content
stringlengths 1k
24.2k
| category
stringclasses 6
values |
---|---|
WAZIRI wa Madini, Doto Biteko amewaonya wamiliki wa migodi ya tanzanite Mirerani kwa fedha kidogo wanazochangia za kodi, na kusisitiza kuwa wasipolipa kodi hiyo, rungu litakapowafikia halitowaacha salama.Aidha, waziri huyo amebainisha kuwa mpaka sasa serikali imefuta leseni 12,000 za migodi baada ya kushindwa kulipa kodi halali ya migodi hiyo ya kila mwaka.Biteko aliyasema hayo baada ya kupokea taarifa ya Kamati aliyounda ya kutatua mgogoro wa mipaka (mitobozano) kati ya Kampuni ya Tanzanite One inayomiki kitalu C na wachimbaji wadogo wanaochimba vitalu A,B na D.Aliwataka wamiliki wa migodi ya tanzanite iliyopo Mirerani kulipa kodi halali ya serikali kwani rungu litakapofika halitamwacha mtu salama .Alisema inasikitika kuona katika mgodi yote ya tanzanite katika eneo hilo la Mirerani ni Sh bilioni 2.8 tu zinalipwa hali ambayo hairidhishi ambapo alibainisha kuwa kuna uwezekano wa wamiliki wengine wa migodi hiyo kutolipa kodi halali ya serikali.Waziri alisema kule mkoani Mara mgodi mmoja tu ndio unaweza kulipa zaidi ya Sh bilioni 4.5 kwa miezi sita achilia mbali migodi mingine.“Nawaagiza mlipe mara moja kodi hizi kihalali kabla hatujawafutia leseni, kiasi hiki cha kodi kinachokusanywa hapa Mirerani ni aibu,” alisisitiza.Akizungumzia mapendekezo ya mipaka, alisema mapendekezo zaidi ya 15 ya ripoti ya mitobozano yatafanyiwa kazi kwani serikali ya sasa haina mzaha katika mambo ya msingi hususani migogoro ya wachimbaji madini na wawekezaji.Waziri alisema kumekuwa na kamati nyingi ziliundwa huko nyuma zaidi ya tisajawahi kufanyiwa kazi lakini kamati hiyo mapendekezo yake hayatawekwa kabatini kwani yatafanyiwa kazi mara moja bila kuonea mtu.“Nimepokea taarifa ya kamati hii na naenda kuifanyia kazi kisha majibu mtapewa ila nauliza kwanini hapa Mirerani mnakuwa na maneno mengi kuliko migodi mingine, kama kusema watu wanasemwa sana acheni chuki fanyeni kazi maana serikali inawapenda wachimbaji wote,” alisema.Naibu Waziri wa Madini, Stanlaus Nyongo alisema serikali inaendelea kusimamia rasilimali za taifa na alitoa rai kwa watanzania kuacha tabia ya kutorosha tanzanite na kutotoa rekodi za uuzaji na uwekaji wa rekodi zake kwa makusudi. | uchumi |
SERIKALI ya Kenya inatarajia kuanza utekelezaji wa sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu uingizaji wa magari kutoka nje.Sheria ya jumuiya hiyo inazitaka nchi wanachama, kutoingiza magari kutoka nje yenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea. Wakati Kenya ikichukua maamuzi hayo, Tanzania inaendelea kutekeleza sheria yake ya kuzuia magari chakavu yenye umri wa miaka minane na zaidi. Sheria hiyo imeweka adhabu kwa gari lolote litakaloingizwa likiwa na miaka kuanzia minane na kuendelea, kuwa lazima mmiliki alipe kodi ya uchakavu.Kwa mujibu wa Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ben Usaje alisema magari mapya yenye umri chini ya miaka saba, hayalipiwi kodi ya uchakavu. “Huo ni utaratibu wetu wa sheria ya kodi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Usaje. Uamuzi wa Kenya ulitangazwa na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Kenya, Peter Munya, mjini Mombasa hivi karibuni. Munya alitaja sababu ya kuchukua hatua hiyo kuwa ni kufanya Afrika Mashariki kuwa mahali salama na sio jalala la magari chakavu.Munya alisema sera hiyo ambayo itayahusu magari yote yenye injini yenye uwezo wa zaidi ya 1500 cc, itaanza kutekelezwa Julai Mosi mwaka huu na umri huo utapungua zaidi hadi miaka mitatu kufikia mwaka 2020. Maamuzi hayo ya serikali ya Kenya ni katika kutimiza masharti na maelekezo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo imeweka umri wa magari yote kutoka nje kuwa ni miaka mitano hadi kufika mwaka 2021.Lengo kuu la sera hiyo katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kulinda soko la Afrika Mashariki, ili lisiwe jalala la magari chakavu na pia kulinda viwanda vya ndani vya uzalishaji wa magari kwa baadhi ya nchi wanachama. Kwa mujibu wa taarifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutokuwepo kwa sera mahususi ya kuweka vigezo na masharti ya uingizaji wa magari, kulihatarisha soko la jumuiya hiyo kujaa magari makuukuu na kudhoofisha ukuaji wa viwanda vya magari ndani ya Afrika Mashariki.Kwa sasa nchini Kenya sheria ya uingizaji wa magari kutoka nje, inasisitiza umri wa magari hayo kuwa ni miaka isiyo chini ya minane. Ikiwa sheria mpya itaanza kutekelezwa katika muda uliopangwa, waagizaji wa magari hawana budi kuagiza magari yaliyotengenezwa sio zaidi ya mwaka 2013. Kana kwamba hiyo haitoshi, waagizaji wa magari kutoka nje watalazimika kuwa na cheti cha ubora wa gari kulingana na barabara zilizopo katika nchi yanapopelekwa. Katika hatua hiyo, Shirika la Viwango la Kenya (KBS), litakuwa na mawakala wake katika nchi yanakotoka magari hayo kwa ajili ya ukaguzi.“Tunataka kufikia katika umri wa miaka sifuri yaani itafikia hatua waagizaji wa magari watalazimika kuagiza magari yaliyotengenezwa mwaka huo huo na kuingia sokoni. Serikali itapata fedha zake na itashawishi ukuaji wa viwanda vya ndani,” alisema Munya. Baadhi ya viwanda vya ndani katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, vimesema sheria hiyo itasaidia katika ukuaji wake.Mfano Kiwanda cha Mobius Motors cha mjini Nairobi, kimesema kimepata oda ya magari 300. Kuna uhakika wa asilimia mia moja kwamba ahadi hiyo itatimizwa kutokana na sera ya umri wa magari. Kiwanda hicho kinazalisha magari yenye uwezo tofauti tofauti. Kwa mfano magari yenye uwezo wa 1800cc, yanauzwa kati ya shilingi za Kenya milioni 1.3 na shilingi milioni 158 ikiwa na kodi ndani yake.Kwa mujibu wa waziri Munya, magari yote yenye uwezo wa chini ya 1500cc hayatahusika katika sheria hiyo ili kuwapa nafuu wananchi wa hali ya chini, ambao hawawezi kununua magari hayo kwa bei kubwa. Kenya bado ni muagizaji mkubwa wa magari kutoka nchi za Mashariki ya mbali, ingawa inazalisha magari ya biashara kama vile mabasi na pick-ups. Kwa mujibu wa Shirika la Takwimu nchini Kenya (KNBS), nchi hiyo ilisajili magari 1031 aina ya Saloon mwezi Julai 2018, ikilinganishwa na magari 641 yaliyosajiliwa mwezi Agosti mwaka huo huo wa 2018.Kwa upande wa Uganda, sheria inayosimamiwa na kutekelezwa na Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA), inakataza uingizwaji wa magari yenye umri wa zaidi ya miaka kumi na tano na zaidi. Inatakiwa hadi kufikia mwaka 2021 magari yatakayoingizwa nchini humo yatakuwa na umri wa chini ya miaka mitano. Awali, Bunge la Uganda lilipendekeza muswada wa sheria, unaotaka kikomo cha umri wa magari kuwa miaka nane. Lakini, katika mjadala wake asilimia kubwa ya wabunge waliukataa muswada huo, wakisema Waganda hawataweza bei ya magari hayo. | kitaifa |
Meneja wa kiwanda hicho, Pratap Disodya aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kiwanda hicho hakina sababu ya kuficha sukari kwa kuwa kina uwezo wa kuzalisha tani 300 hadi 500 kwa siku.Alisema pamoja na uzalishaji huo unaochangiwa na upungufu wa miwa kutoka kwa wakulima, kiwanda hicho pia kinalazimika kufungwa kila mwaka ifikapo Desemba hadi Juni kusubiri uzalishaji uanze Juni.Alisema katika kuitikia agizo la Rais John Magufuli la kuwataka wafanyabiashara wote walioficha sukari katika maghala yao kuanza kusambaza mara moja vinginevyo serikali itachukua hatua kali, kiwanda hicho kimethibitisha kutokuwa na akiba ya kutosha ya sukari inayozalishwa kiwandani hapo.Alisema wakulima wakihimizwa kuzalisha miwa kwa wingi uzalishaji utaongezeka na kupunguza uhaba wa sukari nchini. Disodya alisema tangu kuanzishwa kwa kiwanda hicho mwaka 2005 na kuanza uzalishaji mwaka 2007, kimezalisha tani 150 mwaka 2013 pekee.Alisema hatua walizochukua ni pamoja na uongozi wa kiwanda kuendelea kuwahamasisha wakulima wadogo zaidi ya 1,500 kuongeza uzalishaji wa miwa kwa kuwapatia mikopo. | uchumi |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amewataka watanzania kuendelea kuishi katika umoja na mshikamano kama nguzo kuu ya maendeleo nchini.Rais ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam katika hafla ya mashindano maalumu ya usomaji wa Quran barani Afrika yanayoandaliwa na taasisi ya Al-Hikma yaliyofanyika uwanja wa Taifa.Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali, kitaifa na kimataifa akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu awamu ya nne Jakaya Kikwete, Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Waziri kutoka Saudi Arabia, Sheikh Saleh Bin Abdulaziz Alsheikh, Mabalozi wa nchi mbalimbali wajumbe wa Baraza la Mawaziri, na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.Akihutubia umati uwanjani hapo Rais Magufuli amewataka watanzania kuendelea kuishi kwa amani na mshikamano kwa kuwa masuala ya dini yanamgusa kila mtu huku akiwatakia waumini wa kiislamu kuendelea na mfungo wa ramadhani kwa amani.“Kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya serikali, naomba kuendelea kuwatakia kheri ya mfungo waumini wote wa dini ya kiislamu uwe wa amani” amesema RaisAkielezea changamoto ambazo zinapatikana katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Rais Magufuli, ameelezea suala la upandishaji wa bei za bidhaa na kuwataka wafanyabiashara kuacha tabia hiyo kwa kuwa ni kinyume na mapenzi ya Mungu.“Ninawasihi sana watu wa aina hiyo kuacha kufanya hivyo… huwezi kutajirika kwa kutegemea kupandisha bei za bidhaa katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Nitoe wito kwa mamlaka husika za serikali kufuatilia jambo hili kwa ukaribu zaidi” amesema Rais Magufuli.Rais Magufuli pia ameelezea juu ya uhusiano mkubwa uliopo baina ya serikali ya Saudi Arabia na Tanzania huku akiweka wazi mipango mbalimbali iliyofikiwa baina ya nchi hizo ikiwemo ujenzi wa chuo cha kiislamu nchini.Sambamba na hilo ametoa maagizo kwa Waziri TAMISEMI, Seleman Jaffo, kutoa kibali cha utoaji wa kiwanja cha kujenga kituo cha Afya kinachotarajiwa kujengwa na taasisi hiyo.Rais ameipongeza taasisi ya Al Hekma kwa mchango wao mkubwa katika Taifa la Tanzania kwa kujenga misikiti 50, kuchimba visima 110 huku ikisomesha yatima wapatao 400.Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete amemshukuru Rais Magufuli kwa kuitikia wito huo na kuongeza kuwa ujio wake unathibitisha utanzania wa kweli ambao hautenganishwi na udini kwa kuishi katika umoja na mshikamano pasipo kufungamana na upande wowote.Naye Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ambaye ni mlezi wa taasisi hiyo amempongeza na kumwombea Rais Magufuli aendelee na kasi yake ya maendeleo na kuwatumikia Watanzania kwa moyo. | kitaifa |
Mfumo huo ulitambulishwa jana kwa mawakala wa forodha na unatarajiwa kuanza kutumika Machi mosi mwaka huu, sambamba na mfumo unaotumika awali wa ASYCUDA, unatarajiwa kuachwa kutumika kuanzia Aprili mwaka huu baada ya kuonekana kuwa na mapungufu mengi.Naibu Kamishna Uboreshaji na Vihatarishi wa TRA, Bellium Silaa akifungua semina hiyo kwa niaba ya Kamishna, alisema Mfumo huu mpya utasaidia kuondoa mizigo kwa haraka na pia ufatiliaji mizigo kwa wepesi wakati wote huku ukipokea taarifa mbalimbali kupitia mtandao hivyo kuondoa msongamano bandarini.Alisema mfumo huo wa kielekroniki, utamwezesha mtumiaji kuutumia popote na kupata taarifa anazozihitaji kwa wakati tofauti na hapo walihitajika kuzunguka na majalada bandarini.Waziri wa Uchukuzi , Dk Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Fedha, Mkurugenzi Mkuu wa Bandari leo wanatarajiwa kukutana na watendaji wakuu wa Uwakala wa forodha kujadili changamoto mbalimbali, zinazowakabili mawakala wa forodha katika kazi zao bandarini.Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Stephen Ngatunga alisema juzi walikutana na Dk Mwakyembe na kujadiliana naye changamoto mbalimbali zinazowakuta, ambapo aliahidi kukutana tena leo. | uchumi |
BAADA ya kuwa katika hali ya mvutano na Rais Uhuru Kenyatta kwa muda mrefu, Gavana wa Mombasa, Hassan Joho anaonekana kuwa karibu na kiongozi huyo wa nchi tangu mshikamano wa nchi ulipoasisiwa na Uhuru na Raila Odinga.Katika ziara ya hivi karibuni ya Rais Uhuru Kenyatta huko Liwatoni katika Kaunti ya Mombasa ambapo alitunuku kamisheni kwa baadhi ya vikosi vya usalama vya pwani, Gavana Joho alionekana kuwa karibu kabisa na rais kuliko hata makamu wake.Ingawa katika picha waliyopiga pamoja, Rais Uhuru Kenyatta alionekana kuwa karibu zaidi na Joho kuliko hata makamu wake, wachambuzi wa mambo wanasema juhudi za Gavana Joho za kupambana na William Ruto katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2022 zimegonga mwamba sasa anataka sapoti ya rais.Kwa muda mrefu, Joho amekuwa akipingana na Rais Kenyatta kuhusu vipaumbele vya serikali katika kutatua kero za wananchi pamoja na mbinu za kuondoa umasikini kwa wananchi wa Kenya.Katika hotuba yake ambayo Rais Kenyatta aliisikiliza vizuri, Joho alitambia ukaribu wake na Rais Kenyatta uliomwezesha kumsaidia Gavana wa Kilifi, Amason Kingi kurudishiwa pasipoti yake kutoka katika mikono ya wanausalama nchiniItalia.“Mheshimiwa Rais, mzee pia anaweza kupoteza pasi yake ya kusafiria, hicho ndicho kilichotokea kwa rafiki yangu Kingi. Lakini kwa kuwa niko jirani na wewe nilitumia fursa hiyo kumpigia Waziri wa Mambo ya Nje na kumweleza ahakikishe gavana anarudi,” alisema Joho. | kitaifa |
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameanza kazi kwa kuhudhuria kikao kazi cha uongozi wa juu wa wizara hiyo kuelezwa taswira na mwelekeo wa mamlaka hiyo ya Serikali.Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameongoza kikao hicho katika ofisi ndogo za wizara hiyo jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mathew Mtigumwe wamehudhuria kikao hicho.Waziri Hasunga amewataka wasaidizi wake wafanye kazi kwa bidii na kwa kushirikiana ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli ya kuimarisha uchumi kupitia viwanda.Hasunga ametoa taswira ya muelekeo wa wizara hiyo kwa mipango ya muda mfupi na muda mrefu kwa kuzingatia weledi na utendaji uliotukuka kwenye utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020.Miongni mwa mambo aliyobainisha Hasunga ni pamoja na umuhimu wa kuanzishwa Sheria ya Kilimo itakayotoa suluhisho la changamoto zinazamkabili mkulima na sekta ya kilimo kwa ujumla.“Kuna kila sababu ya kuanzishwa haraka sheria ya kilimo na tayari tupo katika hatua za mwisho, kwa sababu hatuna Sheria ya Kilimo na inayotumika sasa ni Sera ya Kilimo iliyotungwa mwaka 2013 ambayo pia inahitaji kupitiwa upya” amesemaAmesema, sheria inayotumika sasa ni ya Bodi za Mazao Mbalimbali, ambayo pia inachangamoto zake na kuna mazao ambayo hayana bodi hivyo ni vigumu kuwatetea wakulima wa mazao hayo.Mazao yaliyo katika utaratibu wa bodi ni pamoja na pamba, kahawa, chai, korosho, pareto na tumbaku, na mazao ya chakula hayana bodi lakini yana mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.Hasunga pia ameeleza kuhusu usajili wa wakulima wa mazao yote na kwamba, bodi za mazao ziliagizwa kuwapa wakulima vitambulisho ili kuwatambua iwe rahisi kuwahudumia.Pia ameeleza umuhimu wa Wizara ya Kilimo kuanzisha Bima ya Mazao kwa kuwa kwa muda mrefu wakulima nchini wamekosa utetezi wanapopata na majanga yakwemo ya uchache wa mvua.Muda mfupi kabla ya kikao hicho Rais Magufuli alimuapisha Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo kuchukua nafasi ya Innocent Bashungwa ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara. | kitaifa |
KWA mara nyingine Zarina Hassan ‘Zari’ ambaye ni mzazi mwenza wa msanii Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kila mara kumfi cha mpenzi wake mpya, hali iliyomfanya kukasirika baada ya watu kuhoji. Miezi mitatu iliyopita mjasiriamali huyo raia wa Uganda alitangaza kuingia kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanamume mwingine baada ya muda mrefu kuachana na Diamond, lakini amekuwa akificha sura yake kila anapomuweka kwenye mitandao ya kijamii.Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram juzi Zari alichapisha picha akiwa na mwanamume huyo kisha baadaye kuzifuta cha ajabu aliificha sura yake na baadhi ya mashabiki zake wakaanza kuhoji kwanini amekuwa akifanya hivyo na Zari aliwajibu. “Wakosa kazi mkikosa kazi munaazisha uongo, kuanzia leo kila mtu ni KingBae hapo vipi? Tafuteni kazi sasa,” alisema Zari. Baada ya mwaka mmoja Zari mwenye watoto watano kuachana na Diamond hakuwahi kumtaja mpenzi wake mpya wala kumuonesha sura licha ya kuweka hadharani kuwa yupo kwenye uhusiano mpya na anatarajia kufunga ndoa. | michezo |
WAKATI binti wa miaka 17 aliyekuwa akifanya kazi za ndani jijini Dar es Salaam akieleza ukatili aliokuwa akifanyiwa na bosi wake, ikiwemo kuwekewa mwiko sehemu za siri hali inayosababisha asione siku zake (hedhi) kwa mwaka mmoja sasa, taasisi mbalimbali zimeelezwa kushangazwa na ukatili wa aina hiyo na kutaka hatua kali zichukuliwe.Mkuu wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Vumilia Nyamoga alilaani ukatili huo uliofanywa na mwajiri wa mtoto huyo, Happines Mathew ambaye ni muuguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na kutaka vyombo vya dola kuchukua hatua katika suala hilo.DC Nyamoga alisema Happiness na mumewe, Dk Tito Lunobo, ni wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na wanawajibika katika suala hilo la ukatili dhidi ya binti huyo. “Ninalaani ukatili wa kijinsia uliofanywa kwa binti huyo ambaye nimemuona kwa macho yangu, ni tukio la kusikitisha sana lazima tulisemee hili tusikae kimya.Unyama aliofanyiwa huyu binti unashangaza na hauingii akilini kama unaweza kufanywa na watumishi wa afya, unawezaje kumwadhibu mtoto wa mwenzio kwa kumuingiza mwiko kama fundisho la kumuonesha uchungu wa kuzaa kwa kosa la kumdondosha mtoto?” Alihoji Nyamoga.“Navitaka vyombo vya dola vichukue hatua kali kwa wote pamoja na watendaji wote ambao kwa njia moja au nyingine wamekuwa wakipotosha ukweli kwa kumkandamiza binti ambaye alipata mateso kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.” Pia mkuu huyo wa wilaya alisema Ofisi ya Ustawi wa Jamii na Polisi (Chamwino na Temeke) wanapaswa kufuatilia na kuangalia upya jalada la kesi ya binti huyo, ilikuwaje lilifungwa na mambo yakaishia nyumbani wakati binti huyo amefanyiwa ukatili ambao ni jinai. Alisema ofisi yake itahakikisha inasimamia haki ya binti huyo ilipokwama na kuhakikisha kuwa binti huyo anafanyiwa vipimo na kupata tiba sahihi.DC Nyamoga alisema anamshukuru hata msamaria mwema aliyetoa habari za kikao cha ukoo kutoa fidia ya Sh milioni 1.3 na huo ni ushahidi kuwa kuna uovu ulikuwa unafichwa.Kauli ya HappinessAkizungumza kwa njia ya simu, Happiness alisema suala liko Polisi, hivyo hawezi kusema kitu na kama kuna jambo lolote waulizwe Polisi.Diwani azungumzaDiwani wa Kata ya Manchali, Mary Mazengo alisema alikwenda kumuona binti huyo na alichokiona ni ukatili ambao unaumiza moyo. “Binti ana majeraha ya kupigwa na mwiko kichwani, nimehesabu ana majeraha 19 na sehemu zake za siri zimeharibika vibaya,” alisema Mazengo na kuongeza kuwa pia binti huyo ana makovu ya kuchomwa na pasi mgongoni, macho na midomo yake, na matatizo ya kiafya.Alisema mara ya kwanza binti huyo alipelekwa hospitali na mama wa mtuhumiwa, lakini kinachoonekana madaktari wa Dar es Salaam na Dodoma wana mawasiliano na huyo binti alipimwa kutokana na maelekezo. Alisema wanataka kutafuta utaratibu ili binti atibiwe na madaktari watakaowachagua wao (halmashauri) na si madaktari wanaopata maelekezo ya familia kwani huyo binti hatapata matibabu kikamilifu.Binti mwenyewe anasemaje?Akisimulia mkasa huo, binti huyo alisema sasa analazimika kuvaa kofia muda wote ili kuficha makovu ya kichwani yaliyotokana kupigwa na mwiko kila mara.Katika mazungumzo hayo, binti huyu alidai pia macho yake yamekuwa mekundu kwa kile alichodai kusuguliwa macho mara kwa mara na mwajiri wake. Anasema kwa sasa ana uoni hafifu. Alisema alimaliza darasa la saba katika Shule ya Msingi Manchali mwaka 2016, hakufaulu ndipo alipochukuliwa na ndugu yake, mtoto wa mama yake mkubwa, Happiness Mathew au Happiness Job ambaye ni Muuguzi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili akafanye kazi za ndani. Alisema katika maisha yake alikuwa akikutana na vipigo vya mara kwa mara kwani mwajiri wake huyo hata akimkuta mtoto analia alikuwa anamwangushia kipigo.Alisema kuna siku mtoto alikuwa akicheza na akaanguka, dada huyo aliporudi akamsema hamuangalii mtoto kwa vile hajui uchungu wa kuzaa na atamfanyia kitu ili asikie uchungu kama huo. Ndipo alipompiga na kuchukua mwiko ambao aliuingiza sehemu za siri na tangu wakati huo ni zaidi ya mwaka sasa hajapata siku zake (hedhi) na amekuwa akipata maumivu anapoenda haja ndogo. Binti huyo anasema pia aliwahi kupewa adhabu ya kulala wima mpaka asubuhi. “Siku hiyo alikasirika akasema utalala ukiwa umesimama, muda wa kulala ulipofika akaniingiza chumbani kwake, akaniambia adhabu yako utasimama hadi asubuhi, basi yeye akalala kitandani mimi kwa hofu nikabaki nimesimama mpaka asubuhi,” alidai.Binti huyo alisema alikuwa akilipwa Sh 50,000 mshahara wa mwezi na fedha hizo alikuwa akitumiwa mama yake mzazi moja kwa moja. Akimbilia polisi “Kuna siku nikajiuliza nitateseka mpaka lini, pale nyumbani aliletwa mfanyakazi mwingine wa ndani, tukapanga tutoroke, lakini nikaamua kwenda hadi Kituo cha Polisi Chang’ombe nikatoa maelezo yangu na mhusika alikamatwa,” alisema. Alisema baada ya mwajiri wake kukamatwa aliwekwa rumande na yeye kutoa maelezo yake na kisha alikwenda kukaa nyumbani kwa mjumbe wa mtaa.Wakata tamaaAlisema isingekuwa rahisi kwao kuendelea na kesi jijini Dar es Salaam kwani hawakuwa na sehemu hata ya kulala. “Tuliamua kesi iishe tu hatuna mtu wa kutusaidia, isitoshe hatukuwa hata na pa kukaa kufuatilia kesi hiyo mpaka iishe, mama aliamua tu turudi nyumbani,” alisema. Alisema waliporudi Dodoma, ujumbe ulifika nyumbani kwao kuja kuomba msamaha. “Mama yake na Happiness alitumwa ili aje kumuombea mtoto wake msamaha ili mambo hayo yaishe na siku ya Jumanne iliyopita nilipelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa X-ray,” alisema.Hata hivyo, haelewi majibu ya vipimo hivyo kwani aliyempeleka alisema hakuonekana na tatizo wakati yeye anaumwa.Maumivu yapo wapi?Anasema hajatibiwa macho kwani hospitali waliyokwenda hakuna daktari wa macho na macho yamekuwa yakimsumbua na hata midomo yake imekuwa imevimba muda wote. Pia alisema amekuwa akipata maumivu ya kichwa kutokana na ukweli kuwa kuna wakati alikuwa akipigizwa ukutani mara kwa mara na maumivu ya shingo kutokana kukabwa mara kwa mara. Alisema anachohitaji sasa ni kusaidiwa ili apate matibabu kwani amekuwa na maumivu makali ya mwili na hajui atapata hedhi lini na hajui kilichovurugwa mwilini mwake hadi anakosa hedhi.“Sijui ule mwiko alioniingiza umeleta madhara gani katika mwili wangu naona nisaidiwe ili nifanyiwe vipimo,” alisema. Alisema alivunja ungo mwaka 2014 na alikuwa akipata hedhi kawaida, lakini baada ya kuingiziwa mwiko haoni kabisa hedhi.Mama mzazi asimuliaMama mzazi wa binti huyo, Rehema Richard alisema mwaka 2017, Happiness alikwenda kumuomba mtoto wake akamsaidie kazi za ndani na aliahidi atakaa naye vizuri. “Kumbe mtoto alikuwa akiteseka na alikuwa hataki nijue mtoto alikuwa akiteseka kwa kiwango hiki,” alisema na kuongeza alijua hayo alipoitwa katika shauri jijini Dar es Salaam.“Nilienda nikakuta mtoto kapigwa hata sura yake imebadilika, nikasema sina la kusema nipeni mwanangu nirudi naye nyumbani,” alieleza mama huyo. Alisema ingawa mama wa Happiness alimchukua binti huyo na kumpeleka hospitali, alipewa tu vidonge vya maumivu, “huyu anahitaji vipimo ili matatizo yake ya mwili yajulikane na yatibiwe.”Milioni 1.3/- kama fidiaMama wa binti huyu alisema baada ya kurudi na bintiye, kuliitishwa kikao cha ukoo iliamriwa suala hilo limalizwe kimila na familia ya Happiness iliagizwa kulipa fidia na yeye mwenyewe kukubali kutoa Sh milioni 1.3 kama fidia.“Januari 22, walitukabidhi hela hizo, nimeziweka tu,” alisema mama mzazi wa binti huyo. Nakala ya barua ya makabidhiano hayo ambayo gazeti hili inalo inaonesha fedha hizo zililipwa Januari 22, mwaka huu. Naye mama yake Happiness, Evelina Mchiwa ambaye pia ni mkazi wa Kijiji cha Manchali, alisema baada ya kupewa taarifa kuhusu kukamatwa kwa mwanawe alifika Dar es Salaam, na kumkuta akishikiliwa katika Kituo cha Polisi Chang’ombe. “Wakaandika jalada niliona suala hili tukalijadili nyumbani japo polisi walikuwa wakitaka suala hilo liende mahakamani,” alisema.Kwa upande wake kuhusu suala hilo la kuendesha kesi katika mahakama za Dar es Salaam, mama wa binti aliyefanyiwa ukatili alisema hakuwa na uwezo wa kuendesha shauri hilo akiwa Dar es Salaam, hakuwa na ndugu wala uwezo ndio maana aliamua kurudi nyumbani. Suala la binti huyo kufanyiwa ukatili liliibuliwa na msamaria mmoja ambaye alipiga simu kwa Ofisa Maendeleo wa Wilaya ya Chamwino, Sophia Swai aliyesema kwamba kuna binti ameletwa kutoka Dar es Salaam anaumwa baada ya kufanyiwa ukatili.Ilijulikana vipi?Sophia alisema kutokana na hamasa kwa wananchi kutoa taarifa juu ya matukio ya ukatili, suala hilo lilibuliwa na msamaria aliyempigia simu juu ya kuwapo kwa binti mwenye afya mbaya aliyefanyiwa ukatili jijini Dar es Salaam na kuamua kufuatilia tukio hilo kubaini ukweli wake. Swai alisema baada ya kupata taarifa hizo alikwenda kuonana na Mkuu wa Kituo cha Polisi Chamwino ambaye alifanya mawasiliano na OCD wa Chang’ombe, ambako ilibainika kuwa faili hilo limefungwa, jambo ambalo lilizua maswali kutokana na hali ya binti kuwa mbaya.Kamanda Temeke azungumzaAkizungumza na gazeti hili jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Awadhi Haji alisema kadhia hiyo ya ukatili ipo katika Dawati la Jinsia na wanasubiri hati ya matibabu (PF3) ili kuifikisha mahakamani na haki itendeke.Alisema binti huyo ambaye anaonekana ana undugu na mtuhumiwa, alifika polisi Januari 4, mwaka huu kulalamikia ukatili anaofanyiwa. Kamanda Haji alisema baada ya kumsikiliza mlalamikaji, Polisi walishughulikia malalamiko hayo kwa kufanya upelelezi pamoja na kumkamata mtuhumiwa Happiness Job kwa mahojiano. Alisema baada ya kukamilika kwa upelelezi, shauri hilo halijaenda mahakamani kwa kuwa mlalamikaji ambaye ndiye shahidi wa kwanza katika shauri hilo, hajarejesha PF 3 kama inavyotakiwa.“Shauri hilo ni kama linakosa ushirikiano, mlalamikaji hajarejesha PF 3 ili twende mahakamani. Nimemwagiza Mkuu wa Upelelezi kuhakikisha kwamba wanalipeleka shauri hili mahakamani kwani suala kama hili halimalizwi kienyeji, kuna ukatili mkubwa hapa,” alisema Kamanda Haji. Kwa mujibu wake, katika mahojiano wakati wa upelelezi, familia hizo zilionekana kutaka suala hilo liishie kienyeji, wao wanataka mlalamikaji huyo kupata haki zake pamoja na waajiri wanaofanyia ukatili wafanyakazi wao kutambua serikali ina mkono mrefu katika kulinda wananchi wake. Alisema jamii inapaswa kukemea vitendo vya kikatili na kuviripoti mara moja Polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe. | kitaifa |
Mfumo huo mpya umetengenezwa katika namna inayowezesha wazee kupata mafao yao ya kila mwezi kupitia katika mashine za kutolea fedha (ATM), TigoPesa na M-Pesa, vituo vya mauzo na mitandao mingine.Akizungumza katika maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) Ofisa Operesheni wa NSSF, Joyce Mruma alisema: “Wazee wenye pensheni ambao ni wanachama wa NSSF, hawatatembea tena na pesa mkononi”.Katika mfumo wa zamani, wanachama wa NSSF wazee walikuwa wanalipwa mafao kupitia ofisi za Posta, hali iliyosababisha matatizo mengi kwa wazee hao, ikiwa ni pamoja na kuibiwa njiani na vibaka.“Lakini sasa tumeamua kubadilisha mfumo wa zamani na kutumia mfumo wa kisasa Hifadhi Smart-Cards. Kuanzia sasa, wazee watalipwa kupitia ‘Smart cards’, ambayo itawaruhusu kupata pesa zao wakati wowote na mahali popote. Hatatembea tena na burungutu la pesa mkononi,” alisema.Alisema kwa kuzingatia umri wao, NSSF imeona ni vema kuwapunguzia wazee usumbufu kwa kubuni njia ya kisasa ya kuwalipa mafao yao na kuongeza kuwa mfumo huo wa kadi mpya umetengenezwa na Kampuni ya Selcom.“’Hifadh Smart-cards’ pia itaunganishwa na mifumo ya maduka makubwa (supermarkets) ili kuwawezesha wazee kununua vitu na huduma mbalimbali kupitia kadi zao,” alisema Mruma. | uchumi |
MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Anna Mwaisumo (23) na mpenzi wake Samson Kisuguta (28), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka manne ikiwemo ya kulawiti na kusambaza picha za ngono kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp.Mwaisomo ambaye makazi yake ni kwenye Hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) huku Kisuguta ni mkazi wa Msasani na mfanyabiashara walifikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa mbele ya Hakimu Mkazi, Salim Ally.Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Janeth Magohe alidai kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya mwaka 2017 na mwaka huu maeneo ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.Magohe alidai katika mashitaka ya kwanza kuwa, washitakiwa wote kwa pamoja katika tarehe na mahali kusikofahamika mwaka jana, ndani ya jiji hilo, walikula njama kutenda kosa la kulawiti, kuchapisha picha za ngono na kulazimisha kupata fedha ili kutochapisha picha hizo.Alidai katika mashtaka ya pili kuwa, Desemba 10, mwaka jana maeneo ya Nyumba ya kulala wageni ya Morgan maeneo ya Msasani wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Kisuguta alimlawiti kinyume na maumbile mwanafunzi mmoja wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT- jina linahifadhiwa). Katika mashitaka ya tatu,inadaiwa Oktoba 7, mwaka huu ndani ya jiji hilo, Mwaisomo pamoja na Kisuguta walichapisha picha za ngono kupitia ukurasa wa WhatsApp kinyume na sheria.Pia alidai Novemba 13, mwaka huu, ndani ya jiji hilo, washitakiwa hao walimlazimisha mlalamikaji huyo kutoa fedha taslimu Sh 250,000 ili wasichapishe picha hizo.Washitakiwa hao walikana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo waliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.Hakimu Ally alitaja masharti ya dhamana kuwa kila mshitakiwa atatakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoa serikali za mitaa watakaosaini dhamana ya Sh 500,000 kila mmoja.Hata hivyo, washitakiwa hao walikosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti hayo na kurudishwa rumande hadi Januari 3, mwakani kesi itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.Inadaiwa kuwa Mwaisumo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mlalamikaji huyo wakati wakisoma sekondari ya juu na baada ya kuchaguliwa kujiunga na vyuo tofauti hawakuwa na mahusiano mazuri. | kitaifa |
Timu hizo za ukanda wa Afrika Mashariki zilifuzu hatua hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kushinda mechi zake za marudiano. Fainali za michuano hiyo zimepangwa kufanyika mapema mwakani nchini Niger.Tanzania, Ngorongoro Heroes imefuzu hatua hiyo kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 6-5 katika mechi iliyochezwa Kinshasa dhidi ya wenyeji wao Congo DR.Timu hizo zililazimika kwenda kwenye mikwaju ya penalti baada ya kutoka suluhu kwa mechi zote mbili, ya nyumbani Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi ujao na ile ya ugenini mjini Kinshasa.Rwanda ilifuzu raundi ya pili kwa faida ya bao la ugenini ambapo ilitoka sare ya 1-1 mjini Nairobi dhidi ya wenyeji Kenya kabla ya kutoka Suluhu mjini Kigali mwishoni mwa wiki iliyopita.Uganda imesonga mbele kwenye michuano hiyo kwa jumla ya mabao 8-1 baada ya kushinda 5-1 nyumbani dhidi ya Sudani Kusini kabla ya kushinda 3-0 ugenini.Timu nyingine zilizosonga mbele raundi ya pili ya michuano hiyo ni Gabon, Ivory Coast, Guinea Bissau, Nigeria, Msumbiji, Afrika Kusini, Zambia, Botswana, Congo Brazavile, Algeria, Ghana, Cameroon, Mauritania, Guinea, Malawi, Angola,Burundi, Sudan, Burkina Faso, Libya, Senegal, Misri, Mali, Gambia na Benin. | michezo |
MADEREVA wa bodaboda kutoka kata nane za Manispaa ya Kinondoni wamepewa msaada wa kofia ngumu na Kampuni ya Mcheza ikiwa ni sehemu ya kutoa hamasa ya kujikinga na ajali za barabarani wao na abiria.Akizungumza kwenye Viwanja vya Biafra baada ya kukabidhiwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Bajaji na Bodaboda Kinondoni, Issa Mustapha alisema waliopewa kofia wengi ni viongozi wa vituo ambao pia ni madereva ili wakawe mfano kwa wenzao kuhamasisha kuvaa helmenti.“Tulipewa kofia ngumu 100, tuna madereva wa bodaboda na bajaji 7,000 lakini kwa sababu kofia tulizopewa hazitoshi kwa wote tukaona tuwape viongozi baadhi wa vituo wakawe mfano kwa madereva wao wakiwa kazini,” alisema Mustapha. Kwa upande wake, Balozi wa Mcheza, Edger Kibwana alisema huu ni utaratibu wao walioanzisha mwaka huu kuhakikisha usalama kwa madereva wa bodaboda unakuwa mkubwa sana wanapokuwa kazini kwa kuwapa vifaa hivyo vitakavyosaidia kutoa huduma bora kwa Watanzania. “Tunawasihi bodaboda kuendelea kuzingatia sheria za usalama kama wanavyoelekezwa na serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, na sisi tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha usalama wao unakuwa mzuri, M cheza ipo pamoja nao Watanzania waweze kunuifaka na huduma yao,” alisema Kibwana.Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Mcheza, Moses Busaimoni alisema utoaji wa kofia hizo ni kuunga mkono juhudi za vyombo vya usalama za kuelimisha umuhimu wa madereva na abiria kuvaa kofia ngumu kujiepusha na hatari ya kupoteza maisha pindi wanapopata ajali. Alisema bado wataendelea kuwaunga mkono madereva hao ambapo hivi karibuni watakuja na shindano linalowahusu lenye lengo la kutoa zawadi za bodaboda kwenye kata mbalimbali. “Nawakumbusha madereva wa bodaboda kuwa tumeandaa shindano dhidi yao washindi watanyakua bodaboda, wajiandae utaratibu tutauweka hadharani hivi karibu ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono,” alisema. | michezo |
PEP Guardiola amesema ni wendawazimu na upuuzi kwa Manchester City kufi kiria kuhusu kutwaa taji licha ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Burnley juzi usiku.City imejikongoja mpaka kufikia tofauti ya pointi nane dhidi ya vinara Liverpool, shukrani kwa Gabriel Jesus aliyefunga mabao mawili na mabao mengine kutoka kwa Rodri na Riyad Mahrez lakini Guardiola anaona bado hana nafasi ya kukipiku kikosi cha Jurgen Klopp.“Kwa umbali tuliona nao na Liverpool itakuwa wendawazimu kufikiria kuhusu kutwaa taji,” alisema Guardiola.“Kama kila mmoja anavyosema tupo nje ya mbio, hatuna nafasi.”“Tunajifikiria wenyewe na mechi ijayo, kufikiria njia za kushinda ili kuwakaribia ni upuuzi.”City ilijiandaa kwa mechi hiyo kwa kuimba wimbo wa Oasis, Wonderwall kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.Na Guardiola alitania kwamba itakuwa hivyo kwenye Uwanja wa Etihad watakapokutana na Manchester United.Jesus ni kama alifanya mazoezi kwa ajili ya debi hiyo kwa kufunga bao lake la kwanza tangu Oktoba na Guardiola alikiri umuhimu wa Mbrazil huyo na namna anavyojiamini huku Sergio Aguero akiendelea kuwa nje kutokana na kusumbuliwa na nyama.“Tulimhitaji kufunga mabao haya,” alisema Guardiola.“Yatamsaidia yeye na timu, tumempoteza mshambuliaji hatari Sergio”. | michezo |
['Mchezaji Bruno Fernandes ameanza mchakato wa kuhamia Old Trafford. Nyota huyo wa miaka 24 anayecheza safu ya kati ya Sporting Lisbon na Ureno anatarajiwa kwenda Manchester kufanya vipimo vya afya. (Sport Witness)', 'Red Devils wanamlenga mlinzi wa Atletico Madrid na Uhispania Saul Niguez, 24, kuchukua nafasi ya Paul Pogba, endapo nyota huyo wa miaka 26 raia wa Ufaransa ataondoka Old Trafford. (Express)', 'Manchester City hawako tayari kulipa pesa zinazoitishwa na Leicester kumnunua Harry Maguire,26, hatua ambayo imeipatia Manchester United nafasi ya kumsajili mchezaji huyo wa Kimataifa wa England. (90Min)', 'Arsenal watamkosa kipa wa Ujerumani wa miaka 21 Markus Schubert, ambaye ameamua kujiunga na Schalke kutoka Dynamo Dresden. (Sport1)', 'Arsenal pia wako mbioni kumsajili Marcelo baada ya beki huyo Mbrazil kuomba kuondoka Real Madrid. (Sport - via Metro)', 'Inter Milan wanachelewa kutoa ombi rasmi la kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Ubelgiji Romelu Lukaku, 26. (Sun)', 'Mchezaji nyota wa zamani wa Tottenham Ossie Ardiles anasema ni "kazi bure" kwa klabu hiyo kujaribu kumzuia Christian Eriksen, 27 asiondoke. (Talksport - via Goal)', 'West Ham United wanajaribu kunyakua uhamisho wa mshambuliaji wa Celta Vigo na Uruguay Maxi Gomez, 22, kutoka kwa Valencia. (Sky Italia - via Inside Futbol)', 'Leicester wataelekeza nguvu zao zote kumsaini beki wa Burnley James Tarkowski endapo Harry Maguire ataenda klabu ya Man United. Hata hivyo, Leicester wataminyana na Wolves katika harakati za kutaka kumsajili Tarkowski. (Birmingham City)', 'Man United inajiandaa kumpatia mkataba mpya wenye thamani ya pauni milioni 85 kipa wao Mhispania David de Gea ambapo atapokea kitita cha pauni 350,000 kwa wiki. (Star)', 'Frank Lampard amepigwa picha katika uwanja wa Stamford Bridge alipokaribia kuwa kocha mpya wa Chelsea. (Mail)', 'Kuidhinishwa kwa Lampard kuwa kocha mpya wa Chelsea kulicheleweshwa Jumatano jioni baada ya mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram kukumbwa na changamoto za kiufundi hali ambayo ilifanya kuwa vigumu kuchapisha picha au kuweka video mtandaoni. (Mirror)', 'Chelsea pia imeanza mazungumzo ya kandarasi mpya ya na kiungo wa kati wa miaka 20 Mason Mount, ambaye aliichezea Derby msimu uliopita chini ya ukufunzi wa Lampard. (Evening Standard)', 'Arsenal wamepewa nafasi ya kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Mbrazil Malcom, 22, lakini azma yao kubwa ni kumnasa mshambuliaji wa Ivory Cost wa miaka 26, Wilfred Zaha kutoka Crystal Palace. (Mirror)', 'Gunners wana pauni milioni 70 wanapojianda kuweka dau la pili la kumnunua Zaha, japo kuwa Palace wanamini thamani ya mshambuliji huyo ni pauni milioni 80(Sky Sports)', 'Agenti wa Romelu Lukaku amaefanya mazungumza mapya na Inter Milan lakini klabu hiyo ya Italia bado inashauriana na Manchester United kuhusu ada ya kiungo huyo wa Ubelgiji aliye na miaka 26. (Sky Sport Italia - in Italian)', 'Manchester United wanataka kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24 kutoka Sporting Lisbon. (Sky Sports)', 'Tottenham imesitisha mazungumzo yake na Real Betis kumhusu kiungo ya kati wa Argentina Giovani Lo Celso, 24, baada ya vilabu kushindwa kuafikiana malipo. (Sky Sports)'] | michezo |
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema baridi inawapa changamoto, lakini anaamini watazoea na kuwa fiti kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa kesho Uwanja wa Borg El Arab.Kwa mujibu wa taarifa kutoka Alexandria, Misri, baridi imekuwa ikiisumbua Simba wakati wa mazoezi, lakini wana uhakika wachezaji watazoea na watafanya vizuri katika mchezo wao huo wa Kundi D. Aussems alisema wamefanya mazoezi ila baridi inawapa changamoto, lakini anaamini watazoea na kuwa fiti kwa mchezo huo. “Jana usiku na leo tumefanya mazoezi ila baridi inawatatiza wachezaji wangu kwa vile walizoea joto, pia tumebahatika kutazama video za mechi mbalimbali za wapinzani wetu,” alisema Aussems.Pia amefurahi kurejea uwanjani kwa mshambuliaji John Bocco na kusema atamtumia kama moja ya silaha katika mchezo huo utakaofanyika kesho mjini Alexandria, Misri. “Bocco amerejea kujiunga na sisi, ni moja ya silaha ambayo ninaihitaji kuitumia kuwafunga Al Ahly, kwani ni mchezaji mzuri na atatusaidia kwenye michuanoi hii,“alisema. Simba inatarajia kupambana na wenyeji Al Ahly ukiwa mchezo wake wa tatu katika Kundi D wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika ikiwa imeshinda mechi moja na JS Suoura kwa mabao 3-0 kabla ya kufungwa na AS Vita Club ya Congo kwa mabao 5-0.Kwa sasa Al Ahly inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne, ikifuatiwa na As Vita yenye pointi tatu, sawa na Simba huku wakipishana kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa huku JS Suoura ikishika mkia katika kundi hilo ikiwa na pointi yake moja. Wakati huohuo, Bodi ya klabu ya Al Ahly ilikutana juzi pamoja na mambo mengine ilijadili mchezo huo wa kesho dhidi ya Simba utakaofanyika Misri usiku. Mkutano huo uliongozwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo, Mahmoud Al Khatib, ambayo ilikutana juzi, ikiwa ni mkutano wao wa kwanza kabisa kufanyika mwaka huu.Kwa upande mwingine, kocha wa Uruguay wa timu hiyo Martin Lasarte, ameelezea furaha yake baada ya kuifunga Wadi Degla 2-1 katika raundi ya 20 ya Ligi Kuu ya Misri uliofanyika kwenye Uwanja wa Petro Sport. Lasarte alisema kuwa kupata pointi tatu ni kitu muhimu zaidi kwa Al-Ahly katika kipindi hiki, akidokeza kuwa kiwango hicho ni mwendelezo kwa ajili ya mechi ijayo. Mechi hiyo itasaidia kurekebisha makosa kabla ya kukutana na Simba ya Tanzania katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika Kundi D.Alisema kuwa timu hiyo juzi iliendelea na mazoezi kujiandaa kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Simba utakaofanyika Jumamosi. Hata hivyo, timu hiyo itamkosa Yasser Ibrahim, beki ambaye aliumia misuli walipocheza dhidi ya Wadi Degla, mchezaji anayetarajia kufanyiwa vipimo ili kuona ameumia kiasi gani na atahitaji muda gani kupona. Mchezaji huyo alitolewa uwanjani walipocheza dhidi ya Wadi Degla. Nafasi yake ilichukuliwa na Saad Samir ambaye naye ametokea katika kipindi cha kupona maumivu, ambayo yamemweka kando kwa wiki kadhaa. | kitaifa |
OFISI ya Waziri Mkuu chini ya Baraza la Taifa la Biashara, kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji, unaotekelezwa katika mikoa ya Kigoma na Dodoma, umeboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika mikoa hiyo kwa kutumia kiasi cha Sh bilioni 16 hadi kufi kia mwezi huu.Mradi huo ambao utekelezaji wake unajikita katika uwekezaji na biashara katika Halmashauri kupitia Mfuko wa SIFF, kuimarisha minyororo ya thamani na kuimarisha majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi, tayari umeboresha mazingira ya biashara kwa wakulima na wavuvi wa mkoani Kigoma.Akizungumza katika ziara yake mkoani hapa wakati wa kukagua shughuli za utekelezaji za Baraza la Taifa la Biashara, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama alifafanua kuwa Baraza la Taifa la Biashara, kwa kushirikiana na mradi huo, wamewawezesha wananchi kiuchumi kupitia uwekezaji kwenye miradi midogo inayochochea ongezeko la ajira na kipato.“Nimetembelea Mwalo na Soko la Samaki la Kibirizi, hapa mkoani Kigoma nimeridhishwa jinsi mradi huu ulivyoboresha miundombinu ya mwalo huu katika kuhakikisha wavuvi wanapunguza upotevu wa mazao ya samaki na dagaa.Niyaombe mabaraza ya biashara ya mikoa na wilaya yaendelee na mfumo wa majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi ili kuhakikisha walengwa wa mradi huu wanaendelea kunufaika,” alisisitiza Jenista. Alifafanua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ni Rais John Magufuli, ambaye amekuwa akisisitiza kupunguza vikwazo na kero kwa wafanyabiashara, lakini pia kuimarishwa kwa mahusiano kati ya serikalii na sekta binafsi na kuongezeka kwa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika mipango ya serikali.Awali, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mratibu wa Mradi (Masuala ya Majadiliano ya Sekta ya Umma na Binafsi), Andrew Mhina alibainisha kuwa mradi huo, unalenga kuhakikisha unaboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, tayari umeandaa mwongozo wa majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi ngazi ya mkoa na wilaya ili kuyajengea uwezo mabaraza ya mikoa, yawe endelevu na yenye ufanisi, ambapo Baraza la Taifa la Biashara kwa kushirikiana. Katika ziara hiyo, Jenista pamoja na kutembelea mwalo wa soko la Samaki la Kibirizi, alitembelea Kituo cha Biashara Kigoma, Soko la Jioni la Mwanga na Mradi wa Kuwezesha Vijana Kushiriki katika Kilimo Biashara na Mnada wa Mifugo Buhigwe. | kitaifa |
Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA, Rished Bade, alisema hayo jana jijini hapa alipozungumza na waandishi wa habari.Wakati kukiwa na mgomo nchi nzima dhidi ya matumizi ya mashine hizo, Bade alisisitiza kuwa wakati wa kufanya biashara bila ya kulipa kodi halali umepitwa na wakati na kila mmoja anapaswa kulipa kodi kutokana na kile alichouza na si vinginevyo.Mbele ya Kamishina wa Kodi ya Ndani, Patric Kayombo na Meneja wa TRA, Mkoa wa Arusha, Evarest Kileva, Bade alisema serikali kabla ya kuanza mfumo huo mpya mwaka 2010, ilitoa elimu nchi nzima.Alisema Serikali haijatoza kodi mpya na kamwe haiwezi kumtoza mfanyabiashara yeyote kodi kubwa wala ndogo bila sababu za msingi.Alisisitiza kuwa kodi inayotokana na mashine hizo ni kodi halali ambayo mfanyabiashara amefanya mauzo yake baada ya kuuza bidhaa iliyokuwa dukani, kodi hiyo inayorekodiwa na mashine hizo ndiyo inayopaswa kulipiwa kodi.‘’Kuna baadhi ya wafanyabiashara wanapotosha ukweli juu ya utumiaji mashine hizi … wanataka kutumia mgomo ku jinufaisha kwa kuwa mashine hizi rekodi yake inaonesha wazi bila kificho, sehemu zote ikiwamo TRA,’’ alisema.Alisema mashine zinazosambazwa nchini kupitia kampuni 11 zilizopewa kazi hiyo, zimetengenezwa kwa maelekezo ya uhalisia wa matumizi ya kitanzania na risiti zake zikitolewa katika maduka ya wafanyabiashara kumbukumbu hizo huoneshwa TRA.Kuhusu mgomo, alisema sheria iko wazi na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.‘’Hakuna kodi mpya iliyoletwa katika mashine hizo bali ni kutaka kila mfanyabiashara auze bidhaa zake na kulipa kodi kutokana na alichouza kihalali bila kificho,’’ alisisitiza.Kamishna Bade alisema awali kulikuwa na changamoto katika suala hilo, lakini walikaa pande zote na kujadili na kupata ufumbuzi lakini anasikitika kuona baadhi ya wafanyabiashara na TCCIA wanaacha kusema ukweli na kudiriki kupotosha umma juu ya ukweli wa mashine hizo.Baadhi ya mikoa nchini juzi na jana, ilikumbwa na mgomo wa wafanyabiashara kufunga maduka yao kushinikiza kuondolewa kwa matumizi ya mashine hizo, na matokeo yake ni kusababisha usumbufu kwa wateja. | uchumi |
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio za 18 za Kilimanjaro zitakazofanyika Machi mwakani, Mwakyembe pia aliwataka wanariadha wa Tanzania kufanya maandalizi ya uhakika ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mbio hizo, ambazo ni kubwa zaidi nchini na hushirikisha watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi.Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa uzinduzi wa mbio hizo, ambazo zitafanyika mjini Moshi Machi mosi, 2020, Dk Mwakyembe alisema ni aibu kwa zawadi zote kwenda nje ya nchi, hivyo aliwataka wanariadha wa Tanzania kujiandaa vizuri ili kuhakiisha zawadi hizo zinabaki nchini. Mwakyembe aliwapongeza wadhamini wa mbio hizo wakiongozwa na Kilimanjaro Premium, ambao hudhamini mbio za kilometa 42, Tigo (kilometa 21), Grand Malt (kilometa 5), ambazo ni mbio za kujifurahisha na hushirikisha watu wengi.“Inatia moyo sana kuona kuwa Kilimanjaro Marathoni sasa ina washiriki zaidi ya 11,000 kutoka nchi zaidi ya 56 kote duniani. Hili ni jambo zuri sana kwa taifa, kwani tunapata fedha za kigeni kutokana na matumizi yanayofanywa na wageni hawa nchini, ikiwemo utalii, “alisema. Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka, alitoa wito kwa washiriki wazalendo kuchangamkia zawadi zinazotolewa na Kilimanjaro Marathoni badala ya kukimbilia kushiriki mbio za nje, ambazo zawadi zake ni ndogo. “Ni vizuri kwenda kupata exposure lakini tusiache zawadi nzuri nyumbani na kufuata hela ndogo huko nje wakati tunaweza kuzipata hapa hapa nchini, “alisema Mtaka. Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli, alisema tangu mashindano yaanze Kilimanjaro Premium Lager imewekeza hela nyingi sio tu kusukuma mauzo ambayo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, lakini pia kutengeneza ajira na kuchangia uchumi kwa ujumla kupitia gharama za kuyatangaza, promosheni na masuala mengine ya kimasoko. Naye Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kampuni yake inajivunia kudhamini mbio za kilometa 21 kwa mwaka wa tano mfulululizo, ambayo ni sehemu ya mbio hizo. “Tunajivunia kuwa sehemu ya tukio hili kubwa ambalo linawaleta pamoja wanariadha wakubwa, “alisema. Kwa mujibu ya waandaaji wa Kilimanjaro Marathon- Wild Frontiers na Executive Solutions, usajili umeshaanza kwa mtandao kupitia www. kilimanjaromarathon.com. Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na mwenyekiti na kaimu katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa, Leodegar Tenga na Neema Msitha, kaimu msaijili wa michezo nchini, Mwita, Bodi ya Utalii na wadau wengine swa mchezo wa riadha. | michezo |
MKAZI wa Mhunze wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga, Raphael Martine (34), anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kumuua Shija Mahoiga (45), kwa kumpiga kwa chuma kichwani, mikononi, na sehemu za mbavu.Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Richard Abwao amethibitisha mauaji hayo ya juzi saa tisa usiku, akisema mtuhumiwa alidai kwenda kwenye nyumba ya Mahoiga na kumfumania akiwa amelala na mkewe Maria Kija.Kamanda Abwao amesema wanamshikilia Martine kwa tuhuma ya kumuua Mahoiga kwa kutumia kipande cha chuma kumpiga nacho kichwani, mikononi na sehemu za mbavu upande wa kushoto.“Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi baada ya mtuhumiwa kumfumania Shija Mahoiga akiwa amelala na mkewe Maria Kija ambaye amejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Jakaya Kikwete, Kishapu. Mbinu iliyotumika ni kuvunja mlango na kuanza kumshambulia kwa kipande cha chuma,” amesema Kamanda Abwao.Katika tukio lingine, Kamanda Abwao alisema Zainabu Shija (28) ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Mhida, Kijiji cha Busangi katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, ameuawa huku chanzo chake ni wivu wa mapenzi.Amesema Zainabu aliuawa hivi karibuni na mtu aliyefahamika kwa jina moja la Emmanuel akishirikiana na wenzake wawili kwa kumkata mapanga na kitu chenye ncha kali usoni na kichwani.“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi baada ya marehemu kukataa kurudi kwa mtuhumiwa ambaye alimfukuza kutokana na kutopata mtoto muda mrefu na kuolewa na mwanamume mwingine na kupata mtoto,” amesema Kamanda Abwao.Aidha, Kamanda Abwao amewataka wananchi kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi, bali waende kwenye vyombo vya sheria vianvyohusika kusuluhishwa. | kitaifa |
Akizungumza hivi karibuni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) , Gabriel Mwalo, amesema kuna faida nyingi katika kilimo cha mkataba lakini kukosekana kwa usimamizi na kutoungwa mkono vya kutosha kutoka serikalini kunawafanya wawekezaji kutochangia fedha nyingi zinazohitajika.Semina hiyo ilikuwa ya kuwaelimisha wahariri na waandishi kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu manufaa ya kilimo cha mkataba.Alisema upinzani unaofanywa na baadhi ya wadau na wakulima kutokana na maslahi binafsi ambayo ni ya wachache lakini bado kilimo hicho kina tija na ahueni kwa wakulima.Amesema sasa wakati umefika kwa serikali kuyaangalia matatizo yanayokwamisha kilimo cha mkataba na mkazo uwekwe kwenye uzalishaji wa pamba pasiwepo ucheleweshaji wa utekelezaji wa sera ya Serikali.“Sekta ya pamba, kupitia msaada wa Serikali, wasindikaji na wawekezaji, ina fursa ya kufanya maendeleo kwa wakulima kwa ujumla na inaendana vizuri na ahadi ya Serikali ya maisha bora kwa kila Mtanzania.Kama Serikali, inapaswa kuingilia kati na kuweka mazingira yatakayohakikisha kunakuwepo na maendeleo na mkulima kuwa endelevu pamoja na kilimo cha mkataba kwa ujumla.“Wawekezaji wakubwa wanahitaji wakulima wanaoweza kuwasambazia pamba zitakazotumika kwenye vinu vyao, huku wakulima nao wanahitaji wawekezaji kuwapa mitaji kuendesha mashamba yao na kuongeza mavuno. “Kama Serikali inaingilia kati na kusimamia vizuri kilimo cha mkataba, basi kitakuwa na mafanikio makubwa sana zaidi ya ilivyo sasa ,” alisisitiza Mwalo.Ameongeza kusema kwamba hivi leo ekari moja huzalisha kuanzia kilo 250 mpaka 300 za pamba na kama kilimo cha mkataba kitaungwa mkono ipasavyo na Serikali na matatizo machache ya msingi kushugulikiwa, panaweza pakawepo na mavuno kuanzia kilo 1,200 mpaka 1500 kwa ekari moja. | uchumi |
MATUMIZI ya pombe yanatarajiwa kuongezeka duniani kwa muongo ujao kutokana na nchi mbalimbali kutotelekeza ahadi ya kuwalinda wananchi wao kutoka katika matumizi mabaya ya vilevi.Tafiti zinaeleza kuongezeka kwa matumizi ya pombe kimataifa yanachangia ongezeko la matumizi hayo ya pombe kwa nchi zenye vipato vya chini. Taasisi ya Kimataifa ya IOGT, imebainisha kuwa matokeo ya utafiti uliopita yalionesha kuwa malengo ya kupunguza matumizi hatari ya pombe hayawezi kufikiwa endapo hatua za haraka za kudhibiti matumizi hayo hazitachukuliwa.Katika taarifa iliyotolewa na Rais wa taasisi hiyo, Kristina Sperkova jijini Dar es Salaam, alisema katika utafiti mpya uliochapishwa na jarida la matibabu umeonesha kuwa matumizi ya pombe kwa watu wazima yameongezeka kwa miongo miwili iliyopita na kwamba yataendelea kuongezeka kwa muongo ujao. Alisema nchi mbalimbali zilitoa ahadi za kisiasa kwamba ifikapo 2025, matumizi ya pombe katika nchi zao yatapungua kwa asilimia 10.Alieleza uchambuzi wa kisayansi uliotolewa hivi karibuni, uliweka wazi kuwa serikali zimeshindwa kutimiza wajibu na ahadi zao za kuwalinda wananchi wao, jamii na jumuiya kutoka kwenye matumizi mabaya ya pombe.“Ni wazi kuwa sera, kanuni na mikakati iliyopo haitoshi. Kwa hiyo, tunaendelea kusisitiza kuhusu Mkataba wa Mfumo wa Kudhibiti Pombe uzingatiwe ili tuweze kufikia malengo,” Ripoti ya dunia ya matumizi ya pombe iliyochapishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ya Septemba mwaka jana, inaonesha jinsi pombe inavyoathiri malengo mengi ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ikiwemo ya kutoa ahadi ya kujenga jamii yenye usawa na iliyo bora.“Sekta ya pombe pekee ndivyo inayonufaika kutokana na hali ya sasa. Lakini kushindwa kupunguza au kudhibiti matumizi ya pombe ambayo yanasababisha athari kiafya, kiuchumi, kijamii na kwa maendeleo endelevu, bila kuchukua hatua za haraka matumizi haya yatakuwa mzigo na yataendelea kuongezeka,” alisisitiza Sperkova. Alieleza kuwa kisayansi pombe inasababisha madhara kiafya pamoja na maendeleo na kwamba ili kuleta matokeo chanya, ni lazima kuwa na matumizi sahihi ya sera zilizopo kwa ajili ya kubadili mwenendo.Septemba mwaka jana, katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, WHO walizindua mpango wenye lengo la kuvumbua sera bora na nzuri za kuzuia na kupunguza madhara ya pombe. “Upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, kujenga mfumo madhubuti wa afya, kuendeleza maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kujenga jumuiya za kjamii zinazostahimili afya na dharura nyingine zote, malengo haya muhimu yanatishiwa na kupanda kwa matumizi ya pombe hususani katika nchi zinazoendelea,” alisisitiza Sperkova.Alifafanua kuwa ni lazima serikali kuhakikisha kuwa wanachukua hatua za haraka za kudhibiti matumizi ya pombe, kutekeleza sera bora za kudhibiti pombe na kutimiza ahadi ya kulinda watu kutoka katika madhara ya matumizi hayo na kufikia afya na maendeleo kwa wote. Hata hivyo, matumizi hayo ya pombe duniani yanakadiriwa kuua watu milioni 3.3 kila mwaka ikimaanisha kuwa kila baada ya sekunde 10 watu hufa kwa sababu ya pombe. Pia inakadiriwa vijana kati ya miaka 20 hadi 39, sawa na asilimia 25 hufa kutokana na matumizi ya pombe ikiwa ni sawa na asilimi 5.9 ya vifo vyote. | kitaifa |
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Awadh Massawe, aliyasema hayo mjini hapa hivi karibuni kuwa, mawakala wa mizigo wana mchango mkubwa wa kujenga mazingira bora ya biashara na kuifanya nchi kuwa shindani barani Afrika.“Tunazidi kuimarisha huduma bandarini, lakini pia ni muhimu wakala wa mizigo wakafanya kazi zao kwa umakini, weledi na uaminifu ili kupata matokeo bora kwa pamoja,” alisema Mkurugenzi huyo wakati wa mkutano kati ya TPA, maofisa wengine wa serikali na wafanyabiashara wa Zambia.Mkutano huo ulilenga kubadilishana mawazo ya namna bora ya kuimarisha biashara kwa wafanyabiashara wanaotumia bandari ya Dar es Salaam kupitisha mizigo yao.“Mawakala wachache wasio waaminifu wasiharibu sifa ya wengine,” alisema na kuongeza kuwa kampuni hizo zina nafasi kubwa ya kuchangia kupungua kwa gharama za kufanya biashara kama zitafanya kazi vyema.Naibu Kamishna anayeshughulikia Biashara katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk Patrick Mugoya, alisema Serikali haitosita kuchukua hatua kali kwa kampuni zitakazokwenda kinyume na taratibu na Sheria za nchi.Kuna zaidi ya kampuni 550 za wakala wa mizigo zilizosajiliwa Tanzania. Alisema TRA kwa kushirikiana na wadau wengine wanajitahidi kuhakikisha kuwa mazingira ya biashara katika bandari za Tanzania kwa ujumla yanaimarika na kuwa na ufanisi zaidi.Mmoja wa wajumbe wa Chama cha Wakala wa Mizigo Tanzania (TAFFA), Adelaide Marijani, aliwataka wafanyabiashara waache kutumia kampuni zisizosajiliwa ili kuepuka matatizo yanayoweza kutokea.“Wafanyabiashara hasa toka nchi jirani wafuate taratibu zinazotakiwa wanaposhughulikia mizigo yao hapa nchini,” alisema, na kuwataka watumie tu kampuni zilizosajiliwa na TRA.Mmoja wa wafanyabiashara kutoka Zambia, Phiri Momba alisema baadhi ya watu wanaojifanya mawakala wa mizigo wamekuwa wakisababisha matatizo kwao.“Unaweza kufanya kazi na mtu na baadae unagundua kuwa ni tapeli,” alisema katika mkutano huo. Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma aliwatahadharisha wafanyabiashara wa Zambia kutotafuta njia za mkato. “Fuateni taratibu zinazotakiwa… tumieni ofisi za TPA zilizopo mjini Lusaka vizuri.” | uchumi |
MABINGWA wa kihistoria Yanga, wamepunguzwa kasi na Mbeya City baada ya kutoka suluhu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa katika Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.Mchezo huo ulianza kwa kasi kwa Yanga kutawala sehemu ya kiungo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao huku wakilisakama lango la wapinzani mara kwa mara, lakini kutokana na umakini wa safu ya ulinzi ya Mbeya City mashambulizi yote yakiwemo ya kushtukiza yalizimwa na hadi wanaenda mapumziko timu zote zilikuwa bado kucheka na nyavu.Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko, ambapo Yanga waliendeleza kumiliki mchezo na kufanya mashambulizi kupitia kwa mchezaji David Molinga, lakini alijikuta kwenye ulinzi mkali na kukosa utulivu.Papy Tshishimbi dakika ya 53 alishindwa kufunga bao, akiwa yeye na mlinda mlango wa Mbeya City, Haroun Mandanda baada ya kupenyezewa pasi na Deus Kaseke.Mbeya City nao kupitia mchezaji Peter Mapunda kwa nyakati tofauti alionekana kulisumbua lango la Yanga lakini alikukosa utulivu na mashuti yake kuishia mikononi mwa kipa wa Yanga, Farouk Shikhalo Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kushika nafasi ya tisa kwenye msimamo wakifikisha pointi 18 baada ya kucheza michezo tisa na kushinda mechi tano, sare tatu na kufungwa mmoja wakati Mbeya City wanashika nafasi ya 18 wakiwa na pointi tisa baada ya kucheza michezo 13 wakishinda mechi moja, sare sita na kufungwa mechi sita.Kufuatia matokeo hayo kocha wa Yanga, Charles Mkwasa alisema mvua ilisababisha uwanja kuwa mbaya huku akimlalamikia mwamuzi Florentina Zabron kuwa moja ya sababu kwa timu yake kugawana pointi na wenyeji hao.“Tumecheza vizuri lakini mvua iliyonyesha isababisha uwanja kuteleza na kuwa na matope hivyo wachezaji kushindwa kumiliki mpira lakini pili fitina zilizofanywa na mwamuzi wa leo (jana) kwa kweli zimechangia kuharibu malengo yetu. Waamuzi kama hawa ni kichefuchefu kufanya nao kazi,” alisema Mkwasa.Naye kocha wa Mbeya City, Amri Said, amekubali matokeo hayo na kusema wametimiza malengo yao kwani wakati wanaingia kwenye mchezo walikuwa na dhamira ya kupata sare kwa kuwa wapinzani wao ni timu bora kulinganishwa na uwezo wa kikosi chake kilichosheheni vijana wengi wasiokuwa na uzoefu.“Matokeo nimeyapokea vizuri, kikubwa nawapongeza vijana wangu kwa kucheza kwa kufuata maelekezo niliyowapa lakini pia ni mwanga mzuri kwangu, kwani nimeanza kazi yangu vizuri hivyo tunaenda kujipanga kwa michezo ijayo,” alisema Said. | michezo |
Katika swali lake, Owenya, alitaka kufahamu ATCL inamiliki ndege ngapi na kati ya hizo, ni ngapi zimekodishwa na zinafanya safari kwenda wapi.Baada ya kujibiwa kwamba ndege inayomilikiwa na ATCL ni moja, Owenya alisema ni aibu kwa shirika kuwa na ndege moja wakati liliwahi kumiliki ndege saba.Ili kuondoa aibu hiyo, Mbunge huyo alipendekeza mali za shirika hilo, zikiwemo nyumba zake katika nchi mbalimbali, ikiwemo ya London, Uingereza, ziwekwe rehani ili kupata mkopo wa kununua ndege hizo.Pia alipendekeza njia za ATCL kwenda katika nchi mbalimbali, hususani ya Dubai, katika nchi za Falme za Kiarabu, Uingereza na Marekani, zikodishwe kuongezea shirika hilo fedha za kujiendesha kwa kuwa kwa sasa halina uwezo wa kutumia njia hizo.Akifafanua mipango ya Serikali ya kufufua shirika hilo, Dk Tizeba alisema mbali na kumiliki ndege hiyo moja aina ya Dash 8 Q 300 yenye uwezo wa kubeba abiria 50, ATCL pia imekodi ndege moja aina ya CRJ 200, yenye uwezo wa kubeba watu 50 kutoka Kampuni ya AXMAX ya Kenya.Kwa mujibu wa Dk Tizeba, ndege inayomilikiwa na ATCL, inatoa huduma zake katika njia za Dar es Salaam, Kigoma, Mtwara na Bujumbura, nchini Burundi.Aidha ndege iliyokodishwa, inatoa huduma zake katika njia za Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Mtwara na Hahaya nchini Comoro.Hali ya sasa ya ATCL, ni tofauti na ilivyokuwa miaka michache iliyopita ambapo haikuwa na ndege hata moja iliyokuwa ikitoa huduma.Mwaka 2011, aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR Mageuzi) bungeni, alisema ATCL ilianzishwa kwa kupewa ndege 11 mwaka 1973, lakini mpaka mwaka huo 2011, hakukuwa na ndege hata moja iliyokuwa ikifanya kazi.Akifafanua mipango ya Serikali ya hivi karibuni, Dk Tizeba alisema ATCL ina mpango wa kununua ndege mbili, kwa mfumo wa kibiashara wa kukodi huku malipo ya ununuzi yakifanyika taratibu. Ndege hizo aina ya D8 Q 400, zenye uwezo wa kubeba abiria 78 kila moja baada ya kununuliwa, zitaongeza wigo wa huduma za ATCL katika njia za Nairobi nchini Kenya, Kigali nchini Rwanda na nchini Uganda.Kwa mujibu wa Dk Tizeba, ununuzi wa ndege hizo utafanyika baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria na kibiashara ambazo zinafuatwa hivi sasa, ili ndege hizo zianze kufanya kazi mwishoni mwa mwaka huu.Baada ya kukamilika kwa utekelezaji wa mpango huo, ambao utafanya ATCL kurusha ndege nne na kutoa huduma za ndani na katika nchi za Afrika Mashariki, Dk Tizeba alisema utafuata utekelezaji wa ununuzi wa ndege nyingine mbili.“Kuna mpango wa kununua ndege mbili ndogo aina ya Y12E, kwa mkopo nafuu wa Exim Bank kutoka China kwa Serikali ya Tanzania, kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 20”, alisema.Mbali na ndege hizo, pia Serikali kwa mujibu wa Dk Tizeba itanunua ndege mbili aina ya ERJ 170 na ERJ 190, zenye uwezo wa kubeba abiria 80 mpaka 100 kutoka nchini Brazil.“Ndege hizi zitanunuliwa kwa utaratibu wa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Brazil,” alisema Dk Tizeba na kusisitiza kuwa baada ya kupatikana kwa ndege hizo, ATCL itaanza kutumia njia zake za kimataifa kwa kuwa bado zipo. | uchumi |
Wachinjaji na wauzaji wanakwepa kushusha mifugo yao katika mnada wa Pugu kwa kutokuwa na vibali vya maeneo watokako na kusababisha ukosefu wa mapato kwa Serikali.Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo aliyasema hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Vingunguti na kuzungumza na wafanyabiashara na wachinjaji wa mbuzi na kuwaambia eneo hilo linatakiwa kufutwa kwa kuwa siyo rasmi kwa machinjio ya mbuzi.Alisema wanyama wote wanaotoka katika mnada wa awali wanahitajika kupelekwa katika mnada wa Pugu na kuhoji katika eneo la Vingunguti wanafanya nini.“Serikali ya awamu ya tano inasisitiza udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali ili kuhakikisha mapato yanapatikana kwa kila eneo ambapo ushuru unatakiwa kulipwa,” alisema Dk Mashingo na kuongeza maeneo mengine wanakouzwa mbuzi kiholela ni pamoja na Jangwani, Tegeta, Mbezi na Kariakoo.Alisema mbuzi wanaouzwa katika eneo la Vingunguti Relini hawalipiwi ushuru, wauzaji hawana vibali stahiki na pia huchinjwa maeneo yasiyo rasmi, hali hiyo ikisababisha serikali kupoteza mapato.Kuhusu sheria ya mifugo, Mkurugenzi wa huduma za afya ya mifugo, Dk Abdi Hyagaimo alisema sheria ya magonjwa ya mifugo namba 17 , inafafanua wazi kuwa wanyama wote wanaotoka katika mnada wa awali waletwe katika mnada wa upili ambao ni Pugu.Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika eneo hilo, wafanyabiashara walijitetea kuwa soko hilo lilianza kutumika kwa muda mrefu, hivyo ni vizuri wakaachiwa waendelee na biashara ya mbuzi na machinjio kwa kuwa wamelizoea na ndiyo tegemeo kwa maisha yao .Mfanyabaishara Yasini Shabani alisema kuwa tangu enzi za wazee wao walikuwa wanafanya biashara hiyo katika eneo hilo na kuomba eneo hilo liboreshwe na kuwa rasmi kwa biashara ya mbuzi na machinjio. | uchumi |
Lipuli iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 45 kupitia kwa Seif Abdallah akiunganisha pasi ya Malimi Busungu kabla ya kuachia shuti lililojaa wavuni.Dakika tatu za nyongeza ziliitosha Yanga kusawazisha bao hilo kupitia kwa Donald Ngoma aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kona wa Thaban Kamusoko. Mwanzoni mwa kipindi cha pili nusura Busungu aifungie Lipuli bao lakini mpira wa kichwa aliopiga akiwa kwenye nafasi nzuri, ukapaa na kutoka nje.Dakika ya 76, Kamusoko alikosa bao la wazi, akiwa yeye na kipa wa Lipuli, lakini kipa huyo Agathon Mkwano aliudaka mpira. Katika mechi hiyo, Lipuli inayonolewa na mchezaji na kocha wa zamani wa Simba, Selemani Matola, ilianza mchezo kwa kasi na kutawala katika kipindi cha kwanza ambapo katika dakika ya 21 ilifanya shambulizi kupitia kwa mshambuliaji wake Abdallah, lakini mpira wake wa kichwa haukulenga lango la Yanga.Dakika sita baadaye, Ngoma aliikosesha Yanga bao akiwa kwenye nafasi nzuri lakini alipiga vibaya mpira wa kichwa na kutoka nje. Yanga imecheza mechi hiyo ikitoka kufungwa kwa penalti 5-4 na mtani wake, Simba wiki iliyopita katika mechi ya Ngao ya Jamii kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi. | michezo |
MAKAMU wa Ris Samia Suluhu Hassan ameahidi viwanja vya kujengea nyumba kwa wachezaji wa timu ya soka ya Taifa ya wanawake, Twiga Stars endapo watafuzu michezo ya Olimpiki 2020, Japan.Twiga Stars ipo kwenye kinyang’anyiro cha kufuzu michuano hiyo, ambapo juzi ilicheza na Congo DR kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kutoka sare ya mabao 2-2.Mama Samia aliyasema hayo jana alipozungumza na wachezaji hao Dar es Salaam ambapo aliwapongeza lwa matokeo ya mechi yao na kuwatakia safari njema katika mechi ya marudiano keshokutwa.Twiga ilitarajia kondoka leo Alfajiri kwenda Kinshasa kwa ajili ya mechi hiyo matudiano itakayofanyika keshokutwa. “Wenzetu wanaume (Taifa Stars) walivyoshinda walipewa zawadi, na mimi nawaahidi mkishinda nitamwomba baba (Rais John Magufuli) awape zawadi kama wenzenu,” alisema. “Jana (juzi) ilikuwa nije lakini nilishindwa kutokana na majukumu ila kwa mara ya kwanza. nilikaa kwenye TV nikatizama mechi dakika zote 90 ingawa kuna wakati nilikasirika na kuna wakati nilifurahi” alisema.Mbali na ahadi hiyo Mama Samia alitoa sh 5,000,000 kwa wachezaji na benchi la ufundi kama mchango wake kwa safari. Aidha, Mama Samia ameahidi kuitafutia timu hiyo wafadhili.“Timu zote za taifa zina wadhimini, mimi kama mama yenu nitawatafutia wadhamini na naomba Jumatatu (kesho) viongozi wenu waje ofisini tuone cha kufanya,” alisema | michezo |
TIMU ya taifa ya riadha itakayoshiriki mbio za dunia za nyika zitakazofanyika Aarhus, Denmark, Machi 30 imetamba kurudi na medali kutoka katika mashindano hayo.Hayo yalisemwa jana na nahodha wa timu hiyo, Marco Sylivestre baada ya kukabidhiwa bendera ya taifa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Sylivestre alisema kuwa wanakwenda Denmark sio kushiriki ila kushindana na Watanzania watarajie mambo makubwa kutoka kwao kwani wamejiandaa vizuri katika kambi yao iliyokuwa jijini Arusha. Alisema makocha wao walikuwa na kazi nzito ya kuwafanyisha mazoezi na ni matumaini yao makubwa mwaka huu watarudi na medali kibao kutoka katika mbio hizo za nyika.Mwakyembe aliwataka wanariadha hao kwenda kupambana na kuhakikisha wanalitetea vizuri taifa katika kipindi hiki ambacho upepo mzuri umeibuka katika michezo nchini kwa timu zetu kufanya vizuri. Alisema kwa Watanzania wanataka kuona nchi inang’ara katika michezo mbalimbali na kurejea na medali kama walivyotamba Alphonce Simbu, ngumi za kulipwa na Serengeti Boys.Kambi ya timu hiyo ilidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na DStv, ambapo jumla ya wachezaji 16 na viongozi wanne wamo katika timu hiyo, ambayo ilitarajia kuondoka jana usiku kwa ndege ya KLM. Viongozi ni makocha Meta Petro na msaidizi wake Madai Jambau wakati meneja na mkuu wa msafara ni Dk Hamad Ndee na Marcelina Gwandu (Matroni).Wachezaji wanaounda timu ya wanaume wakubwa watakaochuana katika kilometa 10 ni Joseph Panga, Francis Damiano, Emmanuel Giniki na Gabriel Geay wakati wanawake wakubwa ni Failuna Abdi, Magdalena Shauri, Angelina Tsere, Mayselina Mbua na Natalia Elisante. Timu ya `relay’ inayoundwa na wachezaji mchanganyiko ni pamoja na Cecilia Giniki, Amina Migoo, Yohana Elisante na Sylivestre wakati timu ya vijana ya wasichana inaundwa na akina Anastazia Dolomingo na Aisha Magelani. | michezo |
Mkazi huyo wa Dodoma aliyekabidhiwa gari ni Ivan Mbogambi anayetoka Kongwa. Akizungumza katika hafla ya makabidiano ya gari yake, Mbogambi alisema: “Nina furaha kubwa leo kwani nimeweza kuwa mmoja wa watu wanaomiliki gari wilayani kwetu.Mimi ni mkulima wa hali ya chini leo hii Airtel imeniwezesha kubadili maisha yangu kwa kunirahisishia katika nyanja ya usafiri, mimi pamoja na familia yangu.”Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Betty Mkwasa alisema, “Ninafarijika sana kuona Watanzania kutoka kada mbalimbali wakiibuka washindi wa promosheni hii. Hii inaonesha ni namna gani Airtel wamejipanga kuboresha maisha ya watanzania.“Kingine ningependa kuwapongeza Airtel kwa kuweza kuboresha maisha ya watanzania kwani kumpatia mtu usafiri ni jambo jema sana itasaidia kuboresha maisha yake na familia yake kwa ujumla, “ alisema Betty.Promosheni hiyo bado inaendelea na kila siku mteja wa Airtel ana uwezo wa kujishindia gari moja kila siku kwa kujiunga na Airtel Yatosha ya siku, wiki au mwezi moja kwa moja anaunganishwa kwenye droo ya Airtel Yatosha na kupata nafasi ya kujishindia Toyota IST. | uchumi |
SERIKALI imeanza mchakato wa kupata wazabuni wa ndani na nje ya nchi wa kubangua korosho kwa lengo la kuharakisha uandaliwaji wake tayari kwa mauzo.Hivi karibuni Rais John Magufuli alitangaza nyongeza ya bei ya kununulia zao hilo kufikia Sh 3,300 kwa kilo huku akiliagiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kukusanya na kubangua korosho.Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye kikao kuhusiana na maonesho ya siku nne ya bidhaa za viwanda vya ndani yanayoanza leo Sabasaba wilayani Temeke, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda alibainisha kuwa uhitaji wa ubanguaji wa korosho hizo ni mkubwa.Kakunda amesema, kwa sasa viwanda vya hapa nchini vina uwezo wa kubangua tani 40,000 kwa siku huku uhitaji ukiwa ni mkubwa zaidi hasa kwa kipindi hiki ambacho serikali inanunua zao hilo.Alisema, kutokana na hali hiyo serikali inaendelea kuimairisha viwanda vya ndani kwa kuvijengea uwezo wa kubangua kiasi kikubwa cha korosho na wakati huo huo ikiendelea kuwasaka wazabuni hao.Katika kuhakikisha hatua ya serikali ya kununua korosho inawanufaisha wakulima, waziri huyo alibainisha kuwa zaidi ya walanguzi 20 wa korosho za wakulima wamefikishwa mahakamani.Alisema, wakati Serikali ikinunua korosho kwa Sh 3,300 kwa kilogramu, kuna walanguzi wamenunua korosho kwa Sh 600 na wanazipeleka kuuza kwa Serikali Sh 3,300 na vyombo vya dola vinawakamata.Alisema:“Rais John Magufuli hakufanya kosa kununua korosho kwa shilingi 3,300 lengo lake ni mkulima anufaike, sasa hao wanaolangua kwa wakulima na kuja kuuza kwa bei ya juu lazima wakomeshwe.”Alitoa mwito kwa walanguzi waliolangua korosho za wakulima kuwarejeshea korosho zao pamoja na fedha ili wakulima hao wakaziuze wenyewe na kunufaika na uamuzi wa Rais Magufuli wa kuuza korosho kwa bei ya Sh 3,300 kwa kilo.Waziri Kakunda akizungumzia zaidi kuhusiana na Manesho hayo ya Biashara yanayoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tantrade) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) chini ya kaulimbiu ya “Tanzania sasa tunajenga viwanda”, alibainisha kuwa yatahusisha washiriki 513.Alisema, pia kesho kutakuwa na Kongamano la kuhamasisha uwekezaji wa kuufikia uchumi wa kati kupitia ujenzi wa uchumi wa viwanda ifikapo 2025.Mwakilishi wa UNIDO nchini, Stephen Kargbo amebainisha kuwa shirika hilo limedhamiria kusaidiana na serikali katika kufikia adhma ya Tanzania ya viwanda huku akisisitiza kuwa litaendelea kusaidia na wazalishaji wa viwanda wadogo na wakubwa. | uchumi |
WILAYA ya Kongwa mkoani Dodoma imeanza mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/19.Mwenyekiti wa Baraza la Biashara wilayani humo, ambaye ni Mkuu wa Wilaya, Deogratias Ndejembi amesema hayo katika kikao cha baraza hilo.Ameongeza kuwa mkakati huo, utahusisha mnyororo wote wa thamani wa zao hilo, wakiwemo wazalishaji wa mbegu, wakulima, wenye viwanda vya kukamua mafuta ya alizeti na wanunuzi wa mashudu."Kitaitishwa kikao cha pamoja cha wadau wote ili kutanua uwigo wa mawazo kuona ni namna gani tunaongeza na kuboresha uzalishaji wa alizeti, " alisema Ndejembi.Takwimu inaonesha kuwa viwanda vyote vya alizeti wilaya ya Kongwa ni 99, lakini bado kuna uhaba wa mafuta, hali hii inaonesha kuwa bado wadau hawajajua juu ya kiwango cha mahitaji ya wateja wao,” alisema.Sebastian Msola ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Baraza hilo kupitia Sekta ya Kilimo alisema mahitaji ya alizeti bado ni makubwa kuliko uzalishaji. Alisema kwa mwaka alizeti inayopatikana kwa mahitaji ya viwandani ni asilimia 30 tu, yaani wasindikaji husindika kwa miezi mitano tu na miezi mingine saba hukaa bila kufanya shughuli yoyote.Ofisa Kilimo wilayani humo, Jackson Shija ambaye ni mjumbe kupitia Sekta ya Umma alisema bado mbegu bora ni changamoto kwa wakulima wa zao hilo.Changamoto nyingine ni kilimo kisichokuwa cha kitaalamu, uvunaji mbaya na uhifadhi.Shija alisema ipo haja ya baadhi ya viwanda, kupewa elimu juu ya kuvitunza kwani baadhi ni vichafu. Baraza hilo lilijadili mambo mbalimbali, ikiwemo utozaji wa tozo za mazao ya bustani kama miwa, vitunguu, nyanya na kabichi, tozo za karanga zilizobanguliwa.Shija alisisitiza kuwa gharama za tozo, ziendane na thamani ya mazao na si ujazo au uzito.Ndejembi ameunda kikosi kazi shirikishi, kikijumuisha wajumbe wa sekta ya umma, sekta binafsi na madiwani kwa kusaidiana na Mtendaji wa Baraza hilo, Luig Mbuya. Kikosi kazi hicho kitatafiti kitaalamu namna ya kutoza ushuru rafiki kwenye vyombo vya usafiri, ikiwemo mikokoteni ya wanyama, magari aina za pickup canter na fuso.Mwakilishi wa Mradi Unaosaidia Kuboresha Mazingira ya Biashara LIC (Local Investiment Climate), Donald Liya alilishauri baraza hilo kuwa lifanye utafiti za kitaalamu za uzalishaji, unaoendana na upatikanaji wa masoko. | uchumi |
NYOTA ya uwekezaji katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), imeendelea kung’aa na itazidi kung’aa mwaka 2019.Ripoti ya Benki ya Biashara ya Rand (RMB) ya Afrika Kusini, imeonesha kuwa Afrika Mashariki itakuwa kitovu cha uwekezaji barani Afrika mwaka huu. Hii ni kutokana na juhudi za nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara, reli hasa ya SGR, umeme, usafiri wa anga na uchimbaji wa mafuta na gesi, ambavyo ni vivutio vya uwekezaji duniani.Utafiti huo uliopewa jina la ‘Wapi Pa Kuwekeza Barani Afrika 2019’ ulihusisha kanda tano za bara la Afrika, za Kaskazini, Magharibi, Kati, Mashariki na Kusini, ukiangalia juhudi na mipango endelevu ya kuimarisha uwekezaji kikanda. Kwa mujibu wa utafiti huo, tangu mwaka 2017 hadi mwaka huu bara la Afrika limepiga hatua kutokana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na baadhi ya mataifa, ambazo zimesababisha kusiwe na ugumu katika upatikanaji wa fedha.Baadhi ya shughuli hizo ni vita dhidi ya rushwa, kuimarishwa kwa miundombinu yenye kuwasaidia wananchi katika kupata huduma mbalimbali na utawala bora. Kwa kuangalia nchi moja moja katika jumuiya hiyo, ripoti hiyo imeonesha kuwa Kenya imeongoza kwa nchi za kanda hiyo, kuvutia uwekezaji kuliko mataifa mengine. Sababu iliyotolewa ambayo iliisaidia Kenya kuwa kivutio kikubwa cha uwekezaji ni kufanyika kwa maridhiano ya kisiasa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi Mkuu wa Upinzani, Raila Odinga yaliyofikiwa mwezi Machi mwaka jana.Hali hiyo inatajwa kuleta mazingira bora ya kuvutia wageni wakiwemo watalii na wawekezaji katika sekta mbalimbali. Ripoti hiyo ilisema sehemu yenye msuguano wa kisiasa, baina ya watu wake, haivutii wawekezaji, badala yake inawafukuza. Nafasi ya pili ya kuwa na mazingira bora ya kuvutia uwekezaji, kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo, imechukuliwa na Rwanda.Taifa hilo limetajwa kuwa lenye uchumi unaokua kwa haraka na limeongeza mara mbili ya mazingira ya ukuaji wa uchumi wake katika kipindi cha miaka kumi. Kitu kingine kilichoifanya Rwanda kupata mafanikio hayo ni juhudi za serikali katika kuwekeza katika ukuaji wa viwanda, vinavyomilikiwa na wazawa na maendeleo ya teknolojia. Nafasi ya tatu imechukuliwa na Tanzania, kwa kuwa na mazingira rafiki ya uwekezaji wa ndani na kimataifa. Mambo yaliyotajwa katika ripoti hiyo yaliyoiinua Tanzania ni usimamizi mzuri wa kodi kwa wawekezaji.Vilevile Tanzania imesifiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na juhudi zake za kuanzisha kanda maalum za uwekezaji. Hali hiyo inatajwa kuwa inawasaidia wawekezaji kuwa na uhakika wa uwekezaji wa fedha zao. Pia, juhudi za serikali za kuwekeza katika miundombinu hasa ya barabara, miundombinu ya reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam kupitia Morogoro na Dodoma.Lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuunganisha reli hiyo hadi Mwanza, hali itakayorahisisha usafiri na usafirishaji kutoka na kwenda Kanda ya Ziwa. Tanzania imetajwa pia katika uwekezaji katika nishati ya umeme na gesi, kiasi cha kuwa kimbilio kwa wawekezaji wa kimataifa. Hii inashajihishwa na uwepo wa usafiri wa uhakika wa ndege, baada ya kufufuliwa kwa Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), ambayo mpaka sasa ina ndege saba.Nchi za Sudan Kusini na Burundi, zimetajwa kuwa ni zenye changamoto ya kiuwekezaji, lakini bado zinapewa nafasi kubwa ya kuwa vivutio vya uwekezaji kutokana na matukio ya kisiasa ya hivi karibuni. Kwa upande wa Sudan Kusini, muafaka wa kisiasa uliofikiwa baina ya serikali na wapinzani, umetoa uhakika wa kuwa na amani katika siku zijazo. | kitaifa |
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa, mauzo ya almasi hizo kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya ‘Williamson Diamond Limited’ yalifanyika nchini Ubelgiji kati ya Februari 2 hadi 9 mwaka huu na kuhudhuriwa na baadhi ya maofisa kutoka wizara hiyo.Amesema, katika mnada huo, jumla ya Karati 54,094.47 ziliuzwa, ambapo kampuni 145 zilishiriki katika mnada huo na kuwasilisha zabuni zao za ununuzi zipatazo 1,019, idadi hiyo ni nyingi kushinda zingine zilizowahi kuwasilishwa katika minada miwili ya awali.“Mrabaha wa awali uliolipwa kutokana na uthaminishaji kabla ya mauzo pamoja na ada ya ukaguzi, umeiwezesha Serikali kupata kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 1.7 kutokana na madini hayo, na hivyo kuchangia uchumi wa nchi yetu,” amesema Biteko.Mbali na hatua hizo, Serikali inatarajia kuanzisha utaratibu wa kufanya minada ya madini hayo na mengineyo hapa nchini ili kujiongezea wigo wa upatikanaji wa fedha za kigeni na kuitangaza Tanzania katika mataifa mengine.Amesema, uanzishwaji wa mnada huo kwa sasa, upo katika mchakato mzuri, huku akiamini kuwa kuanzishwa kwa utaratibu huo, utaliingizia taifa fedha za kigeni na kuitangaza kimataifa, pia itasaidia kukuza utalii wa nchi yetu.Biteko amewataka wananchi na wadau wa sekta ya madini, wenye nia ya kutaka kusafirisha madini kwenda nje ya nchi, kuomba vibali vya usafirishaji wa madini hayo katika Tume ya Madini.Amesema utaratibu huo unatokana na marekebisho ya Sheria za Madini za mwaka 2017 na kusainiwa kwa Kanuni za Madini za mwaka 2018 na Waziri wa Madini, inayotaka vibali hivyo kusainiwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini.Biteko amesema vibali hivyo vitaombwa kuanzia ngazi ya mkoa, hivyo kuwataka wadau wote wa sekta ya madini kuzingatia utaratibu huo ili kuepukana na usuambufu usio na tija.Katika hatua nyingine, serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), wataanza usajili wa vitambulisho kwa wachimbaji wa madini waliopo eneo la Mererani. Lengo la hatua hiyo ni kudhibiti wachimbaji wasio wazawa kuingia katika mgodi huo, hatua itakayosaidia pia ulinzi wa madini hayo ya tanzanite.Amesema, uandikishwaji wa vitambulisho hivyo, unatarajiwa kuanza Jumatatu ijayo hivyo kutoa fursa kwa wachimbaji hao na wananchi wengine kutoka wilaya ya Simanjiro, kupatiwa vitambulisho, vitakavyowasaidia katika shughuli mbalimbali. | uchumi |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya wa Kisarawe Mussa Gama amesema, kufunguliwa jengo la kisasa la abiria kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam ni fursa kubwa ya uchumi kwa wilaya hiyo.Amesema, kufunguliwa kwa jengo hilo kutaongeza idadi ya watalii wanaoutumia hivyo ni fursa ya kujenga hoteli za kisasa kwa kuzingatia ukaribu na urahisi wa kutoka Kisarawe kwenda JNIA.Kwa mujibu wa Gama JNIA upo umbali wa km 18 kutoka mjini Kisarawe na mtu anaweza akatumia takribani dakika 10 kutoka mjini hapo hadi uwanjani.“Ukiangalia hoteli nyingi zimekaa upande wa Dar es Salaam na Dar es Salaam sasa hivi wanaweza wakawa wanachelewa sana kwenda katika uwanja wa ndege lakini ukitokea Kisarawe kwenda uwanja wa ndege ni kilometa chache tu kwa hiyo kun fursa hiyo ya uwekezaji wa hoteli za kisasa” amesema Gama.Amesema, Kisarawe ni eneo sahihi la kujenga hoteli kwa kuwa kuna maeneo kwa ajili ya utalii wa haraka haraka wa siku moja au siku chache wakati mgeni anasubiri siku ya kusafiri kwa kutumia JNIA.Ametoa mfano kuwa, mgeni anaweza akashuka JNIA, akafikia kwenye hoteli iliyopo Kisarawe, akaenda kutalii Kisarawe kwa siku moja na kurudi uwanjanni hapo kuendelea na safari.Gama amesema, misitu ya Pugu na Kazimzumbwi inatumika kwa utalii wa picha, na utalii wa upandaji milima. | uchumi |
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga amesema maonesho ya kwanza ya viwanda mkoa wa Pwani mwaka uliopita yalikuwa na tija kubwa kwa wawekezaji wilayani humo.Amesema ofisini kwake kuwa, wilaya hiyo ilikuwa na washiriki wengi na wamejiandaa vizuri kushiriki maonesho ya mwaka huu yanayotarajiwa kufanyika kwa wiki moja kuanzia Oktoba 17.“Maonyesho ya mwaka jana yalikuwa na manufaa makubwa sana, wawekezaji wetu wengi waliyafurahia na waliyashukuru kwa sababu walipata nafasi kubwa ya kujitangaza na waliweza kufahamika na wengi wigo wa wateja wao umepanuka” amesema Sanga.Amewaeleza wafanyakazi kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuwa, Mkuranga itakuwa na washiriki wengi kwenye maonesho ya mwaka huu kwenye uwanja wa CCM Sabasaba.Ametoa mwito kwa wananchi, wajasiriamali na wawekezaji wakubwa kwa wadogo waende kwenye maonesho hayo kwa kuwa pia watu wengi hawajapata fursa ya kutembelea viwanda wilayani humo.“Ukifika pale kwenye eneo la maonyesho unaweza ukajua viwanda mbalimbali vinavyotengeneza bidhaa mbalimbali zilizopo ndani ya wilaya ya Mkuranga pia na kuona bidhaa zingine ambazo hazizalishwi ndani ya wilaya yetu ya Mkuranga…pia unaweza ukapata masoko”amesema. | uchumi |
HALI ya uzazi wa mpango nchini bado iko nyuma, jambo ambalo linahitaji kuwekewa nguvu kubwa, imeelezwa. Akizungumza katika mkutano uliozikutanisha asasi za kiraia, Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi ya Afya Tanzania, Salvatory Hokororo alisema jamii bado haina elimu ya kutosha.“Kulingana na takwimu za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, tuna asilimia 32 na tungependa kufikia asilimia 60, kwa hiyo kwa takwimu hizi ina maana kwamba bado tuko chini sana,” alisema.Alisema elimu ya uzazi wa mpango haijapewa msukumo mkubwa ndio maana haijasambaa kwa kiasi kikubwa. “Naona halijapewa msukumo mkubwa suala hili la elimu ya uzazi wa mpango, hasa kwa watu wanaohusika kusaidia suala hili, kwa mfano hata wanasiasa hawajui programu hizi na umuhimu wake,” alisema. Alisema umuhimu wa uzazi wa mpango ni pamoja na kumpa nguvu mwanamke kushiriki katika maendeleo ya kiuchumi.Alisema kama mwanamke akizaa kila wakati hawezi kupata muda wa kushiriki katika masuala ya kiuchumi, lakini watu hawajui hili wanaona mwanamke ni kama chombo cha kuzalisha. Aidha, alisema mwanamke anayezaa bila kufuata uzazi wa mpango anashindwa hata kuangalia familia yake, afya ya watoto wengine na usimamizi wa elimu. Alisema jamii iendelee kuelimishwa umuhimu wa kutumia njia za uzazi wa mpango kwani ni muhimu kwa maendeleo ya nchi na pia ya familia. | kitaifa |
ASASI za Kiraia zimesema licha ya muswada wa Sheria wa vyama vya siasa kuwa na baadhi ya vipengele vizuri, kuna haja ya vile vyenye upungufu kufanyiwa marekebisho kabla ya Bunge kuupitisha.Viongozi wa asasi za kiraia walisema jana Dar es Salaam kuna haja ya wabunge kuupa muswada muda wa kutosha kuuchambua kwa kina kabla ya kuupitisha kwani waathirika ni wao, wanasiasa na jamii. Fulgen Masawe kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) alisema baadhi ya maeneo mazuri kwenye muswada huo uliosomwa bungeni kwa mara ya kwanza Novemba 16 mwaka jana una kipengele cha kukataza vyama vya siasa kuanzisha vikundi vya ulinzi, kutoa mafunzo ya aina yoyote ya kijeshi, kiulinzi au yanayofanana na hayo kuepusha vitendo vya uvunjifu wa amani kwa siku za baadaye.Pia wamesifu uwazi katika matumizi ya fedha, mapato na matumizi na uwazi katika maamuzi ya vyama vya siasa kwa kuzingatia maamuzi yanatolewa na viongozi wa ngazi ya juu bila kushirikisha wanachama. Akiorodhesha upungufu kwenye muswada huo, Masawe alisema kifungu cha 5A kinataka Msajili kupewa taarifa kimaandishi na taasisi yoyote ya ndani ama ya nje ya Tanzania itakapotaka kutoa mafunzo ya kiraia ya kujenga uwezo kwa chama cha siasa na kutaja wahusika, malengo na nyenzo zitakazotumika.Msajili anayo nguvu ya kutoa kibali ama kukataa kufanyika kwa mafunzo hayo na endapo yatafanyika bila kibali, taasisi hiyo inaweza kupigwa faini ya mpaka Sh milioni 30 na watu watakaokutwa na hatia ya kwenda kinyume na kifungu hicho wanaweza kufungwa kati ya miezi sita mpaka mwaka mmoja gerezani. Kifungu cha 5B cha muswada kinampa nguvu, Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania kuomba na kupewa taarifa ya chama chochote cha siasa. “Ofisa wa chama cha siasa ambaye ataenda kinyume, yaani kutokutoa taarifa husika atakuwa ametenda kosa na akikutwa na hatia atapigwa faini ya Sh 1,000,000 mpaka Sh milioni 10 au kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miezi 12,”alisema Masawe.Alisema hata baada ya adhabu hiyo, ofisa huyo au chama hicho kitatakiwa kutoa taarifa zilizohitajika na iwapo taarifa itaendelea kuminywa, basi chama hicho kinaweza kusimamishwa ama kufutiwa usajili. Akinyumbulisha zaidi vipengele hivyo, Mkurugenzi wa Twaweza, Aidan Ayakuze alisema Msajili ni mteule wa Rais ambaye analipwa mshahara na serikali hivyo ni vigumu kutofungamana na upande mmoja. “Nchi ilikuwa na maslahi kipindi cha chama kimoja lakini tangu vyama vingi, wabunge wanaangalia maslahi yao na vyama vyao kuliko umma, wanaangalia hoja imetolewa na upande gani wanapinga.“Kifungu cha 6 cha muswada kinamlinda Msajili na wanyakazi wa ofisi yake dhidi ya kufunguliwa mashtaka: “Shauri halitafunguliwa dhidi ya Msajili, Naibu Msajili, Mkurugenzi au maafisa wengine chini ya Msajili kwa lolote watakalolifanya au kutolifanya kwa nia njema chini ya sheria hii,” alisema. Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS), Fatma Karume alisema “Wabunge wa CCM wanadhani wanalindwa na muswada huu, wanasahau sheria ni msumeno, wanaenda kwenye uchaguzi, wanapaswa kujua kuna kura za maoni ni rahisi kukatwa watu wasiopendwa bila demokrasia hivyo wawe makini,” Wakati asasi hizo za kiraia zikiendelea kukazia msimamo wake wa kutaka kufanya marekebisho kwenye muswada huo, tayari CCM kupitia kwa Katibu Mwenezi, Humphrey Polepole wameuunga mkono. | kitaifa |
EMMANUEL Amunike. Namuelewa kwenye namna nyingi za ufundishaji wake. Namuelewa kuwa ni kocha anayependa sana soka la mbinu na matokeo.Lakini leo ningependa kuelewa kile anachokifanya kwa kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto kwenye kikosi chake. Kama walivyo watu wengi ndivyo ilivyo kwa kocha Amunike. Anatambua kipaji cha ajabu alichonacho Fei Toto, anatambua utajiri uliopo kwenye miguu yake, akili ya mpira na namna alivyokomaa kabla ya umri wake.Yote Amunike anayatambua kuhusu kiungo huyu wa Kizanzibari. Lakini Amunike kama kocha aliyewahi kucheza soka kwa kiwango cha juu, anajua Fei Toto ana umri wa miaka 21 tu, anajua yeye ndiye kocha wa kwanza kumpa nafasi kwenye kikosi cha Taifa Stars kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Yote anafahamu fika kwenye mechi hiyo Amunike alimuingiza Fei Toto kuchukua nafasi ya kiungo Mudathir Yahaya na akabadili mchezo kwa kiwango kikubwa na Stars ikaibuka na ushindi wa mabao 2-0. Amunike anafahamu mechi na Lesotho kule Maseru ilikuwa mechi ya pili ya kimataifa kwa Fei Toto, pia alimuingiza kipindi cha pili tukiwa tumeshafungwa bao 1-0 na alionesha kiwango bora japo aliingia Stars ikiwa ishafungwa na zaidi muda ukiwa umekwenda sana. Lakini Amunike hataki kuingia kwenye mtego wa kumuona Fei Toto tayari ameshaiva.Ni kweli amekomaa haraka kiakili kinyume na umri wake. Lakini haiondoi ukweli kuwa linapokuja suala la timu ya taifa, Fei Toto bado chipukizi na anahitaji umakini mkubwa katika kumkuza na Amunike analifahamu hili. Mudathir, Himidi Mao, Jonas Mkude ambao wanagombania namba na Fei Toto kwenye timu ya taifa, wamecheza mechi nyingi zaidi yake. Hasa Himid na Mudathir.Amunike anaamini Himid na Mudathir wana uzoefu mkubwa zaidi ya Fei Toto lakini anaamini kinda huyo ana kipaji kikubwa kuliko viungo hao, hivyo anamkuza taratibu na kwa tahadhari asije kupoteza kipaji hiki maridhawa katika soka la Tanzania. Anamuingiza bado dakika 15 ama 20 anafanya yake. Mdogo mdogo anaizoea timu ya taifa, mdogo mdogo anapata uzoefu, mdogo mdogo anajua kubeba majukumu kwenye mechi za kimataifa.Ndio akili ya Amunike kwa Fei Toto ambapo kimsingi ni jambo zuri kwa wote wenye mapenzi mema na chipukizi huyu mwenye kipaji kikubwa kinachohitaji umakini mkubwa kukikuza. Hana muda mrefu Fei Toto ataingia kwenye kikosi cha kwanza Stars, lakini kwa sasa Amunike anapita kwenye njia sahihi sana za kumkuza.Isije ikatokea Himid ama Mudathir wakaumia na kuwa nje kwa kipindi fulani kwenye mashindano muhimu au wakaboronga kwenye mechi, hapa Fei Toto atakuwa keshaiva na akipewa namba ndio inaweza kuwa moja kwa moja. Namtazama Fei Toto kama nyota atakayekuja kupeperusha bendera ya Tanzania Ulaya kama anavyofanya nahodha wake Mbwana Samatta au hata akawa zaidi ya Samatta. Ana kipaji kikubwa, ni suala la muda tu. | michezo |
WAKATI kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars kikitarajiwa kuwakabili Kenya leo, Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema hatowadharau wapinzani wake.Katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza michuano ya Chalenji ya Baraza la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Kenya ambao walikuwa mabingwa watetezi walipoteza mabao 4-1 dhidi ya Eritrea na Tanzania ikipoteza bao 1-0 dhidi ya wenyeji Uganda.Hivyo Tanzania na Kenya zitacheza kuwania nafasi ya tatu na Uganda na Eritrea zitacheza fainali. Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo wa leo Mgunda alisema kitendo cha Kenya kupoteza mchezo uliopita kwa idadi kubwa ya mabao sio kigezo cha kuwadharau na kuingia uwanjani kwa uhakika wa ushindi bali watapambana wakijua mechi haitakuwa rahisi.“Hatuwezi kuwadharau Kenya kwa sababu wamefungwa, tutaingia kucheza nao tukijua itakuwa ni mechi ngumu lakini mwisho wa yote ni kuhakikisha tunatafuta nafasi ya tatu,”alisema.Katika mchezo wa kwanza Kili Stars ilikutana na Kenya kwenye hatua ya makundi na kufungwa bao 1-0. Huenda leo wakaingia kwa tahadhari kubwa ili kulipiza kisasi na hatimaye kupata matokeo mazuri. Pamoja na hayo, Mgunda alizungumzia namna alivyoumia baada ya kupoteza mchezo uliopita wa nusu fainali dhidi ya Uganda akisema hawana budi kukubali matokeo.‘‘Lazima niwapongeze wachezaji kwa jitihada japokuwa tulipoteza mchezo. Tumejipanga kutafuta nafasi ya mshindi wa tatu,”alisema.Kuhusu mechi ya fainali, katika mchezo wa awali wa makundi wa kundi A, Uganda iliishinda Eritrea mabao 2-0. | michezo |
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vya siasa nchini kutopeleka malalamiko yao katika vyombo vya habari kuhusu masuala ya uchaguzi na badala yake viwasilishe hoja hizo katika Kamati za Maadili za Uchaguzi.Imesema haina mfumo wa kushughulikia malalamiko ya uchaguzi kupitia vyombo vya habari badala yake imetaka utaratibu wa kisheria kufuatwa ili haki itendeke kwa wote. Mkurugenzi wa NEC, Dk Athuman Kihamia alisema hayo akiwasilisha mada ya Uboreshaji daftari la kudumu la wapigakura katika semina ya viongozi wa vyama vya siasa, dini, walemavu, vijana, wanawake, asasi za kiraia na watendaji wa NEC.‘’Pamoja na uwepo wa Kamati za maadili zenye mamlaka ya kutatua migogoro na kuweka mazingira sawa ya ushindani katika chaguzi ndogo, vyama vimekuwa havipeleki malalamiko yao kwenye kamati hizo bali hutoa malalamiko yao kupitia vyombo vya habari, ‘’ alisema. Alizitaja kamati zinazoundwa wakati wa uchaguzi kuwa za maadili ya uchaguzi, kamati ya rufaa, kamati ya maadili ya kitaifa, kamati ya maadili ya jimbo na kamati ya maadili ya kata.Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage alisema kifungu cha 15 (5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343 kikisomwa na kifungu cha 21 (5) cha Sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa kinaipa NEC mamlaka kuboresha daftari la kudumu la wapigakura. Alisema pia NEC iliendesha uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapigakura nchini ambapo kwa mkoa wa Kilimanjaro, iliongeza vituo vya kujiandikisha kutoka vituo 1,273 hadi 1,286.Mwenyekiti wa wanahabari Kilimanjaro, (Mecki), Bahat Nyakiraria aliomba tume kuhakikisha makundi maalumu yanapewa kipaumbele kama ilivyokusudiwa. Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), mkoa wa Kilimanjaro, Awadhi Lema alitaka NEC kutoa matangazo ili wale waliopoteza kadi za kura wapate kadi mpya. | kitaifa |
HOSTELI bubu katika maeneo ya vijijini zimetajwa kuwa ni moja ya chanzo cha mimba za utotoni katika Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.Sababu nyingine za mimba za utotoni ni wengi kutoka familia maskini hawana magodoro wanalalia mifuko ya salfeti au maboksi huku bajeti ya chakula ikiwa ndogo hali inayosababisha kuingia kwenye vishawishi.Wakizungumza wakati wa mafunzo ya vikundi vya malezi kwa wanaume wanaotoka katika kata za Berege na Kibakwe yanayotolewa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), walisema shule nyingi za sekondari ziko mbali na makazi hali inayosababisha wanafunzi kupanga mitaani.Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Mohamed Kizungu, mkazi wa kata ya Kibakwe, alisema wazazi wengi wanawapangishia vyumba watoto mitaani bila kujali watoto hao wana ulinzi kiasi gani. “Utakuta wengi hawana magodoro, wametandika mifuko ya viroba, visalfeti au maboksi wanalala chini, bajeti ya chakula ndogo, akikutana na kijana akimsaidia kidogo hapo ndio mambo yanaanza kuharibika,”alisema.Alisema watoto wanaishi nyumba za kupanga maeneo ya vijijini huku wakiwa hawana ulinzi wowote na nyumba nyingi wanazopanga zimejengwa kwa udongo huku madirisha na milango yake ikiwa si imara.“Mtoto wa namna hiyo hana ulinzi wowote ataenda disko na kwenye kumbi za video, serikali za kata zimekuwa zikiongelea sana suala hilo lakini mwisho wa siku wanashindwa kuchukua hatua,”alisema. Alisema kunahitajika hosteli kwa ajili ya mabinti, kuna hosteli za misheni lakini wazazi wengi wanashindwa kutokana na uwezo wao kwa kifedha kuwa mdogo.Pia alisema ukosefu wa uzio katika shule ya sekondari ya kata hiyo umekuwa ukisababisha vijana kuwanyatia wanafunzi hasa nyakati za jioni, jambo ambalo husababisha tatizo la mimba. Kwa upande wake, Baini Mkwangule kutoka kata ya Berege alisema tatizo la mimba za utotoni lipo kwa kiasi kikubwa na sababu kubwa ikiwa ni umaskini na huduma za jamii ikiwemo shule kuwa mbali na makazi. | kitaifa |
Mkataba huo umeingiwa rasmi jana katika Uwanja wa Taifa na kushuhudiwa na wanachama kutokea klabu mbalimbali za mchezo huo jijini Dar es Salaam.Meneja wa Mauzo na Masoko wa TSN, Januarius Maganga amesema, kwa kuzingatia mkataba huo, TEJA itanufaka na huduma bora za habari kutokea gazeti la Sports Leo, kwa kuwa taarifa zao zitakuwa zikiandikwa na gazeti hilo.Amesema, ushirikiano huo utaendeleza michezo kwa ujumla kwa kuwa kwa kuandika habari za michezo za klabu hiyo itaiwezesha kufahamika zaidi na kupata hata udhamini kwa wadau wengine wa michezo.Alisema: "TSN kupitia gazeti hili la michezo tumekuwa tukiendeleza michezo ya kila aina na kusaidia wanamichezo pia na leo hii tunayo furaha zaidi kuanza safari rasmi na TEJA inayolenga kuendeleza harakati zao za michezo pia."Aliongeza:"TSN kwa kuwa ni wadau wazuri wa maendeleo ya vijana katika nyanja mbalimbali ikiwamo ya michezo, hivyo TEJA itanufaika kwa njia mbalimbali kuanzia kuandikiwa kwa habari zao, makala, picha na hata kupewa ushauri wa kitaalamu kutokea kwa wanahabari mahiri wa michezo wa TSN".Mwenyekiti wa TEJA, Mussa Mtulya amesema, ushirikiano huo utaongeza zaidi hamasa ya michezo kwa wananchama, wakazi wa Temeke na hata wadau wote wa michezo kwa ujumla.Alisema: "TEJA ina wanachama wengi ambapo asilimia kubwa ni vijana, hivyo basi bidhaa hii ya TSN ya SpotiLeo kwa miaka mitatu tumeingia nao mkataba wa kuendeleza harakati zetu za michezo ni hatua muhimu kwetu".Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutokea Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Alex Nkenyenge aliyemwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Harrison Mwakyembe.Nkenyenge alipongeza harakati za SpotiLeo katika kuendeleza michezo hasa kwa kudhamini klabu hiyo na kusisitiza kuwa ushirikiano huo utakuza michezo kwa ujumla."Serikali imekuwa ikisisitiza suala zima la mazoezi na hawa Teja wamekuwa wakiendeleza michezo hasa kwa njia ya mazoezi na hivyo kusaidia kuimarisha afya za vijana ambao kimsingi ndio chachu ya maendeleo, “Sasa SpotiLeo mmefanya kazi nzuri kwenye uandishi wa michezo na kwa ushirikiano huu mmeonesha nia ya dhati kuendeleza ufanyaji wa mazoezi na michezo". | michezo |
Hayo yalisema juzi na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda wakati akifungua kikao cha kazi kilichofanyika Dar es Salaam na kuwashirikisha viongozi wa wizara na wakuu wa taasisi zake.Alisema katika kipindi cha mwaka juzi, sekta hiyo ilikua kwa asilimia 8.2, ikilinganishwa na asilimia 7.8 mwaka 2011. Pia, mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa, uliongezeka kutoka asilimia 9.7 mwaka 2011 hadi 9.85 mwaka 2012/2013.Alisema mwaka juzi sekta ya viwanda vidogo na biashara ndogo, ilichangia asilimia 27.9 katika pato la taifa na kuajiri watu milioni 5.2 wanaofanyakazi katika jasiliamari milioni tatu, asilimia 54.3 ya jasiliamari hizo zinamilikiwa na wanawake na 45.7 wanaume.“Pamoja na ukuaji wa sekta kuongezeka bado tuna changamoto kubwa kwani ongezeko hilo lipo chini ya lengo asilimia 15 lililoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo” alisema Dk Kigoda .Alisema wizara na taasisi zake, zinakabiliwana changamoto mbalimbali, ikiwemo ufinyu wa bajeti inayotolewana serikali, kodi, ushuru na tozo wanazotozwa wenye viwanda, gharama za kufanya biashara na uwekezaji,kutokana na kuongezeka kwa bei ya umeme na maji na kushuka kwa thamani ya shilingi.Alisema anaamini katika kikao hicho cha siku mbili, watatafakari mafanikio hayo na kuweka mikakati madhubuti ya kufanya vizuri zaidi katika kukuza sekta hiyo pamoja na kubainisha changamoto zilizokwamisha mikakati ya awali.Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Uledi Mussa alisema ili kukuza uchumi ni lazima serikali iwe na mchango mkubwa katika uendelezaji wa sekta ya viwanda na biashara na kushirikiana na taasisi binafsi.Profesa Samweli Wange kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema sekta ya Viwanda na Biashara, inatoa mchango mkubwa ingawa kila mwaka tunavyopanga haifikii malengo, mfano mwaka 1970 ilipangwa ikue kwa asilimia 15 na mwaka juzi ikue kwa asilimia 10, lakini mpaka sasa ni asilimia nane. | uchumi |
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu kulipa faini ya Sh milioni mbili au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, baada ya kutiwa hatiani kwa mashitaka ya kukutwa na kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.Sababu zilizochangia Wema kutiwa hatiani ni kitendo cha kukiri mwenyewe kwamba alikutwa na dawa za kulevya aina ya bangi nyumbani kwake, kukubali kwamba alipekuliwa, kusaini hati ya upekuzi na kukiri kuwa mkojo wake ulichukuliwa na kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, ambao ulikutwa na chembechembe za dawa za kulevya.Aidha, washitakiwa wenzake katika kesi ya kukutwa na dawa za kulevya na matumizi ya dawa hizo, Angelina Msigwa na Matrida Abbas wameachiwa huru baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema upande wa mashitaka ulileta mashahidi watano kuthibitisha mashitaka hayo. Alisema baada ya upande wa mashitaka kufunga ushahidi wake, washitakiwa wote walikutwa na kesi ya kujibu na washitakiwa walijitetea wakiongozwa na Wakili Albert Msando.“Ni jukumu la upande wa mashitaka kuthibitisha mashitaka bila ya kuacha shaka na sio mshitakiwa. Mshitakiwa wa pili na wa tatu hawakushiriki kwenye upekuzi na bangi zilikutwa jikoni, chumbani na kwenye kiberiti,” alisema Hakimu Simba.Alieleza kuwa mshitakiwa mwenyewe katika ushahidi wake alikiri kwamba alikutwa na bangi nyumbani kwake, alitia saini katika barua ya upekuzi na alikubali kwamba mkojo wake ulichukuliwa na kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.Alisisitiza kuwa anawaachia huru mshitakiwa wa pili na wa tatu kwa kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao, lakini kwa upande wa Wema hakuna shaka lolote kwamba amepatikana na dawa za kulevya.Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Constantine Kakula alidai kuwa matumizi ya dawa za kulevya yamekithiri katika Taifa na kwamba mshitakiwa ni msanii na ni kioo cha jamii ana watu wengi wanaomuangalia na kumfuata.Alidai mshitakiwa anatakiwa kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wanaotumia au wanaotegemea kujihusisha na dawa za kulevya. Akitoa utetezi kwa niaba ya Wema, Wakili Msando alidai kwa mujibu wa sheria aliyoshitakiwa nayo mteja wake kifungu namba 17 (1) b ya mwaka 2015, inaelekeza kwamba adhabu zake ni faini isiyopungua laki tano au kifungo cha miaka mitatu au vyote kwa pamoja. | michezo |
TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo inarusha kete yake ya pili kwenye michuano ya Afrika kwa kumenyana na Uganda kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Mechi hiyo ya kundi A inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kutokana na matokeo ya timu hizo katika mechi zilizopita ambapo zote zilipoteza. Wenyeji, Tanzania ‘Serengeti Boys’ walipoteza mechi iliyopita kwa mabao 5-4 dhidi ya Nigeria huku wenzao wa Uganda wakipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Angola. Hivyo kila mmoja anahitaji ushindi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu nusu fainali na kukata tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia kwa vijana wa umri huo.‘Wababe’ wa kundi hilo, Nigeria na Angola watacheza mapema kabla ya Serengeti Boys haijacheza na Uganda. Ushindi ni muhimu kwa mechi ya jioni leo, kwani timu itakayofungwa itakuwa imejitoa kwenye mbio za kuwania taji hilo. Uganda ambao watakuwa wenyeji kwenye mchezo huo wataingia wakijivunia kiwango bora walichokionesha kwenye mchezo dhidi ya Angola lakini sana ubora wa kipa wake Jack Komakech ambaye alikuwa kikwazo kwa washambuliaji wa Angola.Nguvu kubwa ya Uganda ipo kwenye eneo la kiungo ambalo linamtegemea zaidi Kawooya Andrew na Abdilwahid Idd kwa ajili ya kuwalisha mipira washambuliaji wao Ibrahim Juma, Rogers Mugisha na Najibu Yiga ambao wana kasi ya ajabu wanapokuwa mbele ya lango. Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo atakuwa na kazi ya kuwajenga kisaikolojia vijana wake ili kupata ushindi ambao utasaidia kuwarudisha mchezoni na kutimiza lengo la kufuzu fainali za Kombe la Dunia Brazil.Akizungumzia mchezo huo jana, Mirambo alisema amekiandaa kikosi chake vilivyo na amesharekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza. Kitu ambacho atatakiwa kufanya ni kurekebisha safu yake ya ulinzi pamoja na kipa ambae alionyesha mapungufu makubwa hadi kupelekea kupoteza mchezo huo tena kwa idadi kubwa ya mabao.Safu ya ushambuliaji pamoja na kiungo imeonesha kuwa ni moto kutokana na kazi nzuri ya kufunga mabao mengi kadri ilivyopata nafasi hasa kupitia kwa washambuliaji wake Edmund John na Kelvin John ambao walionyesha siyo wakufanyiwa mzaha. Ushindani kwenye mchezo huo wa kufa au kupona unatarajiwa kuonekana kwenye eneo la ushambuliaji kwa timu zote mbili ambazo zinajivunia ubora waliokuwa nao kwenye eneo hilo wakati safu zao za ushambuliaji zikionekana kuwa na mapungufu mengi.Mbali na kusaka ushindi lakini Tanzania ndiyo inadeni kubwa kwani ilishafungwa mabao 3-1 kwenye michuano ya kusaka kufuzu fainali hizo kwenye uwanja huo wa taifa hivyo hiyo itakuwa ni nafasi pekee ya kulipa kisasi kwa kushinda mchezo huo wa leo.Timu zote mbili zimekuwa zikitumia mifumo tofauti Uganda wanatumia mfumo wa 4-4-2 wakicheza kwa kushambulia huku wakitumia mipira mirefu wakati Tanzania wanatumia mfumo wa 2-3-3-2 kwa kupiga pasi nyingi hadi kufika kwenye lango la mpinzani hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake ingawa kwenye mapambano ya mmoja kwa mmoja Uganda inaonekana inaweza kushinda kutokana na maumbo makubwa waliyokuwa nayo wachezaji wao. | michezo |
HOSPITALI ya Benjamin Mkapa (BMH) iliyopo Dodoma inatarajia kuendesha kambi ya wiki mbili kwa ajili ya upasuaji wa matundu madogo (endoscopic surgery) kwa wanawake wenye matatizo ya uzazi na ngiri.Hayo yalielezwa jijini hapa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi katika hospitali hiyo, Dk Januarius Hinju. Alisema kambi hiyo ya wiki mbili itakayoanza Juni 7 hadi 21, mwaka huu, itaendeshwa kwa ushirikiano kati ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na madaktari bingwa kutoka Marekani.Dk Hinju alisema ili kupata fursa hiyo wanawake wenye matatizo ya uzazi, kutoshika mimba na ngiri kujitokeza sasa ili kufanyiwa uchunguzi wa kina na kuingizwa kwenye mpango huo. Alisema wananchi watakaokutwa na matatizo wataingizwa kwenye programu hiyo kwa kuwekwa kwenye ratiba ya kufanyiwa upasuaji wakati wa kambi hiyo ya wiki mbili.Akizungumzia upasuaji wa matundu madogo, Dk Hinju ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alisema uchunguzi na upasuaji kwa kutumia matundu madogo ni rahisi na husaidia tatizo la mgonjwa kubainika kwa haraka. “Upasuaji kwa njia ya matundu madogo ni wa kisasa ambao una faida kubwa kwa mgonjwa kulinganisha na upasuaji wa kawaida,” alifafanua.Dk Hinju alitaja baadhi ya faida hizo kuwa ni kutumia muda mfupi kurejea kwenye hali ya kawaida kutoka wiki sita za upasuaji wa kawaida hadi wiki mbili za upasuaji wa matundu madogo na vigumu kwa mgonjwa kupata maambukizi.Hii ni kambi ya pili iliyoendeshwa na Hospitali ya Benjamin Mkapa, ikiwa na lengo la kuimarisha huduma za kibingwa kwa mwaka wa pili mfululizo katika hospitali hiyo. Kambi ya kwanza kama hiyo ilifanyika Julai, mwaka jana, ambapo wagonjwa 26 walifanyiwa upasuaji kwa kutumia teknolojia hiyo ya kisasa ya kufanya upasuaji wa matundu madogo. | kitaifa |
SIKU ya jana ilikuwa ni siku ya huzuni na simanzi zilizotawala kwenye nyuso za waombolezaji waliofurika kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wa Chimwaga wakati wa kumuaga aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Egid Mubofu.Katika maombolezo hayo ambayo yalitanguliwa na ibada takatifu, waombolezaji walipata nafasi ya kutoa salamu zoa na hisia zao mbalimbali za huzuni kwa kiongozi huyo wa chuo kikubwa kinachodaili wanafunzi wengi hapa nchini. Pia watu walifikisha na kutoa hisia zao kwa mitindo mbalimbali ambapo kwaya ya Chuo Kikuu iliwafanya waombolzezaji kulengwa na machozi kutokana na kuimba wimbo maalumu uliochanganywa kwa lugha na miondoko ya kihehe na kugani, shairi lilioimbwa na mhadhiri katika chuo hicho. Profesa Mubofu aliyefariki dunia Desemba 18 mwaka huu, mjini Pretoria, Afrika Kusini alikokwenda kutibiwa. Amefariki akiwa na umri wa miaka 55. Akitoa salamu za rambirambo, Mkuu wa Chuo hicho ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Rais Benjamin Mkapa alimuelezea Profesa Mubofu kama mtu mzuri sana na mwenye ujasiri wa kufanya maamuzi. “Baada ya kukoma uongozi wa UDOM, uongozi ulitukuka wa Profesa Idris Kakula nikiwa mkuu wa chuo nawajibika kumteua makamu mkuu wa chuo mpya. “Na utaratibu ni kuorodhesha wasomi kadhaa waliostahili kufikiriwa, na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Nilipatiwa orodha ya watu wapatao 10 kutoka tume ya usahili na moja wapo alikuwa Profesa Mubofu. “ Baada ya kupima historia, usomi, ufanyaji kazi hasa katika sekta ya elimu, mafaniko kazini mahusiano na ushirikiano kazini. Heshima yake katika jamii na heshima ya jamii kwake. Nilimteua Profesa Mubofu na nilifanya hivyo bila mashaka yoyote. Alisema akiwa mkuu wa chuo hicho, ni mhimili mkuu lakini kiuhalisia kiongozi mkuu wa chuo ni makamu mkuu wa chuo kwa kuwa ndio mwenye mamlaka makubwa kwenye utawala, msimamizi wa utawala na mdhibiti mkuu wa chuo. Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako aliyeongoza maelefu kumuaga kiongozi huyo, alisema: “ Taifa limempoteza mtumishi wa umma mwenye bidii aliyeipenda nchi yake. Alitumia muda wake mwingi kukabiliana na changamoto zilizokuwa zinaikabili taasisi na wafanyakazi, “alisema Profesa Ndalichako wakati wa kumuelezea marehemu Prof Mubofu. Waziri alibainisha kuwa kwa muda mfupi tangu achaguliwe kwa nafasi ya Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Mubofu ameboresha uhusiano kati ya UDOM na vyuo vikuu vya nje na taasisi za kimataifa.Naye, Kaimu Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Peter Msofe alisema Machi, mwaka huu alisimama na kusoma wasifu wa profesa Mubofu, ikiwa ni miaka tisa, amesimama tena kusoma wasifu wake lakini sasa akiusoma kwa huzuni. Naye mwakilichi wa Jumuiya ya WanaUDOM (UDOMASA), Cosmas Mahenge, alisema Profesa Mubofu alikuwa ni kiungo muhimu wa kuunganishwa wafanyakazi na kukisimamia UDOM. Mwili wa marehemu jana mchana ulisafirishwa kijijini kwao Tanangozi, mkoani Iringa na unatarajia kuzikwa leo. Ameishi na mkewe na watoto watatu | kitaifa |
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi tatu zenye thamani ya jumla ya Sh milioni 6 kwa vikundi vitatu vya vijana, Diwani wa kata hiyo, Saidi Nassoro alisema pesa hizo ni za Serikali ambazo zinatokana na kodi za wananchi hivyo kila mtu ana haki ya kupata.Alisema, iwapo pesa hizo zitarudi kwa wakati, kupitia vikao vya Halmashauri ya Wilaya (DCC) atakuwa na nguvu ya kushawishi itolewe mikopo zaidi katika kata hiyo kwa sababu kuna vikundi vya vijana waadilifu na waaminifu.“Kama hatutarudisha kwa wakati, ina maana hata kiongozi wenu nitaambiwa kuwa kata yako tukileta mikopo hairudi kwa wakati..lakini nina hakika nyie mliokuwepo ni wazoefu, na hii pesa ni ndogo kwa hiyo nina uhakika mtairejesha kwa wakati ili tuweze kukopa zaidi,” alisema.Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kila kijana anapata mkopo kwa ajili ya kuendesha shughuli zake za kiuchumi lakini kutokana na ufinyu wa bajeti inalazimika kutoa kwa awamu na wanaporejesha na wengine ndio wanapata.Naye, Ofisa Maendeleo ya Jamii wa kata hiyo, John Samo, aliwataka vijana hao kwenda kuwa mabalozi wazuri kwa vijana wenzao ambao wanaamini kuwa mikopo hiyo inatolewa kwa upendeleo, kwa kuwaambia vigezo vinavyotakiwa ili kikundi kiweze kupatiwa mkopo.Alisema, kigezo kimojawapo ni kwamba lazima wajiridhishe kuwa vijana wanaounda kikundi lazima wawe na miradi ambayo tayari imeshaanza kufanyika na inaendelea, ili mkopo utakaotolewa uwe kwa ajili ya kuongeza nguvu katika mradi na sio kuanzisha mradi mpya.“Sasa kuna wengine wanakuja wakati hawana mradi wowote, wanataka ule mkopo wanaoupata basi ndio waende wakaazishie mradi, kitu ambacho kwa sasa hivi hali jinsi ilivyo inakua ni vigumu baadaye mtu kuweza kurejesha ule mkopo,” alisema Samo.Kwa upande wake, Katibu wa kikundi cha Five Group, Saidi Abdulbary akizungumza kwa niaba ya kikundi chake, ameahidi kurejesha pesa hizo kwa wakati huku akitoa msisitizo kwa vikundi vingine vya mafundi mchanganyiko na vijana, kufanya hivyo.Kikundi cha Five Group kilipata hundi ya Sh milioni 3, kikundi cha vijana reli kilipata hundi ya Sh milioni 2 huku kikundi cha mafundi mchanganyiko kikipata hundi ya Sh milioni 1. | uchumi |
['Polisi wanaochunguza madai ya ubakaji dhidi ya mchezaji wa Brazil Neymar wamesema wametupilia mbali kesi hiyo.', 'Ofisi ya mwanasheria wa São Paulo imesema kesi hiyo imetupiliwa mbali kutokana na kukosekana ushahidi, lakini suala hilo litapelekwa kwa waendesha mashtaka kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.', 'Uchunguzi ulianza baada ya mwanamitindo Najila Trindade alidai kuwa mchezaji huyo alimshambulia katika hoteli jijini Paris, Ufaransa, mwezi Mei.', 'Neymar amekana shutuma dhidi yake akidai kuwa amekuwa akifanyiwa hila.', 'Msemaji wa Neymar ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kuwa hakuwa tayari kuongelea uamuzi wa polisi.', 'Kesi hiyo ilitawala vichwa vya habari vya magazeti ya nchini Brazil.', 'PSG: Neymar anaweza kuondoka ', 'Neymar asusia mazoezi PSG - kunani?', 'Suala hilo kwa mara ya kwanza lilijulikana mwezi Juni, baada ya nyota huyo wa Paris St-Germain kuchapisha video ya dakika saba kwenye ukurasa wa Instagram ikiweka wazi kuwa anahusishwa na tuhuma za ubakaji. Pia alichapisha ujumbe wa Whatsapp na picha zinazodaiwa kuwa za mwanamke anayemshutumu.', "Katika video, anasema alilazimika kuweka hadharani ''kuthibitisha kuwa hakuna kilichotokea''.", 'Bi Trindade kisha akajitokeza hadharani kwenye mahojiano ya televisheni na kutoa picha na video fupi iliyoonyesha wawili hao wakizozana.', 'Polisi baadae walifungua kesi ya udhalilishaji dhidi ya bi Trindade.', 'Mwanamitindo huyo pia aliachwa na wanasheria kadhaa.', 'Waendesha mashtaka sasa wana siku 15 za kutathimini kesi kabla jaji hajatoa uamuzi wa mwisho.', 'Tuhuma', 'Bi Trindade ambaye pia ni raia wa Brazil alisema kuwa alikutana na Neymar katika mtandao wa Instagram.', 'Alikiambia chombo cha habari cha Brasil cha SBT kwamba alivutiwa na mchezaji huyo wa Brazil na alitaka kushiriki ngono naye.', 'Amasema kwamba alisafirishwa kutoka Paris na kulipiwa hoteli na mchezaji huyo.', 'Kilichokuwa kwenye video', 'Kanda ya Video inaonyesha mtafaruku kati ya bi Trindade katika chumba kimoja cha hoteli-ikidaiwa kuchukuliwa na bi Trindade.', 'Wawili hao wanaonekana wakiwa wamelala katika kitanda ambapo baadaye mwanamke huyo anasimama na kuanza kumpiga mwanamume aliyelala kitandani ambaye anajikinga na miguu yake.', 'Mwanamke huyo anasema nitakupiga, unajua kwa nini kwasababu umenipiga , mtafaruku huo ukionekana kuwa mkutano wao wa pili .', 'Neymar amesema kuwa yeye na bi Trindade walikutana mara mbili.', 'Katika mahojiano hayo ya Runinga ya SBT , Bi Trindade alisema kuwa alianza kuelewa kila kitu kilichofanyika baada ya mkutano wao wa kwanza ulipokamilika na kwamba alirudi ili kuthibitisha kitendo kilichofanyika huku akitaka haki kufanyika.', 'Kanda hiyo ya Video ilionyeshwa katika kituo hicho cha Brazil.'] | michezo |
KIWANGO cha ukatili wa kijinsia nchini Tanzania kimeongezeka huku mikoa nane ikitajwa kuongoza kwa ukatili dhidi ya watoto nchini. Mikoa iliyotajwa kuwa na kiwango kikubwa cha ukatili wa watoto ni Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Simiyu, Arusha, Kilimanjaro, Tabora na Singida.Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Malezi Chanya, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Thrive For Community Elevation Foundation (TCE), Marynsia Mangu alisema utafiti uliofanywa na Haki za Binadamu (LHRC) na Jeshi la Polisi nchini mwaka 2016 inaonesha watoto 10,000 walifanyiwa ukatili huku mwaka 2017 watoto zaidi ya 13,000 walifanyiwa ukatili ikiwa ni zaidi ya asilimia 100.Alisema ukatili wa kijinsia uliotokea utotoni ni mkubwa kwani wasichana watatu kati ya 10 na mvulana mmoja kati ya saba walisema walifanyiwa ukatili wa kijinsia kabla ya kufikisha miaka 18.“Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita asilimia sita ya wavulana Tanzania wenye umri kati ya miaka 13 hadi 17 wanasema walifanyiwa tukio moja la ukatili wa kijinsia, kiwango cha ukatili wa kijinsia kwa wasichana wa Kitanzania ni mara mbili zaidi asilimia 14,” alisema.Mangu alisema zaidi ya asilimia sita ya wasichana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 24 ambao walipata mimba wanasema angalau ujauzito mmoja ulitokana na kufanyiwa ukatili wa kijinsia. Ukatili wa kijinsia ulifanyika mara nyingi kati ya waathirika wa ukatili wa kijinsia, takriban wasichana wanne kati ya 10 na wanaume watatu kati ya 10 wanasema walifanyiwa ukatili wa kijinsia mara tatu au zaidi kabla ya kufikisha miaka 18 huku asilimia 91 walifanyiwa ukatili wa kingono.Alisema kufuatia takwimu hizo zimesababisha kuanzisha kampeni hiyo ya malezi chanya ambayo inalengo la kuwakumbusha wazazi umuhimu wa kuwa karibu na watoto wao, kuwasikiliza kwa kuwa unyanyasaji wanaofanyiwa watoto ni kutoka kwa watu wa karibu ambao ni baba, mama, shangazi, mjomba, binadamu na watu wengine wa karibu na familia.Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye ni mwandishi na mchambuzi wa masuala la kijinsia, Richard Mabala maarufu ‘Mabala the Farmer’ alisema lazima jamii na Serikali wahakikishe watoto wa kike na kiume wapo salama. Awali mgeni rasmi alikuwa awe Mama Salma Kikwete ambaye katika taarifa yake alisisitiza umuhimu wa kampeni hiyo kwa wazazi na jamii kwa ujumla kwani inasikitisha kuona vitendo vya ukatili kwa watoto kimwili, kiakili na kihisia vinaongezeka siku hadi siku. | kitaifa |
“NAIPONGEZA timu nzima ya Mkoa wa Arusha iliyobuni mtihani wa pamoja kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa mkoani ambao sasa unasaidia wanafunzi kukuza vipaji vyao na kuwawezesha kuongeza ufaulu zaidi.”Ndivyo anavyosema Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anapozungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa kuboresha elimu mkoani humo, zikiwa ni juhudi za kusaidia mkoa huo kuendelea zaidi kielimu hali iliyouwezesha kushika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2018.Katika mpango huo uliozinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za binafsi na za serikali mkoani humo, watafanya mtihani mmoja unaofanana kwa shule zote kadiri ya madarasa yao. Mpango huo ni matokeo ya juhudi za mkuu wa mkoa huo, watendaji na wadau mbalimbali wa elimu mkoani humo kushirikiana kutatua changamoto za walimu wa shule za msingi na sekondari.Katika kufikia mafanikio hayo, mara kwa mara Gambo amekuwa akifanya vikao na walimu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro pamoja na maofisa elimu na waratibu wa elimu kata. Vikao hivyo na wadau wa elimu wa Mkoa wa Arusha vimekuwa vikilenga kuhakikisha hakuna mazingira yanayokwamisha walimu kufundisha darasani au watoto kutosoma masomo yote. Uchunguzi umebaini kuwa, juhudi hizo za Mkuu wa Mkoa wa Arusha na viongozi wengine wa mkoa, ndizo zimewezesha Mkoa wa Arusha kushika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya darasa la saba ya mwaka huu.Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega anasema mpango huo umesababisha kuwapo matokeo chanya ya darasa la saba mwaka huu. Mkoa huo wenye walimu wa shule za sekondari 4,950, mwaka 2017 ulishika nafasi ya saba katika matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi. Mwaka 2016 ulishika nafasi ya sita. Kwitega anasema mpango ulianza kutekelezwa mwaka 2017 kwa kuanzisha mtihani wa mihula kwa shule zote za sekondari na za msingi.“Tumejifunza mambo mengi katika mpango huu wa uboreshaji wa elimu na baadhi ya masomo vijana wanafaulu vizuri huku masomo mengine wakishindwa kufaulu kutokana na walimu kutofundisha vema,” anasema. Akizindua mpango wa kuboresha elimu uliobuniwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo pamoja na wadau wa elimu wakiwemo viongozi wa dini, Waziri Jafo anaupongeza mkoaa kwa kuzindua mpango wa uboreshaji wa elimu kwa shule za msingi na sekondari.Anasema kutokana na mkoa huo kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba, ameandaa vyeti maalumu kwa mikoa mitatu iliyofanya vizuri ikiwemo wa Arusha ili kuwapongeza walimu na wadau wa elimu kwa kuuwezesha kuwa mkoa wa tatu kitaifa katika masuala ya elimu. Anawataka wadau hao kujipanga vema zaidi na kuongeza juhudi kuboresha elimu ili mkoa huo ushike nafasi ya kwanza kitaifa.Anasema uzinduzi wa mpango wa elimu ni ajenda ya kumkomboa mtoto masikini kwa kuwa Rais John Magufuli amekuwa akitoa Sh bilioni 23.5 kila mwezi kwa ajili ya elimu bila malipo akilenga kuwakomboa watoto wa Kitanzania. Anasema mitambo ya kuchapia mitihani ya pamoja iliyopo mkoani hapo, pia itasaidia kuondoa kero ya walimu kuandika mitihani ubaoni. Imebaini kuwa, mpango huo pia unaondoa majigambo ya baadhi ya walimu kudai wamefaulisha vizuri wanafunzi wao, na badala yake umewezesha shule mbalimbali kufanya vema katika kukuza viwango vya ufaulu kwa wanafunzi.“Jambo hili likisimamiwa vizuri Mkoa wa Arusha utaacha mikoa mingine kwa ufaulu na nawaomba wakuu wa mikoa wengine kuiga mfano wa mkoa huu katika kuboresha sekta ya elimu nchini,” anasema Waziri Jafo. Waziri anamhimiza Mkuu wa Mkoa (Gambo) kuainisha wanafunzi wanaofaulu vema sambamba walimu wanaofanya kazi vizuri ili wapewe zawadi za kiwilaya na kimkoa na kuwataka pia kuandaa siku maalumu ya elimu ili kuhamasisha elimu.Anasema walimu na madaktari ni watu muhimu katika jamii, hivyo hawana budi kupewa motisha sambamba na kuepushiwa adhabu zinazoshusha utu na ari yao ya kazi. “Mwalimu ndiye mtu anayemwandaa mtoto kiakili na anamjenga, hivyo lazima walimu wasikilizwe na wasaidiwe kutatua kero zao…” anasema. Anausisitiza Mkoa wa Arusha kubuni mkakati mwingine wa kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kuandaa jukwaa maalumu la mjadala wa kimaarifa ili kushindana kihesabu, kisayansi na kihistoria, hali itakayochochea ongezeko la maarifa ya wanafunzi.Gambo anasisitiza kuwa, mpango wa kuboresha elimu mkoani Arusha umewezesha kutatuliwa changamoto za ufaulu wa mitihani, likiwamo suala la kutofundisha mada zote na kusisitiza walimu kutunga mitihani kulingana na silabasi wanazofundisha. Awali katika mitihani ya nusu muhula kwa kidato cha kwanza hadi cha tatu kila halmashauri ilionesha hakuna halmashauri iliyofikia asilimia 50 huku somo la Sayansi likiwa na wastani wa asilimia 30 na Fikizia wastani asilimia 44. Kwa somo la Hisabati kidato cha kwanza asilimia 20, kidato cha pili asilimia 13 na kidato cha kwanza asilimia 10.“Kama ungekuwa ni utafiti, tungesema wamefaulu katika utafiti, lakini kutokana na matokeo haya tunasema hapana lazima sasa tufanye jambo la kuboresha elimu kwa Mkoa wa Arusha,” anasema Gambo. Anasema siku ya Ijumaa, masomo huisha saa sita na yanapoisha, kila mwalimu mkuu na mkuu wa shule akae na walimu wa masomo yote kujua kwa nini mwalimu husika hajafundisha somo lake kama lipo. Anasema mwalimu akieleza sababu, lazima zitatuliwe ili kuboresha elimu na waratibu wa elimu kata waangalie changamoto za walimu na kuzitatua, ikiwemo kuziwasilisha kwa maofisa elimu katika halmashauri zote.“Maofisa elimu nendeni mkajue hao wengine wana changamoto gani maana kuna mahali utakuta shule haina vyoo, mazingira yake si rafiki sasa lazima uangalie tatizo lipo wapi na siyo suala la kusimamisha tu, walimu,” anasema Gambo. Anasema: “Mfano, katika Shule ya Msingi Mkonoo kulikuwa na ukosefu wa vyoo walimu walikuwa wakichangia vyoo na wanafunzi. Nilipofika pale Aprili mwaka huu kuangalia yale mazingira, nilihuzunika sana…” “Nilichofanya ni kumchukua Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni ili ajionee hali halisi ya maisha ya walimu hawa na ndipo nilipohakikisha Halmashauri ya Jiji inatenga milioni kadhaa kwa ajili ujenzi wa matundu ya vyoo zaidi ya 20 nimeongeza hapo.”Mchakato wa Mpango wa Elimu ulianza mwaka 2017 kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, hivyo badala ya kununua mashine kwa Sh milioni 20 tulinunua mashine 10 za kuchapisha mitihani kwa Sh milioni 7. Katibu Tawala wa Mkoa (Kwitega) anasema mkakati mwingine ni kuwezesha wazazi kuwa na utaratibu wa kusoma vitabu na watoto wao kwenye maktaba zilizopo mkoani humo.Theresia Mahongo kwa niaba ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri, anasema awali aliona mpango huo hauwezekani, lakini kwa juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, umefanikiwa na kuzaa matunda chanya. Naye Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK), Dk Stanley Hotay anaiomba serikali kuhakikisha mitaala inayotolewa ya kuanzia elimu ya msingi na sekondari inamjenga na kumwandaa mtoto kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa. Mwalimu Ambrose Bashayija kutoka wa Shule ya Edmund Rice iliyopo katika Kata ya Sinon, anasema awali shule za binafsi zilikuwa zikikabiliwa na uhaba wa vifaa vya kuchapisha mitihani pamoja na udanganyifu wa ufaulu, lakini mpango huo utawezesha walimu kujulikana kama kweli wanafundisha vipindi vizuri darasani ama la. | kitaifa |
MTOTO wa tembo mwenye umri wa chini ya mwaka mmoja aliyeokolewa baada ya kutumbukia na kunasa kwenye tope shimoni ndani ya Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa, anatibiwa katika kituo cha kupokea wanyamapori yatima cha Makoa Farm Vertinary clinic mkoani Kilimanjaro.Kituo hicho kipo Machame wilayani Hai huku hali ya tembo huyo ikielezwa kuwa inaendelea kuimarika.Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Mawasiliano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa), ikimkariri Mkurugenzi Mkuu wa Tawa, Dk James Wakibara, imesema mtoto huyo wa tembo amesafirishwa kwa ndege ya Kampuni ya Northen Air Transport yenye namba za usajili 5G- DEB ambayo ilitolewa na Rusell Hasting wa shirika la Freidkin Conservation lenye makao yake jijini Arusha.“Januari 13 mwaka huu, ofisi yangu iliwasiliana na wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri), Idara ya Wanyamapori na Shirika la Uhifadhi la Wildlife Conservation Society(WCS) na kufikia uamuzi tumsafirishe kwa ndege hadi Arusha saa 10:00 jioni,” alisema Dk Wakibara.Alisema Januari 11 mwaka huu, uongozi wa Pori la Akiba Lwafi walipokea taarifa kutoka kwa Salum Summy ambaye ni mmiliki wa shamba la Msipazi linalopakana na pori hilo katika Kijiji cha Kate, kuhusu kunasa kwa mtoto wa tembo kwenye tope aliyetumbukia ndani ya shimo eneo la chini ndani ya pori hilo.“Salum alipata taarifa hizo kutoka kwa wafanyakazi wake waliokuwa jirani baada ya kusikia tembo wakipiga kelele kwa sauti zaidi ya saa moja, baada ya kufuatilia wakaona kundi kubwa la tembo wakijitahidi kumtoa mtoto wao kwenye shimo,” alisema na kuongeza:“Kwa vile tembo walikuwa wengi watu hao hawakuweza kuwasogelea, hivyo waliamua kuwasiliana na uongozi wa Pori la Lwafi kuhusu tukio hilo”.Aliongeza kuwa waliwasiliana na Mkuu wa Kanda ya Lwafi, Asubuhi Kasunga na kumtaarifu kuhusu mkasa huo ambapo bila kuchelewa, aliondoka akiongozana na askari wanne wakiwa na silaha na mahema kwenda eneo la tukio, ambako walifika saa 5:00 usiku na kupata taarifa ya awali toka kwa mashuhuda wa tukio hilo.“Kwa vile ilikuwa usiku sana na kuhofia kuwepo kwa tembo wengine jirani walisubiri hadi kupambazuke alfajiri ya Januari 12, mwaka huu, walifuatana na wafanyakazi wa shamba pamoja na wanakijiji jumla walikuwa 11.“Walifika eneo la tukio na kumkuta mtoto wa tembo mwenye umri chini ya wa mwaka mmoja akihangaika kutoka shimoni. Jitihada za kumuokoa zilifanyika baada ya kupanga mawe ndani ya shimo bila kumdhuru mtoto na hatimaye walimtoa,” alisisitiza Dk Wakibara.Alisema baada ya kumtoa walimpelea hadi Kambi ya Shamba la Msipazi, ambako aliwahoji wafanyakazi wa shamba hilo ili kujua tembo wanaonekana muda gani kusudi wamrudishe mtoto kwenye kundi, ambako walidai kawaida wanapita eneo hilo saa 4:00 usiku.“Muda wote walikuwa wakiwasiliana na daktari wa tiba za wanyamapori toka WCS, Elizabert Stigmaier kutoa ushauri wa chakula cha kumlisha mtoto huyo maana alionekana amechoka. Wakaelezwa wampatie glucose aina ya DNS na aliwaeleza jinsi ya kumpa ili apate nguvu,” alieleza. | kitaifa |
CHAMA cha Riadha nchini (RT), kimetoa baraka kwa wandaaji wa mbio za kujifurahisha Mbezi Fun Run zilizopangwa kufanyika Desemba Mos, jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa RT, Willihelmi Gudagudai amesema leo Alhamisi kuwa RT imetoa kibali kwa wandaaji hao baada ya kufuata taratibu zote."Tumewataka baada ya tamasha lao, wawasiliane na RT ili mbio zao ziingizwe kwenye kalenda ya mwaka ya matukio ya RT, " alisema.Kwa upande wa waandaji hao kupitia kwa katibu Mbezi Fun Run Omary Kimbau alisema mandalizi ya mbio hizo yamekamilika kwa asilimia 90 mpaka sasa, na kwamba kuanzia leo (Alhamisi) wataweka wazi vituo mbali mbali vya kujiandikisha kwa yeyote anayependa kushiriki."Kushiriki ni bure, hakuna kingilio chochote na mlango upo wazi kwa yeyote, ila kuna tisheti na beji kwa wakimbiaji, beji shilingi 10,000 na atakayependa kutumia fulani zetu bei ni shilingi 25,000."alisemaKimbau alisema mbio hizo zimeandaliwa na umoja wa wakazi wa Mbezi Beach zikiwa na lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo na kusaidia kwenye changamoto mbali mbali huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Ummy Mwalimu.“Kama mnavyojua siku hiyo ya Desemba Mosi itakuwa ni siku ya Ukimwi duniani hivyo pia tumemualika Waziri Ummy Mwalimu awe mgeni rasmi na tutafanya nae mazoezi ya pamoja, na pia kutakuwa na zoezi la uchangiaji damu.“Damu salama inahitajika kwenye banki ya damu, kama haijanisaidia mimi itamsaidia ndugu yangu, jamaa au mtanzania yoyote yule, hivyo tumeona siku hiyo pia tuitumie kuchangia damu salama na pia kupima afya yetu kwa kupima maambukizi ya virusi ya ukimwi.” alisemaNaye mwakilishi kutoka kitengo cha afya Angaseege Getruda Kafuko, akizungumza kwa niaba ya mganga Mkuu wilaya ya Kinondoni alisema wamefurahishwa na uamuzi wa waandaaji wa Mbezi Fun Run kuona umuhimu wa kuchangia damu. | michezo |
HAYAWI hayawi sasa yamekuwa, baada ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), kupewa kibali rasmi cha kuanza safari za ndege zake kwenda nchini India.Akizungumza na Habarileo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladslaus Matindi alisema ni kweli wamepewa kibali cha kuanza safari za ndege zake nchini India, kilichotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa nchi hiyo.“Tunashukuru, ni kweli tumepewa kibali cha ndege za ATCL kufanya safari nchini India, kibali kimetolewa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa nchi hiyo, kwa sasa hali ni hiyo ila taarifa zaidi tutazitoa baadaye,”alisema Matindi. Miezi michache iliyopita, akizungumzia kuchelewa kuanza kwa safari hizo nje ya nchi, Matindi alisema ni kutokana na mambo ya msingi yaliyokuwa yakifanywa, ikiwemo nchi kurudishwa katika Jumuiya ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (IATA).“Tulipanga kuzindua mapema safari za nje, ila tulichelewa kwa sababu ya kukamilisha mambo ya msingi yaliyohitajiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (IATA)ambayo kwetu kwa sasa tumeshafikia mwisho,” alisema Matindi. Hata hivyo, ATCL kupitia kwenye mtandao wao yapata miezi kadhaa sasa, imekuwa ikitangaza bei za safari za ruti hiyo ya kwenda India katika jiji la Mumbai, ambapo wamesema bei ya kuanzia itakuwa dola 286 kwa daraja la kawaida na dola 455 kwa daraja la kwanza.Mapema mwaka huu akizungumzia ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 282, ambayo ni moja ya ndege mpya zilizonunuliwa na serikali kwa lengo la kuboresha huduma za usafiri wa ndani na nje ya nchi, Matindi alisema ndege hiyo inaendelea na safari za ndani; na muda wowote kuanzia sasa watafanya uzinduzi wa safari za nje, ambako watazindua ruti ya kwenda Mumbai, India.Akizungumzia safari za nje ya nchi, mwishoni mwa mwaka jana, Msemaji wa ATCL, Josephat Kagirwa alisema huo ni mpango mkakati wa ATCL wa miaka mitano, ulioanza mwaka 2017. Kagirwa alisema mkakati huo ni kuongeza huduma za usafiri wa ndege wa ndani na nje na kwamba mkakati huo utaboresha huduma za kampuni hiyo. “Bei zetu kwa kuanzia ni zitakuwa dola 286 kwa safari ya kwenda au kurudi pekee, huku safari ya kwenda na kurudi itakuwa dola 455 za Marekani”, alisema Kagirwa.Akizungumzia kwa nini wataanza safari kwenda Mumbai, India, Kagirwa alisema wameangalia uhitaji wa soko, ambalo aliesema kwa utafiti waliofanya, kuna wateja wengi wanaotaka ruti ya moja kwa moja kwenda jiji hilo. Alitaja sababu nyingine ni uhusiano wa muda mrefu baina ya India na Tanzania huku akisisitiza kuwa fursa za biashara, pia ni nyingi sambamba na wateja wanaokwenda kupata matibabu na elimu nchini humo.Kwa sasa ndege za ATCL zinafanya safari za kwenda Zambia, Zimbabwe na kwingineko, wakati maandalizi ya kuendea na safari nyingine za nje ya bara la Afrika ikiwemo Thailand, China na India kwa ndege ya Dreamliner na ndege nyingine mbili aina ya Airbus 220-300 yakiendelea. Hadi sasa kampuni ya ATCL ina jumla ya ndege mpya sita, ambazo ni Bombadier Q 400 tatu, Boeing 787-8 Dreamliner moja , A220-300 mbili.Mwaka 1977 ATCL ilikuwa na ndege tisa, lakini kutokana na usimamizi mbaya kampuni hiyo ilishindwa kuendelea kutoa huduma za usafiri ipasavyo. Mwaka 1994 iliunganisha nguvu na kampuni za ndege za Uganda na Afrika Kusini, ambapo zilifanya kazi kwa miaka sita hadi mwaka 2000, ilipotangaza kupata hasara ya Sh bilioni 50. Mwaka 2007serikali ililichukua shirika hilo lililoendelea kwa kusuasua. Mwaka 2015 baada ya Rais John Magufuli kuingia madarakani, moja ya ahadi zake ilikuwa ni kununua ndege mpya, jambo alilotekeleza na hadi sasa zimeshanunuliwa sita. | kitaifa |
KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma imeiagiza Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuhakikisha inapeleka vifaa tiba na dawa katika vituo vya afya vilivyokamilika.Pia wauguzi na wataalamu wa afya, wametakiwa kutoa huduma kwa kuzingatia weledi, kama ambavyo kanuni za taaluma yao zinavyoelekeza.Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa, Godwin Mkanwa wakati wa akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali wilayani Chamwino mkoani Dodoma.Amesema jambo la kushangaza ni kuwa ingawa serikali ilitoa siku moja fedha za ujenzi na za vifaa tiba, MSD wanashindwa kupeleka vifaa na dawa kwenye vituo vilivyokamilika.Alisema kutotimiza wajibu kwa MSD hakuendi sambamba na dhamira ya Rais John Magufuli ya kuwaletea wananchi maendeleo, hasa katika kuboresha sekta ya afya nchini."Nawaagiza MSD mpeleke vifaa mara moja katika vituo vya afya vilivyokamilika ili viweza kufanya kazi na wananchi wapate huduma kama ilivyokusudiwa," alisisitiza Mkanwa.Aidha, Mkanwa alikemea tabia ya baadhi ya watoa huduma kutumia lugha chafu na kuhimiza kufanya kazi kwa upendo, huruma na uadilifu, hali ambayo itawafanya wananchi watatamani kufika katika vituo vya afya na kupata huduma."Ninyi mko Ikulu hivyo kituo chenu kinatakiwa kuonyesha mfano kwa kuwa kituo bora kabisa, na si kujaa malalamiko na sifa mbaya kutoka kwa wagonjwa," alisema.Pia alitumia fursa hiyo kupongeza ujenzi wa majengo mazuri na yenye ubora, yanayodhihirisha thamani ya fedha iliyotolewa na serikali na aliwataka kuyatunza vizuri.Akiwa wilayani Kongwa, Mkanwa alimtaka mkandarasa kuhakikisha anamaliza ujenzi wa Kituo cha Afya Ugogoni ifikapo Februari 4 mwaka huu na kukabidhi majengo kwa uongozi wa wilaya.Kituo cha Afya cha Ugogoni kimejengwa kwa thamani ya Sh milioni nne ambazo zimetolewa na serikali.Pia alikagua majengo ya mradi wa machinjio ya kisasa ya kuku katika eneo Mbande, njia panda ya Kongwa; na mradi wa maji katika mji wa Kongwa.Ametoa maelekezo mbalimbali za uboreshaji wa miradi hiyo. Mkanwa alielekeza kutolewa vyeti na motisha kwa wajumbe wa kamati, wanaosimamia ujenzi wa majengo ya miradi ya serikali ili kuwapa ari ya kufanya kazi hiyo kwa umakini.Awali, akikaribisha wajumbe wa kamati hiyo ya siasa, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi, aliishukuru serikali kwa kuwapatia fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo vituo vya afya.Ndejembi amesema anaiona dhamira njema ya Rais Magufuli ya kuwaletea wananchi maendeleo. Alisema kwamba wilaya ya Kongwa walipokea Sh milioni nane kwa ajili ya ujenzi wa vituo viwili vya afya, ambavyo ni Mlali na Ugogoni. | kitaifa |
TIMU ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inatarajiwa kucheza leo dhidi ya timu ya taifa ya Kenya ‘Harembee Stars’ mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan 2020) utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Mchezo huo ni muhimu kwa Stars kuhakikisha inatumia vyema uwanja wa nyumbani kupata matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga raundi ya mwisho ya kufuzu. Timu hizo zitarudiana Agosti 4.Stars inataka kulipiza kisasi hasa baada ya kufungwa katika mchezo wa makundi kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) Misri bada ya kuchapwa 3-2 licha ya kuongoza mara mbili.Lakini mchezo wa leo utawahusisha wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani na Taifa Stars ndio inaonekana kuwa na faida zaidi baada ya kuwa na asilimia kubwa ya kikosi chake kilichoenda Misri kupata uzoefu mkubwa. Iwapo watatumia vyema uwanja wa nyumbani watajitengenezea mazingira mazuri ya kufuzu.Hatahivyo, Kenya sio timu ya kubeza kwani wako vizuri na wanataka kuutumia mchezo huo kupata matokeo ili kujiweka vizuri kwa ajili ya mchezo wa mwisho utakaofanyika Nairobi wiki ijayo.Katika viwango vya ubora wa soka duniani bado Kenya wako vizuri ukilinganisha na Tanzania, wanashikilia nafasi ya 107, huku ndugu zao wakishika nafasi ya 137.Akizungumzia mchezo huo Kocha Ndayiragije alisema alisema jana kuwa maandalizi yote yako vizuri na kwamba kinachohitajika kwa wachezaji ni umakini kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.“Tunamshukuru Mungu maandalizi yako vizuri hakuna majeruhi na wachezaji wanaonesha morali ya juu, hatuna presha zaidi ya kuhakikisha tunakwenda kupambana na kupata matokeo. Kikubwa ni mashabiki kujitokeza kwa wingi kutuunga mkono, “alisema.Nahodha John Bocco alisema mchezo huo utakuwa mgumu kwani kila mmoja atahitaji matokeo kujiweka katika nafasi nzuri, lakini anaamini kwa morali walionao watapambana kupata matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani.“Kama wachezaji tuna morali, tunaamini kila kitu tutamaliza nyumbani ili tukienda ugenini tunarahisisha mambo, naamini tuna kikosi kizuri cha mapambano,”alisema na kuongeza kuwa, kocha Ndayiragije amekuwa akiwatia moyo na kuwapa morali wakati wote.Bocco aliwaomba Watanzania kutoenda uwanjani na matokeo yaliyopita bali sasa wako vizuri kulipiza kisasi kwa kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.Tanzania kwa mara ya mwisho ilishiriki fainali za Chan zilipofanyika Ivory Coast 2009 ikiwa ni miaka 10 sasa, hivyo itataka mwaka huu iweke rekosi tena kwa kufuzi fainali hizo.Fainali za kwanza za Chan zilifanyika mwaka 2009 na lengo la Shirikisho la Afrika (Caf) ni kutoa nafasi kwa wachezaji ambao hawajasajiliwa nje ya nchi zao na kuwawezesha kujitangaza. | michezo |
Benki hiyo iliyoanza kutoa huduma zake Agosti,1997 ikiwa na tawi moja jijini Dar es Salaam, kwa sasa ina jumla ya matawi 30 hapa nchini na matawi saba nje ya nchi huku rasilimali yake ikitajwa kuwa na thamani ya Sh trilioni 1.1 hadi kufikia Juni mwaka huu.Akizungumza juzi kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha baadhi ya wafanyakazi na wateja wa benki hiyo, Ofisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo, Selemani Ponda alisema mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na ukweli kuwa benki hiyo inafanya kazi chini ya bodi ya wakurugenzi iliyo imara.“Siku kama ya leo (juzi) miaka 18 iliyopita ndio benki yetu ilianzishwa. Leo benki ya Exim imesaidia ukuaji wa biashara ndani na nje ya nchi na tunashukuru kuona kwamba baadhi ya wateja wetu wameweza kuhudhuria hafla hii ili tusherehekee pamoja siku hii muhimu,’’ alisema.Kwa mujibu wa Selemani, mbali ya kuwa na idadi kubwa ya matawi ndani na nje ya nchi pia imefanikiwa kuwa na mashine za kutolea fedha 57 hapa nchini, vituo vya mauzo zaidi 250 na kwa sasa ina matawi kwenye mikoa 16 hapa nchini ambayo yanahudumia takribani wateja 180,000.“Miaka yote tumekuwa tukiitumia siku hii pia kutathmini ubora wa huduma zetu kwa wateja na ndio maana tumekuwa tukiendelea kufanya vizuri kila siku. Uhodari wa wafanyakazi wetu imekuwa pia imekuwa ni chachu kwenye mafanikio haya,’’ alibainisha.Kwa mujibu wa Ponda, benki hiyo ndio benki ya kwanza hapa nchini kufungua matawi yake nje nchi ambapo kwa sasa imefungua matawi yake visiwa vya Comoro na nchini Djibouti. | uchumi |
Uwezeshaji huo upo katika kuwapatia elimu ya ujasiriamali pamoja na kuwawezesha vitendea kazi vya kisasa ili waweze kufikia ndoto zao.Mikoa iliyofikiwa na Airtel kupitia mradi huo wa jamii ni pamoja na Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Kagera, Manyara na Dodoma.Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano alisema mikoa 6 tayari imefaidika na shilingi milioni 125 za mradi wa Airtel Fursa na bado mradi unaendelea.Alisema Airtel kila wiki hutumia Sh milioni 20 kwa ajili ya makundi mawili au vijana wawili watakaojitokeza na kuomba kuwezeshwa na mradi wa Airtel Fursa, alisema Singano.“Awali mwaka huu tulitenga jumla ya Sh bilioni moja kwa ajili ya kuwasaidia vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 kuweza kutumia fursa walizonazo na kujiajiri wao wenyewe pamoja na wengine, sasa pesa hizi zipo na zinawasubiri,“alieleza Singano.Katika siku 90 wamesaidia vijana wanaojishughulisha na biashara au ujasiriamali katika utunzaji wa mazingira, ufugaji, kilimo cha kisasa pamoja na biashara mbalimbali, zikiwemo za saluni kwa wanawake, ufundi seremala, uvuvi, pamoja na bucha la nyama kwa familia.Mpango wa Airtel Fursa unawalenga vijana walio katika umri wa miaka 18 hadi 24. Ili kijana ashiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 au barua pepe kwa [email protected]. | uchumi |
IMEELEZWA kuwa asilimia 85 ya upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume unatokana na magonjwa ya moyo na kisukari, hivyo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeamua kuleta dawa za kurejesha nguvu hizo wakati wanaume wakiendelea na matibabu ya vishawishi.Dawa hizo zinatolewa katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo Barabara ya Kilwa katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, ambapo taasisi hiyo katika banda lao wanatoa huduma bure ya upimaji, ushauri na dawa.Akizungumza katika viwanja hivyo, Daktari bingwa na Mkuu wa Idara ya Utafiti na Mafunzo wa taasisi hiyo, Dk Pedro Pallangyo aliliambia gazeti hili kuwa wanatoa huduma za vipimo bure vya urefu, uzito, mapigo ya moyo, shinikizo la damu, sukari, kipimo cha umeme wa moyo (ECG), na kipimo cha utendaji kazi wa moyo (ECHO).Alisema pia kuna mtaalamu wa lishe anayetoa ushauri bure wa lishe na ushauri na baada ya vipimo, watakaobainika kuwa na magonjwa ya moyo na magonjwa ambatano ya kifua, ganzi, shinikizo la damu na upungufu wa nguvu za kiume watapatiwa dawa.“Kwa kiwango kikubwa upun- gufu wa nguvu za kiume unatokana na magonjwa ya moyo na kisukari huku chakula kikisababisha kwa kiwango kidogo cha asilimia tano, hivyo kwa wenye upungufu wa nguvu tuna dawa zitakazowasaidia kwa saa 24 hadi 48 wakati wakiendelea na matibabu ya chanzo cha ugonjwa,”alisema Dk Pedro.Akizungumzia kambi ya taasisi hiyo iliyopo katika viwanja vya Sabasaba, alisema kuwa ina madaktari wanne, watatu wa watu wazima na mmoja wa watoto,wanateknolojia wa moyo, wauguzi watano na daktari bingwa wa lishe.Alisema mwaka huu wameongeza ukubwa wa banda lao mara mbili ili kuondoa msongamano wa watu, mashine za huduma zikiwa za kutosha kuliko miaka mingine. | kitaifa |
Akizungumza na wakulima na wananchi, Dk Shein alisema karafuu ndio alama ya Zanzibar, hivyo ni wajibu wa wananchi kutunza na kuenzi zao hilo kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.Alisema serikali imefanya mabadiliko makubwa ya maendeleo ya zao hilo, ikiwemo kufanya mabadiliko katika Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC).Rais alipongeza shirika kutokana na kwenda sambamba na mabadiliko ya maendeleo, ikiwemo kujenga vituo vya kisasa vyenye hadhi ya zao hilo la karafuu.Kwa mujibu wa rais, serikali imekuwa na mipango maalumu ya kuimarisha karafuu kwa kumpa mkulima asilimia 80 ya bei inayouzwa nje, kuzalisha miche 10,000 kila mwaka na kugawiwa wakulima bure na mpango wa kuilinda karafuu ya Zanzibar.Alisema jitihada hizo za Serikali, zinapaswa kuungwa mkono na wakulima na wananchi kwa kuacha tabia ya kuchanganya karafuu na makonyo, kukaanga na kuanika barabarani.Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazurui alitangaza bei ya karafuu kwa mwaka 2014/2015 ni Sh 14,000 kwa daraja la kwanza, Sh 12,000 daraja na pili na Sh 10,000 kwa daraja la tatu. | uchumi |
KIKOSI cha timu ya soka ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23, leo kiko ugenini mjini Bujumbura kucheza na wenyeji wao Burundi katika mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Afrika ‘Afcon’ kwa vijana wa umri huo.Akizungumza saa chache kabla ya kuondoka jana, kocha msaidizi wa timu hiyo Bakari Shime alisema timu hiyo haijapata maandalizi makubwa ila wanatarajia kuwatumia zaidi wachezaji ambao wanapata nafasi ya kucheza kwenye timu zao.“Tunaondoka leo (jana) na kesho (leo) tutacheza na Burundi na tutarudiana Novemba 20 hapa Dar es Salaam, natarajia kuwatumia wachezaji wanaopata nafasi ya kucheza katika timu zao na naamini tutafanya vizuri kwa sababu nimewasoma vema Burundi,” alisema Shime.Wachezaji wanaounda kikosi hicho ni makipa Ramadhan Kabwili, Metacha Manta, Ally Salim, Mohamed Abdallah, Abdallah Shaibu, Oscar Masai, Abdallah Hamisi, Ismail Aidan, Kelvin Nashon, Adam Salamba, Mbaraka Yusuph na Salum Kihimbwa.Wengine ni Kelvin Sabato, Habib Kiombo, Ibrahim Hamad, Dickson Job, Nickson Kibabaje, Ally Ally, Ally Msengi na Ayoub Masoud. Benchi la ufundi ni kocha Bakari Shime, Zuberi Katwila, Adam Moshi, John Matangwa, Abdul Mgude, Joackim Mshanga na John Mashaka. Timu mbili za soka za Tanzania zimeshafuzu fainali za Afrika ambazo ni ile ya U-17 na ile ya soka la ufukweni na sasa ni zamu yah ii ya U-23 na Taifa Stars. | michezo |
['Barcelona wamesitisha jaribio lao la kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymarkutoka Paris Saint-Germain hadi msimu ujao. (ESPN)', 'Mazungumzo kati ya vilabu hivyo yalivunjika baada ya PSG kulegeza masharti yao licha ya Neymar kujitolea kulipa £17.7m kufikia makubaliano ya usajili wake. (Sky Sports)', 'Mshambuliaji wa Colombia Radamel Falcao alipokelewa na mashabiki 25,000 alipowasili Istanbul siku ya jumapili kabla ya pendekezo la kujiunga Galatasaray kutoka Monaco. (Mirror)', 'Roma wanamatumaini ya kummsaini kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan ,30. (Sky Italy - in Italian)', 'Beki wa zamani wa Liverpool Martin Skrtel amevunja mkataba wake na Atalanta inayoshiriki Ligi ya Serie ya Italia wiki kadhaa baada ya kujiunga na klabu hiyo. (Mail)', 'Mshambuliaji wa Frankfurt mwenye umri wa miaka 25 Mcroatia Ante Rebic anajiandaa kujiunga na AC Milan, huku mshambuliaji Andre Silva, 23 Mreno akitarajiwa kujiunga na klabu hiyo. (Goal)', 'Kipa wa Paris St-Germain Alphonso Areola, 26, anatarajiwa kumilisha uhamisho wake kwenda Real Madrid siku ya mwisho katika mkataba ambao utamwezesha kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 32, kujiunga na klabu hiyo. (Mirror)', 'PSG wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 26, kwa mkopo kutoka Inter Milan. (RMC Sport - in French)', 'Mlinzi wa Bayern Munich Mjerumani Jerome Boateng, 30, anakaribia kujiunga na mabingwa wa Italia uventus. (Bild, in German)', 'Juventus bado wana matumaini ya kumsaini kiungo wa kati wa Barcelona wa miaka 31 Mcroatia Ivan Rakitic - na huenda wakatoa ofa ya kumuachilia mchezaji wa kiungo cha kati Mjerumani Emre Can, 25, kama sehemu ya kufikia mkataba wa kumsajili Ivan Rakitic. (Sport - in Spanish)', 'Meneja wa Napoli Carlo Ancelotti anasema kuwa yuko tayari kumsaini mshambuliaji wa Uswidi Zlatan Ibrahimovic, 37, kutoka LA Galaxy. (Sun)', 'Borussia Dortmund wanapigiwa upatu kumsajili kipa wa Liverpool wa miaka 18 Bobby Duncan ikiwa klabu hiyoo ya Ligi Kuu ya Uingereza ataamua kukomesha mkataba wake . (Mirror)', 'Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27 anaweza kukataa kusaini mkataba mpya na Manchester United ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusajiliwa Real Madrid. (Mirror)', 'Ingawa meneja wa Unites Ole Gunnar Solskjaer amedai kuwa Pogba atasalia Old Trafford.(Express)', 'Bayern Munich inataka kumsaini winga wa Mancity Leroy Sane licha ya kwamba winga huyo mwenye umri wa miaka 23 atauguza jeraha la muda mrefu(Mirror)', 'Alexis Sanchez, 30,amejiunga na Inter Milan katika mkataba wa muda mrefu wa mkopo baada ya meneja wa Manchester United, Solskjae kumwambia kuwa mchezaji huyo anaweza kuchezea mashindano ya vikombe na ligi ya ulaya.(Sun)', 'Mshambuliaji wa inter Milan Mauro icardi 26 ametishia kuishtaki klabu hiyo ya ligi ya serie A kwa kuwa mchezaji kiungo wa Argentina hana raha kuondolewa katika kikosi cha Kwanza cha timu hiyo.', 'Mshambuliaji wa West Ham na Javier Hernandez, 31, ametuma maombi yake ya kuhamia Sevilla.(Mail)', 'Mpango wa Christian Eriksen kutoka Tottenham kwa paundi milioni 72 kwenda PSG imegonga mwamba baada ya Neymarameamua kubaki kwa mabingwa wa ligue 1. (Sun)'] | michezo |
KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amesema walilazimika kubadili mbinu za uchezaji ili kupata matokeo mazuri katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya African Lyon, ambao walishinda 3-0 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.Akizungumza baada ya mchezo huo, Aussems alisema uwanja haukuwa rafiki ndio maana walikuja na mbinu nyingine iliyowasaidia kupata matokeo hayo.“Tunashukuru tumepata pointi tatu, inamaanisha kila mtu anatimiza wajibu wake vizuri, tumeonesha jitihada zetu na kupata ushindi na sasa tunaangalia mchezo ujao,” amesema.Wekundu hao waliingia na mbinu ya kucheza mipira mirefu tofauti na walivyocheza michezo iliyopita walitumia zaidi mipira ya pasi hadi kufika golini.Hata hivyo, amesema matokeo hayo yameshapita na mawazo yao kwa sasa ni mchezo ujao dhidi ya Azam FC utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho.Kutokana na umuhimu wa mchezo huo, Kocha huyo aliwapumzisha nyota wake wengi wa kikosi cha kwanza katika mchezo uliopita dhidi ya Lyon na kuwapa nafasi wale waliokuwa hawatumiki sana. | michezo |
KIPA wa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi Manula, amesema Benno Kakolanya hakwenda Simba kushindana naye ila kushirikiana kuifikisha klabu hiyo inapotaka kufika.Kakolanya amejiunga Simba SC msimu huu akitokea Yanga, hivyo kwa sasa makipa wa Simba ni Manula, Kakolanya na Ali Salim. Manula amesema jijini Dar es Salaam jana kuwa, Kakolanya ni kipa mzuri na amekwenda Simba waunganishe nguvu ili klabu hiyo ifanikiwe.“Kwa hiyo ujio wa Benny ni kitu kizuri na utaongeza nguvu kwenye timu yetu,” alisema kijana huyo aliyejiunga Simba akitokea Azam FC takriban misimu miwili iliyopita.Alisema anafurahi pia kuwa na Juma Kaseja Taifa Stars kwa kuwa miaka ya nyuma alimpa mbinu za kuwa kipa mzuri na sasa wapo pamoja. Kaseja aliyekuwa Tanzania one miaka iliyopita, ameitwa tena kwenye kikosi cha Stars hivi karibuni na kufanya vizuri kwenye mechi zote mbili za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika, Afcon. Aliyasema hayo alipohojiwa kwenye kipindi cha Leo Tena cha kituo cha radio Clouds FM kinachomilikiwa na Clouds Media Group.Manula alisema, wakati Taifa Stars ikifundishwa na kocha Kim Poulsen, alikuwa akimuita ajifunze kwa aliowakuta ili awe kipa Taifa Stars baadaye. Miongoni mwa makipa wa Taifa Stars wakati huo alikuwa Kaseja.“Kwa hiyo leo hii mimi nakuwa na Kaseja kwangu mimi naona ni furaha, ni faraja kwa sababu ni mtu ambaye alikuwa ananifundisha leo hii nacheza nae, nashindana nae kwenye nafasi,” alisema na kuongeza kuwa, anaamini Kaseja naye anafurahi kuwa naye Taifa Stars.Manula amemshukuru Mungu kwa kupata bahati ya kufundishwa na Kaseja na kwamba, miongoni mwa vitu alivyomfundisha ni namna ya kudaka mpira na kutoa pasi uwanjani. Amesema amekuwa na Kaseja kwa muda mrefu na hadi sasa wanakutana na kushauriana mambo mbalimbali na kwamba bado anajifunza kwa kipa huyo wa KMC.“Yaani kumuona Kaseja timu ya taifa kwangu najisikia faraja kwa sababu ukimzungumzia Kaseja kwenye nchi hii ni golikipa ambaye kafanya mambo makubwa sana...ninapopata muda tunakaa pamoja tunapiga stori ananiambia vipi mdogo wangu bwana labda kuna siku ulicheza mechi, labda usikate tamaa, ongeza juhudi hivi,” alisema.Manula alisema alikuwa akicheza kwa presha kubwa alipokuwa Azam FC kuliko Simba na kwa sasa amekomaa. | michezo |
['Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anahofia kwamba hatma ya kazi yake itakuwa haijulikani iwapo timu yake itashindwa kwa mabao mengi ugenini Liverpool.(Mail)', 'Baadhi ya wachezaji wamepoteza matumaini na raia huyo wa Norway anaamini baadhi yao wamekataa kumsikiliza. (Sun)', 'Solskjaer anahitaji kitita cha £300m kutumia katika dirisha lijalo la uhamisho na kumnunua mshambuliaji kama vile mshambuliaji wa Tottenhama na England Harry Kane,26, kulingana na winga wa zamani Lee Sharpe. (Talksport)', 'Kane anafaa kuondoka Tottenham na badala yake kuhamia Manchester City, kulingana na beki wa zamani wa England Glen Johnson. (Betdaq, via Independent)', 'Liverpool huenda ikapokea kitita cha £4.5m kati ya kile cha £84m wanazodaiwa na Barcelona baada ya kumnunua kiungo Philippe Coutinho, 27, ambaye alihamia Nou Camp mwaka 2018. (Mirror)', 'Everton inafikiria kumnunua mchezaji anayelengwa na Manchester United Moussa Dembele katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. Mshambuliaji huyo wa Ufaransa , mwenye umri wa miaka 23 anaweza kugharimu £40m kutoka Lyon. (Star)', 'Chelsea na mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic, 21, amekiri kukasirishwa kwake kwa kukosa muda wa kucheza zaidi tangu uhamisho wake wa £58m kutoka Borussia Dortmund. (Guardian)', 'Mshambulaji wa Arsenal Gabriel Martinelli, 18, anakabiliwa na chaguo katika hatma yake ya kimataifa kwa kuwa anahitajika na Itali pamoja na Brazil. Alizaliwa nchini Brazil lakini lakini babake ni raia wa Itali hivyobasi anaweza kuwakilisha timu zote mbili.. (Mirror)', 'Mshambuliaji wa Venezuela Salomon Rondon, 30, amekiri kwamba angependelea kuandikisha mkataba wa kudumu na klabu ya Newcastle lakini akasema kwamba hakupatiwa fursa kubadili uhamisho wake wa mkopo wa msimu uliopita kuwa kandarasi ya kudumu na hivyobasi akaelekea katika klabu ya China ya Dalian Yifang. (Newcastle Chronicle)', 'Mkufunzi Roy Hodgson anasema kwamba klabu ya Crystal Palace italazimika kumsaini mshambuliaji mpya mwezi januari iwapo wanataka kumaliza katika orodha ya timu sita za kwanza katika jedwali na pia analenga kuwasajili mabeki wawili wapya wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. (Standard)'] | michezo |
Akijibu maswali ya gazeti hili kuhusu faida za gesi asilia katika uchumi wa taifa, Kisamo alisema kuwa matumizi yake yataendelea kuleta unafuu katika uchumi kulingana na jinsi matumizi ya gesi hiyo yatakavyoongezeka nchini siku hadi siku.“Gharama za kununua gesi asilia si za juu kama ilivyo za kununulia mafuta mazito, ya ndege na mkaa, hivyo, matumizi yake ni faida kutokana na kuleta nafuu ya bei. Ikumbukwe kuwa gesi hii haiagizwi kutoka nje”.“…Ukiachilia mbali mkaa unaozalishwa nchini na watu mbalimbali kwa hasara ya kukata miti hovyo na kuharibu mazingira, mafuta yanaagizwa kutoka nje ya nchi kwa gharama za juu, hivyo kufanya matumizi ya gesi asilia kuwa ahueni kwa watumiaji,” Kisamo alisema.Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Gesi, Nobert Kahyoza alisema kuwa gesi asilia inayotumika nchini kwa sasa ni ya Songo Songo ya wilayani Kilwa mkoani Lindi, iliyoanza kusambazwa mwaka 2004 baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya kuisafisha na kuisafirisha kwenda Dar es Salaam, pamoja na gesi ya Mnazi Bay inayozalishwa Mtwara, iliyoanza kutumika mwaka 2006.“Tangu kuanza kwa matumizi yake, gesi asilia imetuwezesha kubakiwa na kiasi cha fedha kilichopangiwa matumizi mengine, hivyo kuchangia maendeleo kwa namna moja au nyingine katika sekta ya nishati,” Kahyoza alisema.Aidha, Kisamo alitaja kiasi kilichookolewa katika kipindi hicho cha Julai 2004 hadi Oktoba, 2013 kuwa ni zaidi ya Sh trilioni 9.22 zilizokuwa zitumike kununua nishati nyingine hasa mafuta kwa ajili ya kuendeshea mitambo na matumizi mengine.Akitoa ufafanuzi wa eneo moja la kubana matumizi ya fedha za kigeni kwa kutumia gesi asilia, Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Injinia Hosea Mbise alisema kuwa ni eneo la kuzalisha umeme lililoiwezesha sekta ya umeme pekee kuokoa Sh trilioni 8.48 katika kipindi hicho.“Hiyo inamaanisha kuwa, badala ya kuzalisha uniti moja ya umeme kwa dizeli ya senti za Marekani 30 (Sh 480) hadi senti za Marekani 45 (Sh 720), kwa kutumia gesi asilia sasa uniti moja ya umeme inazalishwa kwa senti za Marekani sita (Sh 96) hadi senti za Marekani nane (Sh128),” Mbise alifafanua.Hata hivyo, alisema kuwa gesi ya Ghuba ya Mnazi inatumika kuzalisha umeme kwa ajili ya mikoa ya Lindi na Mtwara na kwamba, mitambo ya kuizalisha ni ya uwezo wa MW 18 lakini uzalishaji kwa sasa ni MW 12 kutokana na mahitaji yaliyopo.“Gesi ya Songo Songo inayotumika kuzalisha umeme kwa wastani wa MW501 inachangia zaidi ya asilimia 33.4 ya umeme wote unaozalishwa kwa sasa.Takwimu zilizopatikana kutoka katika ripoti mbalimbali za Wizara ya Nishati na Madini zinazozungumzia maendeleo ya gesi nchini, pamoja na taarifa ya TPDC kwa gazeti hili, tangu mwaka 2004, viwanda 37 vimekwishajiunga na matumizi ya gesi asilia kwa ajili ya kuendesha mitambo ya uzalishaji badala ya mafuta mazito kama vile dizeli.Ofisa Habari wa TPDC, Maliki Munisi alisema kuwa kuanzia kipindi hicho hadi Oktoba mwaka jana zaidi ya magari 60 yamekwisha badilishwa mifumo na kutumia gesi hiyo. | uchumi |
HADI kufi kia juzi Serikali imefanikiwa kulipa jumla ya wakulima 82,835 katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. Jumla ya fedha iliyolipwa kwa wakulima hao, ambao tayari wamefanyiwa uhakiki ni Sh bilioni 83.Walikuwa wamelipwa fedha hizo hadi juzi, ambapo katika mkoa wa Mtwara, wakulima 50,835 wamelipwa, mkoa wa Lindi wakulima 22,131 na mkoa wa Ruvuma wakulima 9,445.Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga wakati akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji wadogo wa korosho kutoka katika mikoa mitano ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Morogoro, uliofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Mtwara.Aidha, Hasunga alisema kuwa vyama 328 vimefanyiwa uhakiki kati ya vyama 504 vilivyopo mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma, ambapo vyama 319 vimekwishalipwa. Aliwatoa hofu wananchi wanaopotoshwa kuwa bado wakulima hawajalipwa kiasi chochote cha fedha. Alisisitiza kuwa wakulima wanalipwa kupitia njia ya benki, hivyo wanapaswa kuwa na utamaduni wa kwenda benki.Hasunga alisisitiza kuwa serikali imedhamiria kuwanufaisha wakulima wa korosho. Alisema tayari amewaelekeza watendaji wa Bodi ya Korosho Tanzania, kuwasajili wakulima wote wa korosho ili watambulike.Waziri huyo alisema kuwa kikao hicho kina lengo la kujadiliana na kukubaliana utaratibu uliopangwa na serikali katika ubanguaji wa korosho mwaka 2018/2019 kwa kuelekeza ubanguaji kufanyika nchini ili kuwanufaisha wananchi katika ajira hiyo. “Tumeiona changamoto ya mitaji kwa wabanguaji wadogo nchini sambamba na wabanguaji wakubwa, hivyo ili serikali iwarahisishie upatikanaji wa mitaji, tumeamua kuwapa kazi ninyi wenyewe,” alisisitiza.Aliongeza kuwa suala la uhakiki, limejikita zaidi kubaini udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wahujumu wa biashara ya korosho. “Kuna watu walikuwa wametoa akaunti za benki, lakini zinatofautiana na majina ya watu, na waliwasilisha korosho zao kwenye maghala ya kuhifadhia korosho,” alisema.Aliongeza kuwa, “Tulipoona soko la korosho linayumba huku lengo la serikali likiwa ni kutaka kuona wakulima wananufaika, tuliamua kuingilia kati na kuanza kununua korosho zote na pia tumeamua kubangua korosho zote hapa hapa nchini.” | kitaifa |
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi 2018/19 hadi 2022/23 wenye lengo la kuimarisha Kampeni ya Kupambana na Ukimwi na kufikia ‘90 tatu’ ifikapo 2023.Akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Ukimwi jijini Dodoma jana, alisema mkakati huo umezingatia matokeo ya mapitio ya Mkakati wa Tatatu wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi 2013/14-2017/18 pamoja na matokeo ya utafiti wa viashiria vya Ukimwi Tanzania wa 2016/17.Mkakati huo pia umezingatia jitihada mpya zinazojitokeza sambamba na matumizi ya teknolojia mpya pamoja na dhamira za kitaifa, kikanda na kimtaifa za kuharakakisha mwitikio wa VVU na Ukimwi ili kufikia malengo ya 93 ifikapo 2020 na hatua za kuelekea kutokomeza Ukimwi ifikapo 2030."Dhamira ya Tanzania katika utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu VVU na Ukimwi la mwaka 2015, malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu 2030 na Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika," alisema.Mkakati huo pia umesianisha na kupanga programu mbalimbali, zinazosaidia mwitikio wa Taifa zikiwemo afua zitakazotekelezwa kupitia Mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa Ukimwi (PEPFAR), Mfuko wa Dunia wa Kudhibiti Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria na jitihada nyingine za makubaliano ya ushrikiano baina ya nchi mbalimbali.Alisema matokeo yanayotegemewa kutokana na kutekeleza mpango huo ni kupungua kwa maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo 2020 na asilimia 85 ifikapo 2023 na kupungua kwa maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa watoto kwa chini ya asilimia tano ifikapo 2023 na chini ya asilimia mbili ifikapo 2030.Vile vile, kupungua kwa vifo vinavyohusiana na Ukimwi kwa asilimia 50 ifikapo 2020 na asilimia 70 ifikapo 2023 na kupungua kwa unyanyapaa na ubaguzi ifikapo 2023 na kuelekea kutokomeza kabisa ifikapo 2030.Waziri Mkuu alisema tangu amezindua Kampeni ya Furaha Yangu Juni 19, mwaka huu watu zaidi ya 13,689 wamejitokeza katika kupima ili kuhakikisha wanajua afya zao."Lakini pia katika wiki nzima ya maadhimisho ya Ukimwi nchini tangu Novemba 26 hadi Desemba mosi, zaidi ya watu 1,817 wamepima na kujua afya zao miongoni mwao wanaume ni 1,183 sawa na asilimia 55 na wanawake 634 sawa na asilimia 35.Akizungumza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, Jenista Mhagama amesema katika kudhibiti Ukimwi wanajenga vituo 20 vya kupima waendesha malori mipakani kitendo kitakachochangia kujua afya zao.Alisema pia Sh milioni 249 zimetumika kujenga kituo cha kuhudumia watu wenye Virusi Vya Ukimwi katika eneo la Mirerani, kutokana na eneo hilo kuwa na maambukizi mengi kuliko maeneo mengine mkoani Manyara.Waziri Jenista alisema Mfuko huo pia utagemea kupata Sh bilioni 24 kwa ajili ya kufanya tathmini ya maambukizi katika mwambao wa ziwa Tanganyika na Victoria kwa lengo la kutokomeza ugonjwa huo.Alisema tangu kuanzishwa mfuko wa Ukimwi umetumia Sh milioni 660 kwa ajili ya kutibu magonjwa nyemelezi katika maeneo mbalimbali ambacho yamekuwa chimbuko la kuangamiza watu wengi.Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile aliagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha asilimia 50 ya WAVIU wanapata kinga ya Kifua Kikuu hadi Desemba 31, mwaka huu.Alisema kinga hiyo ni muhimu kwani kati ya wagonjwa wa VVU 34.8 wanaugua TB na asilimia 35 wanaugua TB sugu na asilimia 5.6 husababisha vifo vyao kutokana na kuugua TB.Dk Ndugulile alisema mkakati uliopo ni kuhakikisha kwamba mpango wa kutoa dawa kwa WAVIU unasambaa nchi nzima, ili kuhakikisha kwamba hawapotezi muda kwenda kufuata dawa hizo mbali na kwa gharama kubwa.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo alisema viongozi mbalimbali wakiwamo wakuu wa mikoa 26 na wilaya 139 na viongozi wa halmashauri 185 wameshiriki katika kampeni ya kutokomeza maradhi ya Ukimwi kwa kutekeleza maagizo mbalimbali ya serikali lengo ni kuhakikisha huduma mbalimbali za avya zinawafikia wananchi.Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA), Leticia Moris amesema kutokana na wagonjwa hao kunyanyapaliwa katika sehemu za kutolea huduma wanatakiwa kuwaajiri au kuwapa nafasi ya ajira WAVIU ili kuwapa dawa wagonjwa wenzao.Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Dk Leonard Maboko alisema upimaji kitaifa unaonesha kwamba wanawake asilimia 52 wamejitokeza kupima wanawake na wanaume ni asilimia 48 na mikoa iliyoongoza kupima ni Mwanza, Tabora na Njombe.Mikoa ambayo wanaume wameongoza kupima ni Morogoro asilimia 76, Mbeya asilimia 71 na Ruvuma asilimia 68, tangu kampeni hiyo imezinduliwa mwezi Juni 19 mwaka huu. | kitaifa |
TIMU za vijana waliochini ya umri wa miaka 17 za Ethiopia na Uganda leo zinatarajiwa kucheza fainali wa mashindano ya Cecafa ya kutafuta kufuzu Afcon 2019 utakaochezwa saa 11:00 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Ethiopia imefuzu fainali baada ya kuifunga Rwanda kwa penalti 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya mabao 2-2.Uganda nayo imefuzu baada ya kuifunga Serengeti Boys kwa mabao 3-1 katika mchezo ambao ulijaa burudani kutokana na jinsi Serengeti Boys walivyotandaza kandanda safi, lakini wakaishia kupoteza. Serengeti Boys wao watacheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Rwanda kwenye uwanja huo kuanzia saa 8:00 mchana.Akizungumza kocha wa SerengetiBboys, Oscar Mirambo alisema baada ya kupoteza nafasi ya kucheza fainali watahakikisha wanashinda mchezo wa leo ili wawe washindi wa tatu.“Kufungwa na Uganda nimeona mapungufu hasa katika set play hivyo tutahakikisha tunafanya marekebisho ili mwakani tufanye vizuri katika fainali za Afcon,” alisema Oscar “Pia nawaomba mashabiki wasikate tamaa waje kuishangilia timu yao kwani naamini watafanya vizuri na wataendelea kufanya vizuri, kilichotokea jana (juzi) ni sehemu ya mchezo,” aliongeza Oscar.Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya soka kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Nicholaus Musonye amesema watatoa zawadi kwa bingwa, mshindi wa pili na mshindi wa tatu tu pamoja na mchezaji bora, golikipa bora na mchezaji bora.Bingwa ataungana na Tanzania kuwakilisha ukanda wa Cecafa katika fainali za vijana za Afcon zitakazofanyika hapa nchini mwakani.Mashindano ya Cecafa yalianza Agosti 11 yakichezwa katika Uwanja wa Azam Complex na Taifa, Dar es Salaam yakishirikisha timu tisa ambazo ni wenyeji Tanzania, Uganda, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Burundi, Djibouti, Sudan na Sudan Kusini. | michezo |
WATAALAMU wameshauri wanaume nchini waache kula vyakula vilivyokaangwa zikiwemo chipsi, baga, unywaji wa pombe, uvutaji sigara.Wameshauriwa wale zaidi vyakula aina ya njugu kama vile karanga, korosho, mbegu za maboga na jamii ya aina hiyo ili kuimarisha mbegu zao za uzazi.Wamesema, wanaume pia wanapaswa kula vyakula visivyokobolewa, matunda, mboga za majani, samaki, nyama na kuepuka vyakula vya mafuta mengi ili kuimarisha viungo vyao vya uzazi.Utafiti Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam kuonesha asilimia 24 ya wanaume wana tatizo la nguvu za kiume kutokana na uchafuzi wa mazingira, uvutaji sigara na aina za vyakula.Wataalamu wamesema kuna ushahidi kuwa ulaji wa chakula bora unasaidia masuala ya uzazi na kwamba karibu pea moja ya wenza kati ya saba ina ugumu katika kushika mimba na asilimia 40 hadi 50 ya tatizo ni wanaume.Daktari wa tiba na lishe viwandani, Sweetbeth Njuu amesema vyakula jamii ya njugu hupunguza hatari ya mtu kupata magonjwa ya kisukari, moyo, shinikizo la damu la kupanda, na saratani ya utumbo. Dk Njuu amesema, magonjwa hayo kwa kiasi fulani huchangiwa na sumu zinazojikusanya mwilini.Amesema, njugu zina virutubisho na madini ambayo hupunguza sumu zinazochangia kupata magonwa hayo.“Upungufu wa nguvu za kiume unachangiwa na kutokula lishe bora vyakula vinavyojenga mwili kama mboga mboga, nyama, mayai, maziwa na vyakula vinavyoongeza nguvu kama ugali wa dona, muhogo na matunda ya aina mbalimbali kama nanasi, tikiti maji, ndizi mbivu, chungwa, matango na mengine watu hawali kwa mpangilio,” alisema.Kwa mujibu wa Dk Njuu, njugu zina mkusanyiko wa virutubisho vingi hasa protini, wanga, mafuta ya omega-3, na omega -6, madini, vitamins na vitoa sumu mwilini.“Mazoezi nayo ni changamoto, kwa sababu ya mfumo wa maisha, unakuta mtu anakosa hata muda wa kufanya mazoezi ambayo yanasaidia pia kumwimarisha, hivyo unawaathiri pia,” amesema.Amesema pia msongo wa mawazo ni chanzo kikuu cha upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwa tendo la kujamiana linahitaji utulivu wa akili ili uweze kuridhishana na kulifurahia tendo hilo. | kitaifa |
Meneja Mkuu wa Kodi wa kampuni hiyo, JosephThogo alisema kushindwa kwa nchi hizo kuwa na vifaa vya kutosha vya kuhifadhia mafuta kunamaanisha kwamba zitashindwa kujikusanyia mafuta ya kutosha kwa bei nafuu kama zinavyofanya nchi nyingine duniani.Alisema kwa miezi michache iliyopita, bei ya mafuta duniani imeshuka kwa zaidi ya nusu na kufikia chini ya dola 50 za kimarekani kwa pipa kwa mara ya kwanza tangu Mei mwaka 2009.“Kushuka kwa bei kumesababisha kushuka kwa uhitaji kwenye nchi nyingi ambao umetokana na kushuka kwa ukuaji wa kiuchumi na upatikanaji wake kuwa mkubwa zaidi; na kufanikiwa kwa uchimbaji ambao umeleta mapinduzi ya uzalishaji wa mafuta nchini Marekani na kusababisha kupungua kwa utegemezi wa kuagiza mafuta kutoka nje,” alisema.Alisema utafiti huo wenye jina la ‘Kushuka kwa bei za mafuta – Wanaofaidika na Wanaopata hasara’ umeainisha kuwa sekta ya anga ndiyo itakayofaidika kwa kiasi kikubwa na kushuka huko kwa kasi kwa bei ya mafuta duniani.“Wakati mwito wa kushuka kwa bei ya mafuta ukitolewa kuwanufaisha mpaka watumiaji wa mwisho kabisa, inakadiriwa kuwa gharama za mafuta ya ndege, ambayo ndiyo hugharimu zaidi uendeshaji wa sekta hiyo, unaweza kushuka mpaka kufikia asilimia 13,” alisema.Alisema waendesha vyombo vya moto Afrika Mashariki, wamekuwa wakilalamika kuwa kushuka kwa bei hakuendani na mwenendo mzima wa bei za mafuta. | uchumi |
RWANDA imeshika nafasi ya pili kwa umaarufu Afrika katika kuandaa mikutano na makongamano ya kimataifa. Shirika la Kimataifa la Uandaaji Mikutano (ICCA) imeeleza kuwa Afrika Kusini imeshika nafasi ya kwanza.Mwaka jana Kigali ilishika nafasi ya tatu ikitanguliwa na Cape Town na Morocco. Taarifa iliyotolewa na ICCA, inajikita katika idadi ya mikutano iliyofanyika kwa mwaka katika nchi tatu tofauti na zaidi ya washiriki 50 ambapo mwaka jana Kigali ilikuwa mwenyeji wa mikutano 26.Kwa sasa Rwanda ina wajumbe 4,000 wanaoshiriki mkutano wa Mabadiliko Afrika 2019 pamoja na mkutano wa mwaka wa maofisa uhusiano Afrika. Akizungumzia nafasi hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya mikutano Rwanda, Nelly Mukazayire alisema nchi hiyo ina lenga kufanya vizuri zaidi katika nyanja hiyo katika mwaka ujao.Alisema Rwanda imepokea wageni 38,745 mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la mwaka 2017 walipopokea wajumbe 28,308 kwa kuingiza asilimia 20 ya mapato ya utalii kwa kuingiza dola milioni 56 mwaka 2018 na mwaka huu wamepanga kuingiza dola milioni 88. | kitaifa |
Kwa mujibu wa ratiba hiyo iliyotolewa juzi, Rwanda itacheza na Kenya mchezo wa raundi ya kwanza ya kufuzu huku mchezo wa kwanza ukipigwa Nairobi kati ya Machi 30 na Aprili mosi, na marudiano yatafanyika Aprili 20-22.Mshindi wa jumla wa mechi hizo mbili kati ya Rwanda na Kenya atakutana na bingwa mtetezi Zambia katika raundi ya pili ya kufuzu Mei.Raundi ya mwisho ya kufuzu itafanyika Julai, ambapo washindi watapata nafasi ya moja kwa moja kucheza fainali zijazo za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa chini ya miaka 20.Katika ratiba zingine za raundi ya kwanza, Mauritania itacheza dhidi ya Morocco, Guinea Bissau itacheza na Sierra Leone, Algeria itacheza dhidi ya Tunisia.Mechi zingine, Liberia itakabiliana na Benin, Gabon dhidi ya Togo, wakati Ethiopia imepangwa dhidi ya Burundi.Zambia, Guinea, Nigeria, Gambia, Burkina Faso, Libya, Ivory Coast na Sudan zote zimetinga raundi ya pili bila kuingia uwanjani. Zambia ndio mabingwa watetezi baada ya kushinda taji hilo mwaka jana wakati fainali hizo zilipofanyikia nchini humo na kushinda 2-0 dhidi ya Senegal katika fainali.Katika mashindano yaliyopita yaliyofanyika Juni 2016, Rwanda ilitolewa katika raundi ya pili baada ya kufungwa kwa penalti 2-3 kufuatiwa kutoa sare.Rwanda waliandaa fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji chini ya miaka 20 na walimaliza katika nafasi ya tatu katika kundi lao, ambalo pia lilikuwa na Ghana, Cameroon na Mali. | michezo |
MBUNGE wa Viti Maalumu, Mariamu Ditopile amewataka wakazi wa kijiji cha Godegode na Pwaga, wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, kuwa wavumilivu wakati serikali inaendelea kukabiliana na tatizo la ukosefu wa maji kama ilivyoahidi.Kauli hiyo aliitoa baada ya kusikiliza kilio cha wakazi wa eneo hilo wakati akiwa katika ziara ya kamati ya utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) alipotembelea tarafa zote mkoani Dodoma.Ditopile alisema serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 iliahidi kumtua mama ndoo ya maji kichwani kwa kufikisha huduma hiyo karibu na wananchi, jambo ambalo linaendelea kutekelezwa.“Kilio chenu nimekisikia nawaomba muwe wavumilivu wakati suala hili linashughulikiwa. Niwaahidi nitahakikisha nashirikiana na uongozi wa ngazi za juu akiwemo Waziri wa Maji ili kutatua changamoto hii kwa haraka,” alisema.Pia aliwataka wananchi hao kuendelea kuchapakazi kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji hicho ili kuleta maendeleo kwa haraka kwa kuwa hakuna mafanikio yanayopatikana kirahisi.Mkazi wa Kijiji cha Godegode, Pili Machela alisema wamekuwa wakipata shida kutafuta maji kwa muda mrefu na kuiomba serikali iwaboreshee miundombinu ya maji.“Tatizo hili limekuwa sugu na kusababisha shughuli nyingine kushindwa kuendelea, tunaomba upokee kilio chetu,” alisema.Machela pia alilalamikia kijiji hicho kukosa huduma za afya za zahanati changamoto inayosababisha wagonjwa kutoka kijiji hicho kwenda kutibiwa katika Kituo cha Afya cha Mpwapwa.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, Bill Chidabwa alisema kutokana na Rais John Magufuli kuhamishia Makao Makuu ya Serikali kuwa Dodoma, vijana wote wanatakiwa kuchangamkia fursa zilizopo ili kuweza kuleta maendeleo yenye tija katika mkoa na Taifa kwa ujumla.Pia aliwaasa wananchi wa kijiji hicho kuacha kuwabagua viongozi wao bali wawaache wafanye kazi kwa utaratibu ili waweze kutekeleza ilani ya chama hicho.Aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika kujenga Taifa lenye usawa kwa kila mtu na kuongeza kuwa hakuna mwenye hati miliki ya uongozi.Katika ziara hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, Ditopile alitoa mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya sekondari Godegode.Pia alitoa ahadi ya madawati 20 katika Shule ya Sekondari ya Godegode na mabati ili kusaidia kuendeleza ujenzi wa shule ya msingi Maswaga, lakini pia alitoa fedha na jezi kwa ajili ya kuendeleza michezo katika kijiji hicho. | kitaifa |
NDEGE nyingine mbili kubwa zilizonunuliwa na serikali ili kuendelea kuboresha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) zitawasili nchini Desemba, mwaka huu.Hayo yalibainishwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe wakati akifungua mjadala wa wazi wa siku mbili, ulioshirikisha wadau wa sekta ya anga jana, ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wenye kaulimbiu inayosisitiza ‘Matumizi ya Anga katika Kufikia Uchumi wa Kati.Kamwelwe alisema awali ndege hizo mbili, zilikuwa zinunuliwe mwaka 2020/2021, lakini kutokana na umuhimu wa sekta ya anga katika kukuza uchumi wa nchi, serikali imeona ni vema izinunue mapema zaidi.Alisema sekta ya anga inaweza kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati na ndege hizo, zikianza kwenda nje ya nchi, zitaiongezea mapato zaidi serikali. Aliwataka wadau wa anga, kujadiliana njia bora za kuchagiza maendeleo ya nchi kupitia sekta ya anga. Alisema, usafiri huo unaweza kusaidia nchi kufikia uchumi wa kati kwa kusafirisha bidhaa hasa za vyakula kama vile samaki na nyama, ambapo nchi za Ulaya zinahitaji zaidi ya tani 200 za samaki.Alisema kwenye sekta ya nyama, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeshakamilisha ujenzi wa kiwanda cha nyama, ambacho kitapaswa kuhudumia soko la nyama la nchi za nje pia. Alisema;“Tangu kuingia madarakani Rais John Magufuli amekuwa akisisitiza mchango wa sekta ya viwanda katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo basi ifahamike kuwa sekta hii ya usafiri wa anga inaweza kutoa mchango kwa asilimia kubwa zaidi.“Kikubwa ni kwamba mnatakiwa kuja na mapendekezo ambayo nitayatekeleza kwa wakati hata ikiwa ni mabadiliko ya sheria yanayolenga kuimarisha usafiri wa anga nyie leteni tu. “Ninafahamu kuwepo kwa changamoto kadhaa kama vile idadi ya marubani na hata mafundi wa ndege, hayo yote yanafanyiwa kazi ili kuongeza idadi ya wafanyakazi hao watakaofanya kazi kwenye ndege zetu na kuiongezea ufanisi sekta hii.”Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari alibainisha kuwa katika kongamalo hilo, watajadiliana namna ya kutumia mashirika madogo ya huduma za ndege katika kuongeza pato la nchi.Hivi karibuni serikali iliipatia ATCL ndege ya Fokker 50, na kuifanya ATCL kuwa na jumla ya ndege saba ikiwemo Boeing 787-8 Dreamliner, ndege mbili za Airbus A220-300 na ndege tatu aina ya Bombardier Dash Q400. Rais John Magufuli aliwahi kusema kuwa ndege nyingine ya pili aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, itawasili nchini mwishoni mwa mwaka huu na ndege nyingine ya nne aina ya Bombardier Dash 8 Q400, nayo itawasili mwishoni mwa mwaka huu au mwaka ujao mwanzoni. | kitaifa |
WADAU wa bandari kutoka Afrika na baadhi ya nchi za Bara la Ulaya wamekutana jijini Dar es Salaam kujadiliana kuhusu masuala yanayohusu bandari zikiwemo fursa za kiuchumi za uendelezaji wa bandari hizo.Mkutano huo wa tatu ujulikanao kama ‘Utanuzi wa Bandari Afrika’ pamoja na kujadili masuala yanayohusu upanuzi wa bandari, pia unahusisha miradi mingine ya maendeleo ya ujenzi wa barabara kuu, madaraja inayoendelea kufanywa katika nchi za Afrika.Akizungumza baada ya ufunguzi wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Fransisca Muindi alisema mkutano huo pamoja na mambo mengine, utatoa nafasi kwa wadau hao kutumia fursa za bandari ya Dar es Salaam na kuitumia.Muindi alisema mkutano huo pia utatumika kuitambulisha bandari hiyo hususani kuhusu upanuzi unaoendelea kufanywa na serikali ukihusisha mipango iliyopo ya kupunguza mizigo bandarini na kuipeleka katika bandari kavu zilizopo na zinazoendelea kujengwa, hatua aliyosema itasaidia kuongeza ufanisi wa bandari hiyo.“Kupitia mkutano huu tunaamini nchi yetu itazidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kukua kiuchumi ikizingatiwa kuwa sekta ya bandari hapa nchini kwa sasa inazidi kupata msukumo wa kipekee unaoendana na mipango ya serikali kukuza uchumi wake,” alisema Muindi.Aidha, alisema Tanzania kwa sasa inazidi kupiga hatua kubwa katika sekta hiyo ya bandari ikijiandaa kuziunganisha nchi ya Rwanda kupitia ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambao unaoendelea kwa awamu tofauti kuanzia Dar es Salaam kwenda Dodoma, baadaye Mwanza na Kigoma kisha kuifikia Rwanda kupitia Isaka.Katika hatua nyingine, mkurugenzi huyo alisema ipo mipango inayoendelea chini ya serikali kupitia TPA kuwezesha mizigo inayokwenda na kutoka Rwanda kutumia bandari ya Dar es Salaam kama zamani. | uchumi |
KOCHA wa zamani wa timu ya Soka ya Taifa,Taifa Stars Dk. Mshindo Msolla amemshauri kocha wa timu hiyo Emmanuel Amunike kufanya kazi kwa uhuru hususani kwenye uteuzi wa kikosi kinachoenda kuiwakilisha nchi kwenye michuano mikubwa.Msolla ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache zimepita baada ya Amunike kuteua kikosi cha wachezaji 31 tayari kwa maandalizi ya michuano ya Afcon inayotarajiwa kufanyika Misri mwezi ujao. Akizungumza na gazeti hili jana, Dk. Msolla alisema kuifunga timu ya Uganda sio kwamba timu hiyo imekamilika kwani bado kikosi hicho kina mapungufu makubwa ya kiufundi yanayohitajika kuyafanyia kazi kabla ya kuingia kwenye michuano hiyo mikubwa.“Tukichukulia kwamba tumeifunga Uganda basi kila kitu tumemaliza tukienda Misri tutaendelea kulitia taifa aibu , nivema benchi la ufundi lifanye kazi ya kuijenga timu kwa kuaandaa mipango ya haraka kuisaidia,”alisema.Aidha Msolla alisema kwenye uteuzi wa wachezaji ni vema akawashirikisha na makocha wengine wamsaidie kwa kuwa nchi inamakocha wengi ambao wanaweza kumsaidia kuibua wachezaji wengine wenye vipaji walio maeneo mbalimbali na wanaweza kuisaidia timu kulikokuendelea kuchagua walewale kwakuwa lengo ni kujenga sio kubomoa “ Mimi ni mfano hai nilipokuwa kocha timu hiyo niliwashirikisha makocha mbalimbali akiwemo Charles Mkwasa kuifundisha timu, lakini hadi sasa siamini kama kweli kikosi kile anateua mwenyewe ninawasiswasi na watu wanaomzunguka wanafanya kazi hiyo jambo ambalo ni hatari,” alisema. | kitaifa |
HOSPITALI ya Rufaa ya taifa ya Mirembe haikujengwa mkoani Dodoma kutokana na mkoa huo kuwa na wagonjwa wengi wa akili (vichaa) bali kuwepo kwa gereza la Isanga ambalo wanafungwa wahalifu wakubwa na wauaji wanaotakiwa kupimwa akili zao.Naibu Waziri wa Afya, Maendelelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alitoa kauli hiyo baada ya Spika Job Ndugai kutaka kujua kama hospitali hiyo ya kutibu wagonjwa wa akili ilijengwa hapo kufuatia Dodoma kuwa na wagonjwa wengi wa akili.Dk Ndugulile alisema hospitali hiyo ilijengwa hapo kutokana na Dodoma kuwa na gereza la Isanga lenye wafungwa wa mauaji na wahalifu wakubwa ambao hutakiwa kupimwa akili zao.Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) aliyetaka kujua kwa nini dawa za kifafa na ugonjwa wa akili wilayani Ulanga mgao wake ni kidogo wakati wilaya hiyo inaongoza nchini kwa kuwa na wagonjwa wengi wa maradhi hayo. Dk Ndugulile alisema ni kweli Morogoro hasa wilaya ya Ulanga kuna wagonjwa wengi wa kifafa na akili, lakini atafuatilia kujua kwa nini dawa hizo hazifiki huko wakati zipo za kutosha.Akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Njombe Mjini, Edward Mwalongo (CCM) aliyetaka kujua serikali inajipangaje kuwatibu, kuwapa mavazi na makazi wagonjwa wa akili mitaani. Dk Ndugulile alisema wizara inaendelea kuimarisha huduma za afya nchini ikiwemo huduma ya afya ya akili. Uimarishaji huo wa huduma ya afya ya akili unakwenda hadi ngazi ya afya ya msingi ambako ndiko jamii ilipo.“Pamoja na kuongezeka kwa wagonjwa wa akili wanaorandaranda barabarani, sheria ya afya ya akili ya mwaka 2008 inawataka ndugu na jamii kuibua wagonjwa wa akili na kuwapeleka vituo vya kutolea huduma wapewe tiba,” alisema. Alisema wagonjwa wakipata nafuu, huruhiswa kukaa na familia zao na jamaa zao. Jukumu la kwanza la kulinda afya ya jamii huanzia ngazi ya familia, lakini jamii zinawanyanyapaa, kuwabagua, kuwatenga hivyo kuranda mitaani. | kitaifa |
KAMATI ya Kudumu ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, imeipongeza kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) kwa kuja na mbinu mpya za kujiendesha kibiashara.Kwa sasa kampuni hiyo inayozalisha magazeti ya HabariLEO, Daily News na SpotiLeo, imekuja na miradi mipya ikiwamo kuwa na shirika la habari (news agency) litakaloandaa habari na kuziuza kwa vyombo vingine vya habari ndani nan je ya nchi.Pamoja na hayo, kampuni hiyo ya TSN imekuja na mradi wa uchapishaji kidigitali, kuwa mshauri wa masuala ya habari, kupiga picha kibiashara na kutengeneza dokumentari.Akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo kwa kampuni ya TSN jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Musa Foum Musa, alisema ubunifu huo wa TSN utaiwezesha kampuni hiyo kujiongezea mapato, lakini pia kufikia lengo la kuwahabarisha Watanzania habari kutoka maeneo mbalimbali ikiwamo vijijini.“Tunaomba tu hii miradi mingine mnayofikiria kuianzisha muanze kuitekeleza haraka ili kama kuna watu wanaotaka hata kuwaiga ikiwamo sisi Zanzibar tuwaige. Maana hata wahenga walisema chema chajiuza,” alisema.Kaimu Meneja wa kiwanda cha uchapishaji cha TSN, Boniface Mwajombe, akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo, Tuma Abdallah, alisema mipango na mikakati hiyo ina lenga kukuza kipato cha kampuni hiyo, lakini pia kuwa chombo bora na cha kuaminika cha habari nchini.“Vision (dira) ya kampuni yetu ni kuwa chombo kinachokubalika na kuaminika nchini. Tunataka TSN iwe mouth piece (mdomo) wa serikali, kuelezea sera za serikali, kuwawezesha wananchi kupata habari kuhusu nini serikali yao inafanya na kuchukua mawazo ya wananchi na kuyachapisha kwenye vyombo vyetu vya habari,” alisema.Mwajombe alisema TSN ina amini katika kasi na teknolojia kutokana na mabadiliko ya duniani, ubunifu wa miradi mipya na kutumia njia rahisi kufanya biashara na kufikia masoko na umma ili wateja na wadau wapate bidhaa zenye ubora na kwa muda muafaka.Ametoa mfano namna TSN ilivyomuinua mwanafunzi wa Simiyu, aliyefanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne licha ya kusoma katika mazingira duni, hali iliyosababisha sasa kijana huyo kupata misaada mbalimbali ikiwamo kuendelezwa kielimu na wazazi wake kujengewa nyumba na wadau mbalimbali.“Katika eneo la ubunifu, TSN inataka kuwa shirika la habari, mradi wa uchapishaji ikiwamo uchapishaji wa kidijitali, huduma ya ushauri, kupigapicha kibiashara na kuziuza kwa wateja na kutengeneza dokomentari.”“Katika eneo hili la dokomentari tunawakaribisha wabunge na wawakilishi kupitia mradi wetu wa jimbo kwa jimbo hasa kipindi hiki cha uchaguzi. Hii ni fursa ya kuitumia ili watu wajue kiongozi wao amefanya nini kipindi chote cha uongozi wake,” alisema.Mwanjombe alieleza namna kampuni hiyo ya magazeti ya serikali inavyoshirikiana na Wakala wa Uchapaji ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Shirika la Magazeti ya Serikali (SMS).Alisema ushirikiano huo ulianza zamani kwani wamekuwa wakishirikiana kitaaluma, ambapo wamekuwa wakibadilishana ujuzi, lakini pia kwa TSN imekuwa ikichapisha gazeti la Zanzibar Leo.“Mara ya mwisho kuchapisha Zanzibar Leo ilikuwa mwaka 2016 lakini kwa bahati mbaya tulikuwa tunadai zaidi ya Sh milioni 300, lakini walipunguza hadi kufikia Sh milioni 289, tunaomba wapunguze angalau Sh milioni 10 au 20 kila mwezi,” alisema.Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Saleh Mneno, alikiri kufahamu deni hilo na kuahidi kukutanisha pande zote mbili TSN na SMS ili kuangalia namna ya kulilipa. | uchumi |
WASOMI wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) wakishirikiana na Umoja wa maveterani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamemuomba Rais John Magufuli kuruhusu lugha ya Kiswahili kutumika kufundishia elimu ya sekondari nchini.Wasomi hao wakiongozwa na Profesa Aldin Mutembei walikutana jana Dar es Salaam na uongozi wa umoja huo uliongozwa na Mwenyekiti wake, Kapteni Mohamed Ligola. Akizungumzia jinsi walivyojipanga kufanikisha malengo hayo ya kutumia Kiswahili kufundishia nchini, Mutembei alibainisha kuwa wameanza kwa kutunga vitabu vya kufundishia kidato cha kwanza.Alivitaja vitabu hivyo kuwa ni vya siasa, fizikia, kemia, hisabati, kilimo na vingine huku akibainisha vikiruhusiwa kufundishia kidato hicho cha kwanza wawekezaji wengi watajitokeza na kuwawezesha kutunga vitabu vya kidato cha pili na kuendelea hadi vya vyuo vikuu.Alisema, tangu mwaka 2015 walishatunga vitabu hivyo na wanachosubiria kwa sasa ni ruhusa ya kuanza kutumika kwake ili ichangie kuinua kiwango cha elimu nchini. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Walimu wa Hesabati nchini na Mhadhiri wa Hisabati UDSM, Saidi Sima aliyetunga kitabu cha hisabati kidato cha kwanza kwa Kiswahili, alisema matumizi ya lugha hiyo kufundishia itaongeza kiwango cha ufaulu nchini.Alisema, nchi itaendelea zaidi na kubainisha kuwa mwaka 1973 vitabu vya masomo mbalimbali vilivyokuwa kwa lugha ya kiingereza vilitafsiriwa kwa kiswahili na kuongeza kuwa ni muda mwafaka wa kurejesha lugha hiyo shuleni na vyuoni.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Veterani hao wa CCM, Ligola alibainisha, mchakato wa kuwasilisha mapendekezo hayo kwa Rais Magufuli ulishaanza na kuwa wana imani atafanyia kazi hoja hiyo. Alisema, Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele kuendeleza lugha ya Kiswahili na hasa kutokana na tabia yake ya kukipigania kwa kukizungumza kila mahala anapokuwapo. | kitaifa |
MITI 4,170,076 sawa na asilimia 73.4 kati ya mti 5,356,887 iliyopandwa kati ya mwaka 2017 na 2018 mkoani Lindi imepona na kuendelea kukua.Taarifa hiyo imetolewa na Ofi sa Maliasili na Mazingira wa Mkoa wa Lindi, Zawadi Jilala wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti kimkoa iliyofanyika wilayani Kilwa. Jilala alisema katika taarifa yake hiyo kwamba lengo la kupanda miti kwa miaka hiyo lilikuwa 7,500,000 hivyo miti iliyopandwa 5,356,887 ni na asilimia 71.3 ya lengo.Katika hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya kutwa ya Kilwa ambapo miti 600 ilipandwa katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi aliwataka watendaji wakuu wote wa halmashauri sita za mkoa huo kuhakikisha kwamba shughuli ya upandaji miti ni endelevu na wala si la matukio.Alisema Mkoa wa Lindi wenye jumla ya kilometa 67,855.32 sawa na hekta 6,785,532 ambazo kati ya hizo hekta 5,238,431 sawa na asilimia 77.2 ya eneo la mkoa zimefunikwa na uoto wa asili ambao ni misitu na mapori, ni lazima kukazana kupanda miti ili kuendelea kuwa na hali njema.Zambi alisema mapinduzi ya viwanda yanawezekana kwa kuhifadhi mazingira na kuhakikisha uvunaji wake unakwenda kwa mujibu wa taratibu. “Ingawa mkoa una misitu isiyoingiliwa sana na kuharibiwa sana ukilinganisha na mikoa mingine, ipo haja ya kuhakikisha rasilimali hizi haziharibiwi,” alisema mkuu wa mkoa katika hotuba iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai.Mkoa wa Lindi una msitu ya hifadhi isiyopungua hekta 829,510.5 ambayo imehifadhiwa kisheria. Miongoni ma misitu hiyo kuna msitu ya hifadhi ya taifa hekta 370,504, misitu ya hifadhi ya vijiji hekta 453,283.5;misitu ya mikoko hekta 44,038 na misitu ya kupandwa hekta 3,000. Misitu ya hifadhi ya vijiji mingi ipo katika Mradi wa usimamizi shirikishi wa misitu (PFM) ambao umewezeshwa na Shirika la kuendeleza na kuhifadhi Mpingo (MCDI) chini ya ufadhili wa WWF.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka alisisitiza haja ya upandaji wa miti kuwa endelevu kwa kuwa kila kitu anachohitaji binadamu msingi wake mkubwa ni miti na misitu. Mtendaji wa zamani wa misitu na Mwenyekiti wa bodi ya MCDI, Dk Felician Kilahama aliwataka wanamuziki kuhamasisha upandaji wa miti kupitia muziki ambao upo katika kila basi la abiria. Aidha Kaimu katibu tawala mkoa wa Lindi Dk Bora Haule alitaka kuwepo na kanzidata ya miti iliyopandwa na kupona. | kitaifa |
MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba jana walilipa kisasi baada ya kuifunga Mashujaa ya Kigoma kwa bao 1-0 katika mchezo wa kirafi ki uliofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.Ushindi huo wa Simba ni sawa na kulipa kisasi baada ya vigogo hao wa soka nchini kufungwa 3-2 na kutolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho na timu hiyo ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam msimu uliopita.Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na watazamaji wengi kwenye uwanja huo, bao hilo pekee la Simba lilifungwa katika dakika ya 56 na mchezaji wa kimataifa wa Sudan, Sharaf Shaiboub aliyeunganisha mpira wa pasi ndefu ulipigwa na kiungo wa kati Said Ndemla.Aidha, huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Simba baada ya juzi kuibuka na ushindi kama huo kwenye mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Bandari FC ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Katika mchezo mwingine wa kirafiki jana, Azam FC ilifunga African Lyon kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, huku mabao yake yakifungwa na Iddi Kipagwile na Joseph Mahundi.Yanga nayo iliifunga Friends Rangers kwa mbaoa 4-3 katika mchezo wa mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini wakijiandaa kwa mechi ya mtoano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids ya Misri Oktoba 27 CCM Kirumba Mwanza. | michezo |
WIZARA ya Fedha na Mipango imetoa orodha ya kwanza ya wadaiwa sugu wafanyabiashara 15 walionufaika na Mpango wa Kusaidia Uingizwaji wa Bidhaa nchini (CIS) na FACF, wafanyabiashara Mohamed Dewji na Yusuf Manji ni kati ya wadaiwa hao.Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na wizara hiyo, imewataka wadaiwa hao kulipa madeni yao haraka iwezekanavyo kabla hatua za kisheria kuchukuliwa. Watu wengine mashuhuri waliopo kwenye orodha hiyo ni pamoja na mwanasiasa aliyekuwa Waziri kwenye utawala uliopita, Stephen Wassira kupitia kampuni yake ya Siza Cold Storage Co. Ltd pia mwanasiasa Hashim Rungwe kupitia kampuni yake ya Bahari Motor Co. Ltd.Ikizungumzia madeni hayo, taarifa hiyo ilifafanua kuwa yanatokana na mkopo wa masharti nafuu kwa Taasisi, Kampuni, Viwanda na Wafanyabiashara ambapo wakopaji walitakiwa kulipa deni husika bila ya kutozwa riba katika kipindi cha miezi 18 tangu muda waliopewa mikopo hiyo.Ilinukuu kifungu cha sheria cha CIS ya mwaka 2008 (1)(b), inayosema kuwa mkopaji akichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18 tangu kupatiwa mkopo, atapaswa kulipa riba ya asilimia sawa na kiwango kinachotozwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inapoikopesha serikali katika kipindi husika. Ilielezea kuwa zaidi ya kampuni 980 zimekopeshwa chini ya utaratibu huo ambapo tangazo hilo lililotolewa jana lilikuwa ni la mara ya mwisho kwa kuwa imeshatangaza mara kwa mara na wadaiwa wameshindwa kuitikia mwito.Ilisema matangazo yalitolewa mnamo Desemba 30 mwaka 2015 na Aprili 4 mwaka jana, lakini hakuna jitihada za ulipaji wa madeni hayo zilizofanyika. Ilielezea kuwa wadaiwa ambao majina yao yametajwa jana kwa hiyo mara ya mwisho wakishindwa kujitokeza na kulipa hatua za kisheria zitachukuliwa. Kwa upande wa mfanyabiashara Mohamed Dewji anadaiwa kupitia kampuni zake za 21st Century Textiles na Afritex Ltd huku Manji akidaiwa kupitia kampuni zake za Farm Equipment Tanzania Ltd, Quality Group Ltd, Dunhill Motors Ltd, Quality Seed Ltd, Quality Garage Ltd. | kitaifa |
UBALOZI wa Tanzania nchini Ujerumani umesikitishwa na kitendo cha Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutoa tuhuma nzito dhidi ya Rais John Magufuli na serikali kuhusu ufi nyu wa demokrasia nchini.Kwa mujibu wa ubalozi huo, kitendo anachoendelea kukifanya mbunge huyo cha ziara za vyombo vya habari katika nchi mbalimbali duniani, kinaonesha ameshapona na anahitaji kurejea nchini Tanzania, kuendelea na majukumu yake kama mbunge.Katika taarifa yake aliyotoa kwa vyombo vya habari, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Posi , amesema ubalozi huo umesikitishwa na tuhuma alizotoa mbunge huyo dhidi ya serikali ya Tanzania katika mahojiano yake na Kituo cha Televisheni cha DW.Amesema tuhuma nyingi anazotoa Lissu ikiwemo kushambuliwa kwake na ukosefu wa demokrasia hazina ukweli, zaidi ya kumchafua Rais Dk Magufuli na serikali ya Tanzania.“Inasikitisha Mbunge huyu ambaye bado anaendelea na matibabu anaanzisha ziara katika nchi mbalimbalina kutunga tuhuma nzito dhidi ya nchi yetu,” alisema Dk Posi.Amesema watanzania pamoja na wapiga kura wa jimbo lake, walitarajia mbunge huyo kama ameshapona na ana uwezo wa kusafiri sehemu mbalimbali duniani, kama anavyofanya sasa, angerejea nyumbani Singida na kuendelea na majukumu yake ya kuwatumikia wananchi wake.Balozi huyo alieleza kuwa inaeleweka kuwa shambulio la risasi dhidi ya Mbunge huyo lililotokea Dodoma Septemba 17, mwaka juzi, lilikuwa la kutisha, kwa kuwa ni moja ya matukio machache kutokea nchini, ingawa yanaweza kutokea pia katika nchi nyingine.“Ilikuwa ni siku moja pia ambayo jijini Dar es Salaam alishambuliwa ofisa wa juu wa jeshi aliyestaafu na watu wasiojulikana na kumjeruhi vibaya na risasi. Rais alitoa taarifa ya kukemea matukio yote mawili na kuagiza uchunguzi wa kina ufanyike,” amesema.Amesema Dk Magufuli alimuagiza Makamu wa Rais na viongozi wengine waandamizi wa serikali, kumjulia hali Lissu alipokuwa hospitali Dodoma, Nairobi nchini Kenya na Brussels, Ubelgiji akipatiwa matibabu.“Inasikitisha kuona mbunge huyu anageuza hatua hizi zenye nia njema za Rais na kumtuhumu mambo mazito yasiyo na ukweli. Kwa sasa nchini Tanzania anasubiriwa mbunge huyu na dereva wake watoe maelezo ili uchunguzi uendelee,” amesema.Hata hivyo, alieleza kuwa baada ya tukio tu, uchunguzi ulianza, lakini ni lazima mbunge huyo atoe maelezo yake, kwa kuwa ni muhimu katika kesi hiyo.“Mpaka sasa vyombo vya dola havijaupata upande wa mbunge huyo kuhusu kile kilichotokea,” amesema.Akielezea madai ya ukosefu wa demokrasia nchini, hasa baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe kuwekwa mahabusu, alisema suala hilo liko kisheria.Posi alisema kiongozi huyo alipatiwa dhamana, lakini alirejeshwa mahabusu baada ya kuvunja masharti ya dhamana, baada ya kutotokea mahakamani bila sababu za msingi. | kitaifa |
SERIKALI imesema itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kuwa inaongeza uwiano wa jinsia baina ya wanaume na wanawake katika vyombo vya uamuzi ili kufi kia 50 kwa 50.Ili kufikia hilo, imetaja mikakati iliyoanza kuchukuliwa ili kuzijengea uwezo jinsia zote, ikiwemo ya kufuta kodi za pedi za kike ili kuwezesha watoto wa kike kupata elimu bila kuathiriwa na siku za hedhi.Mikakati mingine ni kujenga zahanati ili kupunguza vifo vya wanawake na watoto wakati wa kujifungua, kuimarisha elimu ya sekondari ili kupanua wigo wa elimu, na kuanzishwa kwa kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani ili kumpa muda zaidi wa kushiriki katika shughuli za maendeleo.Mikakati hiyo iliainishwa jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizindua Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge, wenye lengo la kuhimiza uwiano wa jinsia wakati wa uendeshaji wa shughuli za mhimili huo.Mbali ya kusifu Bunge kwa hatua mbalimbali za utekelezaji wa uwiano wa kijinsia, alisema serikali pia imekuwa inachukua hatua mbalimbali kufikia azma hiyo kupitia Sera ya Jinsia ya mwaka 2000 na itifaki mbalimbali za kimataifa.“Bado haitoshi, ni lazima jitihada zaidi zifanywe ili uwiano huu wa kijinsia uweze kufikia 50 kwa 50,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa. Alisema miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na serikali ni kuondoa kodi kwenye taulo za kike, yanayoagizwa kutoka nje ili kushusha bei ya taulo hizo na kuwafanya watoto wengi wa kike kuyanunua na kuyatumia wakiwa shuleni wakati wa hedhi bila kuhofia kudhalilika.Alisema baada ya hatua hiyo ya serikali, imebainika kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wa kike wanaohudhuria masomo wakati wote kutokana na kumudu gharama za kununua taulo hizo na kuzitumia wakati wa hedhi wakiwa masomoni.Hata hivyo, alionya kuwepo kwa wafanyabiashara ambao bado wanauza taulo hizo kwa bei ya juu licha ya serikali kufuta kodi. Alisema hatua kali zitachukuliwa dhidi yao, ikiwa ni pamoja na kuwafutia leseni za biashara.Alisema pia serikali imeendelea kuimarisha utoaji wa elimu ya sekondari ili kuwafanya watoto wengi, kunufaika na elimu hiyo huku ikiongeza madarasa na kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia.Alisema hadi sasa takwimu zinaonesha kuwa katika elimu ya juu uwiano wa kijinsia ni kati ya asilimia 30 kwa wasichana na asilimia 70 kwa wavulana, kwenye ajira ni asilimia 37 kwa wanawake na asilimia 63 kwa wanaume na kwenye uongozi ni asilimia 15 ya wanawake na asilimia 85 kwa wanaume.“Nichukue nafasi hii kulipongeza Bunge kwa kufikia asilimia 40 kwa wanawake na asilimia 60 kwa wanaume, lakini ni matakwa yangu kuona uwiano unaongezeka na kufikia asilimia 50 kwa 50,” alisema.Awali, Naibu Spika wa Bunge, ambaye ni pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mpango huo, Dk Tulia Ackson alisema mpango huo utaongeza ushiriki sawa wa wanawake na wanaume ndani ya Bunge na katika utekelezaji wa kazi zake zote.Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Godfrey Mulisa alisema Tanzania ni moja ya nchi, ambazo zimepiga hatua kubwa katika kuhamasisha uwiano wa kijinsi katika uendeshaji wa vyombo mbalimbali vya uamuzi. | michezo |
SERIKALI imeeleza mpango wake wa kusukuma mbele viwanda na kufanya biashara nchini kwa kuhakikisha inatekeleza mfumo rafi ki wa uwekezaji na ufanyaji biashara nchini. Imesema katika kuendeleza ujenzi wa uchumi wa viwanda serikali itaendelea kuweka vivutio na kufanya maboresho katika maeneo kadha yanayoleta vikwazo ili sekta binafsi ishiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi. “Pamoja na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji katika viwanda na biashara, utekelezaji wa Blue Print utakuwa tiba ya changamoto zinazotatiza sekta binafsi,” alisema Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake Bungeni jana. Alisema sekta binafsi ni injini ya kujenga uchumi wa viwanda hivyo serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha sekta hiyo inashiriki kikamilifu ujenzi wa uchumi.Alisema lengo ni kushawishi ujenzi wa viwanda vitakavyo ongeza thamani ya mazao yanayozalishwa nchini ili kuondokana na uuzaji wa malighafi nje ya nchi. Aidha, kwa msukumo wa sasa wa serikali, inatarajiwa kwamba sekta binafsi itajenga viwanda vinavyotoa ajira kwa wananchi kwa wingi na vile vinavyozalisha bidhaa zinazotumiwa na Watanzania walio wengi. Pia, serikali imesema itaimarisha taasisi zake za viwango na mfumo wa stakabadhi ghalani katika manununuzi, vituo maalumu vya mauzo ili kuwa chachu ya ulinzi wa viwanda na mlaji. Imesema itaboresha mifumo ya usajili wa biashara na leseni kutoka Brela na pia halmashauri kwa kuhakikisha inatoa mafunzo ya Tehama ili kumudu mfumo wa Dirisha la Taifa la Biashara (NBP) ambao ndio unaotoa leseni za biashara. Kakunda alisema kwa mwaka 2019/2020 serikali itaendelea na miradi ya kimkakati, urasimishaji wa viwanda na biashara ndogo na za kati, uongezaji thamani ya mazao ya kilimo na malighafi na kuunganisha masoko. Alisema ni lengo la serikali kufanya tathmini ya hali halisi ya uzalishaji na mahitaji ya bidhaa viwandani katika viwanda vya sukari, korosho, mafuta ya kula chuma, ngozi nguo na dawa za binadamu. | kitaifa |
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeanza kuhakiki malipo kwa ajiri ya wanachama wake, waliokuwa wakifanya kazi zisizo za weledi kwenye sekta mbalimbali kabla ya kuachishwa kazi.Hatua hiyo imekuja baada ya agizo la Rais John Magufuli alilolitoa, alipokutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Desemba 28 mwaka jana Ikulu, Dar es Salaam, la kutaka wafanyakazi wa aina hiyo kupewa fao lao la kuachishwa kazi.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meneja Kiongozi wa Matekelezo wa NSSF, Cosmas Sasi alibainisha kuwa malipo yatalipwa mara tu baada ya mfanyakazi husika kuhakikiwa.Sasi alisema uhakiki huo utachukua siku 30, tangu mfanyakazi kuwasilisha ombi lake na kuwa kwa maombi yatakayotiliwa shaka, yatafanyiwa uchunguzi kwa muda wa mwezi mmoja.Alisema NSSF imejipanga vyema kutekeleza uhakiki huo kwa wakati na muda mwafaka ili kila mwenye haki apewe haki yake kwa wakati, huku akiwataka wenye kustahili kulipwa fao hilo kutosita kuwasilisha maombi kwenye ofisi za NSSF zilizopo kila mkoa.“Tumejipanga kuwalipa kwa wakati hawa wafanyakazi wote waliokuwa kwenye ajira ya muda na ambao labla ajira imesitishwa au mradi kuisha, hawa watapewa mafao yao yote,” alisema. Alifafanua kuwa kila mhusika akishapewa fedha zake zote, alizokuwa amechangia NSSF, ataongewezewa na asilimia nyingine ya fedha kama nyongeza, ambazo hakuwa tayari kuziweka wazi kuwa ni ngapi.Alisema kwa wafanyakazi wanaofanya kazi za kitaaluma na walikuwa wakichangia zaidi ya miezi 18, wakisitishiwa ajira zao, watalipwa asilimia 33.3 ya mshahara waliokuwa wakilipwa kwa miezi sita kabla ya kupata ajira nyingine.Alibainisha kuwa kwa wale waliokuwa wakichangia chini ya miezi 18, watalipwa asilimia asilimia 50. Kwa upande wake, Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele akizungumzia kuhusu malipo ya pensheni kwa wastaafu wanaonufaika na mfuko huo, alibainisha kuwa wastaafu ambapo hawatakuwa wamehakikiwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu, malipo yao yatasitishwa.“Wastaafu ambao hadi sasa hawajahakikiwa wanaombwa kuwasilisha nakala stahiki kwenye ofisi za NSSF kwenye mikoa wanayotokea ili uhakiki ufanyike wakati,” alisema Mengele. “Kwa kuwa tunazo ofisi 65 Tanzania Bara ni dhahiri kuwa hakuna sababu za wastaafu hao kushindwa kwenda kuhakikiwa wajitokeze kwa wingi wakahakikiwe ili waje kunufaika na mapato na pia hata wale waliokuwa wakifanya kazi za muda mfupi na wamesitishiwa au kufukuzwa kazi au mradi kuisha, nao walete vielelezo wahakikiwe tayari kwa malipo stahiki,” aliongeza.Katika kikao cha Rais Magufuli na viongozi wa vyama vya wafanyakazi, aliagiza wastaafu kulipwa mafao yao kwa kufuata vikokotoo vya awali kwa muda wa miaka mitano ya mpito kuanzia sasa, tofauti na mapendekezo yaliyokuwa yametolewa chini ya Kanuni za Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).SSRA ilipendekeza kikokotoo cha asilimia 25 kwa wastaafu kwa mkupuo, kisha kuendelea kulipwa asilimia 75 kila mwezi hadi kufa kwao. Rais Magufuli alipinga hatua hiyo na kuagiza kuwa kuanzia sasa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na wa sekta binafsi NSSF, iliyoanza kufanya kazi mwaka jana, ianze kulipa wastaafu kwa kutumia kikokotoo cha zamani kwa mujibu wa mifuko waliyokuwemo kabla haijaunganishwa. | kitaifa |
MBUNGE wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) amesema ni aibu Tanzania kuchukua makocha kutoka nje huku kukiwa na wazawa wenye uwezo mkubwa.Akichangia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2018-2019, Nkamia alisema ni aibu kwa kocha wa mpira wa miguu kutoka Burundi. “Ni aibu kocha wa mpira wa miguu kutoka Burundi huku wazawa wakiwa hawapewi nafasi,” alisema.Nkamia aliyewahi kuwa kiongozi kwenye klabu ya Simba miaka ya nyuma alisema pia kwa sasa Ligi ya Soka ya Wanawake na Ligi Kuu imekuwa mahututi kutokana na timu kulia njaa. “Hata Ligi ya Wanawake hali sio nzuri, mfano timu inatoka nyumbani na ugenini timu inatoka Njombe haina hata sehemu ya kulala kwa sababu ya ukata, hatuwezi kuendesha mpira hivyo.”Kutokana na kauli hiyo, Spika Job Ndugai alisema: “Mheshimiwa Nkamia, sio timu za kina dada tu hata timu fulani zinatembeza bakuli mheshimiwa Nkamia.” Katika hatua nyingine, Mbunge wa Konde Khatibu Said Haji (CUF) amehoji ni kiasi gani cha fedha ambacho kimekuwa kinatolewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA).Akiuliza swali jana bungeni, Haji alihoji: “FIFA inatoa misaada ya fedha kwa kupitia TFF. Je, ni kiasi gani cha fedha TFF imekuwa ikiipatia Zanzibar kupitia ZFA?” Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alisema ni kweli FIFA inatoa msaada wa fedha kwa mashirikisho ya mpira wa miguu ikiwemo TFF kwa ajili ya miradi na programu mbalimbali.Alisema fedha hizo huwa ni maelekezo maalum kwa lengo la kusaidia na kuendeleza maeneo ya Ligi ya Wanawake, Vijana pamoja na masuala ya kiutawala. “Kuanzia mwaka huu FIFA itakuwa inatoa jumla ya dola za Marekani milioni 1.25 kila mwaka kwa wanachama wake ikiwemo ZFA ambayo ni sehemu ya TFF,”alisema. Akifafanua mchanganuo wa fedha hizo, Shonza alisema fedha za miradi kiasi cha dola za Marekani 750,000, fedha kwa ajili ya kuendesha ofisi dola za Marekani 500,000.“Hata hivyo kwa muda wa miaka mitatu kutokana na kutokuwepo kwa uwazi katika matumizi ya fedha na kukidhi vigezo vya utawala bora, TFF wamekuwa hawapati hizo fedha,” alisema Shonza. Shonza alisema kazi kubwa imefanyika kurekebisha dosari zilizokuwepo za kiuhasibu na utawala bora hivyo uwezekano ni mkubwa TFF na ZFA kuanza kupokea msaada huo wa fedha mapema mwaka huu. | michezo |
Hatua hiyo inatoa fursa kwa huduma hii mpya ya malipo ya kabla ya kutumia kadi ya kielektroniki la daraja la juu inayotumia mfumo wa kibenki, kufanyika katika wigo mpana ndani na nje ya Tanzania.Makubaliano hayo sasa, yatamwezesha mtumiaji wa huduma za B-PESA kuweza kufanya mwamala nje ya Tanzania katika mashine za kutolea fedha milioni 1.6 na kwa mawakala zaidi ya milioni 12 katika nchi 142.Mbali na UnionPay, taasisi nyingi za kibenki hapa nchini zimeonesha nia ya kushirikiana na Kampuni ya Smart Banking Solution (SBS) kuanza kutoa kadi za B-PESA kwa wateja wake, huku wakurugenzi wakuu wa taasisi hizo, wakiahidi kutoa kadi hizo kwa wateja wake mapema ili kunufaika na fursa hii.Haya yanatokea siku chache tu baada ya huduma ya malipo ya awali ya B-PESA kuzinduliwa nchini Tanzania, ikiwa na lengo la kutengeza mfumo madhubuti wa malipo kwa taasisi za kibenki na wateja walioko Tanzania na Afrika kwa ujumla.Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mwakilishi Mkuu wa UnionPay International Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Li Zhixian alisema kampuni yake ina furaha kubwa kushirikiana na B-PESA, sababu huduma zote mbili zinalenga kuleta mapinduzi katika mfumo wa malipo wa kielektroniki.“Baada ya kuangalia kwa undani sifa za B-PESA, naamini huduma hii itaweza kuubadilisha muundo wa malipo nchini Tanzania na hususani zaidi kuweza kuiboresha miundombinu ya malipo katika nchi hii. “Ukiwa kama mfumo wa malipo wa kimataifa unaochipukia, Union- Pay imekuwa ikijizatiti zaidi kurahisisha huduma ya malipo katika kila nchi. Wazo hili linaendana na la B-PESA. UnionPay na B-PESA tumesaini makubaliano haya leo kuangalia ni jinsi gani tunaweza kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja ili kuiongezea nguvu B-PESA kuweza kufikia masoko ya kimataifa,” alisema Li.Aliongeza “tungependa kuzikaribisha taasisi zenu za kibenki kujiunga na mpango huu ili kutoa kadi za UnionPay - B-PESA nchini. Wateja wenu watapata fursa ya kufurahia matumizi ya kadi za B-PESA nchini, na kwa kupitia UnionPay huduma yenu itatolewa kwenye nchi zaidi ya 140 duniani.”Alisema kuwa wazo la kushirikiana na B-PESA liliendana na lengo la kutumia mifumo hiyo miwili ya malipo ili kuipa msukumo zaidi sekta ya biashara baina ya China na Afrika.Kwa mujibu wa rekodi za kibiashara, China ni mbia mkubwa zaidi wa kibiashara nchini Tanzania na chanzo cha pili kwa ukubwa katika uwekezaji.Biashara baina ya nchi hizi mbili mwaka 2012 zilikuwa ni zaidi ya dola za Marekani bilioni 2.47, ambayo ni ongezeko la asilimia 15.2. China ni chaguo la kwanza kwa wafanyabiashara wa Tanzania katika masuala ya ugavi.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SBS, Gustav Vermaas alisema ushirikiano huo unaziongezea ubora kadi hizo na upekee zaidi, kwa maana wateja wa B-PESA watakuwa katika mstari wa mbele wa kuibadilisha Tanzania na Afrika kwa ujumla kuwa jamii isiyotegemea fedha taslim. | uchumi |
WATAZAMAJI wanatakiwa kutoa kiasi cha Sh 5,000 ili kuiona Simba ikicheza dhidi ya Mbabane Swallows ya eSwatini katika mchezo wa awali wa kuwania kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.Mchezo huo wa kwanza wa raundi ya awali, umepangwa kuanza majira ya saa 10:00. Ofisa Habari wa mabingwa hao wa Tanzania Bara, Haji Manara alisema kuwa kiingilio cha chini katika mchezo huo kitakuwa Sh 5,000 kwa majukwaa ya mzunguko.Viingilio vingine ani pamoja na Sh 7,000 kwa eneo la VIP C, 10,000/- eneo la VIP B na 20,000/- kwa watakaokaa VIP A. Manara alisema kwamba maandalizi ya mchezo huo yamekalika na tayari kikosi cha Simba kinasubiri kushuka dimbani kwa ajili ya mchezo huo. “Tunakwenda kuwakabili Mbabane Jumatano (leo) tukijua ni timu nzuri na mabingwa wenzetu, lakini tunajua matarajio ya Watanzania na wana Simba kwetu.Kwa kweli hatutawaangusha na tunaahidi furaha kwenu,” alisema Manara. Simba imepania kufika mbali msimu huu katika michuano ya Afrika baada ya msimu uliopita kutolewa katika Raundi ya Kwanza tu na Al Masry ya Misri kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.Na ikiwa chini ya kocha mpya, Mbelgiji Patrick Aussems – Simba imepania kutimiza hazma yake, baada ya kusajili kikosi kiapana chenye kusoka la kuvutia. Kikosi cha Simba ni kipana na kinataka kudhihirisha kuwa kiko vizuri katika mashindano ya kimataifa, hivyo leo kinaweza kutoa kichapo kwa wageni wake hao, ambao nao wako vizuri katika mashindano ya Afrika. | kitaifa |
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imekuwa inatumia wastani wa Sh bilioni tatu kila mwaka kusafi risha wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya kupata huduma za matibabu, tayari imeanza kuchukua hatua za kukabili changamoto hiyo.Hatua iliyochukuliwa ni ile ya kuingiwa kwa makubaliano baina ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mnazimmoja mjini Unguja, ili wagonjwa wa Zanzibar waweze kutibiwa Muhimbili.Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazimmoja, Jamala Taib alisema jana kuwa makubaliano hayo ya miaka mitatu lengo lake ni kuboresha huduma za afya kwa kushirikiana kwa pamoja.Alisema wapo zaidi ya wagonjwa 110 wanaosubiri huduma za matibabu ya nje ya nchi, idadi ambayo ni kubwa inayohitaji fedha nyingi. ‘’Makubaliano yetu ya miaka mitatu lengo lake kubwa ni kuwapatia huduma za matibabu wagonjwa wetu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ina uwezo mkubwa wa kutoa matibabu ya aina mbalimbali,” alisema.Jamala alisema Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imepiga hatua kubwa katika kufanya upasuaji wa aina mbalimbali kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambayo hufanyika katika baadhi ya nchi za Ulaya.Alisema makubaliano hayo yataokoa fedha nyingi za kigeni ambazo zilikuwa zitumike kusafirisha wagonjwa kwenda katika nchi mbalimbali za Ulaya na Asia. Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shufaa Nassor Ali alisema hayo ni makubaliano muhimu ambayo yamelenga katika kuimarisha huduma za afya za wananchi wa Zanzibar kuwa bora.Alisema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeridhishwa na aina ya huduma ambazo zitapatikana katika Hospitali ya Muhimbili kwa wananchi wanaohitaji matibabu nje ya nchi. Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar husafirisha wagonjwa wengi kwenda nje ya nchi ikiwemo India na Israel, wakiwemo watoto wanaokabiliwa na maradhi ya moyo. | kitaifa |
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Gor Mahia, Meddie Kagere ameibuka na kusema kuwa nusura atue kwa wapinzani wa timu hiyo ya Kenya, AFC Leopards kabla ya kusajili Gor.Akizungumza katika mahojiano na Sunday Nation, Kagere mwenye umri wa miaka 32 aliendelea kuichezea K’Ogalo kwa sababu tu viongozi hawakutokea kuzungumza naye kuhusu maslahi binafsi, ili ajiunge na Leopards.Kagere, ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Simba ya Tanzania aliongeza kusema kuwa pia alifikiria kujiunga na Tusker, lakini aliwamwaga baada ya uongozi wa timu hiyo kumtumia tiketi ya basi ya safari ya kama kilometa 1200, badala ya kumpatia tiketi ya ndege, usafiri ambao angetumia saa moja tu.“Gor walikuja lakini nilikuwa nataka kujiunga na AFC Leopards. Ukweli, makubaliano yalikuwa katika hatua ya juu kabisa.Tatizo kubwa la Tusker wenyewe walitaka niende Nairobi kwa basi kutoka Kigali.“Walitakiwa kunitumia mimi tiketi ya ndege na badala yake Gor Mahia walifanya hivyo na nikawakwepa Tusker na kutua Gor," alisema Kagere.“Wakati huo, Gor walikuwa hawajanifikia mimi bado. Kupitia Musa (Mohammed), walipata mawasiliano yangu na kunipatia tiketi ya ndege, wakisisitiza nisijiunge na wapinzani wao (AFC Leopards).”“Baada ya msimu wangu wa kwanza pale Gor Mahia, Zamalek ya Misri walinifuata lakini matatizo ya viza yaliua mpango huo.Wakati fulani mambo hayakuendei vizuri sio kwa sababu hauna bahati ila Mungu anakuwa hajapanga ufanikiwe kwa hilo.Hivyo tangu dirisha lifungwe ilinibidi kukaa miezi sita bila ya klabu," alisema Kagere.Kagere, ambaye aliwahi kuichezea timu ya Tunisia na Ulaya, sasa ameitosa Gor Mahia na kutua Simba na yuko timu hiyo katika kambi ya mazoezi Uturuki wakijiandaa kwa msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa. | michezo |
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekanusha taarifa zisizo rasmi kuhusu kuwepo kwa viwango vipya vya michango ya uanachama katika kupatiwa huduma za afya.Hata hivyo ilibainishwa jana kuwa upo mchakato wa kuunda vifurushi tofauti vya uchangiaji kwa makundi tofauti ya uanachama ili kuwezesha watu kujiunga kulingana na uhitaji wao. Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya uhusiano, taarifa zinazosambaa sio rasmi kwa hiyo zipuuzwe. Ilieleza kuwa mfuko umeanzisha vifurushi vya makundi mbalimbali ya wanufaika kama waajiriwa, watoto, wakulima na hata wajasiriamali. Kuhusu taarifa rasmi ikoje katika eneo hilo la kuongeza viwango vipya vya uchangiaji, Ofisa Mahusiano na Elimu kwa Umma, wa NHIF, Grace Kisinga alisema taarifa ya mfuko kuhusu suala hilo ndivyo ilivyo na kwamba wanachama wanachangia kwa taratibu zilizopo.Kuhusu kuongeza wigo wa wanufaika, alisema ili kuongeza wanufaika, mfuko pia ulishaanza mchakato wa kuunda vifurushi tofauti vya uchangiaji kwa makundi tofauti ya uanachama ili kuwezesha watu kujiunga kulingana na uhitaji wao. Alisema mchakato huo upo katika hatua za kukamilika katika ngazi mbalimbali za uongozi na utakapokamilika taarifa rasmi zitatolewa na mfuko wa umma. Iliongeza kuwa kwa sasa Mfuko unaendelea kusajili wanachama kupitia taratibu zilizopo za uchangiaji..Hata hivyo, NHIF, iliomba radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa na taarifa hizo zisizo rasmi na kuendelea kuwahimiza wananchi kufuatilia taarifa za NHFI kupitia tovuti yake. Wakati huo huo, kupitia tovuti ya mfuko huo, umeanza utaratibu wa uhakiki wa wanachama waliosajiliwakwa kwa wastaafu ili kuhuisha taarifa na kuweka kumbukumbu sahihi tangu Januari Mosi ukitarajiwa kukamilika Machi 30, mwaka huu.Ilielezwa kuwa kazi ya uhakiki unawahusu wanachama wastaafu walioandikishwa katika mfuko huo kuanzia Julai 2009 hadi Septemba 2018. Ilieleza kuwa uhakiki huo unafanywa kwa ofisi zote NHIF zilizopo Tanzania bara na Ofisi za Zanzibar. Mwanachama mstaafu atahitajika kufika katika ofisi yoyote ya NHIF akiambatana na mwenza wake (endapo yupo) na iwapo mwanachama mstaafu amefariki, mwenza aliyebaki atatakiwa kufika katika ofisi za mfuko huo kwa ajili ya uhakiki.Aidha mstaafu huyo atatakiwa kufika katika uhakiki huo akiwa na vitambulisho vya NHIF, cheti cha ndoa (mstaafu mwenye mwenza), na kitambulisho cha uraia, mpiga kura, leseni ya gari au hati ya kusafiria. Iliongeza kuwa wanachama wastaafu wanahimizwa kufuatilia taarifa hiyo na muda uliowekwa ili kuepuka usumbufu wakati wa kupatiwa huduma za afya. | kitaifa |
KOCHA wa Tanzania Prisons, Mohammed ‘Adolf’ Rishard, amesema hawatakubali rekodi yao ya kutokufungwa kwenye Ligi Kuu ivunjwe na Yanga kwenye mchezo utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Sokoine, mkoani Mbeya.Tanzania Prisons ambayo imecheza michezo 13 na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 na ikiwa imeshinda mechi tano, sare michezo nane, inakutana na Yanga inayoshika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 18.Adolf Richard ametoa tahadhari hiyo kwa Yanga ikiwa ni siku moja baada ya kupunguzwa kasi kwa kugawana pointi na Mbeya City kwenye mchezo wa ligi hiyo uliochezwa kwenye Uwanja Sokoine ambao ndio utakaotumika kwa mchezo wa kesho. “Tumejijengea falsafa moja ya kuwaheshimu wapinzani na tutaindeleza kwa Yanga ila wasije wakatarajia watakuja kupata matokeo kirahisi.Baada ya kutoka sare mechi iliyopita hatuwezi kukubali rekodi ya kutokufungwa ivunjwe na Yanga tena katika uwanja wetu wa nyumbani,” alisema. Alisema wanaiheshimu Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wazoefu na wenye uwezo wa kubadilisha matokeo wakati wowote, lakini kupitia mechi iliyopita wameona udhaifu wao mwingi, hivyo wamejipanga kuhakikisha dakika 90 zitaamua mshindi kuwa wao.“Wachezaji wote wako fiti kwa mchezo, kikubwa tubaomba mashabiki wa Mbeya na sehemu za jirani kujitokeza kwa wingi kutushangilia kwani ushindi wetu ni sifa ya mkoa wa Mbeya na Nyanda za Juu Kusini,” alisema Adolf Richard.Gazeti hili lilipomtafuta kocha wa Yanga, Charles Mkwasa, kuzungumzia maandalizi ya mchezo dhidi yaTanzania Prisons, aligoma kuzungumza kwa madai yupo kwenye mapumziko ya sikukuu ya Krismasi“Kama unataka taarifa kuhusu maandalizi ya timu kujipanga na mchezo ujao mtafute Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, atakuambia lakini kwa sasa nimechoka na sitaki kuongelea maana nipo mapumziko nasheherekea sikukuu ya Krismasi hapa Mbeya,” alisema Mkwasa. | michezo |
UONGOZI wa JKT Oljoro ya jijini Arusha ambao ndio wamiliki halali wa timu ya Arusha United wameiuza timu hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti. Hatua hiyo imekuja wiki chache baada ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo kudaiwa kushindwa kuiendesha timu hiyo ikiwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.Meneja wa timu hiyo, Jumanne Ahmed alisema ni kweli timu imenunuliwa na Alexander Mnyeti, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara ambaye sasa ndiye mkuru- genzi wa timu hiyo. Meneja huyo alisema timu hiyo inaitwa Gwambina FC na itaendeshwa kwa mfumo wa kisasa wa kampuni.“Timu itakuwa na mas- kani yake Misungwi mkoani Mwanza, ambako pia tunajenga uwanja mkubwa utakaojulikana kama Gwambina Complex na timu pamoja na uwanja vitazinduliwa Juni 21 mwaka huu, itaendeshwa kisasa kwa mfumo wa Kampuni,” alisema Ahmed.Akithibitisha hilo Meja Iddy Musila ambaye ni kaimu wa kikosi 833 Oljoro JKT alisema ni kweli wameamua kuiuza timu kumpa mdau mwingine wa soka ili aiendeleze mwenyewe, kwani awali waliitoa timu hiyo bure kwa mkuu wa mkoa Arusha kwa sababu alionesha nia ya kuiendeleza na kukuza michezo.Alisema wakati timu iko katika Ligi Daraja la Kwanza haikufikia hatua ya kumaliza ligi hiyo, mkuu wa mkoa aliamua kujitoa kuisimamia kutokana na kutofautiana na waendeshaji wa Bodi ya Ligi kwa madai kuwa hawakuwatendea haki hivyo timu ikabaki haina mwenyewe.“Tulihakikisha inamaliza ligi hiyo na baada ya hapo akatokea mdau ambaye alikuwa anatafuta timu na hatukuwa na sababu ya kuendelea nayo kwani uwezo hatukuwa nao katika suala zima la kiuchumi,” alisema Musila.Alisema suala la uchumi limepelekea timu waiuze kwani kuendesha timu ni gharama na ikizingatiwa kipindi kile mkuu wa mkoa ameiacha walitumia gharama sana kumalizia zile mechi tano zilizokuwa zimebaki, hivyo wakaona kabla ya kuanza kwa msimu waitoe kwa mdau.“Hivi sasa hatuna mpango wowote wa kuanzisha timu, kwani tayari JKT ina timu hivyo hatuna sababu ya kuwa na timu ila tutakuwa na timu za huku kikosini ambazo vijana watacheza mechi za ujirani mwema, lakini kwa upande wa timu katika ligi hatuna mpango huo tena,” alisema Musila. | kitaifa |
UPELELEZI katika kesi ya kuchapisha video ya ngono kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram inayomkabili, Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, bado haujakamilika.Wakili wa Serikali, Jenipher Masue alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Maira Kasonde kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado unaendelea.Hakimu Kasonde aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 12, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kwamba dhamana ya mshitakiwa bado inaendelea. Akisoma mashitaka hayo katika kesi namba 322, Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono alidai kuwa Oktoba 15, mwaka huu katika sehemu tofauti za Mkoa wa Dar es Salaam, Wema alichapisha video za ngono kupitia ukurasa wake wa Instagram jambo ambalo ni kinyume na sheria.Hii ni mara ya pili kwa mlimbwende huyo ambaye alishinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, kufikishwa mahakamani hapo kwa mashitaka tofauti ambapo awali alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na kutumia bangi. Wakili wa utetezi, Reuben Simwanza aliomba mahakama hiyo impatie dhamana yenye masharti nafuu mteja wake kwa kuwa ni haki yake.Hata hivyo, Wakili Kombakono aliomba mahakama hiyo kumpatia mshitakiwa masharti magumu ya dhamana ili iwe fundisho kwake na kwa wengine kwa sababu ni msanii mwenye wafuasi wengi wanaomuangalia hususan watoto. Hakimu Kasonde alimtaka mshitakiwa Wema kuwa na mdhamini mmoja watakaosaini kulipa bondi ya Sh milioni 10 pia alimpiga marufuku Wema kuchapisha au kuweka picha na maneno yoyote ya kingono katika ukurasa wake huo wa mtandao wa Instagram.Oktoba 25, mwaka huu Wema katika mkutano wake na waandishi wa habari aliomba radhi watanzania kwa video za ngono zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii hususani Instagram.Katika maelezo yake, Wema aliomba radhi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bodi ya filamu, familia yake, ndugu, jamaa na marafiki ambao wanamuangalia kama kioo cha jamii pamoja na kumuomba radhi mama yake mzazi.Pia alikiri kuwa aliwadharirisha na kuwafedhehesha watu wengi pamoja na kuwaathiri na kwamba lengo la kuomba radhi si kwa kuomba huruma ya mtu yoyote bali kwa kugundua kosa lake. Hata hivyo, baada ya kuomba radhi Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) lilimfungia muigizaji huyo kutojihusisha na kazi zozote za sanaa kwa muda usiojulikana. | kitaifa |
MAREKEBISHO ya Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Sura ya 230 yanayojumuisha mapendekezo ya kuzirasimisha kumbi au vibanda vinavyotumika kuoneshea video na hivyo kuratibiwa na sheria hiyo ya filamu, yamepitishwa rasmi na Bunge.Aidha, marekebisho hayo yameweka masharti kwa mtu au kampuni ya kigeni inayotaka kutumia eneo lolote Tanzania kutengeneza filamu, ikiwemo kuwasilisha nakala ya awali iliyotumika kutengeneza filamu husika.Marekebisho hayo yamepitishwa kupitia Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali 8, namba 3 wa mwaka 2019, unaojumuisha marekebisho ya sheria hiyo ya filamu uliowasilishwa bungeni Dodoma jana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi.Akiwasilisha marekebisho hayo alibainisha kuwa muswada huo unapendekeza marekebisho yaliyolenga kuboresha usimamizi na kuweka ubora wa kumbi za sinema na vibanda vinavyoonesha video. Pia alisema yamelenga kuongeza mapato kupitia maboresho ya usambazaji wa filamu kwa watendaji wa filamu pamoja na kuongeza mapato ya serikali.Profesa Kilangi alieleza kuwa lengo la marekebisho hayo ni kuhakikisha kumbi na vibanda vinavyotumika kuoneshea video vinapaswa kurasimishwa chini ya kifungu cha 10 cha Sheria hiyo.“Sehemu hiyo pia inapendekeza kuongezwa kwa kifungu kipya cha 6A, ambacho kimeweka masharti mapya kuhusu utengenezaji wa filamu nchini, yanayomtaka mtu au kampuni ya kigeni kuwasilisha nakala ya awali iliyotumika kutengeneza filamu husika ili kupata kibali cha kutumia eneo la Tanzania katika kutengenezea filamu hiyo,” alisema Profesa Kilangi. | michezo |
Akizungumza jana Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa, Uchuuzaji na Mikakati wa Benki hiyo, Musa Kitoi alisema mashine hizo za kisasa za i-ATMs zimetengenezwa kwa teknolojia ya juu na zina sifa ya kipekee.Alisema huduma mbalimbali kama kuweka na kutoa fedha taslimu na hundi sasa zinaweza kufanyika kupitia mashine hizo mpya na kurahisisha huduma za kibenki kwawateja wao.Aliongeza kwamba benki hiyo itaendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wake kwa ufanisi wa hali ya juu ikizingatia uhakiki wa huduma bora kwa wateja wake na kurahisisha maisha yao kwa ujumla.“Barclays tunawajali wateja wetu na siku zote tunanuia kuwapa huduma za hali ya juu kufuatana na matakwa yao, pia bidhaa na huduma zetu hupangwa kufuatana na mahitaji ya wateja wetu.“Tunapenda kuwathibitishia kwamba tuko katika kiwango cha juu sana kiteknolojia. Katika soko na baadhi ya huduma zetu za kiteknolojia ya juu kama mfumo wa kutoa na kuchukua fedha bila kujaza fomu, utumaji wa fedha kwenye mashine, benki kwa njia ya simu na mwaka jana tumezindua service guarantee ikimaanisha uhakiki wahuduma na kutimiza ahadi na kuwapa wateja huduma bora na za uhakika,” alisema.Meneja Miradi na Mikakati wa Benki hiyo, Jane Mbwilo alisema huduma hiyo ni saa 24 na mteja anaweza kuweka kiasi chochote kwenye mashine hizo za ATM hapa nchini.Alifafanua kwa sasa mashine zipo 24, lakini wapo katika mkakati wa mwisho kuongeza mashine hadi kufika 30 katika maeneo kadhaa ya jijini la Dar es Salaam. | uchumi |
TIMU ya Yanga jana ilipindua meza kibabe baada ya kuwa nyuma kwa mabao 3-1 na kulazimisha sare ya 3-3 na kunusurika na kichapo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Huu ni mchezo wa pili kwa Yanga kushuka dimbani baada ya kucheza mchezo wa kwanza, ambao walipoteza dhidi ya Ruvu Shooting kwa mabao 2-0 katika mchezo wa mwanzo.Yanga ilikuwa na jukumu la kuliwakilisha taifa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, na ndio maana haikucheza mechi zake za awali. Sasa timu hiyo inasubiri ratiba ya mechi za mtoano kwa ajili ya kucheza hatua ya makundi ta Kombe la Shirikisho Afrika. Katika mchezo huo wa jana, Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mchezaji wake mkongwe, Mrisho Ngassa.Hata hivyo, Polisi Tanzania walisawazisha katika dakika ya 32 kupitia kwa Ditram Nchimbi, huku timu hiyo nusura ifunge tena katika dakika ya 39 baada ya Marcel Kaheza kushinda kutumia vizuri nafasi ya kufunga baada ya kupaisha juu mpira. Dakika ya 55 Polisi Tanzania waliandika bao la pili kupitia kwa Ditram kabla ya dakika mbili baadaye mchezaji huyo kufunga la tatu na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kufunga hat-trick na kuondoka na mpira.Yanga walifunga bao pili katika dakika ya 65 likiwekwa wavuni na Dsvis Moliga baada ya kupata pasi kutoka kwa Makame kabla ya kufunga la tatu katika dakika ya 68 kwa mpira wa adhabu, uliokwenda moja kwa moja wavuni. Katika dakika ya 90, Polisi walipata pigo baada ya mchezaji wake, Yassin Mustapha kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuupiga mpira nje wakati tayari mwamuzi alipuliza filimbi.Yanga katika mchezo huo walionekana kucheza bila kujituma zaidi na wengi walitarajia timu hiyo ingefungwa na Polisi Tanzania iliyocheza vizuri. Vikosi, Yanga: Meacha Mnata, Juma Abdul, Ali Mtoni, Kelvin Yondani, Lamine Moro, Abdulaziz Makame, Mrisho Ngasa, Feisal Salum, David Molinga, Juma Balinya/Balama Mapinduzi na Sadney Urikhob/Desu Kaseke.Polisi Tanzania: Kulwa Said, William Lucian, Yassin Mustapha, Pato Ngonyani, Idd Mobby, Baraka Majogoo, Andrew Chamungu, Hassan Maulid, Ditram Kapama na Sixtus Sabilo/Mohamed Mkopo. | michezo |