Halotel, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Nguyen Cong na Kampuni ya Viattel. Awali waliposomewa mashtaka Machi 27 mwaka huu mbele ya Hakimu Simba, washtakiwa hao walidaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia faida. Inadaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, kwa pamoja walitumia masafa ya redio bila kupata kibali kutoka TCRA. Pia inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu maeneo hayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Vietnam kwa pamoja walitengeneza mfumo ambao ulitumia huduma za mawasiliano zinazojulikana kama Virtual Private Network (VPN) kinyume na taratibu. Katika shtaka la nne, inadaiwa washtakiwa hao walikwepa kulipa kodi kwa TCRA kwa kutumia mitambo ya mawasiliano yaliyounganishwa Viettel Tanzania na Vietnam kinyume na sheria. Inadaiwa Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo hayo kwa kutumia masafa ya redio bila kupata kibali cha TCRA walisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 75. Pia wanadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu kwa kutumia mitambo ya VPN waliisababishia TCRA hasara ya Sh bilioni 3.03. Katika shtaka la saba, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 3.03 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuongoza genge la uhalifu. Kampuni ya Viettel Tanzania inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu ilitakatisha Sh bilioni 3.03 na shtaka la tisa na 10, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 75 wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu. | 0uchumi
|
KATIKA juhudi kubwa za kuondoa changamoto zinazokabili awamu ya kwanza ya huduma za usafiri kati ya Kimara- Kivukoni-Gerezani na Morocco, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umesema wanatarajia Julai mwaka huu mwekezaji mwenye hadhi ya kimataifa atakuwa ameanza kazi.Aidha wakala huo umesema kwamba Machi mwaka huu watatangaza zabuni hiyo ya kimataifa na ametaka kampuni za wazalendo kujitokeza kwani ni matarajio yake kampuni hizo zitakuwa na nafasi ya kushiriki katika utoaji huduma kama inavyofanyika katika nchi nyingine .Kutokana na changamoto za uendeshaji katika awamu ya kwanza, awamu ya pili inayoanza ujenzi wake rasmi mwezi ujayo hakutakuwa na mwendeshaji wa mpito na kampuni itakayoendesha huduma hiyo itapatikana wakati wa hatua za mwisho za kukamilisha mradi huo utakaotumia mabasi zaidi ya 200.Kwa sasa mwendeshaji wa huduma za usafiri wakati wa mpito UDART ana mabasi ya kasi 140 na mwendeshaji mpya atafanya kuongezeka kwa mabasi kufikia 305 hivyo kuongeza tija ya usafiri huo jijini Dar es SalaamMtendaji Mkuu wa Dart, Ronald Rwakatare amesema pamoja na kutangaza zabuni mapema mwezi ujao, ifikapo Julai kampuni hiyo itakamilisha taratibu zote ikiwemo kuingiza mabasi na hivyo changamoto ya usafiri katika awamu ya kwanza ya mradi kuisha.“Ni kweli kwa sasa tuna changamoto kubwa ya usafiri kwa kuwapo ongezeko kubwa la watu na mabasi kuwa machache, huku mwendeshaji wa mpito akikabiliwa na changamoto mbalimbali , jambo ambalo tumejifunza; katika awamu hii ya pili inayoanza kampuni ya kuendesha mradi itapatikana mapema na hakutakuwa na mwendeshaji wa mpito,”alisema.Ofisa mtendaji huyo amesema kwa kampuni za kizalendo zinaweza kujitokeza katika zabuni kwani kama wanatoa huduma ya usafiri na usafirishaji kwa njia ya malori na mabasi katika maeneo yenye umbali wa kilometa 600 watashindwaje kutoa huduma katika njia ambapo hata kilomita 30 hazifiki.“Ikiwa anakidhi vigezo na wataalamu katika masuala ya uendeshaji kama ukatishaji tiketi na mengineyo wanaweza kufanya biashara hii kwa uhakika hivyo ni vema kujitokeza kutumia fursa hiyo,”alisema.Alibainisha kuwa watatumia kasoro nyingi zilizojitokeza katika awamu ya kwanza ya mradi, kuhakikisha awamu ijayo ya barabara ya Kilwa itakayojengwa kwa awamu mbili haitakuwa na changamoto.Katika ujenzi wake, majengo, karakana na kituo kikuu itachukua miaka miwili na nusu kukamilika huku ujenzi wa barabara ikiwemo barabara za juu katika maeneo mawili zitajengwa kwa miaka mitatu.Katika awamu hiyo ya pili ujenzi utafanyika barabara za Kilwa, Kawawa, Sokoine, Gerezani, Bandarini na Chang’ombe yenye urefu wa kilometa 20.3.Alisema kwa sasa mkandarasi tayari amepatikana na tayari fidia zimelipwa. Hata hivyo alisema ujenzi rasmi unaanza mwezi ujao.Alieleza kuwa kwa tathmini ya sasa mabasi yanayohitajika si chini ya 200 lakini kila wakati wanafanya tathimini ya kuhuisha upya umbali wa njia kutokana na wananchi wengi kuhamia maeneo ya Kongowe, Vikindu. Awali njia hiyo ilipangwa kuishia Rangi tatu.Baada ya kuanza kwa awamu hiyo, itafuata awamu ya tatu ya barabara ya Nyerere hivyo kukamilisha awamu tatu za mradi huo kwa lengo la kurahisisha huduma za usafiri jijini Dar es Salaam. | 1kitaifa
|
UONGOZI wa klabu ya Rangers jana umemsimamisha kwa wiki tatu kiungo wa timu hiyo, Joey Barton, baada ya kukutwa na hatia ya kupigana na mchezaji mwenzake, Andy Halliday. Uamuzi huo ulifanyika ikiwa ni siku sita baada ya nyota huyo kurudishwa kwao kutokana na kutuhumiwa kufanya kitendo hicho. Barton mwenye umri wa miaka 34, alikiri kufanya kitendo hicho katika kikao kilichofanyika jana klabuni hapo. Kwa mujibu wa Meneja wa klabu hiyo, Mark Warburton, klabu hiyo inahitaji muda na nafasi ya kujadili tatizo hilo. “Mmoja kati ya Barton au Halliday, anatakiwa kuandaa maelezo kuhusu tukio hilo,” alisema Warburton. Inafahamika kuwa ugomvi kati ya wachezaji hao ulitokea wiki iliyopita wakati timu yao ilipofungwa mabao 5-1 dhidi ya wapinzani wao Celtic. Baada ya kutokea kitendo hicho, klabu iliwataka kuondoka na kurejea jana ambapo uongozi wa klabu hiyo ulifanya uamuzi. Katika utetezi wake, Barton alikiri kukosea na aliomba msamaha kwa kitendo chake cha kumvamia mchezaji mwenzake. “Miongoni mwa vitu nilivyofanya havikuwa sahihi, sikutakiwa kufanya nilichofanya, naomba nisamehewe. “Kuomba msamaha haimaanishi kuwa kila siku nitakuwa na makosa na mtu mwengine atakuwa sahihi, maana yake ni kuongeza uhusiano zaidi kwa wengine,” alisema Barton. Kosa jingine alilolifanya nyota huyo ni kuzungumza katika vyombo vya habari bila kupewa ruhusa na klabu hiyo. | 2michezo
|
BEATRICE KAIZA MREMBO anayefanya vyema kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Wema Sepetu, wiki hii amekuwa gumzo baada ya picha yake kusambaa mtandaoni ikimwonyesha amepungua mwili tofauti na ilivyozoeleka. Swaggaz tumepata nafasi ya kufanya mahojiano ‘X-clusive’ na Wema Sepetu ambaye jana alitangazwa kuwa balozi wa bidhaa za nywele chapa, Angels Hair Collection na hapo chini anafunguka mengi kuhusiana na mwonekano wake mpya. SWAGGAZ: Kuna warembo wengi hapa Bongo, unadhani kwanini dili hili la ubalozi limekuja kwako? Wema: Nimepata hili dili kutokana na ubora wangu, nina mashabiki wengi pia mimi huwa nafanya kazi na kampuni zenye bidhaa bora, siwezi kufanya kazi na watu wenye bidhaa mbovu na nitakuwa balozi kwa muda wa mwaka mmoja lakini nitaendelea kufanya nao kazi sababu wana bidhaa nzuri. SWAGGAZ: Wiki hii umekuwa gumzo mtandaoni baada ya mashabiki zako kukushambilia kwa kuwa umepungua sana, je ni kweli unaumwa? Wema:Kitu cha kuwaambia mashabiki zangu ni kwamba mimi ni mzima wa afya, sina ugonjwa wowote na kuhusu mashabiki kunitukana kuwa nimepungua sana, nimeshawazoea kwani hapo nyuma nilinenepa na nilikuwa nasemwa pia. SWAGGAZ: Lakini kwanini umekuwa ukiwajibu mashabiki zako kwamba umepungua sababu una Ukwimwi? Wema:Ukiona nimemjibu shabiki kwenye picha ambayo nimeweka mtandaoni ni kwa sababu ya maneno yao, mimi pia nina moyo kuna maneno mengine yanauma. Pia ni kuwakera tu ila kuhusu kuumwa siyo kweli ni juzi tu nimepima na nimeweka vipimo vyangu kwenye mitandao ya kijamii, mimi ni mzima jamani wa afya njema. SWAGGAZ: Kwahiyo sasa hivi una kilo ngapi na kipi kilisababisha upungue? Wema: Nimefikisha kilo 65 na lengo langu lilikuwa nikuwa na kilo hizo, nimekuwa mwepesi kupita maelezo pia kuna kipindi nguo ambazo navaa ni madera tu ila kwasasa naweza kuvaa nguo yoyote nikapendeza na kuwa na mwonekano mzuri. Kilichofanya nipundue ni dawa, nilitumia madawa mengi mpaka kuwa na mwili huu. SWAGGAZ: Mwaka umeanza, mashabiki zako watarajie nini? Wema:2020 ni mwaka wangu, nimejipanga kufanya vema kwenye tasnia, wakae mkao wa kula kwani Wema wasasa sio wa yule wa miaka ya nyuma. SWAGGAZ: Asante kwa muda wako. Wema: Nashukuru sana. | 4burudani
|
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Monduli kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Julius Kalanga amemtaka Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa asimdharau kwa sababu ya umasikini.Amesema anamwachia Mungu kwani ndiye atahukumu kwani alimtii Lowassa kama baba yake alipokuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lakini anashangaa sasa anamtukana yeye ni maskini.Kalanga amesema hayo eneo la Mto wa Mbu wakati alipokuwa akiomba kura ili awe mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM baada ya awali kuchaguliwa kuongoza jimbo hilo kuanzia mwaka 2015 kabla ya kujiuzulu hivi karibuni na kuhamia chama tawala ambako anawania kurejea tena bungeni.Alisema anamshangaa Lowassa kwa kudai kuwa amekopa benki zaidi ya shilingi milioni 600 na kuwa anadaiwa akisisitiza kwamba kudaiwa ni jambo la kawaida na kamwe nyumba yake haiwezi kuuzwa.“Namwambia Lowassa hata kama mimi masikini, asinidharau. Mimi ni maskini, lakini dharau sitaki na kwa haya aliyosema hapa Mto wa Mbu namwachia Mungu na nyie wazee wa mila nawaachia mtajua nini la kufanya,” amesema na kuongeza Lowassa si rais wala hana serikali hivyo hawezi kumfuata amsaidie.Awali Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu Msukuma, alisema CCM ‘haibipu,’ huku naye akimshangaa Lowassa kwa kusema Kalanga anadaiwa akihoji unawezaje kuwa tajiri bila kukopa.“Kwa nini mwanaume aweke gundi mdomoni kwa sababu ya kumfurahisha mwenzie..nawaambia hivi unakaa kwenye eneo ambalo ng’ombe wanataka kuondolewa halafu wewe unafunga mdomo.“Nawaomba Wana-Monduli mtoke kwenye magunia kaeni kwenye eneo safi ili muwe na dagaa bora kwani Lowassa anatembelea gari la serikali na analipwa mshahara na serikali kwa nini huyo Lowassa anawaambia lindeni kura kwa rungu wakati yeye yupo Dar es Salaam. Kwa nini hilo rungu lisimlinde huko kwake Dar es Salaam,” amehoji. | 1kitaifa
|
Awataka kutorudi nyuma kunadi sera zao, atoa neno kwa wabunge wa vyama tawala Na Deogratias Mushi -Johannesburg RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, amevionya vyama tawala katika Bara la Afrika kuacha kasumba ya kuvichukulia vyama vya upinzani maadui bali viwaone kama washindani. Kikwete ambaye tangu astaafu baadhi ya wapinzani wamekuwa wakimkumbuka na hata kufuta kumbukumbu za mashtaka ya kufinya demokrasia, kutokana na kile wanachodai kubanwa zaidi na uongozi wa sasa, aliyasema hayo wakati akichangia mada ya Utawala Bora na Utawala wa Sheria iliyowasilishwa na Profesa Barney Pityana, ambaye ni Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Afrika Kusini kwenye Kongamano la Uongozi barani Afrika yaani ‘African Leadership Forum 2017’. Kikwete aliliambia kongamano hilo la siku mbili lililomalizika jana jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini na kukutanisha viongozi mbalimbali akiwamo mtangulizi wake, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kuwa vyama tawala kuvichukulia vyama vya upinzani kama maadui ni kusababisha uadui usiokuwa na faida kwa nchi. Katika hilo, Kikwete alivitaka vyama vya upinzani barani Afrika kutokurudi nyuma katika kunadi sera zao kwa wananchi. Alisema vyama vya upinzani barani Afrika vinapaswa kuelezea vyema sera zao kwa wafuasi wao ili wazielewe na ufikapo wakati wa uchaguzi wapiga kura wawe na uelewa wa kutosha kuhusu mipango yao ya kuongoza nchi. “Vyama vingi vya upinzani barani Afrika bado ni vichanga na kwa Tanzania viliruhusiwa tena mwaka 1992 na kwa sasa vinapaswa kujijenga kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi husika,” alisema Kikwete wakati anachangia mada hiyo. Akielezea umuhimu wa vyama vya upinzani katika Taifa lolote lile, Kikwete alisema ni kuvifanya vyama tawala kuwa macho si kulala. “Pia kazi ya upinzani ni kuiambia Serikali kile inachofanya ni kibaya, ambacho katika chama chako hawawezi kuona au wanaweza kuona lakini wasiwe na ujasiri wa kusema kipi sahihi. “Wakati nikiwa rais nilikuwa nikiwaambia wanachama wangu, jukumu lenu ni kuisimamia Serikali, si kwa sababu unatokea chama tawala usiseme kuwa jambo hili baya, isipokuwa linapokuja suala la kura, basi piga kura na chama chako,” alisema. Kikwete alisema utawala bora unatokana na kuwepo kwa demokrasia, mahali ambapo kuna udikteta kunakuwa hakuna demokrasia. Kauli hiyo ya Kikwete imekuja wakati ambako malalamiko ya vyama vya upinzani nchini dhidi ya chama tawala kuhusu kubana demokrasia yakizidi kuongezeka. Kutorusha Bunge ‘live’, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara, kukamatwa na kufunguliwa kesi watu wanaoikosoa Serikali hususani wanasiasa wa wapinzani, ni miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na wapinzani nchini kuwa yanabana demokrasia. Mbali na hilo la demokrasia, Kikwete pia alitoa rai kwa wabunge wa vyama vilivyopo madarakani kuhoji Serikali pale mambo yanapokuwa hayaendi vizuri, kwani kufanya hivyo kunaimarisha utawala wa sheria. Alisema wabunge wa chama tawala barani Afrika inabidi waangalie ilani za vyama vyao na kuhoji pale Serikali haitekelezi kama ilivyoahidi, huku akisisitiza hali hiyo isichukuliwe kama kuipinga Serikali, bali kuiweka katika mstari. “Tunapaswa tusifike hatua ambayo washirika wa chama chako hawawezi kusema kitu kibaya ambacho Serikali inafanya. Kwa sababu kitakachotokea ni watu wataenda kupigia kura upinzani ambao wana ujasiri wa kuwaambia Serikali ukweli,” alisema. Akilizungumzia Bunge alisema ni chombo muhimu kwani linasimamia shughuli za Serikali bila kuogopa na linasema kipi kilicho bora na kibaya. “Kama Bunge halifanyi hivyo, Serikali haiwezi kuonywa, makosa yataendelea na kutakuwa hakuna utandawazi na uwajibikaji,” alifafanua Kikwete. Kwa upande wa chaguzi mbalimbali zinazofanyika Afrika, Kikwete alisema: “Lazima tuwe na tamaduni ya kukubali kushindwa, migogoro mingi katika Afrika inatokea baada ya uchaguzi. Uchaguzi wa haki usiwe kama ni kushinda tu,” alisema Kikwete. Alisema utawala bora ni jambo muhimu ambalo nchi za Kiafrika zinapaswa kutilia maanani. Pamoja na hayo, Kikwete alipongeza baadhi ya nchi ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa zinatilia maanani misingi ya utawala bora. “Si kweli kuwa barani Afrika hakuna utawala wa sheria au kila kitu Afrika ni kibaya hapana. Kumekuwa na juhudi nyingi za kuhakikisha kuwa migogoro inayozikumba baadhi ya nchi inatatuliwa ili kuwe na amani na utulivu katika nchi hizo,” alisema Kikwete. Kauli hizo za Kikwete zilionekana kumkuna mwanasiasa na kiongozi wa upinzani wa chama cha Democratic Alliance (DA) cha Afrika Kusini, Mmusi Maimane. Maimane aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa: “Rais Kikwete ameibua hoja ya umuhimu wa upinzani Afrika kama kazi ya utawala bora. Si maadui lakini washindani.” Hoja hiyo ya Maimane ilimwibua mmoja wa wanasiasa wa upinzani hapa nchini, ambaye pia na mwanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kipo kwenye mgogoro mkubwa wa kiuongozi, Ismail Jussa. Jussa kupitia ukarasa wake wa Twitter aliandika kuwa: “Ni uongo wa hali ya juu, maneno matupu. Ni Kikwete ambaye alituma jeshi kwenda Zanzibar, Oktoba 2015 na kufuta uchaguzi kwa sababu CUF ilikuwa inashinda.” Akizungumza na wanahabari jana jijini Johannesburg, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, alivitaka vyombo vya habari barani Afrika kuwa wazalendo kwa kuandika habari zitakazosaidia kutatua migogoro na kuleta maendeleo. Mkutano huo wa siku mbili ulihudhuriwa pia na marais wastaafu Olusegun Obasanjo (Nigeria), Thabo Mbeki (Afrika Kusini), Mohamed Marzouki (Tunisia), Hassan Mohammed (Somalia), Bakili Mulizi (Malawi), Mwanasheria Mkuu wa Uganda, Bart Katureebe. Ulimalizika jana kwa kuwataka viongozi barani Afrika kuunganisha nguvu zao katika kujenga amani na utulivu barani humo. | 1kitaifa
|
MKUU wa Mkoa wa Kagera, Marco Gaguti amemaliza mgogoro wa wakulima na wafugaji, uliodumu kwa zaidi ya miaka 11 katika Kijiji cha Kahundwe wilayani Karagwe.Alikutana na wananchi wa kijiji hicho na kutoa msimamo wa serikali na kuonya juu ya uvunjifu wa amani uliowahi kutokea kutokana na mgogoro huo mwaka 2008.Awali kabla ya kwenda Kijijini Kahundwe, alianza kwa kuwasikiliza wakulima na wafugaji na kumaliza mgogoro huo, kisha akaunda timu ya wataalamu kupitia nyaraka mbalimbali kuhusu kijiji hicho na kuwasikiliza wananchi pande zote mbili ili kubaini ukweli na chanzo cha mgogoro, ambapo timu hiyo ilifanya kazi yake na kuwasilisha majibu kwake.Baada ya kupitia taarifa ya timu hiyo aliwasili kijijini Kahundwe kusikiliza pande zote mbili za wakulima na wafugaji, kisha akawaeleza kuwa tayari serikali ilishabaini ukweli wa ni nani mmiliki halali wa eneo hilo la Kijiji cha Kahundwe baina yao.“Mwaka 1987 mamlaka za vijiji vinne zilikaa na kukubaliana kutenga eneo la kufugia mifugo yao na lilitengwa eneo la Kijiji Kahundwe kuwa eneo la wafugaji na kusajiliwa kisheria, Lakini kuanzia mwaka 2008 hadi 2015 baadhi ya wananchi kutoka maeneo mengine walivamia eneo hilo, wavamizi sita walikamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na kupatikana na hatia na kufungwa jela miezi sita kila mmoja,”alisema.Aliendelea kuwaeleza wananchi kuwa tangu wakati huo kumekuwa na uvamizi wa wakulima kutoka nje ya kijiji hicho na kuleta mgogogro mkubwa kati yao na wafugaji.Aidha, alisema kuwa serikali tayari imebaini ukweli wa uhalali wa nani anatakiwa kuwa katika eneo hilo, itasimamia ukweli huo wa mwaka 1987 na kama kutakuwa kuna wananchi wanataka mabadiliko wafuate sheria kama wenzao walivyofanya katika kutenga eneo hilo kuwa la wafugaji.“Natambua kuwa kuna wakazi au wafugaji 200 lakini 43 kati ya hao ni wavamizi si wenyeji nataka jambo hilo liishe mara moja,” alisema.Kupitia ziara hiyo aliyoifanya katika kijiji hicho alimwagiza na kumpa wiki moja Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka kuanzia jana kufanya uhakiki na utambuzi wa wafugaji wadogo ambao walisajiliwa katika kijiji hicho. Pia kuwaondoa wavamizi ambao ni wakulima na wafugaji wakubwa waliotoka maeneo mengine.Aidha alimtaka mkuu huyo wa wilaya na timu yake wafanye uhakiki wa mifugo ili kubaini wafugaji ambao kwanza si raia wa Tanzania, kubaini wingi wa mifugo kama kuna wafugaji wakubwa wenye mifugo mingi waondolewe ili wafuate sheria za kuomba vitalu vya kufugia kama wafugaji wakubwa au wawekezaji katika vitalu.Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Karagwe, Bernard Sau alisema Kijiji cha Kahundwe kilisajiliwa mwaka 1987 | 1kitaifa
|
kauli Mwenyekiti wa Jumuiya Vjana ya CCM (UVCCM) Taifa, Kheri James kuhusu kuwatia mimba wanawake wa watu wote wanaodhani serikali ya Rais Mgufuli hifanyikazi imeleta gumzo mitandaoni baada ya watu mbalimbali kumshambulia kwa kile wanachodai ni kauli ya udhalilishaji. Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa mkoani Kagera jana wakati wa uzinduzi wa Kagera ya Kijani, Kheri amewataka Watanzania waendelee kuwa na imani na Rais Magufuli na kusema: “Ukimsikia mtu anasema hakuna kilichofanyika ujue nao ni ugonjwa, tunatafuta dawa yake, mtu aliyeamua kufumba macho na hana tatizo la macho, asitengenezewe miwani, mfanye aone.” “Magufuli anafanya kazi kubwa, ukimsikia mtu anasema hakuna kilichofanyika huo ni ugonjwa, mpaka tumtie mimba mkeo ndiyo ujue tunafanya kazi.” Kauli imepokelewa na hisia tofauti na watu katika mitandao mbalimbali ya kijamii na kuamua kutoa maoni yao juu ya suala hilo. “Very Sad to My Fellow Youth Leaders, CCM imechoka sana na hawana ushawishi zaidi ya mabavu, kauli hizi si tu zinatolewa na viongozi vijana wa CCM, Heri (Kheri James), Gambo (Mrisho Gambo), Muro (Jerry Muro), Hapi (Ally Hapi), hata viongozi wakubwa, Mkapa (Benjamin)-wapinzani MALOFA, JPM Ministers-Wapumbavu,” ameandika Patrick Ole Sosopi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA). “Hivi kwanini hawa ccm awamu hii wanawadharau sana wanawake? Huyu mpaka mke atiwe mimba kwenye korosho tungeanza na mashangazi kwanini wanawadharau wanawake hivyo?” ameandika Shedrack Richard. Mwingine anayeitwa Nnko N Nnko ameandika: “Unadhalilisha sana wanawake lakini kuna siku itafika mtabaki mkitazama mazingaombwe.” Duh Kuna watu wana kauli hapa mjini. But alichosema kina facts na pia kwenye kukoselewa pakosolewe, hatuwezi kusifia kila Jambo ilhaLi vipaumbele vya taifa havizingatiwi, ni vizuri kuwa na uongozi wenye kupokea na kukubali ushauri lakini sio kusifia kila kitu bila kujali wahitaji.” ameandika MAGNET “Huyu dogo amevuka mipaka ya madaraka yake,namshauri aweke akiba ya maneno maana kesho haya anayosema atayakataa,ametukana watu kbs mpuuzi huyu,” ameandika Mussa Saidi Mussa. “Magufuli anafanya kazi kubwa, ukimsikia mtu anasema hakuna kilichofanyika huo ni ugonjwa, mpaka tumtie mimba Mkeo ndo ujue tunafanya kazi?, wanaona ila wameamua kufumba macho, watengenezewe mazingira ya kufumbua macho, kama mtaona ngumi itafumbua macho peleka ngumi”-M/KITI UVCCM pic.twitter.com/RQT1SW4G2X — millardayo (@millardayo) July 28, 2019 | 2michezo
|
KITENDAWILI cha mrithi wa Gadiel Michael ambaye anatajwa kutua Simba akitokea Yanga kimejibiwa kwa Yanga kumsainisha beki wa kushoto wa Malindi ya Zanzibar, Muharami Salum ‘Marcelo’.Marcelo alisaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea Yanga juzi usiku ikiwa ni siku chache baada ya beki huyo mwenye umri wa miaka 24 kusaini mkataba wa kuichezea Singida United pia ya Ligi Kuu Tanzania Bara.“Suala la mbadala wa Gadiel limemalizika, Yanga imekubaliana na Singida United imchukue Marcelo na tayari usajili wake umeshafanyika jana (juzi) usiku. “Hakuna pengo, Marcelo ni kijana mdogo na ana uwezo mkubwa wa kufanya kazi, Yanga wajisikie wenye furaha,” alisema mtoa habari wetu.Usajili huo wa Marcelo inamaanisha Yanga sasa imeachana rasmi na Gadiel, ambaye awali ilionekana kana kwamba anaisumbua klabu hiyo katika usajili.Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla alipoulizwa jana kuhusu usajili wa beki huyo alisema Kamati ya Usajili ndiyo yenye jukumu la kuzungumzia.Hata hivyo alikiri klabu hiyo kutafuta mbadala wa Gadiel na kwamba beki huyo ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa na nafasi kubwa ya kusajiliwa Yanga.“Ni kweli kulikuwa na mazungumzo ya kumsajili Marcelo, sijapata taarifa mpya lakini naamini wakati wowote jambo lake litamalizika au limeshamalizika,” alisema Dk. Msolla.Yanga ilishindwa kumsainisha Gadiel Michael ambaye mkataba wake wa miaka miwili ulimalizika hivi karibuni, ikidaiwa beki huyo aliyetua Yanga akitokea Azam, alikuwa hatua za mwisho za kujiunga na Simba.Wachezaji waliosajiliwa Yanga hadi sasa ni kipa wa timu ya taifa ya Kenya, Farouk Shikalo, ambapo wachezaji wengine wa kigeni ni Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Sadney Urikhob, Maybin Kalengo, Juma Balinya, Lamine Moro na Suleyman Mustapha.Wachezaji wazawa waliosajiliwa kabla ya Marcelo ni Ally Mtoni ‘Sonso’, Ally Ally, Mapinduzi Balama na Abdulaziz Makame. | 2michezo
|
Matokeo hayo yanaifanya Azam kufikisha pointi 35 na kuwashusha nafasi ya pili mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 33, huku timu zote mbili zikilingana kwa idadi ya mechi walizocheza 13.Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, timu zote zilionesha kiwango cha juu na kushambuliana kwa zama huku wenyeji Azam wakipoteza nafasi za wazi katika dakika za mwanzoni kabla ya Mtibwa kujibu mashambulizi hayo lakini hadi mapumziko hakukuwa na timu iliyoona lango la mwenzake.Kipindi cha pili makocha wa timu zote mbili, Stewart Hall wa Azam na Mecky Maxime wa Mtibwa walionekana kuwaongezea mbinu wachezaji wao na mchezo kuongezeka kasi, lakini milango iliendelea kuwa migumu huku kosakosa nyingi zikitokea kwa pande zote mbili.Azam walilazimika kufanya mabadiliko kadhaa kwa kuwatoa, Farid Mussa na Didier Kavumbagu na nafasi zao kuchukuliwa na Kipre Tchetche na Ramadhani Singano, mabadiliko ambayo yalionekana kuisaidia timu hiyo na kuanza kuwaelemea wapinzani wao, Mtibwa Sugar.Mtibwa Sugar wanaoshika nafasi ya tatu kwenye ligi hiyo nao waliendelea kupambana kwa kupanga vizuri mashambulizi yao, huku ikimtumia kiungo wake Shabani Nditi na mkongwe Hery Joseph, lakini washambuliaji wao walionekana kukosa mbinu za kuwabenya mabeki wa Azam.Wakati mashabiki wakiamini timu hizo zitatoka sare nahodha wa Azam, John Bocco, aliifungia timu yake bao pekee dakika ya 87, akiunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa katikati ya uwanja na kuwapa ushindi huo watatu mfululizo.Kwa matokeo hayo, Azam imefanikiwa kumaliza mwaka 2015, ikiwa kileleni ikiongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi mbili nyuma ya mabingwa watetezi Yanga wakati Mtibwa nayo ikimaliza mwaka huu katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 27. | 2michezo
|
NEW DELHI, INDIA WAISLAMU wa dhehebu la Shia nchini India, Anjuman-e-Haideri
wamesema watalipia gharama za matibabu yote ya Ibraheem Zakzaky, ambaye ni
kiongozi wa kundi la Shia lililopigwa marufuku nchini Nigeria. Sheikh Zakzaky na mke wake, ambao wamekuwa gerezani kwa
miaka minne sasa nchini Nigeria, waliwasili nchini India Jumatatu
wakisindikizwa na walinzi wa serikali
kuhakikisha wanarudi baada ya kupewa ruhusa ya kwenda kutibiwa nchini humo. Katibu Mkuu wa Anjuman-e-Haideri,
Bahadur Naqvi, aliliambia Shirika la
Utangazaji la Uingereza la BBC kuwa wameiandikia barua hospitali ya Medanta ambako
Sheikh Zakzaky na mkewe wamelazwa kuhusu
kuwalipia gharama zote za matibabu. “Tuna ripoti ya kitabibu na itawachukua miezi sita
kutibiwa, na madaktari wanasema inaweza kuchukua mwaka mmoja au miwili kwa sababu ya sumu iliyoko kwenye damu yake,”
alisema Naqvi. kwa msingi wa ripoti waliyopatiwa na hospitali hiyo alisema
kuwa wanakadiria gharama za matibabu kuwa Dola za Marekani 500,000 (£414,000). Hata hivyo hakusema iwapo hospitali ya Gurgaon imekubali
msaada huo. Anjuman-e-Haideri si kundi pekee linalotaka kusaidia
gharama za matibabu ya Sheikh huyo. Tume ya Kiislamu ya
Haki za binadamu ya nchini Uingereza (IHRC) pia imeripotiwa kutaka
kusaidia matibabu yake, lakini chanzo cha habari kililidokeza BBC, kuwa huenda
mamlaka za nchini India isiipe nafasi hiyo kwa kuwa ni taasisi ya kigeni. Sheikh Zakzaky (66), anakabiliwa na tuhuma za mauaji na
makosa mengine ambayo yote ameyakana. Pia amekana kwamba taasisi ya Shia aliyokuwa akiingoza
ambayo inaendesha hospitali na shule katika baadhi ya majimbo nchini Nigeria
eneo la kaskazini inapata msaada kutoka
Iran. Hivi karibuni Serikali ya Nigeria ilitangaza kulifuta
dhehebu la Shia kwa kile ilichoeleza kuwa limekuwa sehemu ya machafuko na
mipango na kutaka kupora madaraka kupitia huduma inazozitoa kama shule na
hospitali. | 3kimataifa
|
SERIKALI itaendelea kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa watumishi wa umma watakaofanya ubadhirifu katika miradi ambayo serikali imeweka fedha nyingi kwa maendeleo.Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William ole Nasha ameyasema hayo alipozungumza na watendaji wa serikali ya mkoa wa Morogoro baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya elimu kutoka Ofisa Elimu mkoa, Mwalimu Joyce Baravuga.Amesema sekta ya elimu imepewa kipaumbele kikubwa na serikali ya awamu ya tano kwa kutengewa fedha nyingi.Ukiacha miundombinu, wizara yake pekee inapokea Sh trilioni 1.4 katika bajeti ya mwaka na kwenye fedha za maendeleo upatikanaji wake ni asilimia 100.“Tanzania inasifiwa Afrika kuwa kati ya nchi ya kwanza kuongeza bajeti ya elimu hadi asilimia 21.2 ya bajeti ya taifa,” amesema Waziri Nasha.Naibu Waziri huyo alisema kipaumbele kikubwa cha serikali ya awamu ya tano ni sekta ya elimu hivyo ni wajibu wa viongozi wenye dhamana kusimamia na kufuatilia miradi yake ya maendeleo ngazi ya mikoa na wilaya kwa kutoka ofisini na kwenda kufuatilia utekelezaji wake pasipo kusubiri viongozi wa ngazi za juu.Alisema kuanzia mwaka 2016, serikali inatekeleza mpango wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na imekuwa ikitumia kila mwezi, Sh bilioni 20.8.Ameipongeza Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi ( VETA) Kanda ya Mashariki na Chuo cha Veta Kihonda kwa kutumia vyema fedha za ujenzi wa karakana mbili ya fani ya useremala na ya umeme wa magari chuoni zilizogharimu Sh bilioni 1.8 zilizotolewa na serikali.Akitoa taarifa kwa Naibu Waziri huyo, Ofisa Elimu wa mkoa wa Morogoro, Baravuga alisema wana uhaba wa walimu 4,248 wa shule za msingi na 796 wa sekondari, vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, matundu ya vyoo, madawati, ofisi za walimu na maabara. | 1kitaifa
|
Kulwa Mzee, Dar es Salaam Wabunge wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
wanaokabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko isivyo halali na kusababisha chuki
na uchochezi wa uasi, John Heche, Mchungaji Peter Msigwa, Halima Mdee na Ester
Bulaya leo wameiangukia mahakama wakiomba isiwafutie dhamana. Washtakiwa hao wamejieleza leo Jumanne katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kufikishwa Mahakamani
hapo kutoka Kituo cha Polisi Osterbay. Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai mahakama ilitoa amri
washtakiwa hao wakamatwe kwa kushindwa kufika Mahakamani Novemba 15 mwaka huu na kwamba Jamhuri
wanaomba dhamana ya washtakiwa hao ifutwe. Wakijieleza kwanini wasifutiwe dhamana kwa nyakati tofauti akianza
Msigwa aliomba radhi kwamba haikuwa nia yake kuidharau mahakama, tangu kesi
ianze hajawahi kuchelewa, hajawahi kukaidi amri ya mahakama na kwamba
anaheshimu kiti cha hakimu. Amedai alitokea Dodoma alidhani kesi ni saa nne na nusu kama kawaida
akiwa na Heche lakini walipofika walikuta kesi imeisha na jitihada za kumuona
hakimu kumaliza tatizo hilo zilishindikana. Kwa upande wake Mdee pia ameomba radhi, ameonyesha jinsi anavyoiheshimu
mahakama na kwamba alichelewa kwa kuwa alipitia kupima presha zahanati na
alipofika kesi ikawa imeisha na amri imeshatolewa na wadhamini wake waliwahi
lakini hawakufanikiwa kumaliza tatizo hilo Novemba 15 kwa kuwa waliambiwa amri
ilishatolewa. Heche amedai aliomba asifutiwe dhamana, anadai anaheshimu mahakama,
hajawahi kuidharau, siku ya kesi ilikuwa Dar es Salaam lakini alijua kama
kawaida kesi yao inasikilizwa saa nne na nusu hivyo alipofika alikuta
imeahirishwa. Akijitetea Bulaya amedai Novemba 14 alienda msibani Singida kumzika mama
yake mdogo lakini aliwapa taarifa wadhamini wake ambao siku ya kesi walikuwepo
katika eneo la mahakama. Baada ya washtakiwa hao kujieleza bado mawakili wa pande zote mbili
kuwasilisha hoja kisha mahakama itoe uamuzi wa kuwafutia dhamana ama la. Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Februari
Mosi na Februari 16, mwaka huu Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake
wakiwa Kinondoni, Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama na wengine ambao hawapo mahakamani ya kutenda kosa
la jinai ikiwamo kuendelea na mkusanyiko isivyo halali na kusababisha chuki na
uchochezi wa uasi. | 1kitaifa
|
Na Mwandishi Wetu VYOMBO vya dola vimetakiwa kuharakisha upelelezi wa kesi za waislamu wakiwamo masheikh na maimamu waliopo magerezani, ili haki iweze kutendeka. Wito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiislamu ya Imam Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatima ya waislamu na baadhi ya masheikh waliopo rumande kwa tuhuma za ugaidi, ambao wanaendelea kuteseka. Alisema umefika wakati kesi hizo ziharakishwe ili wakosaji watiwe hatiani na wasiokuwa na makosa waachiliwe huru, kwani waislamu zaidi ya 200 wanashikiliwa katika magereza mbalimbali nchini kwa makosa ya kubambikiwa. Sheikh huyo alisema, waislamu hao wanasota magerezani na wengine makosa yao yakiwa hayajulikani, jambo ambalo ni kinyume na haki za binadamu na Katiba ya nchi. Kiongozi huyo aliwataka waislamu kote nchini kuungana kupigania haki za masheikh na waislamu waliopo magerezani. “Tunawaomba Waislamu kuendelea kuwachangia Waislamu wenzetu walioko magerezani wakitumikia vifungo visivyokuwa rasmi pamoja na kuwatembelea mpaka pale watakapotiwa hatiani na mahakama. “Hivi kweli sisi ni waislamu wa hakika wakati waislamu wenzetu masheikh zetu wanateseka na kushikiliwa bila ukomo na hawasikilizwi kwa lolote na wakati huo huo sisi tumebwetweka na wala hatushughulishwi na madhila yanayowakuta kisha tunasema kuwa Waislamu wote ni ndugu?,” alihoji. Pamoja na hayo Sheikh Khalifa alitoa wito kwa Serikali. “Tunaitaka Serikali pamoja na vyombo vyote vinavyohusika na utungaji wa sheria wairejee upya sheria ya ugaidi ya mwaka 2002 ili kuondoa mapungufu ambayo kwa mujibu wa Katiba yetu yanaweza kumaanisha ubaguzi miongoni mwa raia hususan Waislamu ambao ndio waathirika pekee wa sheria hiyo,” alisema. Sheikh Khalifa alisema taasisi yake inaunga mkono kauli ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa aliyoitoa mwezi uliopita, ambapo alimtaka Rais Dk. John Magufuli, kutafakari juu ya hatima ya masheikh wa Jumuiya ya Uamsho wanaosota gerezani kwa zaidi ya miaka mine sasa bila kesi yao kusikilizwa. “Kama Lowassa aliyasema yale kisiasa sisi huko hatupo ispokua tunaunga mkono alichosema kwa kua kinalenga kutetea haki za watu. “Katika hili tunamwomba Rais Magufuli alitazame kwa jicho la tatu, akina Sheikh Farid alikamatwa tangu mwaka 2012 mauaji ya Kibiti yameibuka 2017 hawa watu wanahusikaje? “Tunajua Rais ndiye mkuu wa nchi taarifa nyingi anazo, lakini taarifa nyingine anazopewa si sahihi. Hawa masheikh walikamatwa Zanzibar na sababu za kukamatwa kwao zilitolewa na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tofauti na hizi anazosema Rais Magufuli. “Kimsingi sisi hatusemi waachiliwe tu, bali tunataka mashitaka yao yasomwe mahakamani, makosa yao yajulijkane na wao wapate fursa ya kujitetea kama ni kuhukumiwa wahukumiwe au waachiwe huru kuliko kuendelea kuwatesa. “Hatukumchagua Rais Magufuli kuwa mfalme, bali tulimchagua kuwa mtumishi. Kuwa mtumishi ni pamoja na kujali na kuthamani haki za watu,” alisema. | 1kitaifa
|
WAKATI jana tukishuhudia Liverpool ikiifunga Arsenal bao 3-1 kwenye mechi ya Ligi Kuu ya England, DStv Tanzania imeona vyema ikapunguza vifurushi ili watanzania waweze kufurahia burudani ya soka la Ulaya.Hivyo kampuni hiyo ambayo ina haki za kurusha matangazo ya mechi za Ulaya mubashara imethibitisha rasmi kupunguza kwa kiasi kikubwa ada ya mwezi ya vifurushi vyake kuanzia Septemba Mosi, 2019Mabadiliko hayo yanakuja muda mfupi tu baada ya kuanza kwa msimu wa soka ambapo ligi kubwa maarufu diniani zimeanza hivyo kuwawezesha wateja wa DStv kushuhudia ligi hizo kwa bei nafuu sana.Akithibisha punguzo hilo la bei, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso amesema kuwa muda wote wamekuwa wakisikiliza maoni ya wateja wao na moja ya mambo watejawaliyoshauri ni kupunguzwa kwa bei za vifurushi.“Wateja ndiyo moyo wa biashara yetu na muda wote tunawasikiliza na kutekeleza maoni yao pale inapowezekana. Kwa msingi huu, tumeamua kupunguza bei ili wateja wetu waendelee kufurahia burudani kabambe kwa bei nafuu zaidi,” alisema Jacqueline.Amezitaja bei hizo mpya kuwa kifurushi cha DStv Premium kutakuwa na punguzo la Sh 40,000 kutoka bei ya sasa ya Sh 169,000 hadi 129,000; Kifurushi cha DStv Compact+ punguzo la Sh 25,000 kutoka 109,000 hadi 84,000; Kifurushi cha DStv Compact punguzo la Sh 25,000 kutoka 69,000 hadi 44,000; na kifurushi cha DStv Family punguzo la Sh 10,000 kutoka 39,000 hadi 29,000.Kuhusu vifurushi maalum, Jacqueline amesema kifurushi chenye nyongeza maalum ya chaneli za Asia- DStv Premium+Asia Addon kitapungua kwa shilingi 40,000 kutoka 220,050 hadi 170,050 wakati kile chenye chaneli za ziada za Kifaransa DStv Premium+French addon nacho pia kitapungua kwa 40,000 kutoka 259,000 hadi 2019,000.Mkurugenzi huyo amewahakikishia wateja wa DStv kuwa kushuka huko kwa bei hakutasababisha mabadiliko wa chaneli katika vifurushi hivyo mteja ataendelea kupata chaneli zile zile alizokuwa akipata awali ila sasa atakuwa analipa bei ndogo zaidi. | 2michezo
|
BARAZA la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limetoa waraka mzito unaochambua masuala ya jamii, uchumi, maisha ya siasa, umuhimu wa Katiba Mpya na matukio yaliyo kinyume na tunu na misingi ya taifa. Waraka wa baraza hilo linaloundwa na idadi ya maaskofu 27, akiwamo Askofu Mkuu wa KKKT, Dk. Fredrick Shoo, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii jana asubuhi na umekusudiwa kusomwa leo na wiki ijayo katika makanisa yote ya KKKT hapa nchini. Mmoja wa watumishi wa KKKT na askofu ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini, alithibitisha kwamba waraka ulioonekana jana katika mitandao ya kijamii ndio ulioandaliwa na baraza hilo. Pia waliliambia MTANZANIA Jumapili kwa nyakati tofauti kuwa hadi jana waraka huo ulikuwa tayari umesambazwa kwa maaskofu na wachungaji wote wa kanisa hilo nchini na ulitarajiwa kusomwa leo. MTANZANIA Jumapili lilipomuuliza Askofu Shoo kwa simu jana kama ni kweli baraza hilo liliandaa waraka huo ulioonekana katika mitandao ya kijamii, alishindwa … | 1kitaifa
|
Akizungumza na gazeti hili, Makamu Mwenyekiti wa African Sports, Abdul Ahmed “Bosnia” alisema timu yao imejindaa kufanya vizuri katika michezo yote ya Ligi Kuu hususan mchezo wa ufunguzi dhidi ya Simba na kuwataka mashabiki wao kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuishangiliana timu yao.Abdul alisema wanafahamu kwamba Simba ni timu kubwa na imesajili wachezaji wengi wa kigeni, lakini wao hawataangalia hilo, bali wanachotaka ni kushinda mchezo huo ili kupata pointi tatu ambazo zitawapa wachezaji morali ya kushinda katika mchezo unaofuata.“Unajua hizi timu kubwa zinapokutana na timu ndogo kama African Sports huwa wanaona wamekutana na kibonde na kwamba wanaweza kushinda mabao mengi labda kwa ugeni wetu katika Ligi Kuu, hilo halitowezekana. Tumejipanga kupambana kwa kila hali ili kuweza kushinda mchezo huo,” alisema Abdul. | 2michezo
|
LIVERPOOL, ENGLAND BEKI wa kati wa Liverpool, Virgil van Dijk, amewatoa
wasiwasi mashabiki wa timu hiyo baada ya safu yake ya ulinzi kuruhusu mabao
matatu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi dhidi ya Red
Bull, Jumatano wiki hii. Katika mchezo huo ambao Liverpool walikuwa kwenye
uwanja wa nyumbani walifanikiwa kushinda kwa mabao 4-3, lakini mashabiki
walishangaa kuona safu yao ya ulinzi inaruhusu mabao matatu ambapo ni idadi
kubwa ya mabao. Kitendo hicho kimempa wakati mgumu beki hiyo wa
kati, lakini amewatoa wasiwasi mashabiki na kuwaambia makosa waliyoyafanya
hayawezi kurudiwa tena. “Bila shaka kila shabiki lazima
achukizwe, lakini wanatakiwa kujua tulishinda mchezo huo, hivyo hakuna sababu
ya kutoa lawama, kwa sasa siangalii mabaya tuliyoyafanya, ila ninachokiangalia
ni jinsi gani tutaisaidia timu kufanya vizuri. “Kikubwa mashabiki wanatakiwa kujua
kwamba sisi ni binadamu, hatuwezi kufanya vizuri muda wote, kuna wakati tutakuwa
tunakosea, hivyo kuna wakati kuzidiwa inatokea lakini sio kusudio la wachezaji
kufanya vibaya. “Lakini jambo zuri ni kwamba bado
tunaendelea kufanya vizuri msimu huu, ila mashabiki wajue hata sisi wachezaji
hatukuwa sawa baada ya kuruhusu mabao matatu japokuwa tulishinda mchezo huo. “Hakuna sababu ya mashabiki
kuchukia, wanatakiwa kutulia na kuangalia jinsi gani tutakuja kivingine kwenye
michezo inayofuata, tunatarajia kucheza dhidi ya Leicester City, tunaamini tutafanya
vizuri kwenye mchezo huo,” alisema beki huyo. Leicester City ambayo inashika
nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi nchini England, ipo chini ya kocha wa
zamani wa Liverpool, Brendan Rodgers, hivyo mchezo huo wa leo utakuwa na
ushindani wa hali ya juu japokuwa Liver watakuwa nyumbani. Rodgers alikuwa Liverpool tangu
mwaka 2012 hadi 2015 alipokwenda kujiunga na timu ya Celtic kabla ya mwaka huu
kupewa jukumu hilo Leicester City. | 2michezo
|
NEW YORK, MAREKANI MKALI wa muziki nchini Marekani, Ciara Harris, juzi alijikuta akiwa na kigugumizi wakati wa utoaji tuzo za Billboard. Ciara alipata nafasi ya kuwataja wasanii wa hip hop wanaowania tuzo hizo huku likiwemo jina la mpenzi wake wa zamani Future. Ciara alipata nafasi hiyo akiwa na mkali wa hip hop, Ludacris, lakini watu walimshangaa kwa kuhangaika kulitaja jina la Future baada ya kukamilisha kuyataja majina mengine ya Drake na Fetty Wap, huku jina la tatu likiwa la Future. Ciara na Future walifanikiwa kupata mtoto mmoja baada ya kuvishana pete Oktoba 2013, lakini uhusiano huo ulivunjika Agosti 2014. Kwa sasa, Ciara yupo na mchumba mpya ambaye ni mwanamichezo anayejulikana kwa jina la Russell Wilson ambao uhusiano wao ulianza Julai 2015. | 4burudani
|
BENJAMIN MASESE-MWANZA WAZIRI Mkuu Kassim
Majaliwa amewaagiza wakurugenzi wote
nchini kufanya tathmini kwa kila halmashauri kwa kupitia ahadi zote za Rais
Dk. John Magufuli alizozitoa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Alitoa agizo
hilo jana jijini Mwanza wakati akifungua mkutano wa 35 wa
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat). “Rais wetu Dk. Magufuli anafanya kazi kubwa kweli kweli, ikumbukwe
mwaka huu ni wa nne tangu ameingia madarakani, sasa naomba kila halmashauri ipitie ahadi
alizozitoa wakati akiomba kura alipopita halmashauri zetu, fanyeni tathmini na
andaeni ripoti inayoonesha
zile zilizotekelezwa. “Sote tunajua Rais wetu anarudi kwa wananchi ifikapo 2020 kuomba
ridhaa tena, hivyo ikiwa atapata ripoti hizi itamsaidia kwa kipindi hiki kujua
ahadi zilizobaki na kuzitekeleza, najua tunapozunguka sisi tumebaini moja ya
changamoto iliyobaki kubwa ni
upungufu wa madaktari na walimu,” alisema. Alieleza kushangazwa kwa kitendo
cha baadhi ya watu kumsimanga Rais Magufuli anapoibua miradi mbalimbali huku akiwataka kuacha tabia hiyo. Akijibu maombi ya risala ya Alat
iliyosomwa na Mwenyekiti wake, Gulamhafeez Mukadam, alisema
mwaka huu ni wa uchaguzi, hivyo aliwaagiza wakurugenzi kuendelea kuratibu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na
kuhamasisha wananchi kujiandikisha. Aliwataka wenyeviti
wa halmashauri na wakurugenzi kusimamia miradi ya maendeleo huku akishangazwa
na namna baadhi ya majiji nchini yalivyoshindwa kuanzisha miradi mikubwa ya
maendeleo. Alisema Serikali haijafanya
kosa kukusanya fedha zote katika mfuko mmoja kwani walifanya tathmini
na kuona ni heri fedha ikatunzwa eneo moja. “Tumeelekeza kila halmashauri kubuni mradi wa kimkakati na kutuletea
kwa ajili ya kuwapa fedha, lakini baadhi ya wakurugenzi wameshindwa kufanya
hivyo, hawajui hata kuandika
andiko, wakiandika wakileta linatupwa, sasa kama hamjui kutetea kile unachokitaka kuanzisha ni heri
ukakodi mtu akuandikie. “Mpaka sasa halmashahuri 17 zimekidhi matakwa katika miradi 22, hawa
tunawapa mabilioni ya
fedha ili kuanzisha miradi ya kimkakati, awamu ya pili halmashauri 12
zimeonekana kukidhi vigezo, nazo zitapewa. “Ndiyo maana inafikia hatua Rais Magufuli anakuwa mkali kwenu, hasa
kwa wale wanaofuja fedha, naomba kila halmashauri ipange mipango ya maendeleo,” alisema. Alizitaka halmashauri kumi za
mwisho zilizotajwa kwa kushindwa kukusanya mapato na kufikia asilimia 80
zijitathmini. Awali, Mwenyekiti wa Alat, Mukadam, alisema moja ya changamoto
kubwa inayowakabili ni posho ndogo na kiinua mgongo cha madiwani. Pia aliomba kufanyika kwa mgawanyo wa kata, vijini na mitaa kwani baadhi ya maeneo ni makubwa
sana jambo ambalo linaleta changamoto kwa viongozi. | 1kitaifa
|
Na FLORENCE SANAWA-MTWARA ULAJI wa panya umekuwa ukiwashangaza wengi huku wengine wakistaajabu juu ya ulaji wa mbwa, konokono, vyura, kenge na chatu. Viumbe hivi huliwa katika maeneo mengi duniani na hata kwa baadhi ya makabila nchini huvitumia kama kitoweo hali ambayo hufanya wengine kustaajabu pale wanapoona makabila hayo yakila. Kwa Mkoa wa Mtwara baadhi ya watu wamekuwa wakila panya, vyura na kenge. Utegaji na uuzaji wa panya umekuwa ukiwanufaisha watu wengi katika Kijiji cha Chikoweti, Kitongoji cha Mbuyuni wilayani Masasi mkoani Mtwara. Kijiji hicho kilichoko Kaskazini mwa mji wa Masasi kinakaliwa zaidi na watu wa kabila la Kimakua ambao wamekuwa na historia ya kutumia panya katika maisha yao ya kila siku kama kitoweo muhimu katika mlo. KWANINI PANYA? “Ukiangalia kihistoria, uhaba wa samaki ndio ulitufanya tuanze kutega panya kama kitoweo, wanatusaidia kwa kuwa hawana msimu. “Panya anayeliwa huwa ni mweupe yaani ana manyoya meupe, wengi hudhani kuwa panya anayeliwa ni yule wa majumbani lakini yule hapaswi kuliwa kwa kuwa anakula vitu vingi huenda akawa na sumu mwilini,” anasema Edgar Mpupua ambaye ni maarufu kwa uwindaji, utengenezaji wa mitego na uuzaji wa panya. Naye Petro Kaonje mkazi wa Kijiji cha Chikoweti anasema ladha ya panya ni tofauti na nyama alizowahi kula ndio maana haachi kula kitoweo hicho. “Unajua unaweza kumuangalia ukamdharau lakini panya ni mtamu, sisi tunaoishi huku hatuna mabwawa wala mito ndio maana panya wanalika kutokana na uhaba wa samaki kijijini kwetu. “Sisi Wamakuwa, Wayao na Wamakonde tunapenda kula panya, hii ni asili yetu huwezi kuikana kwa kuona aibu. “Mbona wenzetu Wachina wanakula hadi mende lakini wanafurahia tu maisha, panya ni kitoweo na ambacho kinapendwa,” anasema Kaonje na kuongeza: “Panya wanaoliwa sisi tunawafahamu na wasioliwa hatuhangaiki nao, tunapomkamata tunamchoma kisha tunakula na wali ama ugali ile ni mboga nzuri. Naye Samwel Mbaga anasema yeye si panya tu, bali pia anakula kenge, vyura na wanyama wengine ambao humpa burudani zaidi. Anasema ulaji wa kenge umekuwa ukimpa burudani zaidi kutokana na kazi kubwa ya kumpa panya hivyo kuwa rahisi kwake kumpata kenge. Kwa upande wake Martha Mkuti anasema ulaji wa panya ni wa mazoea kutokana na kutokuwa na kitoweo mbadala katika maeneo wanayoishi. “Ni kweli ladha ya panya ni kama samaki ndio maana tunaridhika kula, wapo watu wanaunga kwa nazi, ni watamu mno na wengine hupenda kula chukuchuku (kuweka chumvi bila kuchanganya na kitu kingine). “Raha ya panya unakula kila kitu hadi mifupa, ni wanyama shambani lakini nyumbani ni mboga. Mara nyingi tunapenda kula baada ya kumchoma halafu ndio unaiunga,” anasema Mkuti. Samwel Minjale Mkazi wa Kijiji Chikoweti, anasema katika maisha yake amejifunza kula vyakula vingi lakini amevutiwa zaidi kula panya kitoweo ambacho ni rahisi kupatikana. “Mimi namfahamu kwa kumla na si kwa kumsikia, huwezi kumfananisha na samaki kwani ana mafuta ya pekee na hutumii nguvu kumuandaa. “Huwezi kumfananisha na kiumbe mwingine wala kuku, yaani panya ukishamkamata unamchoma na ana mafuta ya kujitegemea ila unaongeza chumvi tu,” anasema Minjale. MITEGO Mzee Mpupua ambaye anajishughulisha kutengeneza mitego ya panya, anasema kazi hiyo ameifanya kwa zaidi ya miaka 36. “Nilianza kutengeneza mitego mwaka 1982 na maisha yangu kwa kiasi kikubwa naendesha kwa biashara hii,” anasema. Anasema uuzaji wa panya umeshamiri katika miaka ya hivi karibuni baada ya wategaji kuongezeka hali iliyosababisha kupandisha bei ya mitego. “Awali nilikuwa nauza mtego kwa Sh 100 baadae ikapanda hadi Sh 200, hivi sasa nauza mitatu kwa Sh 1,000 na tunaofanya biashara hii siku hizi ni wengi. “Mara nyingi huwa tunakwenda porini tunawavuna panya kisha tunawakausha kwa moto na kuwauza kwa mafungu. Nimekuwa nikimaliza mipango midogo midogo ya kifamilia kwa kuuza panya na mambo yamekuwa yakienda sawa,” anasema Mpupua. SOKO LA PANYA Soko kubwa la panya liko katika maeneo ya Mtandi, Migongo, Mwimbaka, Mbarika na Kanyimbi ambako ndiko kuna wateja wengi wa kitoweo hicho. Kitoweo hicho huuzwa kwa mafungu ya panya watano kwa Sh 500 na fungu lingine ambalo huwa na panya wanane ambao ni wakubwa huuzwa Sh 1,000. Anasema kwa siku wanaweza kuvuna zaidi ya panya 2,000. Hata hivyo, Mpupua anasema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utegeji wa kitoweo hicho na hivyo wakati mwingine kuhatarisha maisha yao. “Tunapata shida kwa sababu wengi wetu tunatembea bila kuvaa viatu, hata wanaovaa wamekuwa wakitumia viatu ambavyo haviwazuii kujikinga na wanyama hatari kama nyoka na wengineo,” anasema Mpupua. MTAALAMU WA LISHE Ofisa Lishe Mkoa wa Mtwara, Herieth Kipuyo, anasema ulaji wa nyama una faida kubwa kwenye mwili wa binadamu. “Unajua panya yupo kwenye kundi la vyakula vyenye protini, yupo katika kundi la nyama kati ya makundi matano ya vyakula. Makundi haya yana umuhimu ndani ya mwili wa binadamu kwa kuujenga ili uweze kufanya kazi vizuri. “Lakini siwezi kusema moja kwa moja kwamba nyama ya panya ni muhimu kwa kiasi gani au ina madhara kiasi gani,” anasema Kipuyo. | 5afya
|
VYAMA vya ushirika vimekumbwa na kashfa nzito ya ubadhirifu na wizi wa zaidi ya Sh bilioni 124.05, ambazo ni fedha za wanachama kutokana na ukaguzi wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika (Coasco) katika mwaka 2018/19.Orodha ya vyama vilinavyotuhumiwa kuhusika na ubadhirifu wa Sh 124,053,250,874.00, amekabidhiwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Brigedia Jenerali John Mbungo kwa ajili ya kuchunguza na kuwafikisha mahakamani wahusika wa ubadhirifu wa fedha hizo.Akizungumza na wanahabari jijini hapa jana, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema ripoti ya Coasco inaonesha kuna dosari katika vyama hivyo, ndio maana vingi kati yake vimepata hati zenye mashaka, isiyoridhisha na hati mbaya baada ya kufanyiwa ukaguzi maalumu unaonesha kuna ubadhirifu na viashirika vya wizi.Amesema kati ya fedha hizo, Sh bilioni 113.4 hazionekani zilipo zimeyeyuka na hazionekani zimekwenda wapi, Sh 87,694,976,970 zimepotea kwa nia ovu, lakini Sh bilioni 22.9 ni hasara kutokana na kutendwa kwa uzembe huku Sh bilioni 2.8 zimeibwa.Alisema ukaguzi maalumu uliofanyika kati ya mwaka 2018/19, ulibaini kwamba Sh bilioni 10.66 zilikuwa zimepotea, ambapo kati yake Sh bilioni 6.3 zimepotea kwa nia ovu, wakati Sh bilioni 2.6 ni hasara na Sh bilioni 1.7 zimepotea kwa wizi na ubadhirifu na hivyo kufanya Sh bilioni 124.05 kupotea.Hasunga alisema hadi 30 Juni 2019, vyama vya ushirika vilivyosajiliwa vilikuwa 11,410 ambavyo kati ya vyama hivyo, vyama hai ni 6,463, vyama sinzia ni 2,844 na vyama ambavyo havipatikani 2,103.Alisema hadi 30 Juni 2019, Coasco ilikagua vyama vya ushirika vipatavyo 4,413 sawa na asilimia 102.63 ya lengo la serikali la kukagua vyama 4,300.Alisema katika vyama hivyo 4,413 vilivyokaguliwa, vyama 303 sawa na asilimia 6.87 vilipata hati inayoridhisha, vyama 2,378 sawa na asilimia 53.89 vilipata hati yenye shaka, vyama 879 sawa na asilimia 19.92 vilipata hati isiyoridhisha na vyama 853 alisema 19.32 vilipata hati mbaya.Katika orodha ya vyama 4,413, vilikuwapo vyama vikuu 38, vyama vya mazao (Amcos) 2,710, vyama vya akiba na mikopo (Saccos) na vyama vingine 217.Katika orodha ya vyama vikuu 38, vyama vinne vilipata hati safi, vyama 22 vilipata hati yenye shaka, tisa vilipata hati isiyoridhisha na vitatu hati mbaya.Vyama vikuu vitatu vilipata hati mbaya kuhusu hoja zenye viashiria vya ubadhirifu, navyo ni Runali Sh milioni 856.35, SCCULT Sh milioni 4.9 na KYECU ambayo kulikosekana hati za kuhesabu mali za kudumu mwisho wa mwaka.Alisema Chama Kilele ambalo ni Shirikisho la Vyama vya Ushirika (TFC), kimepata hati isiyoridhisha, ambayo inajumuisha fedha benki zisizofanyiwa malinganisho na pia kutooneshwa katika taarifa za fedha kiasi cha Sh bilioni 1.5.“Katika orodha hiyo ya vyama vya Ushirika wa Mazao (AMCOS) 2,710 vilivyokaguliwa, vyama 15 vilipata Hati Safi, 1347 Hati yenye Shaka, 599 Hati Isiyoridhisha na vyama 749 vilipata Hati Mbaya,” alisema waziri.Alisema matatizo makuu katika Amcos ni kushindwa kuandika vitabu vya hesabu, malipo mengi kutokuwa na vielelezo vya malipo, mifumo dhaifu ya udhibiti wa makusanyo na mauzo ya mazao, kukosekana kwa daftari la mali za vyama na watendaji wa vyama kutokuwa na weledi wa kuandika vitabu na taarifa za fedha za vyama.Aliwataka waajiri ambao wanakata fedha za wanachama na kutozifikisha kwenye vyama vya akiba na mikopo wafanye hivyo mara moja. Kutokana na uchunguzi huo, kati ya Saccos 1,448, 261 zilipata hati safi, 887 yenye shaka, 218 isiyoridhisha na 82 hati mbaya.Alisema matatizo makuu ya Saccos ni kushindwa kuandika vitabu ipasavyo, marejesho ya mikopo ya wanachama kutofanyika kwa wakati, baadhi ya waajiri kuchelewesha kuwasilisha makato ya wanachama, madeni makubwa yanayothiri utendaji, miamala ya benki kutofanyiwa malinganisho na baadhi ya miamala kuwa na ubadhirifu.Alisema Wizara ya Kilimo inakabidhi Takukuru taarifa ya Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika ya Mwaka 2019 ili itumie sheria na madaraka kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali Mbungo alisema wanatoa nafasi kwa waliohusika na ubadhirifu wa mamilioni ya fedha kuzirudisha, na kama watashindwa kufanya hivyo, Takukuru itachukua hatua za kutaifisha mali zao, mifugo, nyumba na rasilimali zao wanazomiliki hadi sasa.Alisema hakuna jiwe litakalosalia juu ya lingine.Alisema wale watakaobainika kuhusika na ubadhirifu wa mali na rasilimali na fedha za wana ushirika na vyama vya ushirika, watataifishwa mali zao zote ili kufidia.Alisema watakaoshindwa kurudisha, basi uchunguzi ukikamilika, watawafikishwa mahakamani na lengo ni kuhakikisha fedha hizo wanazirudisha.Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Dk Titus Kamani alisema watatoa ushirikiano kwa Takukuru, kuhakikisha wale wote waliojichukulia mali za vyama vya ushirika na waliodai mali za ushirika hazina mwenyewe na kuzitumia kwa maslahi yao, wanarudisha mali hizo. | 1kitaifa
|
Na JUDITH NYANGE-MWANZA JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Deus Chacha (20), mkazi wa Mtaa wa Nyanza, Kata ya Mkolani, wilayani Nyamagana, kwa tuhuma za kuanzisha kiwanda bubu cha viroba. Kiwanda hicho kinadaiwa kujihusisha na kubadili vifungashio vya pombe zilizohifadhiwa kwenye mifuko ya plastiki maarufu kama viroba aina Pama Dry Gin na kuzihifadhi kwenye chupa za plastiki zenye ujazo wa mililita 100 na 200 kisha kubandika stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Agosti 1, mwaka huu, saa 10:30 jioni katika Mtaa wa Nyanza, Kata ya Mkolani, akiwa na boksi 33 za chupa za plastiki ambazo huzitumia kufungasha upya pombe hizo aina ya viroba ambazo zilipigwa marufuku na serikali Machi, mwaka huu, pamoja na bando la stika zenye nembo ya TRA. Alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akikata pombe hizo na kuweka kwenye ndoo na kisha kuziweka katika chupa hizo zilizokuwa na lebo ya blue sky na baadaye kuweka stika zenye nembo ya TRA. Alisema awali polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa katika maeneo ya Nyanza yupo mfanyabiashara mwenye kiwanda bubu kinachotengeneza pombe zinazohifadhiwa kwenye mifuko ya plastiki maarufu kama viroba vikiwa na nembo ya TRA, kisha kuwauzia watu wa maeneo jirani. Alisema polisi kwa kushirikiana na maofisa wa TRA walifanya ufuatiliaji, msako na upelelezi wa kumtafuta mtu huyo anayedaiwa kufanya biashara hiyo haramu ya pombe za viroba na waliweza kubaini mahali anapoishi na kufanikiwa kumkamata, huku akiwa na boksi 33 za pombe za viroba. “Kitu kilichotushangaza zaidi ni polisi kumkuta mtuhumiwa akiwa na bando la stika zenye nembo ya TRA ambazo huzibandika kwenye chupa baada ya kumaliza kufungasha upya pombe hizo ili kuwadanganya wananchi kuwa bidhaa inatambulika na mamlaka hiyo. “Tutawashirikisha TRA katika uchunguzi ili tuweze kufahamu uhalali wa stika hizo, upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa unaendelea na pindi utakapokamilika atafikishwa mahakamani, msako dhidi ya wafanyabiashara wengine wanaoshirikiana na mtuhumiwa kwa namna moja au nyingine katika biashara haramu ya pombe za viroba bado unaendelea,” alisema Kamanda Msangi. Kamanda Msangi amewaomba wakazi wa jiji la Mwanza kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi pale wanapoona au kubaini kuwapo kwa watu wanaofanya uhalifu kama huu, kwani vitendo hivi vinahatarisha afya za watumiaji, lakini pia kukosesha serikali mapato. Katika tukio jingine, polisi wanawashikilia Seif waziri (37) na Daud Mwakalinga (35), wote wakazi wa mkoani Dodoma, kwa tuhuma za kupatikana na Sh milioni 2, dola elfu 20 pamoja na silaha aina ya shotgun yenye namba 011765714 na CAR namba 00107210. Kamanda Msangi alisema watuhumiwa hao walikamatwa mkoani Singida wakiwa na vitu hivyo, ambavyo walivipora mkoani Mwanza Julai 14, mwaka huu, eneo la Kiseke A, wilayani Ilemela, baada ya kuvamia Kampuni ya Weish AST Ltd, ambayo hujishughulisha na biashara ya mabondo, ambapo walipora fedha kiasi cha Sh milioni 40, dola 190,000 pamoja na silaha aina ya shotgun. Kamanda Msangi alisema polisi wapo katika mahojiano na watuhumiwa wote watatu na pindi uchunguzi utakapokamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani, msako wa kuwasaka wenzao wawili ambao bado hawajapatikana unaendelea. | 1kitaifa
|
Na JUDITH NYANGE- MWANZA MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema Serikali itahakikisha inafuatilia matibabu na masomo ya mtoto mwenye umri wa miaka 11 (jina linahifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nyabulugoya, aliyebakwa na Mtendaji wa Kata ya Mkuyuni, James Chilagwire (42). Sambamba na hilo, Mongella amesema atahakikisha anafuatilia mwenendo wa kesi hiyo ili haki itendeke. Kauli hiyo aliitoa juzi alipoitembelea familia hiyo ili kufahamu maendeleo ya mtoto huyo aliyefanyiwa unyama huo Novemba 16, mwaka jana saa 1:00 jioni katika Mtaa wa Nyabulugoya. Inadaiwa Chilangwire alikwenda nyumbani kwa mwanafunzi huyo na kumkuta akiwa ndani peke yake na kumbaka. Baada ya tukio hilo, mwanafunzi huyo alifikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure na kufanyiwa uchunguzi na madaktari ambao walibaini kuwa ameharibiwa vibaya sehemu za siri na kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambako alifanyiwa upasuaji. Mongella akiwa hapo alisema amepata taarifa kuwa mama wa mtoto huyo wanapokea vitisho kutoka kwa watu hivyo alimtaka kutotishika kwa lolote huku akimwagiza Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyaguluboya kulisimamia suala hilo hatua kwa hatua. “Tumesikia unapokea vitisho sana kutoka kwa watu mbalimbali, niseme tu usitishike kwa lolote, Serikali itahakikisha mtoto wako anapona na kurejea shuleni pamoja na kufuatilia mwenendo mzima wa kesi yako mpaka pale hukumu itakapotolewa na mahakama,” alisema Mongella. Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto huyo, Ester Otieno, alisema mtoto wake kwa sasa bado ana maumivu sehemu za siri na hajapona kutokana na upasuaji aliofanyiwa hivyo ameshindwa kuhudhuria shuleni kuendelea na masomo yake. Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyaguluboya, Keffa Dickson, alimshukuru Mongella kwa kumtembelea mama huyo kwani ilifikia kipindi walikata tamaa. Alisema mama wa mtoto huyo ni mjane ambaye anaishi katika mazingira magumu na pia anategemewa na watoto wengine wanne. | 1kitaifa
|
MAKALA haya yanaangalia matumizi ya maneno ya Kiswahili ambayo waandishi wa habari na watangazaji mara nyingi wamekuwa wakiyatumia kinyume na maana zake halisi.Usuli wa tatizo lenyewe ni baadhi ya waandishi na watangazaji kuandika habari huku wakibadilisha matumizi ya baadhi ya maneno kwa lengo la kuvutia wasomaji. Madai ya matumizi ya aina hii mara nyingi yamekuwa yakielezwa kuwa fani hiyo ina mtindo maalumu wa kutumia maneno kwa kuyabadilisha au kuyaongezea vionjo ili kuipata hadhira hamasa kubwa ya kusoma habari inayohusika.Matumizi ya maneno kwa namna hiyo hushuhudiwa sana katika tasnia ya uandishi wa habari ikijumuisha uandikaji wa habari katika magazeti na utangazaji wa baadhi ya vipindi katika redio na televisheni.Hatahivyo, utumiaji wa lugha wa aina hii wakati mwingine huweza kupotosha maana iliyokusudiwa au kujenga taharuki isiyo ya msingi kwa wasomaji. Makala haya yanaonyesha baadhi ya maneno hayo na pia kupendekeza namna nzuri ya utumiaji wa maneno kwa mtindo huo. Msamiati “yatua” Msamiati huu umetokana na mzizi “tua” wenye maana ya “shusha chini, teremka kutoka katika chombo cha usafiri”, lakini waandishi wengi wa magazeti wamekuwa wakilitumia neno hili kwa namna tofauti na maana yake ya msingi. Tuingalie mifano michache kutoka katika magazeti yanayoandikwa hapa nchini:o CCM yatua Ikulu.o TAKUKURU yatua maduka ya kubadili fedha Mwanza.o Papa Francis atua falme za Kiarabu. Kulingana na mifano iliyotolewa hapo juu lugha ya kawaida tungeterajia kukuta maandishi ya sentensi hizo yakiwa kama ifuatavyo:o CCM yaingia Ikulu.o TAKUKURU yawasili katika maduka ya kubadili fedha Mwanza.o Papa Francis azuru falme za Kiarabu. Au Papa Francis awasili falme za Kiarabu. Ubadilishaji wa maana ya msingi ya neno hilo wakati mwingine unaweza kudhoofisha utajiri wa msamiati katika lugha ya Kiswahili.Mwandishi anang’ang’ania neno moja “kutua” badala ya kucheza na maneno mengine kadhaa kama yalivyoonyeshwa hapo juu. Aidha, mwandishi wa makala haya aamejiuliza je, matumizi ya neno “tua” yameongeza mvuto kwa msomaji? Bila shaka wasomaji wa makala haya watakuwa na maoni tofauti.Msamiati “watupwa” Msamiati huu umetokana na mzizi “tupa” wenye maana ya ondoa kitu mahali ambapo hakitakiwi kuwapo mfano takataka, au weka kitu jaani baada ya kuisha matumizi, au rusha kitu.Kutokana na maana hizi za msingi za neno hili kwenye uandishi linaweza kupewa sura nyingine mfano: o Watu watano watupwa jela. o Mzazi atuhumiwa kuwatupa watoto wake kwa zaidi ya miaka ishirini.Katika mfano huo tunaona msamiati “watupwa” umetumika tofauti na maana yake sanifu kwani watu huwa hawatupwi jela, bali hufugwa jela. Hivyo mwandishi ametumia “kutupwa” pengine ili kuweka mvuto wa lugha anayotumia. Halikadhalika, neno “kuwatupa watoto” katika mfano wa pili maana yake ni kuwatelekeza watoto.Mwandishi wa makala haya anakiri kuwa kwa Mswahili kindakindaki ataelewa kilichokusudiwa lakini anajiuliza je, iwapo msomaji wa habari hiyo si Mswahili anayeelewa matumizi tofauti ya maneno ataweza kuipata maana iliyokusudiwa?Msamiati “walamba”Msamiati huu “walamba” umetokana na mzizi ‘lamba’ wenye maana ya onja au safisha kitu kwa kutumia ulimi.Mfano Juma amelamba mwiko wa ugali. Vivyo hivyo neno hili kwenye tasnia hii huweza kuvishwa maana nyingine mfano: o Madaktari 122 Walamba ajira. o Mtoto katika familia maskini alamba dume. Maana iliyokusudiwa hapo ni kwamba madaktari 122 wamepata ajira na mtoto katika familia maskini amebahatika kupata kitu fulani. Matumizi katika sentensi ya pili yanatokana na maneno yanayotumiwa kwenye mchezo wa karata. Hivyo tunaona dhahiri kuwa maneno yote matatu yaliyotolewa mfano hapo juu yamebadilishiwa maana yake ya msingi.Ubadilishaji huu wakati mwingine huweza pia kukengeusha maana iliyokusudiwa. Pamoja na madai hayo ya mtindo wa uandishi lakini ni vema mwandishi akatumia maneno kwa usahihi na pale anapoamua kubadilishia neno maana basi achague neno linalosadifu.Aidha, neno linalobadilishiwa maana yake ya msingi yafaa lionyeshwe kwa kulifungia katika alama za mnukuo. Inashauriwa waandishi kuwa makini katika uteuzi wa misamiati ili kukuza lugha ya Kiswahili bila kumkanganya msomaji.Aidha, badala ya kudai ni mtindo wa uandishi yafaa tuangalie usahihi wa matumizi wa maneno. Kwa upande wa mwandishi analo jambo ambalo angetaka kila atakayesoma makala haya ajiulize “Je, matumizi ya neno sanifu na fasaha huondoa au kuunguza ladha ya lugha? Bila shaka kila mtu atajihoji kuhusu swali hili. Upo umuhimu mkubwa wa kutumia lugha kwa usanifu na ufasaha pasipo kuikengeusha kwa kisingizio cha mtindo.Inashauriwa kuwa kama mwandishi atatumia msamiati kwa namna tofauti basi atumie alama za mnukuo “” ili kuonesha kuwa neno hilo limetumiwa kwa maana nyingine. Hali kadhalika tuangalie mifano mingine michache ya namna waandishi wanavyotumia misemo kwa namna tofauti. Yamkini watumiaji hawa hawajui kama wanatumia visivyo. Hebu tuangalie mifano ya misemo na kabla ya hapo tujikumbushe nini maana ya misemo. Misemo ni kauli fupifupi zinazotumiwa na jamii kusisitiza ukweli wa jambo fulani. Fungu hili la maneno huwa na maana mahsusi na lengo huwa ni kutoa mafundisho kwa jamii.“Matajiri wa kupindukia na maskini wa kutupwa” Pamoja na kwamba matumizi ya msemo huu ni wa miaka mingi lakini bado kuna kuchanganya dhana. Kama tujuavyo tajiri ni mtu mwenye fedha na mali nyingi na maskini ni mtu asiye na vitu hivyo. Maisha ya maskini ni magumu ili hali maisha ya tajiri ni ya raha mustarehe. Utajiri unapotajwa kuwa wa kupindukia maana yake ni utajiri mkubwa kupita kiasi. Umaskini ndio wa kutupwa kwa maana ya kwamba umezidi viwango na hakuna ambaye anautaka kwa utashi wake. “Kuona cha mtema kuni” Waandishi kwa sasa wanabadilisha maneno katika msemo huu; badala ya kuona cha mtema kuni sasa wanasema “kuona cha moto”.Mtema kuni ni mtu anayepasua vitu kama magogo au miti. Kazi hii ni ngumu na inahitaji kutumia nguvu nyingi. Msemo huu unatumiwa kumwasa mtu anayetenda kinyume na inavyotakiwa. Maneno haya hutumiwa kumtahadharisha asije kuingia katika shida, taabu au misukosuko. Aidha, mtu akisema amekiona cha mtema kuni maana yake ameshuhudia shida na adha nyingi zilizomsabibishia athari kiakili na kimwili.“Toka nje” Matumizi ya kifungu hiki cha maneno yamekuwa yakikosewa kila mara. Wanajamii hutumia maneno haya kumwamuru mtu aliye ndani kutoka nje. Hata hivyo katika uhalisia na kwa mantiki ya lugha mtu anayeambiwa atoke nje huwa yuko ndani. Hivyo, basi alipaswa kuambiwa “toka ndani” ikimaanisha kuwa anatakiwa kwenda nje.Lakini kwa mtu anayeambiwa atoke nje maana yake ni kwamba aingine ndani. Kosa hili si la waandishi bali ni la watumiaji wa lugha ya Kiswahili kwa ujumla wao. Ushauri ni kwamba jamii ibadilike kwa kutathmini mantiki ya kinachozungumzwa. Tuangalie mifano ya misemo michache inavyotumiwa na waandishi:o Real Madrid yakiona cha moto.o Naibu waziri atema cheche.o Carragher ampigia debe Rashford Man United.o Akoleza moto mku tano wa TFF.Tuhitimishe makala haya kwa kuwataka waandishi wa habari kujali zaidi usanifu na ufasaha wa lugha. Pia, wanaweza kutumia mtindo wa kiuandishi lakini wakizingatia usanifu wa lugha. Aidha, pale wanapotumia misemo au kubadilisha maana ya msingi ya neno basi watumie alama za mnukuo. Mwandishi wa makala haya ni mwanafunzi wa mwaka wa pili shahada ya awali ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Yuko BAKITA kwa mazoezi ya vitendo). | 1kitaifa
|
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa niaba ya Serikali ya Tanzania imetoa msimamo wake kwa jumuiya ya kimataifa kuhusu kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda siku za hivi karibuni.Wizara umeieleza jumuiya ya kimataifa, vyombo vya habari vya nje na ndani kuwa alichokianzisha RC Makonda si msimamo wa serikali bali ni wa kwake binafsi.Serikali imetumia fursa hiyo kueleza jumuiya hiyo kuwa Tanzania itaendelea kuheshimu mikataba ya kimataifa ambayo imeiridhia.“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kulinda haki kama zilivyoanishwa katika katiba yake,” inamalizia taarifa ya Wizara hiyo. | 1kitaifa
|
WADAU wa Maendeleo nchini kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo katika Sekta za Umma wameitikia wito wa serikali na kujitokeza kufanikisha kazi ya uimarisha mfumo wa uendeshaji wa shughuli za afya katika maeneo yote ya kutolea huduma za afya serikalini.Wadau hao wameitika wito kufutia maelekezo ya serikali kutaka mfumo huo uimarishwe kwa kuongezewa maeneo ya kiutendaji.Akizungumza na wadau hao wa maendeleo jana, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Zainab Chaula, wakati wa kikao cha pamoja baina ya Wizara hiyo na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ORTAMISEMI) alisema umefika muda kwa wadau kuungana na kujenga mfumo wa GoTHOMIS, kwani mfumo huo umeonesha kuwa na tija na ufanisi kwenye nyanja ya afya.“Kwa Muda mrefu tumeshuhudia mifumo mbalimbali lakini yote hii ikiwa kwenye maeneo machache ya nchi ikifanywa kwa majaribio ambayo hata hivyo tija yake imekuwa sio yakuridhisha… suala la kutuambia unafanya shughuli ya jamii halafu hatuoni tija ya unacho kifanya sio wakati wake kwa sasa, lazima wote tuungane na tukubali kutembea kwa pamoja na mfumo huu ambao umeonesha tija na ufanisi,” alisema.Wito wa Katibu Mkuu huyo, ulikuja wakati ambapo tayari mfumo ulikuwa umesimikwa kwenye maeneo yakutolea huduma za afya yapatayo 383 ikiwepo zahanati 91, vituo vya afya 180, Hospitali Teule za Wilaya 12, Hospitali za Wilaya 77 na Hospitali za Rufaa za Mikoa 23 na kufanya asilimia sita ya maeneo yote yakutolea huduma za afya nchini.Akiwasilisha mada katika kikao hicho juu ya uboreshaji wa mfumo wa GoTHOMIS, Mkurugenzi wa TEHAMA, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Erick Kitali amesema shabaha iliyo mbele yao ni kuimarisha mfumo kwa kutumia wataalam wazawa na wanaamini katika nguvu ya pamoja ikiwepo kushirikiana na wadau wa maendeleo wote.Akizungumza mbele ya wataalam wanaoendelea na kazi ya uimarishaji wa mfumo huo mkoani Morogoro, Mtaalam kutoka Global Supply Chain Tanzania, Alfredy Mchau alisema wamewiwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha mfumo huo wa GoTHOMIS kwani ni moja ya vipaumbele vyao katika kushirikiana na serikali kuboresha huduma za afya kwa ajili ya upatikanaji wa taarifa sahihi na kwa wakati.“Alipotoa wito Katibu Mkuu, kwa wadau juu ya kuunga mkono suala hili, sisi kama Global Supply Chain Technical Assistance Tanzania (GHSC TA – TZ), tulielewa nini dhamira ya Serikali katika sekta ya afya, ambayo kimsingi ndio msingi wa maendeleo ya nchi yoyote,” alisema.Mmoja wa wafanyakazi kutoka mradi wa kuimarisha Mifumo ya Sekta za Umma nchini PS3, Revocutus Mtesigwa alisema huo ni muendelezo wa juhudi ambazo wamekuwa nazo hususan katika uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma nchini.Serikali bado inaendelea kuwakaribisha wadau wa maendeleo kujitokeza kwa ajili ya kufanikisha uboreshaji wa Mfumo wa GoTHOMIS, ambao utakuwa madhubuti na wenye tija katika ngazi zote za kutolea huduma za afya nchini. | 1kitaifa
|
MANENO SELANYIKA Na MAMII MSHANA (Tudarco)–Dar es Salaam ALIYEKUWA Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, amejitosa kuwatetea ndugu watatu wa kiume kutoka familia moja wanaokabiliwa na tuhuma za mauaji ya dada yao. Tendwa ambaye kwa sasa ni wakili wa kujitegemea, anawatetea watuhumiwa hao ambao ni Robert Bugaisa, Richard Bugaisa na Godfrey Bugaisa. Watuhumiwa hao walifikishwa juzi katika Mahakama ya Kinondoni mbele ya Hakimu, Boniphace Lihamwike, Wakili wa Serikali Tumaini Mfikwa, aliomba tarehe nyingine kwa kutajwa kwa sababu upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika. “Mheshimiwa PI kesi namba 14/2016 watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama yako wanakabiliwa na shtaka la mauaji, lakini bado jalada la kesi hii lipo kituo cha polisi kwa uchunguzi wa tukio hilo,” alidai Wakili Tumaini. Wakili wa utetezi, Tendwa alidai kwamba hana pingamizi dhidi ya maelezo ya upande wa mashtaka yaliyowasilishwa mahakamani hapo. Naye Hakimu Lihamwike, alisema kwa mujibu wa sheria mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kwamba pindi upelelezi utakapokamilika kesi hiyo itahamishiwa Mahakama Kuu. Hivyo mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28, mwaka huu itakapokuja kwa kutajwa. Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo, imedaiwa kuwa Julai 26, mwaka jana saa 4 usiku maeneo ya Boko CCM, marehemu Selina aliingiliwa na watu wasiojulikana na kuuawa. | 1kitaifa
|
Na LILIAN JUSTICE, MVOMERO
WANANCHI wa vijiji vya Kunke na Mlumbilo wilayani Mvomero, mkoani Morogoro, wamemuomba Rais Dk. John Magufuli kuwasaidia ili wabakie kwenye maeneo yao.
Hatua hiyo imetokana na agizo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kutoa tamko la kuwataka kuhama ifikapo Agosti 30, mwaka huu, kwa kile kinachodaiwa kuvamia msitu wa hifadhi.
Wananchi hao walitoa ombi hilo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika vijiji hivyo na kutoa kilio chao mbele ya Diwani wa Kata ya Mtibwa, Lucas Mwakambaya.
Baadhi ya wananchi hao, Hassan Suleman, mkazi wa Kitongoji cha Mafleta B –Pagale alisema kuna waraka umesambazwa kuwataka wajiandae kuhama kwa madai wamevamia msitu wa hifadhi wa Pagale.
“Tumekaa hapa muda mrefu kabla ya msitu wa hifadhi kuwekewa mipaka mwaka 1952 na wakoloni, tunashangaa kuambiwa tuhame bila ya kuitishwa mkutano kuelezwa rasmi,” alisema Suleman.
Naye Enedius Mpesa, mkazi wa Kitongoji cha Masangarawe, Kijiji cha Mlumbilo, alisema wanatekeleza agizo la Rais Dk. Magufuli la kutoitegemea Serikali kuwapa msaada.
Naye Diwani Mwakambaya aliwaomba wawe watulivu kwa sababu Serikali ni sikivu na jambo hilo linatafutiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake, Meneja Hifadhi ya Misitu Wilaya ya Mvomero (TFS), Husna Msagati, alipoulizwa kuhusu sakata hilo aliwaondoa hofu wananchi hao kuwa wao hawana lengo la kumfukuza mwananchi, bali wanatekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, la kuhakikisha maeneo ya hifadhi za misitu yanapimwa. | 1kitaifa
|
Kulwa Mzee -Dar es salaam MHASIBU Wizara ya Afya, Luis Lymo (54) na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
Christian Social Services Commission, Peter Maduki (61), wamefikishwa mahakamani
wakikabiliwa na mashtaka 280 yakiwamo ya wizi na kutakatisha Sh bilioni 1.7. Washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Dar es Salaam jana na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,
Augustina Mmbando. Walisomewa mashtaka hayo na mawakili wa Serikali, Zakaria Ndaskoi
akisaidiana na Genes Tesha. Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 150 ya kughushi, 128
kuiwasilisha nyaraka za uongo, wizi shtaka mmoja na kutakatisha fedha shtaka
moja. Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya mwaka 2017 na 2019 ndani ya Jiji
la Dar es Salaam. Katika mashtaka hayo, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kughushi
hundi mbalimbali na kuzisaini kwa jina
la Upendo Mwingira bila ridhaa yake, huku wakijaribu kuonyesha kuwa mshtakiwa
Luis Lymo alikuwa akilipwa fedha hizo kama kamisheni na Taasisi ya Christian
Social Services Commission wakati si kweli. Katika mashtaka ya kuwasilisha nyaraka za uongo, washtakiwa wanadaiwa
kuwasilisha hundi mbalimbali walizoghushi katika Benki ya Standard Chartered. Inadaiwa washtakiwa hao kwa nyakati tofauti waliandaa taarifa ya fedha
ya uongo (bank statement), wakionyesha akaunti namba 01080002404200 iliyopo
katika Benki ya Standard Chartered, NIC Life House ilikuwa na zaidi ya Sh
bilioni 1.7 wakati wakijua ni uongo. Katika shtaka la wizi, kati ya Machi 30 mwaka 2017 na Oktoba 2018
katika benki hiyo, washtakiwa wanadaiwa waliiba zaidi ya Sh bilioni moja mali
ya Taasisi ya Christian Social Services Commission. Kwa upande wa shtaka la utakatishaji fedha, washtakiwa hao wanadaiwa
kutakatisha zaidi ya Sh bilioni moja wakati wakijua fedha hizo zilitokana na
zao la kosa la kughushi. Washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo
haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi. Shtaka la utakatishaji wa fedha halina dhamana, hivyo washtakiwa
walipelekwa rumande hadi Januari 20, kesi yao itakapotajwa. | 1kitaifa
|
NA ASIFIWE GEORGE SHINDANO la shika ndika linaloendeshwa na Redio EFM litaanza kuchezeshwa kesho. Ofisa Habari wa EFM, Aneth Mrindoko, alisema shindano hilo litawahusisha wakazi wa Dar es Salaam katika Wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni pamoja na wakazi wa Mkoa wa Pwani katika Wilaya ya Bagamoyo na Kibaha. “Mwaka huu EFM inalisongesha kwa kutoa zawadi ya magari mawili aina ya Suzuki carry pamoja na pikipiki aina ya boxer ili kuendelea kuwa karibu na wasikilizaji wake kama ilivyotoa zawadi ya gari mwaka jana. “Washiriki 40 kutoka kila wilaya watatakiwa kushiriki nusu fainali na baadaye washiriki 10 watakaopita watapata nafasi ya kushiriki katika fainali za mwisho kutoka kila wilaya na hatimaye washindi wawili wa kwanza mwanamke na mwanamume wataibuka na ndinga na wengine kuibuka na pikipiki. “EFM Redio hufanya shindano hili kwa lengo la kuwawezesha wasikilizaji wake kuongeza na kukuza kipato kitakachochangia kuimarisha maisha. | 4burudani
|
VATICAN CITY, VATICAN KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, anasema anatambua kwamba anaweza kuwa mlengwa wa shambulio la kigaidi, lakini ataendelea na ziara zake bila ya kutumia mavazi na magari ya kiusalama yenye kuzuia risasi kwa sababu anataka kuwa karibu na watu. Hii ni kwa mujibu wa maelezo katika utangulizi wa kitabu chake kipya, ambacho kimeandikwa na mwandishi wa Italia Andrea Tornielli. Tofauti na watangulizi wake waliotumia mavazi na magari ya kiusalama, Papa Francis hutumia mavazi na magari ya kawaida katika ziara zake nje. Kitabu hicho kiitwacho ‘Kusafiri’, kinahusu ziara 17 ambazo Papa Francis amefanya katika nchi zaidi ya 25 tangu achukue wadhifa huo mwaka 2013. Francis amesema anafahamu hatari zilizopo, lakini hana woga kumhusu bali kwa wanaosafiri naye na zaidi wale anaokutana nao katika nchi mbalimbali. ‘Daima kuna hatari kutoka kwa kichaa, lakini Bwana daima yupo kwa ajili yetu.” Papa, anatarajia kufanya safari mbili za kimataifa mwaka huu, moja nchini Ureno, nyingine India na Bangladesh. Alisema: “Nafahamu fika hitaji la usalama na ninashukuru wanausalama, lakini askofu ni mchungaji, baba, hivyo hapaswi kuwa na vikwazo vingi baina yake na watu.” ‘Kwa sababu hii nilishaweka wazi tangu mwanzo kuwa nitakuwa tayari kusafiri pale tu nitakapoweza kuonana na watu.” Kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, polisi wa Italia wameongeza ulinzi eneo kuzunguka Vatican, taifa huru lililopo katikati ya Rome, kufuatia mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wenye itikadi kali Ulaya. | 3kimataifa
|
UTUMIKISHWAJI wa watoto wa kike ili kusaidia familia, umaskini, mazingira magumu kwenye shule, mimba za utotoni ni miongoni mwa sababu zinazowafanya wasichana kuacha shule katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.Akizungumza wakati wa mahojiano jana, Mratibu wa Programu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED), Luhaga Makunja alisema kuna idadi kubwa ya wasichana wanaoacha shule kutokana na sababu mbalimbali.Alisema shirika hilo lilikuwa likitekeleza mradi wa kutatua changamoto za unyanyasaji wa kijinsia katika elimu ya msichana ambapo eneo la mradi lilikuwa kata nne za Chibelela, Mapanga, Mtitaa, Mwitikila na Chipanga. Alisema mradi huo ulilenga watoto wetu umri kuanzia tisa hadi 19 ambao wako shuleni."Ukatili mkubwa tuliouona ulikuwa ni kuachishwa masomo kutokana na mimba za utotoni," alisema.Alisema kulingana na takwimu walizopata kutoka Idara ya Elimu wasichana 3,179 walioanza shule 2013 miongoni mwao 1,238 hawakumaliza kidato cha nne mwaka 2017 ambapo ni asilimia 39 sababu kubwa ikiwa ni mimba za utotoni.Makunja alisema tulikuwa na wasichana kutumikishwa kazi za majumbani ambapo wasichana wamekuwa wakiachishwa shule na kwenda mijini kufanya kazi za ndani kusaidia familia."Bado kuna mila na desturi ambazo hazioni thamani ya mwanamke kwenye elimu hata inapofikia umri wa mtoto kuandikishwa shule suala la kusoma linaokana sio muhimu," amesema.Makunja amesema umasikini, utumikishwaji wa watoto kusaidia familia, mazingira magumu shuleni kutokana na umbali kutoka makazi Hadi shuleni inaonekana ni kikwazo cha elimu kwa mtoto wa kike."Kuna wanafunzi wanalazimika kwenda kupanga vijijini ili wawe karibu na shule, wanakosa ulinzi wa wazazi na kujikuta wakiingia kwenye ngono na hivyo wengi hujikuta wakikatisha masomo kutokana na ujauzito," alisema.Pia amesema mazingira magumu ya nyumbani hupelekea watoto kufika shule wakiwa hawajala huku akitembea umbali mrefu kufika shuleni."Anatoka nyumbani hajala anakaa muda mrefu na njaa, hata masomo haelewi vizuri anajua atafeli tu alishakata tamaa anaona amalize tu shule," amesema.Makunja amesema ukosefu wa mabweni na chakula unasababisha watoto kutoshawishika kwenda shuleni.Alisema kumekuwa na mtazamo hasi wa wazazi na walimu juu ya elimu kwa wasichana."Jitihada kubwa zinahitajika kuhakikisha elimu inatolewa ili kupunguza unyanyasaji wa kijinsia unaosababisha wasichana kukosa elimu,” alisema.Pia amesema wasichana wengi walikuwa hawashiriki katika maamuzi hata kwenye mipango ya shule na vijiji.Aidha alisema msichana akipata mimba kuna mtazamo hasi kwa jamii inabidi atoroke kwenda mbali kuepuka adha ya matusi hata kipigo.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa MED, Davis Makundi alisema kuna umuhimu mkubwa juu ya ujenzi wa mabweni. | 1kitaifa
|
NEW YORK MAREKANI MKALI wa filamu nchini Kenya, Lupita Nyongo, amepania kufanya makubwa kwa mwaka 2016 ili kuweza kutangaza jina lake zaidi. Mrembo huyo ambaye aliwahi kuchukua Tuzo ya BET mwaka 2014 na Tuzo za Oscar mwaka 2015, amekuwa akifanya vizuri katika filamu na sasa amekuja kivingine katika filamu mpya ya ‘Star War’. “Ninahitaji kufanya makubwa kwa mwaka 2016 hasa katika maisha ya filamu, najua kwamba kuna ushindani wa hali ya juu lakini natakiwa kupambana ili kuzidi kutangaza jina langu zaidi ya miaka iliyopita. “Yote yanawezekana kikubwa ni kujipanga vya kutosha ili kuhakikisha natimiza malengo yangu, watu wanasema ninafanya vizuri lakini kwa upande wangu ninasema kuwa bado nina safari ndefu,” alisema Lupita | 4burudani
|
TURIN, ITALIA MAMA wa Cristiano Ronaldo, Maria Dolores Aveiro, amekanusha taarifa kwamba, alimtaka staa huyo kurudi katika klabu ya zamani ya Manchester United mara baada ya kumalizana na Real Madrid. Kuna baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari jijini Manchester, vilitoa taarifa kwamba mama wa mchezaji huyo anamtaka mwanaye kurudi viwanja vya Old Trafford katika klabu yake ya zamani ya Man United ikifikia hatua ya kumalizana na Madrid. Kwa sasa mchezaji huyo tayari amejiunga na klabu ya Juventus, hivyo mama yake amefunguka kwa mara ya kwanza na kudai hakuwahi kusema lolote juu ya mchezaji huyo kurudi katika klabu yake ya zamani. “Ni uongo kwamba niliwahi kusema kuwa nataka mwanangu arudi katika klabu yake ya zamani ya Manchester United, kila siku nimekuwa nikifurahia maamuzi yake. “Familia kwa ujumla tuna furaha kutokana na maamuzi yake, ninaamini mtoto wangu atafanya makubwa. Haya ni maisha yake mapya, alikuwa na furaha wakati yupo Real Madrid, lakini sasa ameamua kutafuta changamoto nyingine,” alisema mama wa staa huyo. Ronaldo mwenye umri wa miaka 33, ameondoka Real Madrid baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka tisa, huku akichukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mara nne pamoja na kuwa kinara wa mabao ndani ya klabu hiyo huku akiwa na jumla ya mabao 450 katika michezo 438 aliyocheza. Wakati anakipiga katika klabu ya Man United, aliweza kuweka historia ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara tatu na kutajwa kuwa mmoja wa wachezaji bora duniani. | 2michezo
|
Anna Potinus-Dar Es Salaam Licha ya rais Dk John Magufuli kutoa zawadi ya viwanja vya kujengea
nyumba Mkoani Dodoma kwa wachezaji, viongozi wao na bondia Hassan Mwakinyo kama
ishara ya kuonyesha furaha yake kwa Tanzania kufuzu kushiriki mashindano ya
Mataifa ya Afrika pia amempa zawadi nyingine mchezaji wa zamani wa Taifa Stars,
Peter Tino. Peter Tino ambaye ndiye alifunga goli pekee lililoiwezesha Tanzania
kufuzu mashindano hayo kwa mara ya kwanza mwaka 1980 amepewa zawadi ya Sh
5milioni kwa ajili ya kumsaidia kufanyia biashara zitazomuwezesha kuendesha
maisha yake. “Kwa nafasi ya kipekee labda nimuombe Tino aje hapa mbele aseme kitu kwa
ajili ya wenzake, na anaweza akatueleza changamoto maana tulikuwa tukisikia tu
Peter Tino, Peter Tino,” amesema Dk Magufuli akimkaribisha kuzungumza. Naye Peter Tino amewapongeza watanzania kwa kuivusha kushiriki
Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa mara nyingine tangu mwaka 1980. Baada ya Peter Tino kuzungumza na wananchi, Dk Magufuli alitaka kufahamu
shughuli anayofanya na baada ya kumweleza akamtaka ataje kiasi cha fedha
anachotaka lakini mwenyewe akataka afikiriwe na rais. JPM: “Unafanya shughuli gani?” Peter Tino: “Najishughulisha na uuzaji wa vifaa vya michezo?” JPM: “Kwa hiyo wewe ulikuwa unataka nini?” Peter Tino: “Nilikuwa nahitaji kiasi hivi?” JPM: Kama shilingi ngapi?” Peter Tino: “Unifikirie tu kama rais” JPM: “Kuna katibu hapa! Ebu mtafutie shilingi milioni tano huyu mzee ili
akakuze mtaji wake”. | 2michezo
|
Mohamed Hamad, Kiteto Shirika la Ujamaa Community Resouce Team (UCRT), lenye makao yake makuu mkoani Arusha, limeikabidhi hospitali ya Wilaya ya Kiteto vifaa vya kujinginga na maambukizi ya ya virusi vya corona kama njia ya kuisaidia serikali kuhudumia jamii Vifaa hivyo vimetajwa kuwa na thamani ya Sh milioni nne moja ambavyo vitatumika katika mapambano dhidi ya virusi vya corona ambapo imeelezwa kuwa serikali na wadau wameamua kuungana katika vita hivyo ili kunusuru wananchi wake. Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Pascal Mbota akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa hivyo amesema msaada huo umefika wakati muafaka ambao hospitali ina uhaba mkubwa wa vifaa hivyo. “Kila siku natumia laki mbili kwa ajili ya kununua Baracoa, hakuna mtumishi anayekubali kutibu mgonjwa bila kuchukua tahadhari, kwahiyo tuna uhitaji mkubwa sana wa vifaa hivi hasa katika wakati huu,”alisema Mbota. Akikabidhi vifaa kwa niaba ya shirika hilo, Mwanasheria wa shirika la Ujamaa Community Resource Team, Edward Ole Kaita alivitaja kuwa ni baracoa, madumu ya kunawia mikono, sabuni na vitakasa mikono. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona katika makabidhiano hayo naye alisema kutokana na uhaba wa vifaa katika hospitali hiyo waliomba wadau mbalimbali ili kukabiliana na ugonjwa hatari wa Corona. “Tunaomba mashirika mengine zaidi yajitokeze kutusaidia hasa katika kipindi hiki..hawamsaidii mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi bali watakuwa wameisaidia jamii ya Kiteto bado tuna changamoto kubwa,”alisema Kambona. | 1kitaifa
|
Dataset Card for Swahili : News Classification Dataset
Dataset Summary
Swahili is spoken by 100-150 million people across East Africa. In Tanzania, it is one of two national languages (the other is English) and it is the official language of instruction in all schools. News in Swahili is an important part of the media sphere in Tanzania.
News contributes to education, technology, and the economic growth of a country, and news in local languages plays an important cultural role in many Africa countries. In the modern age, African languages in news and other spheres are at risk of being lost as English becomes the dominant language in online spaces.
The Swahili news dataset was created to reduce the gap of using the Swahili language to create NLP technologies and help AI practitioners in Tanzania and across Africa continent to practice their NLP skills to solve different problems in organizations or societies related to Swahili language. Swahili News were collected from different websites that provide news in the Swahili language. I was able to find some websites that provide news in Swahili only and others in different languages including Swahili.
The dataset was created for a specific task of text classification, this means each news content can be categorized into six different topics (Local news, International news , Finance news, Health news, Sports news, and Entertainment news). The dataset comes with a specified train/test split. The train set contains 75% of the dataset and test set contains 25% of the dataset.
Supported Tasks and Leaderboards
[More Information Needed]
Languages
The language used is Swahili
Dataset Structure
Data Instances
A data instance:
{
'text': ' Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema, itafanya misafara ya kutangaza utalii kwenye miji minne nchini China kati ya Juni 19 hadi Juni 26 mwaka huu.Misafara hiyo itatembelea miji ya Beijing Juni 19, Shanghai Juni 21, Nanjig Juni 24 na Changsha Juni 26.Mwenyekiti wa bodi TTB, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.“Tunafanya jitihada kuhakikisha tunavuna watalii wengi zaidi kutoka China hasa tukizingatia umuhimu wa soko la sekta ya utalii nchini,” amesema Jaji Mihayo.Novemba 2018 TTB ilifanya ziara kwenye miji ya Beijing, Shanghai, Chengdu, Guangzhou na Hong Kong kutangaza vivutio vya utalii sanjari kuzitangaza safari za ndege za Air Tanzania.Ziara hiyo inaelezwa kuzaa matunda ikiwa ni pamoja na watalii zaidi ya 300 kuja nchini Mei mwaka huu kutembelea vivutio vya utalii.',
'label': 0
}
Data Fields
text
: the news articleslabel
: the label of the news article
Data Splits
Dataset contains train and test splits.
Dataset Creation
Curation Rationale
[More Information Needed]
Source Data
Initial Data Collection and Normalization
[More Information Needed]
Who are the source language producers?
[More Information Needed]
Annotations
Annotation process
[More Information Needed]
Who are the annotators?
[More Information Needed]
Personal and Sensitive Information
[More Information Needed]
Considerations for Using the Data
Social Impact of Dataset
[More Information Needed]
Discussion of Biases
[More Information Needed]
Other Known Limitations
[More Information Needed]
Additional Information
Dataset Curators
[More Information Needed]
Licensing Information
Creative Commons Attribution 4.0 International
Citation Information
@dataset{davis_david_2020_5514203,
author = {Davis David},
title = {Swahili : News Classification Dataset},
month = dec,
year = 2020,
note = {{The news version contains both train and test sets.}},
publisher = {Zenodo},
version = {0.2},
doi = {10.5281/zenodo.5514203},
url = {https://doi.org/10.5281/zenodo.5514203}
}
Contributions
Thanks to @yvonnegitau for adding this dataset.
- Downloads last month
- 140